MWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI



MWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI 

Yohana 4:23-24

[23]Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 

But the hour cometh, and now is, when the true worshippers shall worship the Father in spirit and in truth: for the Father seeketh such to worship him.

[24]Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. 

God is a Spirit: and they that worship him must worship him in spirit and in truth.

>> Kumwabudu Mungu katika roho na kweli kunawezekana tu kwa Roho Mtakatifu! Lazima uwe umejazwa Roho, unamtii Roho, na unaongozwa na Roho huyo Mtakatifu!

>> Kuabudu katika roho maana yake roho yako iliyozaliwa mara ya pili ( Yohana 3:6-7) ikiwa imeunganika na Roho wa Kristo (1Kor 6:17) NA KUWA MMOJA NA YESU (becoming one with Jesus!) kama vile Yesu alivyokuwa mmoja na Baba, inamtolea Mungu ibada ya kumpendeza katika roho kwa Roho Mtakatifu 

John 10:30

[30]I and my Father are one. 

Mimi na Baba tu umoja.

>> mimi na Baba tu mmoja na siyo umoja! UMOJA SIYO SAWA NA KUWA MMOJA! Kule kuwa mmoja na Yesu ni kuwa mmoja na Neno lake, kama Yeye mwenyewe alivyokuwa, na pia ni kuwa mmoja Baba Aliye Roho (Yohana 4:24). Mapenzi ya Mungu ni WEWE MWANA WA MUNGU UWE SAWA NA YESU MWANA WA MUNGU VILE VILE KAMA YEYE ALIVYOKUWA, NA KUENENDA, NA KUTENDA!! (1 Yohana 2:6 & Efeso 4:13, 15)

>> Muunganiko huu na Yesu katika roho ndio msingi wa kumuabudu Mungu katika roho na kweli!! Lazima kwanza;

1) UZALIWE MARA YA PILI ROHO YAKO (YOH 3:3-7).HAPA UNAPEWA MOYO MPYA NA ROHO MPYA NA KUWA KIUMBE KIPYA ( EZEKIEL 36:25-26 & 2 KOR 5:17)

2) KISHA UJAZWE ROHO MTAKATIFU NA KUUNGANIKA NA BWANA YESU KATIKA ROHO. YAANI, UNAMPOKEA ROHO NA NGUVU ZAKE KWENYE roho YAKO NA KUGEUZWA KUWA MTU MWINGINE ( EZEKIEL 35:27 & 1 SAMUEL 10 6)

1 Corinthians 6:17

[17]But whoever is united with the Lord is one with him in spirit.

17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. 

1 Wakorintho 6:17

3) HUYU ROHO ALIYEUNGANIKA NAWE KATIKA ROHO ANAANZA KUKUONGOZA WEWE roho YAKO, NA KUZIELEKEZA HATUA ZAKO KWA NENO LAKE, KWA NGUVU ZAKE ILI USITENDE DHAMBI WALA USIMILIKIWE NA UOVU (ZABURI 119:133, MATENDO 1:8, WARUMI 8:14)

>> ROHO MTAKATIFU ANAKUONGOZA SASA KUYAISHI MAISHA MAPYA YA NENO LA MUNGU! UNAISHI SASA KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU (MATHAYO 4:4) KWA NGUVU ZA MUNGU. NA HAYO NDO MAISHA MATAKATIFU!!

>> Roho Mtakatifu ndiye anayekukirimia, kutoka kwenye Neno lake, kupitia imani yako kwa Yesu,  roho ya sifa, roho ya shukrani,  roho ya kicho au kumcha Bwana, roho ya heshima, roho ya kumpa Mungu utukufu, roho ya unyenyekevu kwa Mungu,  roho ya uaminifu, roho ya kujidhili, roho ya kujikana, ............na kila roho ya Neno! Maana maneno ya Mungu yote ni roho na pia ni uzima (Yohana 6:63)  Ni ile roho ya neno na nguvu zake ndiyo inayokuongeza na kukufanya ukue kiroho na uongezeke nguvu rohoni!! Ndivyo unavyozidi kumjua Mungu wewe mwenyewe kibinafsi maana ni roho yako inazidi kuunganika na Neno lake katika roho kadiri unavyozidi kuliamini neno na kulitiii!!! ( Yaani, unazidi kujaa Roho kwa neno lake!!)

