TOFAUTI KATI YA TOBA YA MTAKATIFU NA TOBA YA MTENDA DHAMBI



TOFAUTI KATI YA TOBA YA MTAKATIFU NA TOBA YA MTENDA DHAMBI

>> Ipo tofauti kubwa sana kati ya toba ya mtakatifu na toba ya mtenda dhambi kama vile mbingu zilivyo juu kuliko nchi!

1) TOBA YA MTENDA DHAMBI

>> Toba ya mtenda dhambi ni hii:

Marko 1:14-15

[14]Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, 

Now after that John was put in prison, Jesus came into Galilee, preaching the gospel of the kingdom of God,

[15]akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. 

And saying, The time is fulfilled, and the kingdom of God is at hand: repent ye, and believe the gospel.

>> TOBA YA MTENDA DHAMBI INAKUJA BAADA YA KUISIKIA NA KUIAMINI INJILI

>> AKIISIKIA INJILI, AKAHUKUMIWA MOYO KWA DHAMBI YAKE, AKAAMUA KUTUBU DHAMBI ZAKE ILI KUZIACHA MOJA KWA MOJA ( YAANI, AKAAMUA KUACHANA KABISA NA MAISHA YA DHAMBI)

>> AKIAMUA HIVYO KWA KUWEKA IMANI YAKE KWA YESU KRISTO MWOKOZI, NA AKAMPOKEA AWE BWANA NA MWOKOZI WAKE MOYONI NA MAISHANI MWAKE, NDIPO MTENDA DHAMBI HUYU ANASAMEHEWA, NA KUONDOLEWA DHAMBI ZAKE ZOTE! SI KUSAMEHEWA TU PEKE YAKE BALI KUSAMEHEWA NA KUONDOLEWA DHAMBI ZOTE ROHONI, NAFSINI, NA MWILINI MWAKE!! YAANI, ANAOSHWA KABISA UCHAFU NA VINYAGO VYAKE VYOTE!! NA HII HAIISHII HAPO BALI AKIISHAKUOSHWA NA KUSAFISHWA DHAMBI ZOTE, HUPEWA UZIMA WA MILELE!

>> TOBA YA MTENDA DHAMBI NI LAZIMA IELEKEZWE KWA YESU ALIYEKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YAKE, NA ALIYEFANYA UPATANISHO KATI YAKE NA MUNGU KWA DAMU NA MAUTI YAKE! (Rum 5:8-11 & 2 Kor 5:18-21)

1 Wakorintho 15:1-4

[1]Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, 

Moreover, brethren, I declare unto you the gospel which I preached unto you, which also ye have received, and wherein ye stand;

[2]na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. 

By which also ye are saved, if ye keep in memory what I preached unto you, unless ye have believed in vain.

[3]Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; 

For I delivered unto you first of all that which I also received, how that Christ died for our sins according to the scriptures;

[4]na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; 

And that he was buried, and that he rose again the third day according to the scriptures:

>> ALIKUFA NA KUFANYA UPATANISHO WA DHAMBI YA ULIMWENGU , YEYE KAMA MWANAKONDOO WA MUNGU ALIYETOLEWA KAMA SADAKA YA DHAMBI (SIN OFFERING), (Yohana 1:29) ALIMWAGA DAMU YAKE ISIYO NA HATIA KWA AJILI YA WENGI KWA ONDOLEO LA DHAMBI. DAMU YAKE ILIKUWA NI DAMU YA AGANO JIPYA KATI YA MUNGU NA WANADAMU AMBAPO:

1. DAMU PEKEE INAYOKUBALIKA MBELE ZA MUNGU SASA NI DAMU YA YESU ILI KUOSHA DHAMBI ZA KILA AMWAMINIYE

2. KWAMBA MAUTI YA MWANA WA MUNGU YESU ILIKUWA NI MAUTI YA UPATANISHO PIA KWA SABABU YEYE HAKUTENDA DHAMBI NA HAKUSTAHILI KUFA! MAANA IMEANDIKWA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI, NA HIVYO HAIKUWEZEKANA MAUTI IMSHIKE, NA NDIYO MAANA MAUTI IKAMTAPIKA!! NA SASA KILA AMWAMINIYE HAFI TENA BALI AMEPITA KUTOKA MAUTINI NA KUINGIA UZIMANI!! 

Yohana 5:24-27

[24]Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. 

Verily, verily, I say unto you, He that heareth my word, and believeth on him that sent me, hath everlasting life, and shall not come into condemnation; but is passed from death unto life.

[25]Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. 

