TOBA YA MTAKATIFU



2) TOBA YA MTAKATIFU

>> Pengine unaweza kujiuliza kwamba huyu mtu ni mtakatifu sasa kwa nini atubu? Kwa swali kama hili naweza kuanza kulijibu kwamba MAISHA YA MTAKATIFU NI MAISHA YA TOBA ENDELEVU! Labda tuangalie maandiko ili tuelewe vema:


Isaya 57:15

[15]Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu. 

For thus saith the high and lofty One that inhabiteth eternity, whose name is Holy; I dwell in the high and holy place, with him also that is of a contrite and humble spirit, to revive the spirit of the humble, and to revive the heart of the contrite ones.

>> MUNGU WA MILELE NI MTAKATIFU,  AMEKETI MAHALI PA JUU PALIPOINUKA  NA AMETUKUKA SANA

>> YEYE ANAKAA MAHALI HAPO PA JUU PALIPOINUKA PATAKATIFU PAMOJA NA YEYE MWANADAMU 

1. Mwenye roho iliyotubu ( repentant/ contrite spirit)

2. Mwenye roho iliyonyenyekea kwake ( humble spirit)

>> HAKUNA MTENDA DHAMBI MWENYE SIFA HIZI, NA HAKUNA MTENDA DHAMBI ANAYEWEZA KUMKARIBIA MUNGU MTAKATIFU,  ACHA TU KULE KUKAA NAYE MAHALI PAMOJA KATIKA ROHO!

>> Mtenda dhambi hana moyo wa toba au roho ya toba; na pia mtenda dhambi hana moyo wa au roho ya unyenyekevu 

>> Anapookoka Mungu anafanya uumbaji mpya ndani yake kama nabii Ezekieli anenavyo;

Ezekieli 36:25-26

[25]Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. 

Then will I sprinkle clean water upon you, and ye shall be clean: from all your filthiness, and from all your idols, will I cleanse you.

[26]Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 

A new heart also will I give you, and a new spirit will I put within you: and I will take away the stony heart out of your flesh, and I will give you an heart of flesh.

>> MUNGU HUWA ANAUONDOA ULE MOYO WA JIWE WA MTENDA DHAMBI NA KUWEKA MOYO WA NYAMA NDANI YAKE

>> NENO MOYO WA JIWE HAPA LINAMAANISHA ULE MOYO USIO NA TOBA WALA UNYENYEKEVU 

>> YAANI, MOYO WA JIWE HAUNA roho ya toba (iliyotubu) wala roho iliyonyenyekea

>> MOYO WA JIWE HAUMTAKI MUNGU NA WALA HAUKUBALIANI NAYE KWA KUWA HAUMWAMINI!

>> MTENDA DHAMBI ANAPOTUBU NA KUIAMINI INJILI NDIPO MUNGU ANAMUOSHA KWA MUJIBU WA EZE 36:25 HAPO JUU, UCHAFU WAKE WOTE KWA LILE NENO (MAJI SAFI)

>> NA KISHA ANAFANYA UUMBAJI MPYA KWA KUUTOA MOYO WA JIWE, AU roho ile iliyokufa kwa sababu ya dhambi (Eze 18:4 & 18:20), NA KISHA KUTIA roho mpya ndani yake ya utakatifu!! Yaani, roho iliyotubu na kunyenyekea mbele za Mungu! Hii ndiyo maana ya mtu kuwa KIUMBE KIPYA (2 KOR 5:17)

[KIUMBE KIPYA = moyo mpya + roho mpya]

>> MOYO MPYA NI HUU:

Mathayo 11:29

[29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 

Take my yoke upon you, and learn of me; for I am meek and lowly in heart: and ye shall find rest unto your souls.

>> MOYO MPYA NI roho ya upole na unyenyekevu ya Yesu ndani yako

>> Utagundua hapa neno moyo linatumika kuonyesha ni roho ya namna gani inaongelewa!

>> WOKOVU NI BADILIKO KATIKA ROHO YA MWANADAMU AMBALO LINAMBADILISHA KABISA KUWA MTU MWINGINE AU KIUMBE KIPYA MWENYE MOYO MPYA NA ROHO MPYA KUTOKA KWA BWANA YESU

>> Mwanadamu ni roho mwenye nafsi anayeishi katika mwili. Badiliko lolote la mwanadamu huyu lazima liwe ni badiliko la rohoni kwanza na siyo nafsini au mwilini!

