USIHUKUMU BALI REJEZA

 


USIHUKUMU BALI REJEZA

DO NOT DRAW CONCLUSIONS!!/ USITOE HUKUMU, BALI HUBIRI, FUNDISHA, KEMEA, KARIPIA, SHAURI, ONYA, NA ELEKEZA, KWA UVUMILIVU WOTE!!

>> HAYO YOTE YANAKUWA NA NGUVU KUBWA SANA YA MUNGU KAMA MSINGI WAKE NI MAOMBI, MACHOZI, UPENDO, NA HURUMA YA KRISTO NDANI YAKO

>> KAMA HUNA HAYO NDANI YAKO HIYO ITAONEKANA KWENYE MISISITIZO YAKO, MISIMAMO YAKO, NA MITIZAMO YAKO YENYE KUWAFUNGIA WATU MLANGO WA MBINGUNI!!

>> WAKATI UNAHUBIRI AU KUFUNDISHA,  "HUINGII MBINGUNI!","HAWATAINGIA MBINGUNI!", " HUWEZI KUINGIA MBINGUNI ", N.K. UJUE MWENYE MBINGU ANASEMA:

1)2 Petro 3:9

[9]Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. 

The Lord is not slack concerning his promise, as some men count slackness; but is longsuffering to us-ward, not willing that any should perish, but that all should come to repentance.

>> HAPENDI MTU YEYOTE APOTEE, AWE MCHAWI, MBISHI, MKAIDI, MZINZI, ANAINGIA KANISANI NA KAPTURA, ANAINGIA KANISANI AMELEWA, MUUAJI, ANA KAHABA, ANA WAKE SABA, MBAKAJI, MLEVI WA MADAWA YA KULEVYA, FISADI, NA MTENDA DHAMBI YEYOTE MUOVU SANAAAAA UNAYEMUONA HIVYO!! HUYO  MUNGU HAPENDI APOTEE BALI ANATAKA NA HUYO AFIKILIE TOBA!!

>> ANAFIKIAJE TOBA PASIPO KUHUBIRIWA, KUFUNDISHWA, KWA HURUMA NA UPENDO, PAMOJA NA KUVUMILIWA SANA NA KUCHUKULIANA NAYE SANA??!! JE! KUNA MWISHO WA KUOMBEA WATU WA AINA HII???!!! KAMA UNAWAKATIA TAMAA HAWA ETI KWA KIGEZO KUWA HAWABADILIKI AU HAWASIKII WEWE NDIWE UMECHOKA KUMFUATA YESU AMBAYE NDIYE UPENDO WA MUNGU!! UMEWEKWA KUWALETA WATU KWA YESU NA SIYO KUWAAMBIA HUINGII MBINGUNI!! UNAJUAJE KAMA HAWATATUBU MILELE? JE! MUNGU AMEKUAMBIA KUWA AMEWAKATAA? KAMA MUNGU AMESEMA NAWE KUWA AMEWAKATAA LABDA UNGEKUWA NA HOJA! LAKINI MUNGU AMESEMA HAPENDI MTU AWAYE YOTE APOTEE!! UNADHANI MISISITIZO YAKO YA KIMWILI NDIYO ROHO MTAKATIFU??!!

2) Yakobo 4:11-12

[11]Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu. 

Speak not evil one of another, brethren. He that speaketh evil of his brother, and judgeth his brother, speaketh evil of the law, and judgeth the law: but if thou judge the law, thou art not a doer of the law, but a judge.

[12]Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine? 

There is one lawgiver, who is able to save and to destroy: who art thou that judgest another?

