MKRISTO WA KWELI NI YUPI?
☆☆ 1 Wakorintho 6:19
[19]Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
What? know ye not that your body is the temple of the Holy Ghost which is in you, which ye have of God, and ye are not your own?
>> MKRISTO NI YEYE ALIYEOSHWA KWA DAMU YA YESU NA ROHO MTAKATIFU ANAKAA NDANI YAKE (MATENDO 2:38)
☆☆ 1 Wakorintho 3:16
[16]Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
Know ye not that ye are the temple of God, and that the Spirit of God dwelleth in you?
>> MKRISTO NI YULE ALIYEOKOKA NA SASA MWILI WAKE NI HEKALU TAKATIFU MAANA ROHO WA MUNGU MTAKATIFU ANAKAA NDANI YAKE
☆☆ 1 WAKORINTHO 3:17
[17]Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
If any man defile the temple of God, him shall God destroy; for the temple of God is holy, which temple ye are.
>> MKRISTO NI HEKALU TAKATIFU LA MUNGU, NA LAZIMA ALITUNZE HEKALU KWA KUDUMU KATIKA UTAKATIFU PASIPO KUTENDA DHAMBI. UKILIHARIBU HEKALU KWA KUTENDA DHAMBI NA MUNGU ATAKUHARIBU!
☆☆ UKRISTO UNAANZIA HAPA:
Matendo ya Mitume 2:38
[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Then Peter said unto them, Repent, and be baptized every one of you in the name of Jesus Christ for the remission of sins, and ye shall receive the gift of the Holy Ghost.
☆☆ Warumi 1:7
[7]kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
To all that be in Rome, beloved of God, called to be saints: Grace to you and peace from God our Father, and the Lord Jesus Christ.
>> KANISA NI WALE WALIOITWA KUWA WATAKATIFU KATIKA KRISTO YESU, KAMA KANISA LA RUMI (THE ROME CHURCH WAS HOLY)
☆☆ 1 Wakorintho 1:2
[2]kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.
Unto the church of God which is at Corinth, to them that are sanctified in Christ Jesus, called to be saints, with all that in every place call upon the name of Jesus Christ our Lord, both theirs and ours:
>> KANISA NI WAKRISTO WALE WALIOTAKASWA KATIKA KRISTO YESU, NA KUITWA WAWE WATAKATIFU HAPA DUNIANI!! USIYE MTAKATIFU WEWE SI MKRISTO
☆☆ 2 Wakorintho 13:12-13
[12]Salimianeni kwa busu takatifu.
Greet one another with an holy kiss.
[13]Watakatifu wote wawasalimu.
All the saints salute you.
>> PAULO ALIHUBIRI INJILI NA WOTE WALIOIAMINI, NA KUIPOKEA, NA KUTUBU, WALIKUWA NI WATAKATIFU WALIOOSHWA DHAMBI ZAO KWA DAMU YA YESU
>> MKRISTO NI MTAKATIFU NA UKRISTO NI UTAKATIFU KWA NEEMA YA KRISTO KWA NJIA YA ROHO WAKE MTAKATIFU AKAAYE NDANI
☆☆ 2 Wakorintho 1:1
[1]Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu; kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walioko katika nchi yote ya Akaya.
Paul, an apostle of Jesus Christ by the will of God, and Timothy our brother, unto the church of God which is at Corinth, with all the saints which are in all Achaia:
>> KANISA LA KORINTHO LILIKUWA TAKATIFU, NA AKAYA YOTE ILIJAA MAKANISA YA WATAKATIFU!! UTAKATIFU HAUPATIKANI BAADA YA KUFA BALI KWA KUOKOKA LEO!!
☆☆ Wagalatia 4:6-7
[6]Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
And because ye are sons, God hath sent forth the Spirit of his Son into your hearts, crying, Abba, Father.
[7]Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.
Wherefore thou art no more a servant, but a son; and if a son, then an heir of God through Christ.
>> MKRISTO NI MWANA WA MUNGU
☆☆ Warumi 8:9
[9]Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
But ye are not in the flesh, but in the Spirit, if so be that the Spirit of God dwell in you. Now if any man have not the Spirit of Christ, he is none of his.
>> KAMA HUNA ROHO WA KRISTO WEWE SI WA KRISTO! YAANI, SI MKRISTO
>> UKITIMIZA MATENDO 2:37-38 UTAKUWA MKRISTO!
☆☆ Warumi 8:14
[14]Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
For as many as are led by the Spirit of God, they are the sons of God.
>> MKRISTO NI YULE ALIYEZALIWA MARA YA PILI NA ANA ROHO WA MUNGU AKAAYE NDANI YAKE, ALIYEMPOKEA ALIPOOKOKA!
>> HUYU ROHO ALIYEKUWA NDANI YA KRISTO NDIYE ROHO WA UKRISTO, MWENYE NGUVU ZA UTAKATIFU AMBAO NDIO UKRISTO
☆☆ Waefeso 1:4
[4]kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
According as he hath chosen us in him before the foundation of the world, that we should be holy and without blame before him in love:
>> MUNGU ALITUCHAGUA WAKRISTO TANGU KABLA HATUJALIWA ILI TUJE KUWA WATAKATIFU, WATU WASIO NA HATIA MBELE ZAKE KATIKA PENDO! WATAKATIFU HAWANA HATIA/DHAMBI MBELE ZA MUNGU KATIKA ENEO LOLOTE!
☆☆ Waefeso 1:1
[1]Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko [Efeso] wanaomwamini Kristo Yesu.