Verily, verily, I say unto you, The hour is coming, and now is, when the dead shall hear the voice of the Son of God: and they that hear shall live.

[26]Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake. 

For as the Father hath life in himself; so hath he given to the Son to have life in himself;

[27]Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. 

And hath given him authority to execute judgment also, because he is the Son of man.

3.   KWAMBA DAMU YA YESU INAKUOSHA DHAMBI ZAKO NA KISHA ROHO YAKO INAFUFULIWA KUTOKA MAUTINI KWA KUHUISHWA NA KUFANYWA UPYA NA ROHO MTAKATIFU (TITO 3:3-7)

4.   KWA HUKU KUFANYWA HAI MAANA YAKE UNAPEWA MAISHA MAPYA YASIYOHARIBIKA AMA AMA UZIMA WA MILELE!! (2 TIM 1:10)! HAUFI TENA BALI UTATOKA KWENYE MWILI NA KWENDA KUKAA NA BWANA YESU MILELE

5.   MAUTI MAANA YAKE KUTENGWA NA MUNGU MILELE KUANZIA HAPA ULIPO LEO DUNIANI UNAPOTENDA DHAMBI, MPAKA UTAKAPOKUFA KWENYE DHAMBI ZAKO (USIPOOKOKA) NA KUTENGWA NA MUNGU MILELE KWA KUTUPWA JEHANAMU MILELE KWENYE ZIWA LA MOTO AMBAYO HIYO NI MAUTI YA PILI

Ufunuo wa Yohana 20:14-15

[14]Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 

And death and hell were cast into the lake of fire. This is the second death.

[15]Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. 

And whosoever was not found written in the book of life was cast into the lake of fire.

>> TOBA YA MTENDA DHAMBI INAMTOA MAUTINI NA KUMLETA UZIMANI 

>> TOBA YA MTENDA DHAMBI INAMUONDOLEA DHAMBI ZAKE NA KUMUUMBIA MOYO SAFI (MATHAYO 5:8)

- HAPA TUNAONGELEA AGANO JIPYA KATIKA DAMU YA YESU,  YAANI UKOMBOZI NA WOKOVU WA MTENDA DHAMBI KUPITIA IMANI KATIKA DAMU YA YESU ILIYOMWAGIKA MSALABANI 

Mathayo 26:27-28

[27]Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; 

And he took the cup, and gave thanks, and gave it to them, saying, Drink ye all of it;

[28]kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 

For this is my blood of the new testament, which is shed for many for the remission of sins.

>> YESU ALIDHIHIRISHWA ILI AZIONDOE KABISA DHAMBI MOYONI MWAKO, NAFSINI MWAKO, NA MWILINI MWAKO!!

>> UKISEMA HUNA DHAMBI WEWE NI MUONGO, UKISEMA HUKUTENDA DHAMBI WEWE PIA NI MUONGO.

1 Yohana 1:8-10

[8]Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. 

If we say that we have no sin, we deceive ourselves, and the truth is not in us.

[9]Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. 

If we confess our sins, he is faithful and just to forgive us our sins, and to cleanse us from all unrighteousness.

[10]Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu. 

If we say that we have not sinned, we make him a liar, and his word is not in us.

>> ALIYEZIONDOA DHAMBI NI YESU NA HUYU PEKEE NDIYE UNAYEMWUNGAMIA DHAMBI ZAKO NA KUPOKEA MSAMAHA WAKE NA ONDOLEO LA DHAMBI HIZO 

>> NI MUHIMU SANA UELEWE KWAMBA YESU ANAPOKUSAMEHE NA KUZIONDOA DHAMBI HAFANYI HIVYO ILI KILA SIKU UWE UNAISHI NA KUTENDA DHAMBI TENA NA TENA

1 Yohana 3:4-6

[4]Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. 

Whosoever committeth sin transgresseth also the law: for sin is the transgression of the law.

[5]Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. 

And ye know that he was manifested to take away our sins; and in him is no sin.

[6]Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 

Whosoever abideth in him sinneth not: whosoever sinneth hath not seen him, neither known him.