>> WEWE SIYO MUNGU WA KUAMUA NANI AINGIE MBINGUNI NANI ASIINGIE!! WAJIBU WAKO NI KULIA NA KUOMBOLEZA ILI WENGI IWEZEKANAVYO WAINGIE!! MLANGO UKO WAZI SIKUZOTE!! SASA MBONA UNASEMA HAWATAINGIA??!! MLANGO NANI KAUFUNGA??!! YESU NDIYE MLANGO WA KONDOO!! YESU AMEACHA KUSAMEHE???!!! ROHO MTAKATIFU HAYUPO???!!!! MBONA UNASEMA HAWATAINGIA MBINGUNI??!! WEWE NDO TATIZO!! UPENDO WA MUNGU HAUMO NDANI YAKO BALI CHUKI NA TABIA ZA KIMWILI!! KUCHUKIA UOVU SIYO KUCHUKIA WAOVU!! NENO LA MUNGU SIYO LAKO, MBINGU SIYO YAKO, HAO WATU WAOVU SIYO WAKO, HAUKUWAUMBA WEWE, WALA HAUTAWAHUKUMU WEWE, HIVYO USIJIFANYE HAKIMU LEO!! HUO NI UOVU UNAOITWA KIBURI!!

YAANI, MTU AKITOFAUTIANA NA WEWE HAINGII MBINGUNI!! MUNGU MWENYEWE HAYUKO HIVYO, WEWE UMEITOA WAPI HIYO? TUMEOKOKA LAKINI KABLA YA KUOKOKA TULIKUWA HATUMTAKI MUNGU, NA KAMA MUNGU ANGEKUWA KAMA WEWE DIKU ZILE HALAFU AKASEMA HAMUINGII MBINGUNI TUNGEKUWA WAPI LEO??!! UMESAHAU ULIKOTOKA??!! 

3) Yakobo 5:19-20

[19]Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; 

Brethren, if any of you do err from the truth, and one convert him;

[20]jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi. 

Let him know, that he which converteth the sinner from the error of his way shall save a soul from death, and shall hide a multitude of sins.

>> HUYU MTU HAPA AMEPOTELEA MBALI NA KWELI, SIYO KARIBU!!

>> ANAONGELEA " NDUGU" YAANI, ALIYEOKOKA KUIACHA KWELI NA KWENDA MBALI DHAMBINI

>> ANASEMA AKIWEPO MTU WA KUMREJEZA!!! ( TO RESTORE HIM/HER)......! JE! UNA MOYO WA KUREJEZA? AU UTAMWAMBIA UMEACHA KWELI JIANDAE NA JEHANAMU!!!🙇🏻‍♂️UPENDO NA HURUMA YA KRISTO NDIYO MOYO WA KUREJEZA!! SIYO KUHUKUMU KWAMBA YAANI, HUYU BASI TENA! AMEACHA WOKOVU??!! SHAURI YAKE NA SHETANI WAKE!! UOVU NDIO UNAONGEAGA HIVI!! UNAWEZA KUTUBU NA KUBADILIKA, AU UNAWEZA KUENDELEA HIVYO ILA SIKU MOJA UTAKUMBUKA ROHO  ALISEMA NAWE UKIWA UMECHELEWA!!

>> WANGAPI WALIOACHA WOKOVU, WALIORUDI NYUMA, WALIOPOTELEA KWENYE IMANI POTOFU, WALIOACHA KUJA KANISANI KWA KUKWAZWA NA MAMBO MBALIMBALI, NA HATA WALE WALIOKWAZWA NA MISIMAMO YAKO, UMEWATAFUTA, UMEWAFUATA, UMEWAOMBEA, UNAWAOMBEA, UNAWALILIA, UNAUGUA KWA AJILI YAO ILI WAREJEE??!! ILI KUWAREJEZA??!! KAMA HUFANYI HIVYO PENGINE HUKUTUMWA NA YESU!!! AU UMEMWASI YESU, NA WALA HAUMTUMIKII YESU BALI TUMBO LAKO!!!

Yohana 10:11-13,15

[11]Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 

I am the good shepherd: the good shepherd giveth his life for the sheep.

[12]Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. 

But he that is an hireling, and not the shepherd, whose own the sheep are not, seeth the wolf coming, and leaveth the sheep, and fleeth: and the wolf catcheth them, and scattereth the sheep.

[13]Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. 

The hireling fleeth, because he is an hireling, and careth not for the sheep.

[15]kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 

As the Father knoweth me, even so know I the Father: and I lay down my life for the sheep.

NA TENA;

>> KAMA MUNGU ATAFANYA HAYA WEWE UTAKUWA WAPI??!!

2 Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo? 

Ezekieli 34:2

3 Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo. 

