HAKUNA REHEMA WALA MSAMAHA!!

 


HAKUNA REHEMA WALA MSAMAHA!! 

Mithali 28:13

[13]Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; 

Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. 

He that covereth his sins shall not prosper: but whoso confesseth and forsaketh them shall have mercy.

>> KUUNGAMA KILA WIKI NA KURUDI KWENYE DHAMBI ZILE ZILE KUNAMAANISHA HAUJAZIACHA DHAMBI HIZO, HAUNA MPANGO WA KUZIACHA, AMA HAUMAANISHI (NOT SERIOUS) KUZIACHA!!

>> KWA MAANA YESU HAKUJA KUFUNIKA TU DHAMBI, BALI ALIKUJA KUZIONDOA DHAMBI KUTOKA MOYONI NA MAISHANI MWAKO MOJA KWA MOJA!!

1 Yohana 3:5

[5]Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. 

And ye know that he was manifested to take away our sins; and in him is no sin.

>> YESU ALIDHIHIRISHWA ILI AZIONDOE KABISA DHAMBI ZAKO KUTOKA MOYONI MWAKO, NA KUKUPA WEWE UZIMA WA MILELE AMA MAISHA YA MILELE YASIYOHARIBIKA!!

>> YESU ALIFANYA UPATANISHO KWA KULIPA DENI LA DHAMBI ZETU!! YEYE ALIIKUBALI NA KUISTAHIMILI ADHABU YA DHAMBI ZETU ILI ISITUPATE SISI WOTE TUNAOMWAMINI YEYE!! DAMU YA YESU ILIYOMWAGIKA NI DAMU YA UPATANISHO!! NI DAMU INAYOMWAGIKA KWA AJILI YA WENGI KWA ONDOLEO LA DHAMBI!!

Mathayo 26:27-28

[27]Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; 

And he took the cup, and gave thanks, and gave it to them, saying, Drink ye all of it;

[28]kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 

For this is my blood of the new testament, which is shed for many for the remission of sins.

>> YESU ALIUTOA UHAI WAKE KUPITIA DAMU YAKE ILIYOMWAGIKA MSALABANI, KAMA MAANDIKO YANENAVYO KWAMBA UHAI WA MWILI UMO KWENYE DAMU (Kum 12:23, LAW 17:14)


Yohana 10:11,15,17-18

[11]Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 

I am the good shepherd: the good shepherd giveth his life for the sheep.

[15]kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 

As the Father knoweth me, even so know I the Father: and I lay down my life for the sheep.

[17]Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. 

Therefore doth my Father love me, because I lay down my life, that I might take it again.

[18]Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu. 

No man taketh it from me, but I lay it down of myself. I have power to lay it down, and I have power to take it again. This commandment have I received of my Father.


>> YESU ALIUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YAKO MTENDA DHAMBI, ILI USIFE WEWE NA DHAMBI ZAKO, BALI UISHI MILELE!! IMEANDIKWA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI, LAKINI BADALA YA KUFA WEWE YESU ALIKUBALI KUFA MAHALA PAKO!! KWA SABABU YEYE HAKUTENDA DHAMBI!! (Isa 53), BALI ALITESWA NA KUUWAWA KWA AJILI YA DHAMBI ZAKO ILI GHADHABU YA MUNGU ITIMIZWE KIUKAMILIFU!! NA HAKIKA GHADHABU YA MUNGU ILITIMIZWA KIUKAMILIFU JUU YA MWILI WA YESU ALIYEICHUKUA DHAMBI YA MWANADAMU JUU YA MWILI WAKE PALE JUU MSALABANI!!

1) ULITENDA DHAMBI WEWE 

2) UKAFA KIROHO WEWE

3) KIFO CHA KIMWILI KIKAKUPATA WEWE

4) UNASTAHILI MAUTI YA PILI AMBAYO NI HII:

Ufunuo wa Yohana 20:14-15

[14]Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 

And death and hell were cast into the lake of fire. This is the second death.

[15]Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. 

And whosoever was not found written in the book of life was cast into the lake of fire.

>> MAUTI YA PILI NI WEWE ROHO YAKO KUTUPWA JEHANAMU MBALI NA MUNGU MILELE KWENYE ADHABU YA MILELE!!

