1:0 MAUSIA KWENYE NDOA YA KIKRISTO
1) Mwanzo;"24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."
Mwanzo 2:24
>> NDOA NI MCHAKATO (PROCESS) ENDELEVU WA MAENEO MATATU
1) KUTOKA KWA BABA NA MAMA (WAZAZI, WALEZI, NDUGU NA JAMAA)
- Kutokutoka kabisa huwa kunaathiri ndoa nyingi!! Mke uko chini ya mamlaka ya mume, uangalizi wa mume, na matunzo na ulinzi wa mume sasa na siyo wazazi, walezi, au ndugu!!
- Umekwenda kumsaidia mumeo katika majukumu yako mapya, ya Kuanzisha, kuandaa, na kuendeleza familia na nyumba mpya!!
- kule ulikotoka wanaweza kukushauri lakini siyo kukupangia cha kufanya, au wewe kupanga mipango ya siri na wao pasipo mumeo kujua!!
2) KUAMBATANA NA MUMEO/ MKEO (Amos 3:3)
>> Kuambatana kunakuja pale tofauti za mitizamo na misimamo zinapoibuka kuhusiana na mambo mbalimbali kwenye maisha yenu! Lazima mtofautiane ili mjadiliane kwa upendo, mkubaliane, na kisha kutekeleza makubaliano yenu!! Neno la Mungu ndilo taa ya miguu yenu na mwanga wa njia zenu!! (Zab 119:105)
>> HILO NDILO MAMLAKA YA JUU KWENYE NDOA YENU LINALOAMUA NA KUONDOA TOFAUTI ZENU ZA KIMITAZAMO NA KIMISIMAMO MAANA WOTE MAISHA YENU NI NDANI YA NENO HILO! WOTE MNALITII NA KULITENDA NA HIVYO KUAMBATANA KATIKA ROHO YA HILO NENO, MAWAZO AU FIKRA ZA HILO NENO (MIND OF SCRIPTURE), NIA/MAKUSUDI/MAPENZI (WILL) YA HILO NENO, NA HISIA(EMOTIONS) ZA HILO NENO!!
>> KUAMBATANA KWENU NI KUPATANA NA KUKUBALIANA SAWASAWA NA NENO KUNAKOPELEKEA MUWE ROHO MOJA (MOYO MMOJA) NA HIVYO MWILI MMOJA
>> YAANI, NENO LINAWAUNGANISHA ILI MUWE MMOJA KATIKA ROHO, NAFSI, NA MWILI, KWA HUYO ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YENU!!
3) KUWA MWILI MMOJA
>> KUAMBATANA KWA NAMNA NILIVYOELEZA HAPO JUU NDIKO KUNAKOPELEKEA KUWA MWILI MMOJA!! (ONE FLESH)
>> KUAMBATANA UNTO MWILI MMOJA NI LIFETIME PROCESS (MCHAKATO WA MAISHA)
>> MWILI MMOJA MAANA YAKE NI:
1) MMOJA KIROHO (SPIRITUAL ONENESS)
2) MMOJA KIAKILI (MENTAL ONENESS)
3) MMOJA KIHISIA (EMOTIONAL ONENESS)
4) MMOJA KIMWILI (PHYSICAL ONENESS), na hii inapelekea kumiliki baraka zote za fedha na mali kama mmoja!! ( together as one)
>> MUME NA MKE AMBAO NI MWILI MMOJA SIKUZOTE WAPO PAMOJA WAJAPOKUWA MBALIMBALI!! MAUMIVU YA MMOJA NA MWINGINE ANAYAPATA AJAPOKUWA MBALI!! HAWA HUWA HATA HAWAHITAJI SIMU ZA MKONONI MAANA WANAWASILIANA KILA WAKATI KATIKA ROHO!! WAMEUNGANIKA NA KUWA MMOJA!!
>> TOFAUTI ZIWE NI FURSA ZA KUAMBATANA, NA HATIMAYE KUWA MWILI MMOJA
1:1 USHAURI MUHIMU KUHUSU KAZI NA HUDUMA
>> Biblia imetoa mwanga pia kuhusu "kuambatana"!!
"14 Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthuu akaambatana naye.
Ruthu 1:14
15 Naye akasema, Tazama, shemeji yako amerejea kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urejee wewe umfuate shemeji yako.
Ruthu 1:15
16 Naye Ruthuu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;
Ruthu 1:16
17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami."
Ruthu 1:17
>> MST 14 : ".......RUTHU AKAAMBATANA NAYE"
>> MISTARI 16-17 ANAELEZA KUAMBATANA NI KUPI!!