>> Nafsi (soul) = Mind(akili/mawazo/fikra) + Will (nia/ makusudio/mapenzi) + Emotions (Hisia )

>> ELIMU ZA DUNIANI ZINAONGEZA MAARIFA NA TAARIFA NAFSINI, LAKINI HAZIBADILI ROHO YA MWANADAMU (MOYO WAKE)

>> Sasa Mungu akiisha kuutoa moyo wa jiwe na kuweka moyo wa nyama kwa kuumba roho mpya, huwa haishii hapo!! Mstari wa 27 anasema:

Ezekieli 36:27

[27]Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. 

And I will put my spirit within you, and cause you to walk in my statutes, and ye shall keep my judgments, and do them.

>>  NAMI NITATIA "ROHO YANGU" NDANI YENU.......! Hakusema hapa roho mpya maana hapo amemaliza kuumba roho mpya na tayari amepata kiumbe kipya! Hapa ANATIA ROHO WAKE MTAKATIFU NDANI YA KIUMBE HUYU MPYA MWENYE ROHO NA MOYO MPYA! HUU SASA NI MUUNGANIKO WA 1 KOR 6:17

1 Corinthians 6:17

[17]But the person who is united to the Lord becomes one spirit with Him.

17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. 

1 Wakorintho 6:17

>> UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU NI MUUNGANIKO WA MWAMINI NA MUNGU KATIKA ROHO

>> MWAMINI SASA AMEKUWA ROHO MOJA NA MUNGU! YAANI, [roho ya mwamini + Roho wa Kristo = 1] katika roho!!

>> Hii unaweza kuiita unganiko la Moyo kwa moyo!!! Ama (Roho kwa roho).  Na hapa ndipo unapozaliwa USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU SAWASAWA NA KWELI ILIVYO MAANA ROHO MTAKATIFU NDIYE ROHO WA KWELI ANAYEKUONGOZA roho yako KUTEMBEA NA KUENENDA KWENYE KWELI YOTE (Yohana 16:13)

>> MTAKATIFU HUYU MPAKA HAPA ANA NEEMA YA MUNGU MAISHANI MWAKE ITOKAYO KWA HUYU ROHO WA NEEMA ALIYEMO NDANI YAKE KUPITIA IMANI YAKE KWA YESU

>> NEEMA MAANA YAKE NI, ROHO MTAKATIFU + NGUVU ZAKE, ANAKUONGOZA NA KUKUWEZESHA KUITII KWELI ULIYOIAMINI NA KUIKUBALI

>> KAMA KWELI INASEMA TUBU AU TOA AU SAMEHE AU OMBA N.K. HII INAINGIA NDANI YA ROHO YAKO NA KUKUPA NGUVU ZA KUITENDA MAANA UMEIAMINI! NIWEKE ANDIKO HAPA ILI IELEWEKE:

Yohana 6:63

[63]Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. 

It is the spirit that quickeneth; the flesh profiteth nothing: the words that I speak unto you, they are spirit, and they are life.

>> MAISHA YA MTAKATIFU YAKO KWENYE ROHO

>> MANENO YA KRISTO NI ROHO NA TENA NI MAISHA/UZIMA (LIFE)

>> MAISHA YA MTAKATIFU NI MAISHA YA NENO

>> ROHO MTAKATIFU NI ROHO WA NENO (KWELI)

>> MTAKATIFU ANAISHI KWA KILA NENO LITOKALO KWENYE KINYWA CHA MUNGU (MATHAYO 4:4)

>> YAANI, MAISHA MAPYA YA MTAKATIFU YAMO KWENYE MWANZO 1:1 HADI UFUNUO 22:21!!

>> UTAKATIFU NI MAISHA YA NENO (KRISTO) KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU KUPITIA IMANI YAKO ILIYO HAI KWA YESU

>> KUTUBU NI MAISHA YA MTAKATIFU MAANA KUMO ROHONI MWAKE, NAFSINI MWAKE, NA KINYWANI MWAKE!!

>> MTAKATIFU  ANAPENDA KUTUBU, ANAFURAHIA KUTUBU, NA ANA UTAYARI WA KUTUBU SIKU ZOTE, WAKATI WOTE NA MAHALI POTE SAWASAWA NA ANDIKO HILI:

Isaya 66:2

[2]Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu. 

For all those things hath mine hand made, and all those things have been, saith the LORD: but to this man will I look, even to him that is poor and of a contrite spirit, and trembleth at my word.