Ezekieli 34:3

4 Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala. 

Ezekieli 34:4

5 Nao wakatawanyika, kwa sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyama-mwitu, wakatawanyika. 

Ezekieli 34:5

7 Basi, enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; 

Ezekieli 34:7

8 Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo zangu walikuwa mateka, kondoo zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu hawakutafuta kondoo zangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo zangu; 

Ezekieli 34:8

9 kwa sababu hiyo, enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; 

Ezekieli 34:9

10 Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu ya wachungaji; nami nitawataka kondoo zangu mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo; nao wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami nitawaokoa kondoo zangu vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao. 

Ezekieli 34:10

11 Maana, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi, nitawatafuta kondoo zangu, na kuwaulizia. 

Ezekieli 34:11

12 Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo zake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo zake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo zangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza. 

Ezekieli 34:12

14 Nami nitawalisha malisho mema, pa juu ya milima ya mahali palipoinuka pa Israeli litakuwa zizi lao; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli. 

Ezekieli 34:14

15 Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo zangu, nami nitawalaza, asema Bwana MUNGU. 

Ezekieli 34:15

16 Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu. 

Ezekieli 34:16

NA TENA;

1 Yohana 5:16

[16]Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo. 

If any man see his brother sin a sin which is not unto death, he shall ask, and he shall give him life for them that sin not unto death. There is a sin unto death: I do not say that he shall pray for it.

>> WAJIBU WAKO MKRISTO NI KUOMBA KWA AJILI YA WAKRISTO WENZAKO UNAOWAONA WAKITENDA DHAMBI!! KUOMBA NA SIYO KUSENGENYA! KUOMBA NA SIYO KUENEZA HABARI ZAO MBAYA! KUOMBA NA SIYO KUSEMA HAWAINGII MBINGUNI! KUOMBA NA SIYO KUWAFUNGIA MLANGO WA MBINGUNI!! USIPOOMBA WEWE YESU ATAINUA WAOMBEZI WENGINE KWINGINE NA THAWABU YAKO WATAITWAA NA WEWE UTAKUWA WAPI??!! KAMA UNAJUA KUOMBEA REHEMA NA NEEMA WALE WATENDAO DHAMBI NI JAMBO JEMA HALAFU HAUFANYI HIVYO JE! HUO NDIO UTAKATIFU WAKO??!!

Yakobo 4:17

[17]Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. 

Therefore to him that knoweth to do good, and doeth it not, to him it is sin.

>> KAMA HAUKUOMBEA ULITENDA DHAMBI, NA KAMA BADO HAUOMBEI WATENDAO DHAMBI MPAKA WAREJEE BADO UNATENDA DHAMBI!! HAYA NI AINA YA MAOMBI UNAYOOMBA MPAKA WAREJEE! AMA MPAKA BWANA AKUHAKIKISHIE KWAMBA AMEWASAMEHE NA ATAWAREJEZA!! HII INAITWA HUDUMA YA UREJEZO WA WOTE WALIOJIKWAA, WALIOELEMEWA NA DHAMBI, WALIOSHINDWA NA DHAMBI, NA WALIODANGANYWA NA DHAMBI!! MUNGU ANATAKA WAREJEZWE WOTE!! UMEWAHI KUWAREJEZA WANGAPI? UNA MOYO WA KUREJEZA KWA MAOMBI??!! YESU HUWAACHA 99 WALIO SALAMA NA KUMTAFUTA MMOJA ALIYEPOTEA!! WEWE MTENDA DHAMBI UNASEMA SHAURI YAKE APOTELEE KUZIMU NA WAZIMU WAKE, ATAMWACHAJE YESU??!!🙇🏻‍♂️🙆🏻‍♂️🤷🏻‍♂️UMEPOTOKA, UMEDANGANYWA NA KIBURI CHA MOYO WAKO!!

Obadia 1:3

[3]Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, 

Wewe ukaaye katika pango za majabali, 

Mwenye makao yako juu sana; 

Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi? 

The pride of thine heart hath deceived thee, thou that dwellest in the clefts of the rock, whose habitation is high; that saith in his heart, Who shall bring me down to the ground?

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post