KUTUBU BILA KUOKOKA NI KUJIDANGANYA ZAIDI



KUTUBU BILA KUOKOKA NI KUJIDANGANYA ZAIDI

>> Unatubu kila siku fulani ya ibada halafu unarudia dhambi zile zile!!

>> Unatubu kila mwezi fulani wa toba kila mwaka halafu unarudia dhambi zile zile!!

>> Toba inayokubalika mbele za Mungu ni ile inayokupelekea wewe KUTOTENDA DHAMBI TENA!! Yaani, kuziacha dhambi zote!!

>> Yesu alimwambia yule mgonjwa aliyemponya alipomkuta hekaluni:

Yohana 5:14

[14]Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi. 

Afterward Jesus findeth him in the temple, and said unto him, Behold, thou art made whole: sin no more, lest a worse thing come unto thee.

>> UKISAMEHEWA DHAMBI ZAKO USITENDE DHAMBI TENA!!

>> UKISAMEHEWA DHAMBI ZAKO NA KUPONYWA USITENDE DHAMBI TENA!

>> KUENDELEA KUTENDA DHAMBI AU KUISHI KWENYE DHAMBI KUNAMAANISHA HAUJATUBU WALA HUJAPATA ONDOLEO LA DHAMBI

>> AGANO JIPYA NI AGANO LA DAMU YA YESU ILIYOMWAGIKA KWA AJILI YA WENGI KWA ONDOLEO LA DHAMBI

Mathayo 26:27-28

[27]Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; 

And he took the cup, and gave thanks, and gave it to them, saying, Drink ye all of it;

[28]kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 

For this is my blood of the new testament, which is shed for many for the remission of sins.

>> TOBA INAYOKUBALIKA LEO CHINI YA AGANO JIPYA NI ILE YENYE KUINYWA DAMU YA YESU!! YAANI, KUKINYWEA KIKOMBE KILE ALICHOKINYWEA YEYE YESU CHA KUTESWA, KUFA, NA KUFUFUKA KWAKE!! MAUTI YAKE ILIKUWA NI KWA AJILI YA UPATANISHO!! DAMU YAKE NI DAMU YA UPATANISHO IOSHAYO DHAMBI ZOTE!

>> UNAPOMWAMINI YESU NA KUTUBU DAMU YA YESU INAINGIA NDANI YA ROHO YAKO NA KUKUSAFISHA DHAMBI ZAKO KWA NENO LAKE ULILOLIAMINI, KWA NJIA YA ROHO MTAKATIFU! HAPO ROHO YAKO INAKUWA IMEINYWA DAMU YA YESU, NA PIA UNAKUWA UMEULA MWILI WAKE YESU, YAANI, NENO LA MUNGU! MWILI WA YESU NI MWILI WA NENO AMBAYE NI MUNGU 

Yohana 1:1,14

[1]Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 

In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.

[14]Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. 

And the Word was made flesh, and dwelt among us, (and we beheld his glory, the glory as of the only begotten of the Father,) full of grace and truth.

>> ROHO YAKO INAULA MWILI WA YESU NA KUINYWA DAMU YAKE PALE UNAPOAMINI NA KULIPOKEA NENO LAKE! 

KWA NINI MWILI NA DAMU YA YESU?

NI KWA SABABU YESU NDIYE MPATANISHI PEKEE, MWANADAMU ALIYEKUWA NA SIFA ZA KUFANYA UPATANISHO HUO!!

1 Timotheo 2:5

[5]Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 

For there is one God, and one mediator between God and men, the man Christ Jesus;

>> Imeandikwa mshahara wa dhambi ni mauti  lakini wanadamu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Rum 3:10-18)

>> Sasa ni nani atakayemwokoa mwanadamu??!! Lazima huyu awe na sifa kama hizi ili aweze kufanya upatanisho kama kuhani:

Waebrania 7:22-27

[22]basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. 

By so much was Jesus made a surety of a better testament.

[23]Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae; 

And they truly were many priests, because they were not suffered to continue by reason of death:

[24]bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. 

But this man, because he continueth ever, hath an unchangeable priesthood.

[25]Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. 

Wherefore he is able also to save them to the uttermost that come unto God by him, seeing he ever liveth to make intercession for them.

[26]Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu; 

For such an high priest became us, who is holy, harmless, undefiled, separate from sinners, and made higher than the heavens;

[27]ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake. 

Who needeth not daily, as those high priests, to offer up sacrifice, first for his own sins, and then for the people's: for this he did once, when he offered up himself.

