UNATAKA AU UNATAFUTA NINI ZAIDI YA YESU, NENO LA MUNGU??!!



UNATAKA AU UNATAFUTA NINI ZAIDI YA YESU, NENO LA MUNGU??!! 

>> HAKUNA KITU KILICHO MUHIMU DUNIANI KULIKO NENO LA MUNGU!!

>> HAKUNA KITU KILICHO CHA LAZIMA KAMA NENO LA MUNGU

>> HAKUNA UAMUZI BORA NA WA BUSARA KULIKO KULIAMINI NENO LA MUNGU

Waebrania 1:1-2

[1]Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 

God, who at sundry times and in divers manners spake in time past unto the fathers by the prophets,

[2]mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 

Hath in these last days spoken unto us by his Son, whom he hath appointed heir of all things, by whom also he made the worlds;

>> KATIKA SIKU ZA MWISHO MUNGU AMESEMA NA ULIMWENGU WOTE ( BY HIS SON!!) KWA NJIA YA MWANAWE YESU!!!

>> YESU NI NENO LA MUNGU ALIYE HAI KWA ULIMWENGU WOTE LEO!!!

>> KILA UNACHOTAKIWA KUWA, UNACHOTAKIWA KUWA NACHO, UNACHOTAKIWA KUKIFANYA, UNACHOTAKIWA KUKISEMA, UNACHOTAKIWA KUKITAFUTA, UNACHOTAKIWA KUKIFIKIRI/ KUKIWAZA/KUKITAFAKARI KIMO NDANI YA YESU, NA YESU AMEKIELEZA!! 

>> KUMWAMINI YESU NDIKO KUMWAMINI MUNGU!!

>> HUWEZI KUMWAMINI YESU HALAFU UKAENDELEA KUTENDA DHAMBI!!

>> HUWEZI KUMWAMINI YESU HALAFU HUWEZI KUSEMA " MIMI NIMEOKOKA NA NI MTAKATIFU!!"

>> UKIMWAMINI YESU UMEAMINI NENO LA UZIMA/MAISHA

>> MAISHA YA MUNGU ANAYOTAKA UYAISHI YAMO NDANI YA NENO LAKE LILILO HAI LEO!! (YESU)

>> KUOKOKA SIYO KURITHI DINI FULANI AU DHEHEBU KWA WAZAZI, BALI NI KUZALIWA MARA YA PILI ROHO YAKO!! (YAANI, KUUMBWA UPYA ROHO YAKO NA KUWEKWA NDANI YA YESU UKIWA KIUMBE KIPYA!) KUOKOKA NI UUMBAJI MPYA WA ROHO YAKO, UNAOPELEKEA NAFSI MPYA NDANI YAKO KADIRI UNAVYOENDELEA KUFANYWA UPYA NA KUTAKASWA NA NENO LA KRISTO AMBALO NDILO MAISHA YAKO!!

>> MAISHA NI KRISTO,  KUISHI NI KRISTO!! KUWA NJE YA KRISTO NI KUKAA MAUTINI!!! (ABIDING IN DEATH)

Waebrania 4:12-13

[12]Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 

For the word of God is quick, and powerful, and sharper than any twoedged sword, piercing even to the dividing asunder of soul and spirit, and of the joints and marrow, and is a discerner of the thoughts and intents of the heart.

[13]Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. 

Neither is there any creature that is not manifest in his sight: but all things are naked and opened unto the eyes of him with whom we have to do.

>> NI MAMBO GANI SABA MUHIMU YAMEFUNULIWA KWENDE HILI ANDIKO KUHUSU NENO LA MUNGU??!! ( YAANI, NENO LILIVYO NA LINACHOFANYA NDANI YAKO UKILIAMINI NA KULIWEKA MOYONI MWAKO?)

>> HUWEZI KUMPENDA MUNGU KAMA HUMPENDI YESU, HUWEZI KUJA KWA MUNGU PASIPO KUPITIA KWA YESU, HUWEZI KUMWONA MUNGU PASIPO KUWA NDANI YA YESU!! DINI YA YESU NI UPENDO WA AGAPE!! DINI YA YESU NI UTAKATIFU!! UTAKATIFU WA PENDO LAKE NDIO UTUKUFU WAKE!! HEKIMA MBELE ZA MUNGU NI KUSIKIA NA KULITENDA NENO LAKE!! NA HUO NDIO UTAKATIFU NA UPENDO WA MUNGU!!

Yohana 14:21,23-24

[21]Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 

He that hath my commandments, and keepeth them, he it is that loveth me: and he that loveth me shall be loved of my Father, and I will love him, and will manifest myself to him.

[23]Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 

Jesus answered and said unto him, If a man love me, he will keep my words: and my Father will love him, and we will come unto him, and make our abode with him.

[24]Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka. 

He that loveth me not keepeth not my sayings: and the word which ye hear is not mine, but the Father's which sent me.

>> YESU, NA SIYO DINI AU DHEHEBU LOLOTE, NDIYE ATAKAYEKUFIKISHA KWENYE UTUKUFU WA MUNGU JUU MBINGUNI 

Waebrania 7:25

[25]Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. 

Wherefore he is able also to save them to the uttermost that come unto God by him, seeing he ever liveth to make intercession for them.

IMEANDIKWA:

Mathayo 7:24-27

[24]Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 

Therefore whosoever heareth these sayings of mine, and doeth them, I will liken him unto a wise man, which built his house upon a rock:

[25]mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 

And the rain descended, and the floods came, and the winds blew, and beat upon that house; and it fell not: for it was founded upon a rock.

[26]Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 

And every one that heareth these sayings of mine, and doeth them not, shall be likened unto a foolish man, which built his house upon the sand:

[27]mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa. 

And the rain descended, and the floods came, and the winds blew, and beat upon that house; and it fell: and great was the fall of it.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post