UKIPEWA NEEMA FULANI USIJIVUNE WALA KUJIINUA BALI ZIDI KUNYENYEKEA NA KUJIDHILI!!

 


UKIPEWA NEEMA FULANI USIJIVUNE WALA KUJIINUA BALI ZIDI KUNYENYEKEA NA KUJIDHILI!!


36 Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.
Matendo ya Mitume 9:36

37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
Matendo ya Mitume 9:37

38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu.
Matendo ya Mitume 9:38

39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.
Matendo ya Mitume 9:39

40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.
Matendo ya Mitume 9:40

41 Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai.
Matendo ya Mitume 9:41
>> wale watakatifu wa Yafa walituma watu kwa Petro aje kwao kwa sababu walijua neema aliyopewa Petro!!
>> Yaani, walijua jinsi Mungu anavyomtumia Petro kwa namna nyingi ikiwemo kwa karama ya matendo ya miujiza!!
>> siyo kwamba Petro alikuwa ni wa kiroho kuliko wao au mtakatifu kuliko wao!!
>> siyo kwamba Petro alijua mambo mengi kuliko wao
>> wao wenyewe walikuwa ni watakatifu wanaomwamini Yesu
>> tena walikuwa ni watakatifu waombaji  wasiokubali jibu la hapana wakati wanajua jibu sahihi ni ndiyo!!
>> kuyajua mapenzi ya Mungu kupitia neno lake ni kujua jibu la swali ama ufumbuzi wa tatizo!!
>> walijua, kwa ushuhuda wa Roho Mtakatifu ndani yao, kuwa mauti inataka kuwadhulumu kanisa mpendwa wao Tabitha (Dorkasi) kabla ya wakati!!
>> wakasema hapana shetani!!! Huyu haondoki kwa kuwa bado tunamhitaji!!! Unaweza na wewe kuikatalia shida, kuukatalia umaskini, kuukatalia ugonjwa, kuukatalia uhitaji, kukataa chochote ambacho si mapenzi ya Mungu kwako, kwa mkeo/ mumeo, kwa wanao, kwa kanisa, kwa kusanyiko lako, kwa wazazi, kwa kazi ya mikono yako, kwa mchungaji na viongozi wako, kwa washirika wako, kwa taifa lako, n.k. Kataa kisha chukua hatua ya imani inayostahili kama walivyofanya watakatifu  hawa na wajane wa Yafa!!
>> wakatuma watu kwa Petro aje aombe na Dorkasi mpendwa wao afufuke!!! Petro alikuja na Mungu, akiiona imani yao, alimfufua Dorkasi na kumrudisha kwao!!
>> wajane na watakatifu hawa walikata rufaa!! Katia rufaa ukimwi wako au wake, au wa nduguyo, au mshirika mwenzio, katia rufaa tatizo hilo, tatizo lile, usikubali, kataa, goma, mkatalie shetani kwa kwenda mbele za Mungu kwa imani timilifu, ukiwa na hoja zenye nguvu, na Bwana wetu Yesu anasema,
Mathayo 9:29
[29]Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate.
Then touched he their eyes, saying, According to your faith be it unto you.
>> KWA KADIRI YA IMANI YAKO UPATE!!

Mathayo 8:13
[13]Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile.
And Jesus said unto the centurion, Go thy way; and as thou hast believed, so be it done unto thee. And his servant was healed in the selfsame hour.
>> ITAKUWA KWAKO KAMA ULIVYOAMINI!!
>> Kwa nini walituma watu kwa Petro aje?!

9 tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
Wagalatia 2:9
>> WALIIJUA NEEMA ALIYOPEWA PETRO!!
>> HAWAKUJUA KINGINE CHOCHOTE ISIPOKUWA NEEMA YA MUNGU ILIYOKUWA PAMOJA NA PETRO!!
>> MAANA WALIJUA PETRO ASINGEWEZA KUFANYA LOLOTE PASIPO NEEMA HIYO
>> NA HATA PETRO MWENYEWE ALILIJUA HILO, NDIYO MAANA SIKU ILE PETRO NA YOHANA WALIPOMFANYA YULE KIWETE ATEMBEE NA KURUKARUKA, KISHA WATU WAKAWA WANAWATAZAMA WAO NA KUWASHANGAA, PETRO ALISEMA;