>> Kumuabudu Mungu ni kumpenda zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumhimidi zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumpendeza zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumsifu zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumshukuru zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumheshimu zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumtukuza zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumfurahisha yeye zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kujinyenyekeza mbele zake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kujidhili mbele zake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kujitoa kwake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kuwepo kwa ajili yake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumwinua zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kujishusha mbele zake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumtaka na kumhitaji yeye zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumshangilia yeye zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kujimimina kwake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kujiachilia kwake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kusujudu mbele zake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumsifia yeye zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kupendana naye zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumtaka na kumchagua yeye kuliko vyote, kuliko wote, kuliko pote, kuliko zote, kuliko kote, n.k. zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumtii yeye zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kujitakasa ndani yake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumsihi yeye zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumuadhimisha yeye zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumkumbuka yeye zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kujifunza uweponi mwake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa,  kutamani sana, kutaka, na kuhitaji kumwelewa, kumjua, na kumfahamu zaidi na zaidi uweponi mwake kila iitwapo sasa,  kujitoa na kujiweka wakfu kwake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumtegemea na kumtumaini yeye uweponi mwake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kupondeka na kumcha na kutubu mbele zake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, kumkumbatia, kumshika, na kumng'ang'ania katika roho kwa kutotaka kamwe kuupungukia uwepo wake na nguvu zake zaidi na zaidi kila iitwapo sasa, KUUFANYA UWEPO WAKE NA NGUVU ZAKE KUWA NDIYO NYUMBANI KWAKO SIKUZOTE, WAKATI WOTE, MAHALI POTE, KATIKA MAZINGIRA YOTE NA HALI ZOTE ZAIDI NA ZAIDI KILA IITWAPO SASA, NA KUZIDI SANA NA KUONGEZEKA KATIKA HAYO KWA roho YAKO NAFSI YAKO, MANENO YAKO, ( YAANI, MOYO KWA MOYO AU ROHO KWA roho!!) NA MATENDO YAKO ZAIDI NA ZAIDI KILA IITWAPO SASA MAISHA YOTE YA MWILI WAKO!!

>> NENO LA MSINGI NA MUHIMU SANA NI "KILA IITWAPO SASA"!! (WORSHIP IS A NOW AND ALWAYS EXPERIENCE!) KUMUABUDU NI KUFANYA HAYO YOTE SASA KILA ULIPO NA KATIKA KILA ULIFANYALO! MUNGU ANAABUDIWA SASA NA PALE ULIPO KATIKA LILE ULIFANYALO LINALOMPENDEZA YEYE NA LENYE SIFA AU VIGEZO HIVYO HAPO JUU, KWA NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU KUPITIA IMANI YAKO ILIYO HAI KWA YESU KRISTO!!!

>> HAYO YOTE WAWEZA KUYAFANYA UKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU! TRUE WORSHIP IS ABOUT DOING GOD'S WILL IN THE SPIRIT AND POWER OF THE WORD WHICH YOU HAVE BELIEVED!! KUABUDU KWA KWELI KUNAHUSIKA NA KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU KWA ROHO NA NGUVU ZA NENO ULILOLIAMINI!!! LAZIMA HII IANZIE KATIKA ROHO KWA KUPITIA USHIRIKA WAKO NA ROHO MTAKATIFU!!! KWELI NI NENO LA MUNGU!!! IBADA KATIKA ROHO NA KWELI HUWA HAIKOMI NA WALA HAINA MUDA BALI NI YA WAKATI WOTE!! NI YA SASA!! SIYO SIKU FULANI AU MAHALI FULANI, HII NI YA WATU WASIOMJUA MUNGU WA BWANA WETU YESU KRISTO, BABA WA UTUKUFU! HALELUYA!!

>> UHUSIANO WA WEWE NA YESU HAUPO KAMA HAUWEZI KUMUABUDU KATIKA ROHO NA KWELI

>> WOKOVU UNAHITAJI WEWE UMJUE YESU KIBINAFSI KATIKA ROHO. UKIMJUA YESU UTAIJUA KWELI. UKIIJUA KWELI ITAKUWEKA HURU. UKIWA HURU UTAWAWEKA WENGI HURU!!

Yohana 8:31-32,36

[31]Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 

Then said Jesus to those Jews which believed on him, If ye continue in my word, then are ye my disciples indeed;

[32]tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. 

And ye shall know the truth, and the truth shall make you free.

[36]Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. 

If the Son therefore shall make you free, ye shall be free indeed.


NA TENA:


Luka 4:18

[18]Roho wa Bwana yu juu yangu, 

Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. 

Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, 

Na vipofu kupata kuona tena, 

Kuwaacha huru waliosetwa, 

The Spirit of the Lord is upon me, because he hath anointed me to preach the gospel to the poor; he hath sent me to heal the brokenhearted, to preach deliverance to the captives, and recovering of sight to the blind, to set at liberty them that are bruised,

>> UNAPOMUABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI SIKUZOTE UNAKUWA UWEPONI MWAKE NA KATIKA NGUVU ZAKE! UNAZIDI KUMJUA, UNAZIDI KUTAKASIKA, UNAZIDI KUFUNGUKA MACHO NA MASIKIO YA KIROHO, UNAZIDI KUPEWA SIRI ZA UFALME WA MBINGUNI,  UNAZIDI KUPOKEA FUNGUO ZA UFALME, UNAZIDI KUONGEZEKA NGUVU ROHONI, UNAZIDI KUKUA KATIKA HEKIMA, KIMO, UFAHAMU,  KICHO, MAARIFA, SHAURI, UWEZA NA MAFUNUO! YAANI, ROHO ATAZIDI KUMFUNUA YESU KWAKO, NA PIA ATAZIDI KUKUFUNGUA AKILI UELEWE MAANDIKO, ATAZIDI KUKUVIKA UWEZA NA MAMLAKA; NA KUZIDI KUKUMIMINIA UTAJIRI, HESHIMA, NGUVU, UTUKUFU, NA BARAKA!

>> KUMUABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI KUNAZIDI KUKUFANANISHA NA YESU MAANA SIKUZOTE UNAUTAZAMA USO WAKE KWENYE NENO LAKE KATIKA ROHO MTAKATIFU 

>> KUKUA KOTE, KUONGEZEKA KOTE, NI KUZIDI KUWA KAMA YESU KATIKA MAENEO YOTE!!!

>> MWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI

>> HAUJAANZA KUMUABUDU MUNGU ALIYE HAI KAMA BADO UAMINIFU NA UTAMBULISHO WAKO NI KWA DHEHEBU FULANI AU DINI FULANI!! HATA WEWE UNAYEJIVUNIA DHEHEBU LA MATENDO 2:1-4, UNATAKIWA UJIVUNIE YESU, UJITAMBULISHE KUWA NI WA YESU, KWAMBA UNAMWAKILISHA YESU, NA UNAMFUATA YESU, ALIYEKUOSHA KWA DAMU YAKE UKAOKOKA!!

>> DINI YA YESU NI KUOKOKA NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU!

>> DHEHEBU LA YESU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU (KANISA TAKATIFU AMBALO NI MWILI WA KRISTO)

1 Wakorintho 3:16-17

[16]Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 

Know ye not that ye are the temple of God, and that the Spirit of God dwelleth in you?

[17]Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. 

If any man defile the temple of God, him shall God destroy; for the temple of God is holy, which temple ye are.

>> ULIYEOKOKA NA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU MUNGU MTAKATIFU ANAKAA NDANI YAKO 

>> SHIKA DINI YAKO YA UTAKATIFU KWA KUISHI MAISHA MATAKATIFU NDANI YA YESU MAANA WEWE NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU 

2 Wakorintho 6:14-18

[14]Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 

Be ye not unequally yoked together with unbelievers: for what fellowship hath righteousness with unrighteousness? and what communion hath light with darkness?

[15]Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?

Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 

And what concord hath Christ with Belial? or what part hath he that believeth with an infidel?

[16]Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 

And what agreement hath the temple of God with idols? for ye are the temple of the living God; as God hath said, I will dwell in them, and walk in them; and I will be their God, and they shall be my people.

[17]Kwa hiyo, 

Tokeni kati yao, 

Mkatengwe nao, asema Bwana, 

Msiguse kitu kilicho kichafu, 

Nami nitawakaribisha. 

Wherefore come out from among them, and be ye separate, saith the Lord, and touch not the unclean thing; and I will receive you,

[18]Nitakuwa Baba kwenu, 

Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, 

asema Bwana Mwenyezi. 

And will be a Father unto you, and ye shall be my sons and daughters, saith the Lord Almighty.


1 Wakorintho 6:17-20

[17]Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. 

But he that is joined unto the Lord is one spirit.

[18]Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 

Flee fornication. Every sin that a man doeth is without the body; but he that committeth fornication sinneth against his own body.

[19]Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 

What? know ye not that your body is the temple of the Holy Ghost which is in you, which ye have of God, and ye are not your own?

[20]maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu

For ye are bought with a price: therefore glorify God in your body, and in your spirit, which are God's.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post