>> YESU ALIUTOA UHAI WAKE ILI WEWE USIFE BALI UISHI MILELE!! UZIMA WA MILELE NI MAISHA YAKE YESU NDANI YAKO WEWE ULIYEMWAMINI, ANAYOKUPA BAADA YA KUKUSAMEHE DHAMBI ZAKO!!

>> HAKUNA MSAMAHA WOWOTE UTAKAOUPATA KWA YESU KAMA AKIONA HUNA NIA, AU HAUKUSUDII, AMA HAUNA MPANGO WA KUZIUNGAMA DHAMBI ZAKO NA KUZIACHA!! ANDIKO LA MITHALI 28:13 LINAMAANISHA:


[REHEMA/ MSAMAHA WA DHAMBI= KUZIUNGAMA DHAMBI + KUZIACHA]

>> KUUNGAMA AU KUTUBIA DHAMBI KILA WIKI AU KILA MWEZI FULANI KILA MWAKA HALAFU UNARUDI KWENYE DHAMBI NI KUMDHIHAKI MUNGU!! UNAPOKUJA KUTUBU JE! UMEMAANISHA KUACHA MAISHA YA DHAMBI??!! AU UNAKUJA KUMDHIHAKI MUNGU NA KUWADANGANYA WANAOKUONA UMEKWENDA KUUNGAMA??!! JE! UTAISHI KWENYE UDANGANYIFU HUO MPAKA UJIKUTE JEHANAMU??!!

>> UPATANISHO UMEKAMILIKA HAPA DUNIANI, NA MTENDA DHAMBI UNAWEZA KUPATANA NA MUNGU HAPA DUNIANI

>> ANDIKO HILI LINAKUELEKEZA WEWE MTENDA DHAMBI UPOKEE UPATANISHO HUU KWA KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO HAPA DUNIANI, MAANA HAKUNA UTAKASO MWINGINE BAADA YA KUFA!! TOHARA NI MOJA LEO UKIOKOKA HAPA DUNIANI!! UNATAHIRIWA MOYO AU ROHO YAKO NA KUWA KIUMBE KIPYA!!! PATANISHWA KWA KUOKOKA LEO;


2 Wakorintho 5:18-21

[18]Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; 

And all things are of God, who hath reconciled us to himself by Jesus Christ, and hath given to us the ministry of reconciliation;

[19]yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. 

To wit, that God was in Christ, reconciling the world unto himself, not imputing their trespasses unto them; and hath committed unto us the word of reconciliation.

[20]Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. 

Now then we are ambassadors for Christ, as though God did beseech you by us: we pray you in Christ's stead, be ye reconciled to God.

[21]Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye. 

For he hath made him to be sin for us, who knew no sin; that we might be made the righteousness of God in him.

>> MPATANISHI NI MMOJA, YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU 

>> ANAPATANISHA LEO UKIWA HAI NA SIYO BAADA YA KUFA

>> KWA MAANA BAADA YA KUFA INAFUATA HUKUMU NA HAMNA TENA TOHARA WALA TOHARANI WALA ADHABU ZA KABURI BALI KUNA HUKUMU YA MWISHO NA JEHANAMU ITAKAYOFUNULIWA WAKATI HUO!!


Waebrania 9:27

[27]Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; 

And as it is appointed unto men once to die, but after this the judgment:

>> UKIFA NA DHAMBI ZAKO UMEPOTEA MILELE!!

>> DAMU YA YESU BADO INANENA REHEMA ZA YESU NA MSAMAHA KAMA UTAMWAMINI NA KUOKOKA!!

>> HUWEZI KUOKOKA USIPOZIUNGAMA DHAMBI ZAKO NA KUZIACHA!!

>> LAZIMA UFANYE MAAMUZI YA KUACHA DHAMBI KWA KUKIMBILIA KWA YESU MAANA WEWE MWENYEWE PEKE YAKO HUWEZI KWA NAMNA YOYOTE!! MPATANISHI NI MMOJA TU, YESU!! MWOKOZI NI MMOJA TU, YESU!! TOHARA NI MOJA TU, YA YESU! TOHARANI NI PAMOJA TU, MSALABANI! AMBAPO YESU AMESHAPITA HAPO KWA AJILI YAKO!! HIVYO HAUHITAJI KUPITA HAPO!! DAMU YA AGANO IMESHAMWAGIKA MSALABANI AMBAYO ITAKUOSHA KABISA UCHAFU WAKO WOTE NA DHAMBI ZAKO ZOTE, UKIMWAMINI YESU!!