6 Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
Matendo ya Mitume 3:6

7 Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.
Matendo ya Mitume 3:7

8 Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.
Matendo ya Mitume 3:8

9 Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu.
Matendo ya Mitume 3:9

10 Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.
Matendo ya Mitume 3:10

11 Basi alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana.
Matendo ya Mitume 3:11

12 Hata Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi?
Matendo ya Mitume 3:12

13 Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.
Matendo ya Mitume 3:13

>> MST 12  " .......MBONA MNATUKAZIA MACHO SISI KANA KWAMBA TUMEMFANYA HUYU AENDE KWA NGUVU ZETU AU UTAUWA WETU?????!!!!!"
>> SI KWA UWEZO WAKO WALA NGUVU ZAKO, BALI NI KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE!!! NA HIYO NDIYO NEEMA YA MUNGU NDANI YAKO!!
>> ISHARA, MAAJABU, NA MIUJIZA HAITENDEKI KWA SABABU YA UTAUWA WAKO AU UTAKATIFU WAKO, NA KAMA UNAWAZA HIVI TAYARI UMEJIVUNA, TUBU!!
>> UKIJIVUNA UTAJIONA BORA KULIKO WALE WASIO NA NEEMA ULIYOPEWA!! UTAJIONA BORA NA MTAKATIFU ZAIDI  KULIKO WASIOFUFUA WAFU, WASIOPAMBANUA ROHO, WASIOTAFSIRI LUGHA, N.K.
>> UNAJIVUNA KWA NINI KANA KWAMBA HUKUPOKEA?????!!!!!
6 Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.
1 Wakorintho 4:6

7 Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?
1 Wakorintho 4:7
>> KUTOJUA NA KUTOHESHIMU NEEMA WALIZOPEWA WATAKATIFU WENGINE  KUMESABABISHA ROHO MTAKATIFU ASHINDWE KUFANYA KAZI KWENYE MWILI WA KRISTO
>> LAKINI PIA KUMESABABISHA MABISHANO, SHUKU MBAYA, KUTOAMINIANA, KUTOPATANA, KUTOFUNGUKA MIOYONI KWA AJILI YA WATAKATIFU WENZETU, KUWAZIANA VIBAYA, KUHISIANA VIBAYA, NA MIGAWANYIKO ISIYO  NA SABABU, PAMOJA NA KUKOSEKANA KWA USHIRIKA WA WATAKATIFU!!
>> CHANZO KIKUU NI KIBURI NA WATU WASIOITII KWELI, WALIOJIVU NA, WANAOJIONA NI WATAKATIFU KULIKO WENGINE,  WANAODUMU KWENYE KULALAMIKIANA, KUNUNG'UNIKIANA, KUKOSOANA, KUHUKUMIANA, NA KULAUMIANA!!! HUU WOTE NI UOVU DHIDI YA ROHO MTAKATIFU ANAYEHUZUNISHWA NA HAYA YOTE!! WATU NI WEPESI KUSEMA NA KUNYOOSHA VIDOLE LAKINI SI WEPESI KUCHUKUA MIZIGO YA WENGINE, KUOMBEA, NA KUMWAMINI MUNGU KWA AJILI YA WATEULE WENGINE!! UKIAMINI, SI  TATIZO  LINATOWEKA??!! MBONA BADO UNASHIKILIA BANGO TATIZO AMBALO KAMA UNGELIOMBA KWA IMANI KUHUSU HILO, LINGEKUWA LIMEKWISHA KUONDOKA NA KWENDA KUTUPWA BAHARINI????!!!!!
>> UNAJIVUNA KWA SABABU YA VIPAWA ULIVYOPEWA KWA NEEMA??!! SIKILIZA:

10 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.
1 Petro 4:10

11 Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
1 Petro 4:11
NA TENA:

5 Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
1 Petro 5:5
>> JIHADHARI KABLA MUNGU HAJAGEUKA NA KUWA MPINZANI WAKO!!! MUNGU ANAWAPINGA WENYE KIBURI, TUBU!!

Isaya 63:10
[10]Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.
But they rebelled, and vexed his holy Spirit: therefore he was turned to be their enemy, and he fought against them.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post