TUKO HURU KWELI KWELI
"31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
Yohana 8:31
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Yohana 8:32
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli."
Yohana 8:36
>> UHURU WA WATOTO WA MUNGU UKO KWENYE KUIFAHAMU KWELI
>> NA ILI KUIFAHAMU KWELI NI LAZIMA KUKAA (TO ABIDE IN) KATIKA NENO LA KRISTO
>> WAPO WATOTO WA MUNGU AMBAO BADO WAPO UTUMWANI KWA KUTOIFAHAMU KWELI, AMA WAPO UTUMWANI KWA KUTOFUNDISHWA KWELI, AU KWA WANAOWALISHA KUTOIJUA KWELI KWA SABABU YA WAO WENYEWE KUTOKUWA HURU BADO!!
UHURU WETU
1) TUKO HURU MBALI NA DHAMBI
Warumi 6:22
"[22]Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
But now being made free from sin, and become servants to God, ye have your fruit unto holiness, and the end everlasting life."
>> TUKO HURU MBALI NA DHAMBI
>> TUNAISHI MAISHA YA UTAKASO
>> MAISHA YA UTAKASO YANATUSAIDIA NA KUTUWEZESHA KUTUNZA NA KUDUMISHA UTAKATIFU WETU NDANI YA KRISTO YESU
>> KWELI NDIYO INAYOTUTAKASA (1 PETRO 1:22)
2) TUKO HURU MBALI NA SHERIA
>>"21 Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure."
Wagalatia 2:21
>>"1 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?
Wagalatia 3:1
2 Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
Wagalatia 3:2
3 Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?
Wagalatia 3:3
5 Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
Wagalatia 3:5
11 Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.
Wagalatia 3:11
>> 23 Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa."
Wagalatia 3:23
>> "20 Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,
Wakolosai 2:20
21 Msishike, msionje, msiguse;
Wakolosai 2:21
22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
Wakolosai 2:22
23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili."
Wakolosai 2:23
>>"4 Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema."
Wagalatia 5:4
>> "14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema."
Warumi 6:14
3) HURU MBALI NA UCHUNGU WA MAUTI NA NGUVU ZA DHAMBI
1 Wakorintho 15:56
"[56]Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
The sting of death is sin; and the strength of sin is the law."
>> MAUTI YA MWILI HAITUUMI TENA WALA HAITUTISHI
>> NGUVU ZA DHAMBI ZIMEVUNJWA KWETU; NGUVU ZA DHAMBI NI TORATI/ SHERIA/ AMRI KUMI
-HATUISHI KWA AMRI JUU YA AMRI AMRI JUU YA AMRI, KANUNI JUU YA KANUNI KANUNI JUU YA KANUNI (Isaya 24:10,13)
MAANDIKO YANASEMA,
"Yakobo 2:10-12
[10]Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
For whosoever shall keep the whole law, and yet offend in one point, he is guilty of all.
[11]Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.
For he that said, Do not commit adultery, said also, Do not kill. Now if thou commit no adultery, yet if thou kill, thou art become a transgressor of the law.
[12]Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
So speak ye, and so do, as they that shall be judged by the law of liberty."
4) HURU MBALI NA NGUVU NA HOFU YA MAUTI NA HOFU NYINGINE ZOTE
>>"14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Waebrania 2:14
15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa."
Waebrania 2:15
>>"18 Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo."
1 Yohana 4:18
5) HURU MBALI NA UFALME WA, MAMLAKA, NA NGUVU ZA GIZA ZOTE
>> "12 mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.
Wakolosai 1:12
13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
Wakolosai 1:13
14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; "
Wakolosai 1:14
6) HURU NA MBALI NA LAANA ZOTE
>> 3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Waefeso 1:3
>> BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE KRISTO YESU KWA WATAKATIFU ZIMEONDOA NA KUKOMESHA KABISA LAANA ZOTE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
>> TUKO HURU MBALI NA LAANA YA TORATI AU SHERIA YA NAMNA YOYOTE
>>"13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
Wagalatia 3:13
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani."