KUMWAMINI YESU NI KUPI??!!

Yohana 3:16
[16]Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
For God so loved the world, that he gave his only begotten Son, that whosoever believeth in him should not perish, but have everlasting life.


>> KUMWAMINI YESU KUNA MAANA YA:
1) KUMKUBALI, KUMPOKEA MOYONI MWAKO, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA NA UONGOZI WAKE( ROHO NA NENO LAKE), ILI AKUONGOZE MAISHA YAKO SIKU ZAKO ZOTE ZA KUWA KWENYE MWILI WAKO KATIKA "NJIA YA UTAKATIFU " ALIYOINENA NABII ISAYA:

Isaya 35:8-10
[8]Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.
And an highway shall be there, and a way, and it shall be called The way of holiness; the unclean shall not pass over it; but it shall be for those: the wayfaring men, though fools, shall not err therein.
[9]Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.
No lion shall be there, nor any ravenous beast shall go up thereon, it shall not be found there; but the redeemed shall walk there:
[10]Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.
And the ransomed of the LORD shall return, and come to Zion with songs and everlasting joy upon their heads: they shall obtain joy and gladness, and sorrow and sighing shall flee away.
>> YAANI, NI KUWA NA UHAKIKA KWAMBA UNAKWENDA KWENYE NJIA INAYOMPENDEZA MUNGU, ANAYOIKUBALI MUNGU, ALIYOICHAGUA MUNGU, ANAYOITAKA MUNGU, INAYOMFURAHISHA MUNGU, AMBAYO UNAPITA HAPA DUNIANI UKISAFIRI KUELEKEA MBINGUNI,  NA UKIWA KAMA MWAKILISHI WA YESU KWA ULIMWENGU ULIOPOTEA, UKIWA SALAMA NA HURU MBALI NA NGUVU ZOTE ZA GIZA.
2) KUAMINI NI KUWEKA TUMAINI LAKO KWAKE, KUMTEGEMEA NA KUMTUMAINIA YEYE KATIKA YOTE YALIYOANDIKWA KWENYE NENO LA MUNGU, UNAYOYATARAJIA KWAMBA LAZIMA YATIMIZWE KWAKO NA KWENYE MAISHA YA WENGINE VILE VILE KAMA ALIVYOSEMA NA/AMA KUAHIDI YEYE MWENYEWE, ASIYEWEZA KUSEMA UONGO NA ANAYEWEZA KUFANYA NA KUTENDA MAMBO YOTE!!
3) KUMWAMINI NI KUTAMBUA NA KUKUBALI KWAMBA HAKUNA MPATANISHI MWINGINE, HAKUNA KIONGOZI MWINGINE, HAKUNA MWALIMU MWINGINE,  HAKUNA MFARIJI MWINGINE, HAKUNA MLINZI MWINGINE, HAKUNA RAFIKI MWINGINE,  HAKUNA MWAMINIFU MWINGINE,  HAKUNA MPONYAJI MWINGINE, HAKUNA NJIA NYINGINE, HAKUNA UZIMA MWINGINE, HAKUNA MAISHA MENGINE, HAKUNA MEMA MENGINE, HAKUNA WEMA MWINGINE, HAKUNA MTAKATIFU MWINGINE, HAKUNA WA KUTUMAINIWA MWINGINE, HAKUNA WA KUABUDIWA MWINGINE, HAKUNA WA KUHESHIMIWA MWINGINE, HAKUNA BWANA WA MABWANA MWINGINE, HAKUNA MFALME WA WAFALME MWINGINE,  HAKUNA ALIYEKUFA KWA AJILI YA DHAMBI ZA ULIMWENGU MWINGINE, HAKUNA ALIYEFUFUKA KUTOKA KWA WAFU MWINGINE, HAKUNA ALIYESHINDA DHAMBI NA MAUTI KWA AJILI YETU MWINGINE, HAKUNA ANAYEOKOA MWINGINE, HAKUNA MPATANISHI MWINGINE, HAKUNA UPENDO MWINGINE, HAKUNA HAKI KWINGINE, HAKUNA AMANI KWINGINE, HAKUNA FURAHA KWINGINE, HAKUNA USHINDI JUU YA DHAMBI, MAUTI NA SHETANI KWA MWINGINE, HAKUNA BARAKA KWINGINE, HAKUNA UZIMA WA MILELE KWINGINE, HAKUNA UTUKUFU WA MILELE KWINGINE, HAKUNA NEEMA KWINGINE, HAKUNA REHEMA KWINGINE, HAKUNA TOBA NA MSAMAHA WA DHAMBI KWINGINE, HAKUNA HEKIMA, MAARIFA, NA UFAHAMU KWINGINE, HAKUNA KICHO, USHAURI, NA NGUVU KWINGINE,  HAKUNA MAFUNUO YA KWELI KWINGINE,  HAKUNA TUMAINI LA UTUKUFU KWINGINE, HAKUNA MAISHA MAPYA KWINGINE, HAKUNA UKOMBOZI KWINGINE, HAKUNA UPONYAJI NA AFYA YA KIUNGU KWINGINE, HAKUNA ISHARA, AJABU, NA MIUJIZA YA KWELI KWINGINE,  HAKUNA WA KUTHAMINIWA NA KUENZIWA MWINGINE, HAKUNA MTAKATIFU NA ALIYETUKUKA MWINGINE,  HAKUNA ANAYEJUA YOTE, ANAYEWEZA YOTE, NA ALIYEPO MAHALI POTE MWINGINE, HAKUNA MWENYE MIPANGO YA MEMA, NA YA KUTENDA MEMA KWAKO MWINGINE, HAKUNA MWENYE NGUVU MWINGINE, HAKUNA ALIYEMSHINDA SHETANI NA UFALME WAKE WOTE MWINGINE, HAKUNA MWINGINE ALIYEMNYANG'ANYA SHETANI FUNGUO ZA MAUTI NA KUZIMU, HAKUNA MWINGINE ALIYEFANYA UPATANISHO,  HAKUNA MWAMBA MWINGINE WA UTUKUFU,  HAKUNA ROHO MWINGINE ANAYEHUISHA, HAKUNA MTUKUFU KATIKA UTAKATIFU MWINGINE, HAKUNA MSAADA KWINGINE, HAKUNA KIMBILIO JINGINE, HAKUNA TUMAINI JINGINE, HAKUNA MSAADA KWA MWINGINE, [ ISIPOKUWA KWA YESU/ KAMA YESU/ISIPOKUWA YESU/KAMA KWA YESU/ILA YESU/.......YESU!!!]