1) MST 16: USINISIHI NIKUACHE;
- roho ya kuambatana haitaki kusikia habari za kutoambatana! Haikubali wazo wala ushauri wa kutoambatana
2) NIREJEE NISIFUATANE NAWE;
>> suala la wewe mume wangu/ mke wangu kwenda kuishi mbali na mimi kwa sababu yoyote halipo, iwe kazi, ajira, huduma, au sababu yeyote!!
3) MAANA WEWE UENDAKO NITAKWENDA;
>> mimi na wewe tutakwenda pamoja popote uendako mguu kwa mguu/ wewe utakwenda na mimi popote niendako!!
4) NA WEWE UKAAPO NITAKAA
>> MIMI NA WEWE/ WEWE NA MIMI TUTAISHI PAMOJA NCHI MOJA, MJI MMOJA, NYUMBA MOJA, NA TUTALALA KITANDA KIMOJA SIKU ZETU ZOTE, NA KIFO PEKEE NDIO KITATUTENGANISHA!!
5) WATU WAKO WATAKUWA WATU WANGU
>> YAANI, NDUGU NA JAMAA ZAKO WATAKUWA NDIO NDUGU NA JAMAA ZANGU!!
>> NDUGU NA JAMAA WA MKE HUWA NI NDUGU NA JAMAA WA MUME, NA NDUGU NA JAMAA WA MUME HUWA NI NDUGU NA JAMAA WA MKE!! NA HIVYO NDOA TAKATIFU HUUNGANISHA FAMILIA MBILI KUWA MOJA!!
6) MUNGU WAKO ATAKUWA MUNGU WANGU
>> Kwenye ndoa takatifu mume na mke huwa wanamwabudu Mungu mmoja wa Bwana wetu Yesu Kristo!!
>> Ndoa ambayo mke na mume kila mmoja anamwabudu mungu wake haina kuambatana kiroho na italeta shida kubwa, na hawawezi kuwa mmoja kiroho!! Na hii lazima itaathiri mchakato wa maisha wa kuwa mwili mmoja!!
7) PALE UTAKAPOKUFA NITAKUFA NAMI, NA PAPO HAPO NITAZIKWA
>> Ukitazama muktadha wa andiko utaona kwamba Ruthu Mmoabi alitoka kwa watu wake, na kuambatana na Naomi kwenda Bethlehemu, ambako aliolewa na Boaz na akamzaa Obedi, aliyemzaa Yese baba yake Daudi!! (Ruthu 4:13-22)
>> Kule kuambatana na Naomi kulimwingiza Ruthu kwenye ukoo wa Yesu kupitia Boaz mumewe! Hakika watu wa Naomi wakawa ndio watu wake na Mungu wa Israeli akawa ndiye Mungu wake!! Ruthu alimjua Mungu wa kweli!!
>> Kwa kuambatana hivi haileti shida yoyote akifariki Boaz maana Ruthu amekwishakuwa mmoja wao!! Lakini leo ndoa nyingi hazina kuambatana wala kuwa mwili mmoja, na ikitokea mume akifariki mke hana chake tena!! Jukumu la kutengeneza familia moja ni la wanandoa na jukumu hili linafanyika KWA UPENDO WA MUNGU NDANI YAKE KRISTO ambao hata hao ndugu watauona na kujifunza, na wao kuupokea upendo huo mioyoni mwao kwa kumpokea Yesu !!
>> mume penda ndugu na jamaa wa mkeo kama nafsi yako, na mke penda ndugu na jamaa wa mumeo kama nafsi yako!! Hawa ni familia moja!!
>> Kwa wanandoa walioambatana pale anapozikwa mmoja ndipo anapozikwa mwingine!!
8) KIFO TU NDIYO KITATUTENGANISHA
>> WANANDOA WALIOAMBATANA NA KUWA MWILI MMOJA HUWA HAWAACHANI KAMWE
>> KUACHANA KWAO NI PALE MMOJA ANAPOFARIKI DUNIA!!
>> NDOA NI MWILI MMOJA MPAKA KIFO KIWATENGANISHE!!!
- Hizi ndizo maana nane au maeneo nane ya kuambatana!!! Unaweza kuyaita MILIMA NANE YA KUAMBATANA!!!
>> Kwa kuzingatia haya suala la mwanandoa mmoja kuishi kaskazini na mwingine kusini HALITOKI KWA MUNGU!!
2.0 NDOA NI UPENDO WA MUNGU NA UPENDO WA MUNGU NI NDOA
>> Kupenda ni kutoa moyo wako wote kwa ajili yake!!
>> Aliye moyoni mwako ndiye unayempenda!!
>> Moyoni mwako ni rohoni mwako!!
>> Kumpa au kuutoa moyo wako kwake ni kujitoa wewe mwenyewe roho yako kwake!! Maana mtu ni roho, ana nafsi, na anaishi kwenye mwili!!