Wagalatia 3:14
>> UHURU WETU NI KWAMBA HATUTENDI DHAMBI, HATUTAWALIWI NA DHAMBI, TUNACHUKIA DHAMBI, NA TUMEJITENGA NA DHAMBI, TUNA USHINDI JUU YA DHAMBI, TUNA MAMLAKA PIA DHIDI YA NA JUU YA ROHO ZA DHAMBI
>> LAKINI HATUFANYI HAYA YOTE KWA SHERIA ZA NJE KWA JINSI YA MWILI, BALI TUNAYAFANYA YOTE KWA SHERIA YA ROHO WA UZIMA ILIYO NDANI YAKE KRISTO YESU!!
>> NAYO NI SHERIA YA UHURU WA KUTOTENDA DHAMBI WALA KUTAWALIWA NA DHAMBI!! NA PIA NI SHERIA YA UHURU WA NDANI AMBAPO TUMECHAGUA KWA ROHO ZETU (MIOYO YETU) KUMPENDA NA KUMTII YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU KWA HIYARI YA MIOYO YETU NA SI KWA KULAZIMISHWA AU KWA KUTISHWA!! UPENDO WA KRISTO UNATUBIDIISHA,
Warumi 6:17
[17]Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;
But God be thanked, that ye were the servants of sin, but ye have obeyed from the heart that form of doctrine which was delivered you.
>> TUNATII KWA MIOYO YETU
>> 2 Corinthians 5:14
[14]For the love of Christ constraineth us; because we thus judge, that if one died for all, then were all dead:
Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote;
Ayubu 32:18
[18]Kwa kuwa nimejaa maneno;
Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.
For I am full of matter, the spirit within me constraineth me.
>> ROHO WA KRISTO ALIYE NDANI YETU HUTUHIMIZA NA KUTUSUKUMA!!
>> SHERIA YA ROHO WA UZIMA, AU ROHO WA MAISHA YA KRISTO YESU NI SHERIA YA NDANI YA ROHO ZETU AMBAPO MSUKUMO WA KUTII UNATOKA NDANI
>> ILI KUMCHOCHEA MTOTO WA MUNGU KUTII UNATAKIWA KUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKE!! MAANA TUNAHUDUMIA ROHO ZA WATEULE NA MAISHA YAO YASIYOHARIBIKA!! TUNAANZIA NDANI KWENDA NJE, NA SIYO NJE KWENDA NDANI
>> SHERIA HUWA INAANZIA NJE NA HAIFIKI NDANI KWA KUWA SIYO SHERIA YA ROHO !! ILA SHERIA YA IMANI, AU SHERIA YA ROHO WA UZIMA ILIYO KATIKA KRISTO YESU NI SHERIA YA UHURU YA NDANI INAYOTAWALA WATOTO WA MUNGU
>> SHERIA YA UHURU YA KRISTO INATENDA KAZI KWA UPENDO WA ROHO KUPITIA IMANI ILIYO HAI KWA YESU KRISTO!! HAPA NDIPO PENYE NEEMA JUU YA NEEMA!! UNAHITAJI KUHAKIKISHA UNAJAZWA ROHO, AU KUSANYIKO LOTE LINAJAZWA ROHO MTAKATIFU, LINAONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU, NA LINAKUA KATIKA NEEMA NA KATIKA KUMJUA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU!!
2 Petro 3:18
[18]Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
But grow in grace, and in the knowledge of our Lord and Saviour Jesus Christ. To him be glory both now and for ever. Amen.
>> HATUKUI KWA SHERIA, WALA HATUKUI KWA MATENDO YA SHERIA, WALA HATUKUI KWA JUHUDI ZA NJE ZA KUUDHIBITI NA KUUTAWALA MWILI, BALI TUNAKUA KIROHO KWA NEEMA YAKE!! YAANI, KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE!!
11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
Tito 2:11
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Tito 2:12
>> NA TENA;
2 Wakorintho 3:6
[6]Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Who also hath made us able ministers of the new testament; not of the letter, but of the spirit: for the letter killeth, but the spirit giveth life.