>> MTAKATIFU 

A) NI MASKINI NA 

MNYONGE WA ROHO MAANA AMEMTUMAINI NA KUMTEGEMEA MUNGU ASILIMIA ZOTE KATIKA MAMBO YOTE, NA KAMWE HAJIVUNII LOLOTE AU CHOCHOTE AU YEYOTE, NA NDIYO MAANA AMEJAA MUNGU! NI TAJIRI KATIKA ROHO NA UFALME WA MUNGU UMO NDANI YAKE 

B) MTAKATIFU ANA ROHO ILIYOPONDEKA AMBAYO NI ROHO ILIYOTUBU NA KUNYENYEKEA MBELE ZA MUNGU SIKUZOTE! NI ROHO INAYOUGUA NA KUOMBOLEZA KUMTAKA MUNGU NA KUKATAA UOVU NA UBAYA WOTE NA ISIYOTAKA KAMWE KUMKOSEA MUNGU: NA HUU NI MOYO UNAOHITAJI MSAADA WA MUNGU MNO SANA KILA WAKATI KWA AJILI YA NEEMA NA ULINZI WAKE ILI ASIMKOSEE MUNGU KATIKA MAPITO YOTE YA MAISHA YAKE KWENYE MWILI HUU HAPA DUNIANI

C) MTAKATIFU ANATETEMEKA KWA KICHO PALE ANAPOLISIKIA NENO LA MFALME MKUU WA UTUKUFU AMBALO ANAJUA VEMA KWAMBA HALIMRUDII MUNGU BURE KAMWE BALI SIKUZOTE HUTIMIZA MAKUSUDI NA MAPENZI YAKE KAMA ALIVYOKUSUDIA

10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; 

Isaya 55:10

11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. 

Isaya 55:11

>>  NENO LA MUNGU UKILIKUBALI NA KULITII UTAFAIDIKA NALO LAKINI UKILIKATAA NA KULIASI LITAKUDHURU

Isaya 1:19-20

[19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; 

If ye be willing and obedient, ye shall eat the good of the land:

[20]bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya. 

But if ye refuse and rebel, ye shall be devoured with the sword: for the mouth of the LORD hath spoken it.

>> MTAKATIFU AMECHAGUA KULA MEMA YA NCHI MAANA AMEKUBALI NA KUTII (ana roho ya utayari wa kulitenda neno na pia ana roho ya utii)

KWA NINI MTAKATIFU ATUBU?

1) MTAKATIFU ANAMCHA BWANA KWA KUCHUKIA UOVU (MITHALI 8:13) NA PIA ANAJIEPUSHA NA KUJITENGA NA HUO UOVU (MITHALI 16:6)! TOBA NI KAMA MAJI YA KUSAFISHA MOYO NA NAFSI YAKE KILA ANAPOCHAFUKA

2) TOBA YA MTAKATIFU INADUMISHA UTAKATIFU WAKE ALIONAO TAYARI! INAMFANYA ADUMU KATIKA UTAKATIFU, HAKI, NA KWELI (1 PETRO 1:15-16)

3) TOBA YA MTAKATIFU INAMWEZESHA KUDUMU KATIKA MAISHA YA UTAKASO KAMA MAANDIKO YANENAVYO:

2 Wakorintho 7:1

[1]Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. 

Having therefore these promises, dearly beloved, let us cleanse ourselves from all filthiness of the flesh and spirit, perfecting holiness in the fear of God.

1 Petro 1:22

[22]Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. 

Seeing ye have purified your souls in obeying the truth through the Spirit unto unfeigned love of the brethren, see that ye love one another with a pure heart fervently:

>> HUWEZI KUJITAKASA KAMA HAUPENDI USAFI WA MOYO, NA HUWEZI KUJITAKASA KAMA HAUNA MOYO WA TOBA!!

4)TOBA YA MTAKATIFU INAMUONDOLEA LAWAMA ZOTE KATIKA UTAKATIFU WAKE

Waefeso 1:4

[4]kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 

According as he hath chosen us in him before the foundation of the world, that we should be holy and without blame before him in love:

>> TANGU KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU MUNGU ALIKUCHAGUA UJE KUWA NDANI YA KRISTO UKIWA NI MTAKATIFU USIYELAUMIKA MBELE  ZAKE KATIKA PENDO! 1) SHETANI AKOSE CHA KULAUMU 2) WANADAMU WAKOSE CHA KULAUMU, 3) NA MUNGU ASIONE TATIZO NDANI YAKO KWA HABARI YA PENDO LAKO KWAKE

>> HAPA NAPO PAULO ANAWAOMBEA KANISA LA THESALONIKE 

12 Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; 

1 Wathesalonike 3:12

13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote. 