>> Ukimpenda atakuwa juu kabisa katika orodha ya moyo wako kumzingatia, kumtanguliza, kumthamini, kumheshimu, kumtanguliza, kumtendea mema, kuwa naye pamoja, kushirikiana naye, kumkumbuka, kumhitaji, kumtaka, kumnufaisha, kumfaidia, kumlinda, kumpa amani, kuchukuliana naye, kumsamehe, kumvumilia, kutafuta faida yake, kumkusudia mema, kumwazia mema, kumuepusha na mabaya, kumpangia mipango ya mema na si ya mabaya, kumwezesha, kumtatulia, kumfumbulia, kumwinua, kumsaidia, kumjali, kumtunza, kumzawadia, kumwombea, na kiujumla kuyatoa maisha yako kwa ajili yake!!!
>> Kumpenda ni kujitoa wewe mwenyewe VYOTE VILE ULIVYO kwa ajili yake, na VYOTE ULIVYONAVYO kwa ajili yake, na YOTE UYAFANYAYO kwa faida na manufaa yake!! Na hii siku siku moja au siku chache tu bali SIKUZOTE ZA MAISHA YAKO KWENYE MWILI!!
>> Kwenye ndoa Mungu amekusudia wanandoa wakue na kuongezeka katika pendo lao kwake na kwao wenyewe kila mmoja kwa mwenzake!!
"9 Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;
Wafilipi 1:9
10 mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo;
Wafilipi 1:10
11 hali mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu."
Wafilipi 1:11
1) PENDO LA MUNGU LIKIONGEZEKA KWENU WANANDOA
2) KWENYE MAISHA YENU MTAYAKUBALI, KUYAPOKEA, NA KUYAISHI, YALE YALIYO MEMA TU MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU
3) KWA KUYAKATAA YALE MABAYA NA YASIYOFAA, KISHA KUYAKUBALI YALIYO MEMA PEKEE, HII ITAWATAKASA MIOYO YENU, MUWE BILA KOSA, WALA LAWAMA MBELE ZA MUNGU MPAKA SIKU YA KRISTO
>> PENDO LA KRISTO LINATAKASA MAANA PENDO HILO NI TAKATIFU!! (PURE LOVE)
4) KATIKA HALI HIYO YA MIOYO SAFI ILIYOJAA PENDO TAKATIFU LA KRISTO KWA ROHO MTAKATIFU (RUM 5:5), WANANDOA MTAKUWA MNAMZALIA MUNGU MATUNDA YA HAKI KWA NJIA YA KRISTO, KWA SIFA NA UTUKUFU WAKE!!
>> KULE KUMZALIA MUNGU MATUNDA (FRUITFULNESS) NDIKO KUNAKOFANYA NDOA IZIDI KUWA TAMU, NZURI, YENYE RAHA, AMBAMO WANANDOA MNAFAIDI, MNAFURAHIA, MNA AMANI, NA TUNDA LA ROHO LINAONEKANA MAISHANI MWENU (GAL 5:22-23) NA TUNDA LA NURU PIA LINAONEKANA (EFE 5:9)
>> NDOA YENYE MATUNDA NAMNA HII MAANA YAKE WANANDOA WANAZIDI KUWA KAMA YESU (YAANI, KUFANANA NA YESU)
>> WANANDOA WANAISHI SAWASAWA NA 1 KOR 13:1-8 NA HIVYO WOTE, KILA MMOJA WAO, ANAWAJIBIKA KWA KRISTO NA KWA MWENZAKE, VILE VILE KAMA MUNGU ALIVYOKUSUDIA!!
>> MUHIMU NI KUTAMBUA KWAMBA KUNA KUKUA (GROWTH) NA KUONGEZEKA (INCREASE) KATIKA UPENDO, JAMBO AMBALO LINACHUKUA MUDA WOTE WA MAISHA YAO
"15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo."
Waefeso 4:15
>> YESU KWENYE NDOA+ YESU KWENYE FAMILIA = YESU NYUMBANI
>> YESU NYUMBANI + YESU NYUMBANI + YESU NYUMBANI + .........N.K.= YESU KWENYE KUSANYIKO LA WATAKATIFU MAHALI PAMOJA (KANISANI)
>> WATOTO WA KIMWILI, NA WA KIROHO WOTE WATAKUWA NAO NI KANISA TAKATIFU!!!
2:1 UPENDO WA MUME KWA MKE NA UTII WA MKE KWA MUME NI IBADA NA MANUKATO KWA MUNGU
Biblia inasema,
Romans 12:1
"1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
Warumi 12:1
[1]Therefore, I urge you, brothers and sisters, in view of God’s mercy, to offer your bodies as a living sacrifice, holy and pleasing to God—this is your true and proper worship."