>> SISI NI WAHUDUMU WA AGANO JIPYA, SI WA ANDIKO (NENO LILILOANDIKWA), BALI WA ROHO (ROHO YA NENO LILILOANDIKWA)
>> SHERIA INAMLAZIMISHA MTEULE KULITIMIZA NENO/ANDIKO KAMA LILIVYO, LAKINI SI KWA NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU, BALI NI KWA NGUVU, BIDII, NA UWEZA WAKE MWENYEWE, PAMOJA NA KICHO ALICHOCHOKITENGENEZA YEYE MWENYEWE (HUMAN-MANUFACTURED FEAR OF GOD)
22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
Wakolosai 2:22
23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
Wakolosai 2:23
>> HII NDIYO MAANA WENGINE WANAJIFUNIKA MWILI WOTE NA KUACHA MACHO NA PUA TU LAKINI BADO NI WATENDA DHAMBI!!
>> KWENYE AGANO JIPYA HATUMLAZIMISHI MTOTO WA MUNGU KULITENDA ANDIKO KWA NGUVU ZAKE NA UWEZA WAKE KWA KUMTUNGIA SHERIA MBALIMBALI KWA MUJIBU WA ANDIKO, BALI TUNAMFUNDISHA KWELI NA YEYE AKIAMINI ANAPOKEA REHEMA ZAKE BWANA, NA NEEMA INAYOMSAIDIA NA KUMWEZESHA KULITII NENO/ANDIKO KATIKA ROHO , NA KWA NGUVU ZA HUYU ROHO MTAKATIFU!! MAANA YESU ALISEMA:
Yohana 6:63
[63]Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
It is the spirit that quickeneth; the flesh profiteth nothing: the words that I speak unto you, they are spirit, and they are life.
>> ANAHITAJIKA ROHO AMBAYE ANALIFANYA NENO LIWE HAI NDANI YA ROHO YA MWAMINI NA HIVYO KUMHUISHA (QUICKEN!!)
>> HUYU ROHO HAPATIKANI KWA MATENDO YA SHERIA
>> ROHO HUYU MTAKATIFU ANAPATIKANA KWA KUSIKIA KUNAKOTOKANA NA IMANI
2 Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
Wagalatia 3:2
>> JUHUDI NA BIDII ZA KIMWILI ZA KUTAKA KUMPENDEZA MUNGU HAZIFAI KITU ISIPOKUWA IMANI ITENDAYO KAZI KWA UPENDO (WAGALATIA 5:6)
>> PASIPO IMANI HII HAIWEZEKANI KAMWE KUMPENDEZA MUNGU
6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Waebrania 11:6
>> 1 Timotheo 1:9
[9]akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,
Knowing this, that the law is not made for a righteous man, but for the lawless and disobedient, for the ungodly and for sinners, for unholy and profane, for murderers of fathers and murderers of mothers, for manslayers,
>> ULIFAHAMU NENO HILI: KWAMBA SHERIA HAIMHUSU NA WALA HAIKULETWA KWA AJILI YA MTU WA HAKI, BALI WATENDA DHAMBI WALIOTAJWA KWENYE ANDIKO!! SIKILIZA: SHERIA HAIMHUSU MTU WA HAKI!!!
>> SHERIA MPYA YA MTU WA HAKI NI HII:
Warumi 8:1
>> [1]Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
There is therefore now no condemnation to them which are in Christ Jesus, who walk not after the flesh, but after the Spirit.
>> HAKUNA HUKUMU YA ADHABU JUU YAO WALIO KATIKA KRISTO YESU! KWA NINI?
Warumi 8:2
[2]Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
For the law of the Spirit of life in Christ Jesus hath made me free from the law of sin and death.
7) HURU MBALI NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI
>> Warumi 8:2
[2]Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
For the law of the Spirit of life in Christ Jesus hath made me free from the law of sin and death.