1 Wathesalonike 3:13

>> MST 13 ANAOMBA KWAMBA MUNGU AWAFANYE MIOYO YAO IWE IMARA BILA LAWAMA KATIKA UTAKATIFU MBELE ZA MUNGU 

>> KUMBE KUNA LAWAMA NA HATIA KATIKA UTAKATIFU WAKO AMBAZO LAZIMA ZIONDOKE ILI UZIDI KUKUA KIROHO, UZIDI KUWA SAFI UONGEZEKE NGUVU ROHONI, NA KUZIDI KUFANANA NA YESU

Rev 22:11 Douay-Rheims Bible

He that hurteth, let him hurt still: and he that is filthy, let him be filthy still: and he that is just, let him be justified still: and he that is holy, let him be sanctified still.

11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. 

Ufunuo wa Yohana 22:11

>> KAMA UNATAKA NA UNATAFUTA NA UNATAMANI KUFANANA NA YESU, NDUGU MTAKATIFU UNAHITAJI KUTUBU SANA MAENEO MENGI!! (YOU HAVE A LOT OF REPENTING TO DO!!)

Wafilipi 3:12-15

[12]Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 

Not as though I had already attained, either were already perfect: but I follow after, if that I may apprehend that for which also I am apprehended of Christ Jesus.

[13]Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 

Brethren, I count not myself to have apprehended: but this one thing I do, forgetting those things which are behind, and reaching forth unto those things which are before,

[14]nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. 

I press toward the mark for the prize of the high calling of God in Christ Jesus.

[15]Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo. 

Let us therefore, as many as be perfect, be thus minded: and if in any thing ye be otherwise minded, God shall reveal even this unto you.

>> WATAKATIFU WENYE MIOYO ILIYOTUBU NA KUNYENYEKEA

》》HUWA HAWAJIHESABII HAKI NA 

》》WALA HAWAJIONI KUWA SASA WAMEKAMILIKA KATIKA UTAKATIFU 

》》NA WALA HAWARIDHIKI NA KIWANGO CHOCHOTE WALICHOFIKIA CHA KIROHO, 

》》BALI WAO WANAZIDI KUNYENYEKEA CHINI YA MKONO WA MUNGU ULIO HODARI ILI YEYE AWAKWEZE KWA WAKATI WAKE!!

>> WANAOTUBU KWA NAMNA ENDELEVU HUWA MUNGU ANAWAVIKA UWEZA ZAIDI MAANA YEYE ANAPENDEZWA NA UNYENYEKEVU WAO!!

>> WEWE NI MTAKATIFU KWA KIWANGO CHA TOBA ULICHOKIFIKIA MBELE ZA MUNGU 

>> DAUDI ALIMPENDEZA MUNGU KWA SABABU YA MOYO WAKE WA TOBA! NAYE ALIANDIKA;

Zaburi 51:17

[17]Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; 

Moyo uliovunjika na kupondeka, 

Ee Mungu, hutaudharau. 

The sacrifices of God are a broken spirit: a broken and a contrite heart, O God, thou wilt not despise.

>> HUU NDIO MOYO AMBAO ALIKUWA NAO DAUDI LAKINI SAULI HAKUWA NAO!! ( brokenness before God!)

>> MARAFIKI WA MUNGU WOTE WAMEPONDEKA NA KUVUNJIKA!! WANAMTAKA NA KUMHITAJI MUNGU KULIKO CHOCHOTE KINGINE AU YEYOTE MWINGINE!! WANATAKA NA WANATAFUTA KUMPENDEZA MUNGU KULIKO YEYOTE MWINGINE! MAFANIKIO YAO NI MAFANIKIO YA NENO LA MUNGU NA MAPENZI YAKE!! WAMEPONDEKA NA KUVUNJIKA KWA KUUGUA WANAPOONA DUNIA ISIVYOMJALI WALA KUMTAKA MUNGU!!

>> NI WAKATI SASA WA KUTUBU!! USISEME UTUBIE NINI?

1) 1 Yohana 2:6

[6]Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda. 

He that saith he abideth in him ought himself also so to walk, even as he walked.

>> JE! UNATEMBEA NA KUENENDA VILE VILE KAMA YEYE ALIVYOENENDA MWENYEWE YESU!! KUNA MAMBO YA KUTUBIA!!

2) Yohana 14:12

[12]Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 

Verily, verily, I say unto you, He that believeth on me, the works that I do shall he do also; and greater works than these shall he do; because I go unto my Father.

>> UNAAMINI??!! JE! UNAZIFANYA KAZI ZOTE ALIZOZIFANYA YESU??!!