>> SHETANI AMEDANGANYA WENGI KUWA HAIWEZEKANI KUISHI PASIPO KUTENDA DHAMBI 

>> LAKINI NENO LA MUNGU LIMESEMA UKIWA NDANI YA YESU HAUTENDI DHAMBI MAANA NDANI YAKE HAMNA DHAMBI NA WALA HAIKAI DHAMBI

>> KAMA UNATENDA DHAMBI HUJAWAHI KUMUONA YESU, HUJAWAHI KUMJUA YESU, HUJAWAHI KUMTAMBUA YESU, HUJAWAHI KUOKOKA,  NA HUJAWAHI KUWA WA KRISTO, YAANI, HUJAWAHI KUWA MKRISTO!! KWA KUWA MKRISTO NI WA KRISTO NA ANAKAA NDANI YA KRISTO KWA ROHO WA KRISTO ALIYEPEWA ALIPOAMINI!! UNAYETENDA DHAMBI HUJAWAHI KUMWAMINI YESU.

>> TOBA YA MTENDA DHAMBI INAMTOA KWENYE UTAWALA, MAMLAKA, UFALME,  NA NGUVU ZA GIZA ZOTE  NA KUMUINGIZA KWENYE UFALME WA MUNGU NA NGUVU ZAKE!

1 Yohana 3:4-6

[4]Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. 

Whosoever committeth sin transgresseth also the law: for sin is the transgression of the law.

[5]Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. 

And ye know that he was manifested to take away our sins; and in him is no sin.

[6]Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 

Whosoever abideth in him sinneth not: whosoever sinneth hath not seen him, neither known him.

NA TENA;

Wakolosai 1:13-14

[13]Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 

Who hath delivered us from the power of darkness, and hath translated us into the kingdom of his dear Son:

[14]ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; 

In whom we have redemption through his blood, even the forgiveness of sins:

>> TOBA YA MTENDA DHAMBI LAZIMA IPELEKEE KUOKOKA KWAKE MAANA HAKUNA TOBA YA KILA WIKI AU MWEZI MMOJA KILA MWAKA!! HIYO SIYO TOBA BALI NI MBINU NA HILA YA KUENDELEA KUTENDA DHAMBI HUKU UKIONEKANA MSHIKA DINI SANA, AU UNA DINI FULANI, AMA UKO KWENYE DHEHEBU FULANI!! LAKINI DHAMBI UNATENDA NA HUWEZI KAMWE KUSEMA UMEOKOKA AU WEWE NI MTAKATIFU!! AU UNASEMA HAMNA MTAKATIFU!!! Lakini Biblia inafundisha, 

1 Petro 1:15-16

[15]bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 

But as he which hath called you is holy, so be ye holy in all manner of conversation;

[16]kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 

Because it is written, Be ye holy; for I am holy.

>> MUNGU ANATAKA UTAKATIFU UKIWA HAPA DUNIANI 

>> MUNGU ANATAKA UISHI MAISHA MATAKATIFU HAPA DUNIANI

>> KAMA WEWE NI WA MUNGU LAZIMA UWE MTAKATIFU KWA KUWA MUNGU BABA YAKO NI MTAKATIFU 

>> MUNGU ANAKUWA BABA YAKO UKIZALIWA MARA YA PILI (UKITUBU NA KUOKOKA) (YOHANA 3:3-7)

>> MKRISTO NI YULE ALIYEITWA KUISHI MAISHA MATAKATIFU KAMA BABA YAKE WA MBINGUNI ALIVYO MTAKATIFU 

>> TOBA YA MTENDA DHAMBI INAMBADILISHIA HADHI YAKE MBELE ZA MUNGU KUTOKA MUASI MTENDA DHAMBI MPAKA MTAKATIFU MWANA WA MUNGU ANAYEPENDWA UPEO NA ANAYEMTII MUNGU KATIKA MAMBO YOTE!

>> UMEWAHI KUTUBU??!! KAMA BADO UNAWEZA KUTUBU SASA KWA KUFUATISHA MANENO HAYA KWA MOYO WAKO WOTE!!

 

 *"Mungu Baba wa mbinguni nashukuru kwa neno lako! Nimeelewa na kutambua kwamba mimi bado ni mwenye dhambi licha ya kutubu mara nyingi kama nilivyopokea mapokeo tangu utotoni. Bwana Yesu naomba unisamehe dhambi zangu zote na kisha unifanye kuwa kiumbe kipya mwenye moyo mpya safi na mtakatifu.  Karibu Yesu ndani ya moyo wangu sasa, utawale na kuongoza maisha yangu yote. Nimejitoa kwako Yesu milele usiniache nipotee wala kuanguka wala kurudi nyuma mimi na nyumba yangu yote! Asante nakuamini Yesu maana wewe ndiye pekee uliyekufa na kufufuka kwa ajili yangu! Liandike jina langu kwenye kitabu cha uzima. Asante kwa kuniokoa!"* (Itaendelea)


1) TOBA YA MTAKATIFU (loading......)

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post