>> UNAPOKUWA CHINI YA SHERIA HUNA UHURU AU UCHAGUZI MWINGINE TOFAUTI NA KUISHI NA KUENENDA KAMA SHERIA ITAKAVYO!!
>> SHERIA ITAKUTAWALA MPAKA LIWEPO BADILIKO LA SHERIA NDIPO NA WEWE UTAWEZA KUTENDA KWA SHERIA HIYO MPYA
>> SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI INAMTAWALA MWENYE DHAMBI; KWAMBA YUMO DHAMBINI, MAWAZO YAKE NI DHAMBI, FIKRA ZAKE NI DHAMBI, NIA YA MOYO WAKE NI DHAMBI, MAKUSUDIO YA MOYO WAKE NI DHAMBI, MAPENZI YA MOYO WAKE NI DHAMBI, HISIA ZAKE NI DHAMBI; HIVYO LAZIMA AWE MAUTINI KWA MAANA IMEANDIKWA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI: KWA KUWA ANATENDA DHAMBI AMEKUFA KIROHO. NA KIFO CHA MWILI KINAWEZA KUJA WAKATI WOWOTE HATA KABLA YA MUDA WAKE!! NA WALA HAWEZI KUPONYOKA DHAMBINI WALA KUJITOA DHAMBINI!!
>> SHERIA YA ROHO WA UZIMA (THE LAW OF THE SPIRIT OF LIFE) NDANI YAKE KRISTO YESU IMEKUWEKA MTEULE MTOTO WA MUNGU ULIYEOKOKA MBALI NA SHERIA HIYO YA DHAMBI NA MAUTI!! IMEKUFUNGUA NA KUKUTOA UTUMWANI NA KUKUWEKA HURU!! HAUTENDI DHAMBI, HAUWEZI KUTENDA DHAMBI, UNACHUKIA DHAMBI, HAUKUSUDII TOKA MOYONI KUTENDA DHAMBI, HAUTAKI KUTENDA DHAMBI, UKIJIKWAA UKATENDA DHAMBI NI MWEPESI WA KUTUBU NA REHEMA ZAKE BWANA HAZIKOMI KWAKO, NEEMA YA KRISTO IKO JUU YAKO, UNAISHI KWA IMANI TAKATIFU YA YESU KRISTO!! UNAONGOZWA NA KUTAWALIWA NA UPENDO WA MUNGU KWA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAKO!! WEWE NI MTAKATIFU!! UNAMWAMINI YESU NA UNAISHI!! UKO HAI, UNA NGUVU ZA MUNGU NDANI YAKO ZIKITENDA KAZI KWA AJILI YAKO NA KWA AJILI YA WENGINE UNAOWAOMBEA NA KUWAHUDUMIA!! UKO HURU MBALI NA DHAMBI NA MAUTI NA DHAMBI HAIWEZI KUKUTAWALA!!
4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
1 Yohana 3:4
5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
1 Yohana 3:5
6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
1 Yohana 3:6
7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;
1 Yohana 3:7
8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
1 Yohana 3:8
9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
1 Yohana 3:9
10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
1 Yohana 3:10
ZINGATIA HII:
31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
Warumi 8:31
32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
Warumi 8:32
33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
Warumi 8:33
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
Warumi 8:34
>> BADO NINGALI NINAYO MENGI YA KUANDIKA KUHUSU UHURU WETU WANA WA MUNGU, LAKINI UBARIKIWE KWA HAYA MACHACHE AU MENGI, WEWE UTAAMUA, NA BWANA ASEMA,
John 13:17(NIV)
[17]Now that you know these things, you will be blessed if you do them.
John 13:17 (NLT) Now that you know these things, God will bless you for doing them.
17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.
Yohana 13:17
>> KWA KUWA SASA UNAYAJUA HAYO UTABARIKIWA ZAIDI IKIWA UTAYATENDA!!
>> KWA KUWA UMEYAJUA HAYO MUNGU ATAKUBARIKI ZAIDI KWA KUYATENDA!! AMEN, HALELUYA!!
Tags
MAFUNDISHO