HUKUMU YA MACHO VS HUKUMU YA HAKI
Biblia inasema,"1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda."
Isaya 11:1
>> HUYU NI BWANA WETU YESU KRISTO, MWANA WA DAUDI.
"2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;"
Isaya 11:2
>> HIZI NI ROHO SABA ZA MUNGU NDANI YAKE, KWA ROHO MTAKATIFU, AMBAZO NDIYO MACHO SABA YA MUNGU, AU MACHO SABA YA ROHONI ( Zech 4:2,6,10 & Ufu 5:6)
>> YESU AKIWA NDANI YAKO HALAFU AKAKUJAZA ROHO WAKE, UTAFUMBULIWA NA WEWE MACHO SABA YA ROHONI KWA KUTIWA NURU YAKE MOYONI (ROHONI) MWAKO!!
"3 na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;"
Isaya 11:3"
>> MATOKEO YAKE UTAISHI NA KUENENDA KWA ROHO HUYU MTAKATIFU WA KRISTO SIKUZOTE, NA HIVYO KAMWE HAUTAHUKUMU KWA KUYAFUATA YALE UYAONAYO KWA MACHO NA YALE UYASIKIAYO KWA MASIKIO YAKO!! (MAMBO HAYO WANAYAFANYA WATOTO WACHANGA KATIKA KRISTO, NA WALE WATU WENYE TABIA YA MWILINI WASIOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU, WANAOMPINGA ROHO MTAKATIFU, NA WANAOMHUZUNISHA ROHO MTAKATIFU!! KWA NINI? TOFAUTI NA WATOTO WACHANGA, HAWA HAWATAKI KUKAA NDANI YA NENO NA NENO KUKAA NDANI YAO, HIVYO HAWAIFAHAMU KWELI NA HAWAKO HURU BADO KATIKA KRISTO!! USIPOKUWA HURU KATIKA KRISTO INA MAANA BADO UNAENENDA KWA SHERIA JUU YA SHERIA, AMRI JUU YA AMRI, NA KANUNI JUU YA KANUNI KWA MAANA WAMEKATAA RAHA ( REST) IPATIKANAYO KWA ROHO MTAKATIFU;
"10 Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo.
Isaya 28:10
12 ambao aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia.
Isaya 28:12
13 Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa."
Isaya 28:13
Biblia inasema,
2 Wakorintho 5:7
[7](Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)
(For we walk by faith, not by sight:)
>> MAAMUZI, MITIZAMO, NA MISIMAMO AMBAYO MISINGI NA VYANZO VYAKE NI YALE ULIYOYAONA NA UNAYOYAONA KWA MACHO, NA PIA YALE ULIYOYASIKIA NA UNAYOYASIKIA KWA MASIKIO, HUWA HAYATOKI KWA MUNGU!! YESU, TUMESOMA KWENYE ISAYA 11:3 KWAMBA KAMWE HAKUHUKUMU HUKUMU YA MACHO AU HUKUMU YA KUSIKIA!! MTU WA ROHONI, HALIKADHALIKA, HATAKIWI KUHUKUMU KUFUATIA YALE AYAONAYO NA YALE AYASIKIAYO SIKUZOTE!! ( JIHADHARI NA HABARI NA VIDEO ZA MITANDAONI)
1) NATHANIELI
47 Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.
Yohana 1:47
48 Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.
Yohana 1:48
>> YESU ALIMJUA NATHANIELI HATA KABLA HAJASHUHUDIWA HABARI ZAKE, MPAKA NATHANIEL MWENYEWE AKASHANGAA!! YESU HAKUSUBIRI MPAKA AKAE NAE, AMSIKIE HABARI ZAKE, AMUONE ANAVYOONGEA, N.K. NDIPO AMJUE, BALI ALIMJUA KUWA NI MWANAFUNZI WAKE TANGU AKIWA DHAMBINI NA HAJAKUTANA NAYE!
2) SAULI ( PAULO BAADAE)
10 Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.
Matendo ya Mitume 9:10
11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
Matendo ya Mitume 9:11
12 naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.
Matendo ya Mitume 9:12
13 Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;
Matendo ya Mitume 9:13
14 hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako.