NA JE! UNAZIFANYA KAZI KUBWA KULIKO ALIZOZIFANYA YESU?!

>> KAMA SIYO KUNA MAMBO YA KUTUBIA!!

3) Wakolosai 3:1-4

[1]Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 

If ye then be risen with Christ, seek those things which are above, where Christ sitteth on the right hand of God.

[2]Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 

Set your affection on things above, not on things on the earth.

[3]Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 

For ye are dead, and your life is hid with Christ in God.

[4]Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. 

When Christ, who is our life, shall appear, then shall ye also appear with him in glory.

>> JE! UMEFUFULIWA PAMOJA NA KRISTO?

>> JE! UNAYATAFUTA YALIYO JUU, KRISTO ALIKO AMEKETI MKONO WA KUUME WA MUNGU? AU UNAYATAFUTA YA HAPA CHINI YANAYOHARIBIKA?! JE! NI ZIPI HAJA KUU ZA MOYO WAKO?! JE! NI ZA MBINGUNI AU ZA HAPA?! NI ZA UFALME WA MUNGU AU ZA KWAKO?! VIPAUMBELE VYAKO NI VIPI? PENGINE KUNA MAMBO YA KUTUBIA HAPA NAPO!

>> JE! UNAYAWAZA, KUYATAFAKARI, NA KUYAFIKIRI YALIYO JUU AU YALIYO KATIKA NCHI? PENGINE KUNA MAMBO YA KUTUBIWA!!

4) JE! UMERIDHIKA NA KILE AMBACHO HAKIMTUKUZI MUNGU NA UFALME WAKE CHA HAPA DUNIANI NA KINACHOHARIBIKA KAMA MSHAHARA MKUBWA, FAIDA KUBWA KWENYE BIASHARA, CHEO KIKUBWA, FEDHA NYINGI, SIFA NA HESHIMA ZA WANADAMU N.K. AMBAVYO VYOTE HUVITUMII KWA AJILI YA YESU?! PENGINE KUNA MAMBO YA KUTUBIA!!

5) Wafilipi 3:12

[12]Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 

Not as though I had already attained, either were already perfect: but I follow after, if that I may apprehend that for which also I am apprehended of Christ Jesus.

>> JE! UNAJIONA KUWA UMEKWISHA KUFIKA AU KUWA MKAMILIFU?! TUBU!

6) Wafilipi 3:13

[13]Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 

Brethren, I count not myself to have apprehended: but this one thing I do, forgetting those things which are behind, and reaching forth unto those things which are before,

>> JE! UNAJIONA UMEKWISHAMALIZA??!! Labda umeshatoa sana, umeshaomba sana, umeshahubiri sana, umeshafundisha sana, umeshasaidia sana, umeshategemeza sana, n.k. UNAJIVUNIA YALIYOPITA??!! UMESHAJIVUNA!!! NI WEWE ULIYAFANYA AU NEEMA YA MUNGU?! TUBU!

7) Ufunuo wa Yohana 2:4-5

[4]Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. 

Nevertheless I have somewhat against thee, because thou hast left thy first love.

[5]Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. 

Remember therefore from whence thou art fallen, and repent, and do the first works; or else I will come unto thee quickly, and will remove thy candlestick out of his place, except thou repent.

>> NENDA KASOME  HABARI ZA MAKANISA SABA YA UFUNUO ( Ufunuo sura ya 1 & 2) HALAFU UJIPIME UKATUBU!! UTAKUTANA NA VITU KAMA HIVI;

Ufunuo wa Yohana 2:16

[16]Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. 

Repent; or else I will come unto thee quickly, and will fight against them with the sword of my mouth.

>> UTAGUNDUA KWAMBA TOBA YA MTAKATIFU INAMRUDISHA KWENYE MAPENZI YA MUNGU SAWASAWA NA NENO LAKE!!

>> WATAKATIFU WANAISHI MAISHA YA TOBA!! 

>> UKISOMA BIBLIA MUNGU ATAKUONYESHA MAENEO MENGI YA KUTUBU MAISHANI MWAKO ILI UWE AMA URUDI KWENYE MAPENZI YAKE YOTE SAWASAWA NA KWELI YAKE YOTE!!

>> NDIPO UTAJIKUTA MARA NYINGI UKIOMBA REHEMA NA NEEMA ZA MUNGU KILA MARA MARA NDIZO MAHITAJI YAKO MAKUU

Waebrania 4:16

[16]Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. 

Let us therefore come boldly unto the throne of grace, that we may obtain mercy, and find grace to help in time of need.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post