>> YESU NI KUHANI MILELE MAANA AMESHINDA KIFO KWA KUFUFUKA KUTOKA KWA WAFU

>> AMESHINDA KIFO KWA KUWA HAKUTENDA DHAMBI

>> HAKUTENDA DHAMBI KWA KUWA ALIZALIWA KWA MBEGU ISIYOHARIBIKA; YAANI NENO LA MUNGU (YOHANA 1:14 & LUKA 1:35)

>> YESU AMETAJWA KUWA KUHANI MKUU MILELE MFANO WA MELKIZEDEKI

>> YESU NI KUHANI MKUU MTAKATIFU, ASIYEKUWA NA UOVU, ASIYEKUWA NA WAA LOLOTE, ALIYETENGWA NA WAKOSAJI, NA ALIYEPAA JUU KULIKO MBINGU NA KUKETI MKONO WA KUUME WA BABA MBINGUNI!!

>> HUYU HAWEZI NA HASTAHILI KUFA, NA ANAPOUTOA UHAI WAKE KWA KUMWAGA DAMU YAKE TAKATIFU NI KWA KUSUDI LA KULIPA DENI LA DHAMBI ZETU NA KUICHUKUA ADHABU YETU WANADAMU!!

>> TULISTAHILI KUFA SISI LAKINI AKAFA YEYE MAHALA PETU, ILI SISI TUISHI

>> HUKUMU YA MUNGU TULIYOISTAHILI SISI ALIIBEBA NA KUISTAHIMILI YEYE BADALA YETU NA MAHALI PETU

>> ALIUWAWA KWA AJILI YA DHAMBI ZETU, ILI ATULETE KWA MUNGU WATAKATIFU NA WAKAMILIFU TUSIO NA HATIA YOYOTE, SISI TUNAOMWAMINI YEYE!

>> UPATANISHO MAANA YAKE YESU AMETUEPUSHA NA GHADHABU YA MUNGU SISI KWA KUIKUBALI NA KUISTAHIMILI YEYE ILI SISI TUKIMTAZAMA YEYE NA KUMWAMINI TUISHI MILELE

Warumi 5:6,8,10-11

[6]Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. 

For when we were yet without strength, in due time Christ died for the ungodly.

[8]Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. 

But God commendeth his love toward us, in that, while we were yet sinners, Christ died for us.

[10]Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. 

For if, when we were enemies, we were reconciled to God by the death of his Son, much more, being reconciled, we shall be saved by his life.

[11]Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho. 

And not only so, but we also joy in God through our Lord Jesus Christ, by whom we have now received the atonement.

>> NA TENA

2 Wakorintho 5:18-20

[18]Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; 

And all things are of God, who hath reconciled us to himself by Jesus Christ, and hath given to us the ministry of reconciliation;

[19]yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. 

To wit, that God was in Christ, reconciling the world unto himself, not imputing their trespasses unto them; and hath committed unto us the word of reconciliation.

[20]Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. 

Now then we are ambassadors for Christ, as though God did beseech you by us: we pray you in Christ's stead, be ye reconciled to God.

>> ALICHOFANYA YESU NI UPATANISHO KATI YA MUNGU MTAKATIFU NA WANADAMU WAOVU

>> UPATANISHO UMEKAMILIKA LAKINI HAUNA FAIDA MPAKA UPOKELEWE NA MTENDA DHAMBI

>> UPATANISHO UNAPOKELEWA KWA KUTAMBUA KWAMBA NI YESU PEKEE ALIYEKWISHAKUFANYA HUO UPATANISHO NA LAZIMA UJE KWAKE KUUPOKEA KWA KUZIUNGAMA DHAMBI ZAKO KWA KUMAANISHA KUZIACHA!!

>> UPATANISHO MAANA YAKE HAMNA KIKWAZO TENA KATI YAKO NA MUNGU MTAKATIFU 

Mithali 28:13

[13]Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; 

Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. 

He that covereth his sins shall not prosper: but whoso confesseth and forsaketh them shall have mercy.

>> TOBA YA AGANO JIPYA NI TOBA YA AGANO

1) YESU AMEFANYA UPATANISHO NAYE ANATAKA WEWE UUPOKEE HUO UPATANISHO 

2) UPATANISHO ALIOUKAMILISHA UNAPATIKANA KWA KUFANYA AGANO NAYE

3) AGANO JIPYA NI WEWE KUKUBALI KUOSHWA DHAMBI ZAKO KWA DAMU YA YESU KWA KUZITUBIA NA KUZIUNGAMA NA KUWA TAYARI KUZIACHA KABISA

4) YESU AKIONA MOYONI MWAKO UMEAMINI HIVYO ANAKUSAMEHE NA KUKUONDOLEA DHAMBI HIZO, (KUKUOSHA) NA KISHA ANAKUFANYA UPYA ROHO YAKO KWA KUKUHUISHA, AU KUKUTIA UZIMA, AU UHAI ULIOMO NDANI YAKE MWENYEWE KWA ROHO WAKE MTAKATIFU ILI USITENDE DHAMBI TENA 