Matendo ya Mitume 9:14
15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
Matendo ya Mitume 9:15
17 Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 9:17
>> YESU ANAMWAMBIA ANANIA KULE DAMESKI AENDE KUMWEKEA MIKONO SAULI APATE KUONA KULE NYUMBANI KWAKE YUDA, LAKINI YEYE ANAKATAA KWA KUWA INAJULIKANA KOTE KUWA SAULI ANAPINGA KUOKOKA, ANAWATESA NA KUWAFUNGA WALIOOKOKA, NA ALISIMAMIA KUUWAWA KWA STEPHANO, NA AMEKUJA DAMESKI KUENDELEA KULIHARIBU KANISA!!!
>> "15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli."
- YESU ANAMWAMBIA NENDA HUYU NI CHOMBO CHANGU KITEULE!!!! HUYU MNAYEMUONA NA KUSIKIA KUWA NI MUUAJI NI CHOMBO CHANGU KITEULE!! HUKUMU YA YESU ILIKUWA NI HUKUMU YA HAKI LAKINI ANANIA ALIKUWA NA HUKUMU YA KUSIKIA NA KUONA KWA MASIKIO NA MACHO!! ALIPOMWAMINI NA KUMTII BWANA WETU YESU HUKUMU YAKE IKABADILIKA NA KUWA YA HAKI NA SIYO YA MACHO NA MASIKIO TENA!! NDIPO AKAENDA NA KUMWEKEA MIKONO SAULI, AKAONA, NA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU!! NI WANGAPI UNAWAONA NI WATENDA DHAMBI KWA KUWATIZAMA KWA MACHO NA KUSIKIA TU HABARI ZAO MBAYA??!! YESU ALIMUONA PAULO NI MTAKATIFU NA MTUMISHI WAKE AKIWA ANALITESA NA KULIHARIBU KANISA!!! HII NDIYO HUKUMU YA HAKI!! HUKUMU YA MACHO ILIMKATAA SAULI MUUAJI!!
3) ZAKAYO MTOZA USHURU
>> SIKU ILE YESU ALIPOINGIA KULA NA KUNYWA NA KUSHINDA NYUMBANI MWA ZAKAYO MTOZA USHURU AMBAYE JAMII NZIMA ILIMJUA NA KUMUONA NI MTENDA DHAMBI, YESU ALIWAAMBIA;
5 Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako.
Luka 19:5
6 Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha.
Luka 19:6
7 Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi.
Luka 19:7
8 Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.
Luka 19:8
9 Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu.
Luka 19:9
10 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.
Luka 19:10
>> MSTARI WA SABA WANANUNG'UNIKA KWAMBA YESU AMEINGIA NA KUKAA NYUMBANI MWA MWENYE DHAMBI!! INA MAANA JAMII YOTE ILIMJUA NA KUMWONA ZAKAYO NI MTENDA DHAMBI!! LAKINI YESU ALIKUJA KUTAFUTA NA KUOKOA KILICHOPOTEA!! (MST 10 )
>> YESU AKAWAJIBU MAWAZO NA MANUNG'UNIKO YAO;
"........Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu."
Luka 19:9
>> HUYU NAYE NI MWANA WA IBRAHIMU!! NI YESU PEKE YAKE ALIYEKUWA ANAJUA KWAMBA YULE "MTENDA DHAMBI" WALIOMWONA JAMII YOTE HAFAI NI MWANA WA IBRAHIMU
>> NA KAMA NI MWANA WA IBRAHIMU ALISTAHILI NEEMA YA WOKOVU!!!;
>> WENYE HUKUMU YA MACHO HUWA WANAWAFUNGIA, WALE WALIOWAHUKUMU KWA HUKUMU YA MACHO NA MASIKIO, MILANGO YA MBINGUNI MAWAZONI NA MIOYONI MWAO, NA HIVYO KUTHIBITISHA KWAMBA WAO WENYEWE WAKO UPANDE WA SHETANI, WAMEDANGANYWA, NI VIPOFU WANAOPINGANA NA KWELI HUKU WAKIJIITA NI WENYE HAKI!!
>> JAMII ILIKUWA INAMUITA MTENDA DHAMBI, LAKINI YESU ALIKUWA ANAMUITA MWANA WA IBRAHIMU!! HUKUMU YA HAKI INAONA MAPENZI YA MUNGU! INAONA KINYUME NA TOFAUTI NA HALI ILIVYO AU KINACHOONEKANA KWA MACHO!!