Paul, an apostle of Jesus Christ by the will of God, to the saints which are at Ephesus, and to the faithful in Christ Jesus:
>> KANISA LA EFESO LILIKUWA NI WATAKATIFU WANAOMWAMINI YESU
>> KANISA LA KIBIBLIA NI LA WATAKATIFU WANAOMWAMINI YESU! UNAMWAMINI YESU? UMEOKOKA?
☆☆ Waefeso 1:1
[1]Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko [Efeso] wanaomwamini Kristo Yesu.
Paul, an apostle of Jesus Christ by the will of God, to the saints which are at Ephesus, and to the faithful in Christ Jesus:
>> KANISA LA EFESO LILIKUWA NI WATAKATIFU WANAOMWAMINI YESU
>> KANISA LA KIBIBLIA NI LA WATAKATIFU WANAOMWAMINI YESU! UNAMWAMINI YESU?
☆☆ Philippians 1:1
[1]Paul and Timotheus, the servants of Jesus Christ, to all the saints in Christ Jesus which are at Philippi, with the bishops and deacons:
Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo Yesu, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na maaskofu na mashemasi.
>> WATAKATIFU WA FILIPI WALIKUWA NDANI YA YESU
>> KANISA LA YESU NI TAKATIFU NA LAZIMA LIWE NDANI YAKE!!
>> WAKRISTO NI WATAKATIFU WALIOMWAMINI YESU
☆☆ Wakolosai 1:2
[2]kwa ndugu watakatifu, waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
To the saints and faithful brethren in Christ which are at Colosse: Grace be unto you, and peace, from God our Father and the Lord Jesus Christ.
>> WAKRISTO WA/ KANISA LA KOLOSAI WALIKUWA NI WAAMINIFU NA WATAKATIFU WALIOKUWA NDANI YA YESU
>> WEWE NI MTAKATIFU NA MWAMINIFU NA UMO NDANI YA YESU?
☆☆1 Wathesalonike 3:13
[13]apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.
To the end he may stablish your hearts unblameable in holiness before God, even our Father, at the coming of our Lord Jesus Christ with all his saints.
>> WATAKATIFU WA THESALONIKE WALIOMBEWA KWAMBA BWANA AWAFANYE IMARA MIOYO YAO IWE BILA LAWAMA KATIKA UTAKATIFU MBELE ZA MUNGU!! MKRISTO HUWA ANATAKA NA KUTAFUTA SANA UIMARA WA MOYO PASIPO LAWAMA KATIKA UTAKATIFU
☆☆ Wathesalonike 2:13
[13]Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
But we are bound to give thanks alway to God for you, brethren beloved of the Lord, because God hath from the beginning chosen you to salvation through sanctification of the Spirit and belief of the truth:
>> KANISA NI MKRISTO ALIYECHAGULIWA TANGU MWANZO AUPATE WOKOVU, KATIKA KUTAKASWA NA ROHO NA KUIAMINI KWELI! UMEOKOKA?
☆☆ Waebrania 12:14
[14]Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Follow peace with all men, and holiness, without which no man shall see the Lord:
>> HUTAMWONA MUNGU KAMWE BAADA YA MAISHA HAYA KAMA UKIFA PASIPO KUOKOKA NA KUFANYWA UPYA KUWA MTAKATIFU KWA ROHO MTAKATIFU NA NENO LAKE KWA NJIA YA KUMWAMINI YESU
☆☆ 1 Petro 1:15-16
[15]bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
But as he which hath called you is holy, so be ye holy in all manner of conversation;
[16]kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Because it is written, Be ye holy; for I am holy.
>> MUNGU AMEAGIZA UWE MTAKATIFU KWA KUWA YEYE NI MTAKATIFU
>> AMUA KUOKOKA
☆☆ 1 WAKORINTHO 3:17
[17]Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
If any man defile the temple of God, him shall God destroy; for the temple of God is holy, which temple ye are.
>> MKRISTO NI HEKALU TAKATIFU LA MUNGU, NA LAZIMA ALITUNZE HEKALU KWA KUDUMU KATIKA UTAKATIFU PASIPO KUTENDA DHAMBI. UKILIHARIBU HEKALU KWA KUTENDA DHAMBI NA MUNGU ATAKUHARIBU!
☆☆ USIJIDANGANYE, MKRISTO WA KIBIBLIA NI MTAKATIFU NA UKRISTO NI UTAKATIFU
☆☆ 4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
1 Yohana 3:4
5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
1 Yohana 3:5
>> YESU ALIKUJA KUZIONDOA DHAMBI, NA NDANI YAKE HAMNA DHAMBI
☆☆ 1 Yohana 3:6
[6]Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
Whosoever abideth in him sinneth not: whosoever sinneth hath not seen him, neither known him.
>> HUWEZI KUTENDA DHAMBI UKIOKOKA NA KUWA NDANI YA YESU
>> MKRISTO NI MTAKATIFU ALIYE NDANI YA YESU
☆☆ 1 Yohana 3:8
[8]atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
He that committeth sin is of the devil; for the devil sinneth from the beginning. For this purpose the Son of God was manifested, that he might destroy the works of the devil.
>> USIJIITE MKRISTO UKIWA UNATENDA DHAMBI, WEWE NI WA IBILISI NA SI WA KRISTO! OKOKA UOSHWE DHAMBI ZAKO
☆☆ HUYU NDIYE MKRISTO! HATENDI NA HAWEZI KUTENDA DHAMBI!
1 Yohana 3:9
[9]Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
Whosoever is born of God doth not commit sin; for his seed remaineth in him: and he cannot sin, because he is born of God.