5) YAANI, ANAKUFUFUA ROHO YAKO KUTOKA MAUTINI NA KUKUPA MAISHA MAPYA YASIYOHARIBIKA YA UTAKATIFU NA YA MILELE, AMBAYO YANAKUFANYA UWE KIUMBE KIPYA

6) UNAKUWA UMEZALIWA UPYA MARA YA PILI ROHO YAKO NA KUPEWA MAISHA YA MILELE! UZIMA WA MILELE MAANA YAKE ROHO YAKO HAIFI TENA MILELE KWA KUWA DHAMBI HAIKUTAWALI TENA MILELE

7) AGANO LA DAMU YA YESU HALIISHII HAPO BALI ANAKUPA PIA ROHO WAKE MTAKATIFU AKAE NDANI YAKO AMBAYE NI MUHURI WA MUNGU KWAMBA WEWE NI WAKE!!

Waefeso 1:13

[13]Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu. 

In whom ye also trusted, after that ye heard the word of truth, the gospel of your salvation: in whom also after that ye believed, ye were sealed with that holy Spirit of promise,

8) Agano Jipya la damu ya Yesu linataka kwamba ukitubu dhambi zako umpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wako binafsi, akuongoze, akufundishe, akuonye, akuwezeshe, akuonyeshe, akujulishe, na mengi yote mengineyo!! Wewe sasa si mali yako mwenyewe bali ni mali ya Yesu na unaishi kwa ajili yake maisha mapya ya utakatifu,  unyoofu, haki, na kweli!! (2 Kor 5:15)

Warumi 14:7-8

[7]Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. 

For none of us liveth to himself, and no man dieth to himself.

[8]Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. 

For whether we live, we live unto the Lord; and whether we die, we die unto the Lord: whether we live therefore, or die, we are the Lord's.

>> HUWEZI KUTUBU UKAOKOKA HALAFU UKAENDELEA KUISHI UNAVYOTAKA WEWE BALI ANAVYOTAKA YESU MAANA WEWE NI WAKE SASA AMEKUNUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE! 

>> TOBA ISIYOYALETA MAISHA YAKO KWA YESU NI DHIHAKA KWA MUNGU 

>> TOBA ISIYOKUWEKA HURU MBALI NA DHAMBI NI UOVU MBELE ZA MUNGU! YESU AMETUWEKA HURU MBALI NA DHAMBI, NA DHAMBI HAITUTAWALI TENA!!!

Warumi 6:22

[22]Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. 

But now being made free from sin, and become servants to God, ye have your fruit unto holiness, and the end everlasting life.

Warumi 6:14

[14]Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema. 

For sin shall not have dominion over you: for ye are not under the law, but under grace.

>> DHAMBI HAIMTAWALI MTU ALIYEMWAMINI YESU NA KUTUBU

>> DHAMBI HAIMTAWALI ALIYE WA YESU, MAANA NEEMA YAKE INATOSHA NA INAMWEZESHA!!

>> USIJIDANGANYE NA TOBA, UNATAKIWA KUZAA MATUNDA YAPASAYO TOBA!!

Luka 3:8-9

[8]Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. 

Bring forth therefore fruits worthy of repentance, and begin not to say within yourselves, We have Abraham to our father: for I say unto you, That God is able of these stones to raise up children unto Abraham.

[9]Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. 

And now also the axe is laid unto the root of the trees: every tree therefore which bringeth not forth good fruit is hewn down, and cast into the fire.

>> KUZAA MATUNDA YAPASAYO TOBA NI KUISHI MAISHA MAPYA YENYE BADILIKO, MAISHA YA UTAKATIFU YANAYOKUBALIKA NA KUMPENDEZA MUNGU NA WANADAMU!!

>> TOBA ISIYOZAA MATUNDA NDIYO TOBA ZA WALE WASIOOKOKA, NA WANAOTUBU PASIPO KUACHA DHAMBI 

>> HUWEZI KUTUBU PASIPO KUIAMINI INJILI YA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU 

Marko 1:14-15

[14]Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, 

Now after that John was put in prison, Jesus came into Galilee, preaching the gospel of the kingdom of God,

[15]akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. 

And saying, The time is fulfilled, and the kingdom of God is at hand: repent ye, and believe the gospel.

>> TOBA SAHIHI NI PALE UNAPOTUBU KWA KUIAMINI INJILI, NA KUMPOKEA YESU MOYONI MWAKO KAKA BWANA NA MWOKOZI WAKO BINAFSI 

>> USIPOTEZE MUDA KUTUBU PASIPO KUOKOKA, HUWEZI KUSAMEHEWA WALA KUACHA DHAMBI! MWAMINI YESU, AMEMALIZA YOTE MSALABANI!!

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post