>> KUUTOA MWILI WAKO KWA MUNGU UWE DHABIHU ILIYO HAI, TAKATIFU, YA KUMPENDEZA MUNGU NI IBADA YA KUFAA NA INAYOMPENDEZA MUNGU.
>> KIMAANDIKO MKE HANA MAMLAKA JUU YA MWILI WAKE MWENYEWE ISIPOKUWA MUMEWE, NA MUME HANA MAMLAKA JUU YA MWILI WAKE MWENYEWE ISIPOKUWA MKEWE (1 WAKORINTHO 7: 4); NAO WANAFANYA HIVYO KATIKA KUTII AGIZO LA BWANA YESU! UTII UNAMPENDEZA MUNGU, NA KUJITOA MWILI WAKO KWA AJILI YA MUNGU KWA MKEO AU MUMEO NI IBADA YENYE KUMPENDEZA MUNGU, NA NI MANUKATO KWAKE!!
>> BIBLIA INAFUNDISHA KWAMBA,
"3 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
Wakolosai 3:23
24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo."
Wakolosai 3:24
>> HIVYO MUME ANAUACHILIA MWILI WAKE KWA MKEWE MWENYE MAMLAKA NAO, NA MKE ANAUACHILIA MWILI WAKE KWA MUMEWE MWENYE MAMLAKA NAO
>> KWA KUFANYA HIVYO ANAKUWA ANAMTOLEA MUNGU IBADA YENYE KUPENDEZA!!
>> MUME ANAMTENDEA MKEWE KAMA KUMTUMIKIA YESU, NA MKE ANAMTENDEA MUMEWE KAMA KUMTUMIKIA YESU
>> MUNGU ANAPOKEA IBADA YA MUME KUPITIA MEMA ANAYOMTENDEA MKEWE KAMA MANUKATO, NA PIA ANAPOKEA MANUKATO YA IBADA YA MKE ANAVYOMTENDEA MEMA MUMEWE!!
>> WAJIBU WA KIAGANO WA MKE KWA MUME, NA MUME KWA MKE NI WAJIBU WA UPENDO WA YESU KIVITENDO WA KILA MMOJA KWA MWENZAKE KWA JINA LA YESU
>> KWA KIWANGO USICHOMTENDEA MEMA MWENZAKO NDIVYO KWA KIASI HICHO HICHO HUMTENDEI YESU!!
Mfano Biblia inasema,
"33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe."
1 Wakorintho 7:33
34 "................ Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe."
1 Wakorintho 7:34
>> MKE ANAPOJISHUGHULISHA NA MAMBO YA DUNIA HII JINSI GANI ATAKAVYOMPENDEZA MUMEWE HIYO NI IBADA KATIKA ROHO NA KWELI, NA UTUMISHI MBELE ZA MUNGU.
>> NA MUME ANAPOJISHUGHULISHA NA MAMBO YA DUNIA HII JINSI GANI ATAKAVYOMPENDEZA MKEWE HIVYO NI IBADA NA UTUMISHI MBELE ZA MUNGU
>> KWA KUWA SI MUME AU MKE ANAYETENDEWA MEMA YALE BALI YESU KWA MUJIBU WA MAANDIKO!!
>> MKE AU MUME KUTOWAJIBIKA KWA MWENZAKE KATIKA NAFASI ALIYOWEKWA NI UASI WA KWELI NA NI KIKWAZO CHA KUENDELEA MBELE KATIKA UPENDO!! NI KUMPA IBILISI NAFASI
>> MKE MTII MUMEO NA UNYENYEKEE CHINI YA MAMLAKA YAKE; NA MUME MPENDE MKEO NA UJITIE NA KUNYENYEKEA CHINI YA MAMLAKA YA KRISTO!!
"3 Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu."
1 Wakorintho 11:3
>> MKE NENDA KAMSAIDIE MUMEO!! WEWE NI MSAIDIZI USIENDE KUWA KIONGOZI WALA USIJARIBU KUTAKA KUWA KIONGOZI; WEWE SIYO KICHWA NA USIJARIBU KUJIFANYA KUWA NI KICHWA!
>> MUME MPENDE NA UMHESHIMU MKEO, USIJIFANYE BWANA MKUBWA KWENYE NDOA NA USIMFANYE MKEO KUWA NI MTUMWA WAKO! WOTE WAWILI MNA HAKI SAWA KWENYE NDOA!
1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
Likewise, ye husbands, dwell with them according to knowledge, giving honour unto the wife, as unto the weaker vessel, and as being heirs together of the grace of life; that your prayers be not hindered.

Tags
NDOA