4) KUAMINI NI KUUNGANIKA NA KUWA MMOJA NA YESU KATIKA ROHO, NA HIVYO KUISHI NA KUENENDA VILE VILE KAMA YEYE ALIVYOENENDA KWENYE MWILI, UKIYAFANYA MAPENZI YAKE YOTE ALIYOYAFANYA YEYE MWENYEWE,  NA YOTE ALIYOYAFUNUA KWENYE NENO LAKE, KWA ROHO YULE YULE NA NGUVU ZAKE ZILE ZILE, KWA UTUKUFU WA MUNGU!!

5) UKIMWAMINI ANAKUFUNDISHA, ANAKUELEKEZA, ANAKUONGOZA, ANAKUHUISHA, ANAKUTIA NGUVU, ANAKUFANYA IMARA,  ANAKUINUA, ANAKUWEZESHA, ANAKULINDA, ANAKUTETEA, ANAKUPIGANIA, ANAKUTANGULIA, ANAKUFARIJI, ANAKUJENGA, ANAKUTIA MOYO, ANAKUTUKUZA, ANAKUVUMILIA, ANACHUKULIANA NAWE, ANAKUREHEMU, ANAKUSAMEHE, ANAKUTENDEA MEMA, ANAKUWA NA MIPANGO YA MEMA KUKUHUSU WEWE NA SIYO MIPANGO YA MABAYA, ANAKUHEKIMISHA, ANAKUFAHAMISHA, ANAKUJULISHA, ANAKUFUMBUA MACHO UONE YASIYOONEKANA,  ANAKUFUNGUA MASIKIO UMSIKIE YEYE ANENAPO NAWE, ANAKUWEZESHA KUFANYA ASIYOWEZA KUYAFANYA MWANADAMU,  ANAKUSHIRIKISHA TABIA YAKE YA UUNGU, N.K. N.K.




Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post