4) MWANAMKE MSAMARIA
>> MWANAMKE HUYU MSAMARIA ALIKUWA NI KAHABA KWA MUJIBU WA YESU MAANA ALIKUWA ANAISHI NA MUME WA UZINZI, NA ALIKUWA AMESHAISHI NA WAUME WENGINE WATANO.
>> YESU ALIYAJUA HAYA SI KWA KUAMBIWA AU KWA KUONA!! BALI ALIFUNULIWA NA BABA YAKE KWA NENO LA MAARIFA!! ALIFUNULIWA KWA ROHO MTAKATIFU SIRI ZA MAISHA YA HUYU MWANAMKE MSAMARIA!! WALA HAKUHITAJI KUAMBIWA AU KUONA KWA MACHO HABARI ZA HUYU MWANAMKE MSAMARIA ( YOHANA 4:5-42) KAMA ISAYA ALIVYOTABIRI KWAMBA ITAKUWA!! WENYE HUKUMU YA MACHO NA YA MASIKIO WAMEPUNGUKIWA NA UTUKUFU WA MUNGU NA NDIYO MAANA WANATEGEMEA MACHO NA MASIKIO YAO ILI WAONE NA WAJUE KWAMBA HII NI DHAMBI. NA MARA ZOTE HAWAKO SAHIHI MAANA HAWAJASIKIA KWA YESU (NI VIZIWI) KWAMBA HAO WATU NI WAKE AU LA!! HAWANA UFUNUO WA ROHONI (NI VIPOFU) KUJUA KWELI KUHUSU HAO WANAOWAHUKUMU!!
>> NIMALIZE KWA MFANO HUU MAARUFU WA USALITI WA YUDA!
4) YUDA ISKARIOTE
>> YESU ALITEMBEA NA YUDA KWA MIAKA MITATU NA NUSU HUKU AKIMJUA KUWA NI WA SHETANI!! TENA HUYO YUDA ALIPEWA NA UWEKA HAZINA WA HUDUMA YA YESU!! NAYE ALIKUWA NI MPENDA FEDHA NA MWIZI ALIYEIBA KUTOKA KWENYE HUO MFUKO:
"4 Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema,
Yohana 12:4
5 Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini?
Yohana 12:5
6 Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo."
Yohana 12:6
>> LICHA YA KUMJUA YUDA HIVYO BWANA WETU YESU ALINYAMAZA KIMYA MPAKA WAKATI WA KUSULUBIWA KWAKE AMBAPO ALIMSEMA KWA FUMBO:
John 6:70
"[70]Jesus answered them, Have not I chosen you twelve, and one of you is a devil?
Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?"
>> HII NDIYO HUKUMU YA HAKI, HUKUMU INAYOANGALIA MOYONI KUNA roho YA NAMNA GANI!!
>> HUKUMU YA HAKI INAANGALIA PIA MPANGO NA KUSUDI LA MUNGU KWA MTU PASIPO KUANGALIA MUONEKANO WAKE WA NJE AU YALE ANAYOYATENDA KWA SASA!! KWA MTU WA IMANI SASA INAYOONEKANA NI DANGANYIFU NA ISIYODUMU; NA SASA INAYOSIKIKA SASA PIA NI DANGANYIFU!NA YA MUDA KITAMBO TU! YUDA ALIONEKANA ANAJALI MATUMIZI SAHIHI NA MAKINI YA FEDHA KUMBE FEDHA ILIKUWA INAMUUMA, MAANA ALIIITAMANI YEYE MWENYEWE AUZE MARHAMU NA KUIBA ILE FEDHA!!!
HUKUMU YA HAKI
2 Wakorintho 4:18
"[18]tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
While we look not at the things which are seen, but at the things which are not seen: for the things which are seen are temporal; but the things which are not seen are eternal."
>> HUKUMU YA HAKI MSINGI WAKE NI IMANI YA KWELI KWA YESU!!! IMANI YA KWELI KWA NENO LA UZIMA!! IMANI AMBAYO INAKUONDOA KWENYE KUTAZAMA WATU WALIVYO SASA, WANAVYOVAA SASA, WANAVYONENA SASA (USEMI WAO), WANAVYOJIPAMBA SASA, WANAVYOTENDA SASA, NA KIUJUMLA WANAVYOENENDA SASA, NA KISHA KUKUINGIZA KWENYE WALIVYO NA WANAVYOTENDA NA KUENENDA NDANI YA YESU KRISTO KATIKA KWELI YAKE KWA KUWA ULIWAOMBEA NA KUAMININI NA KUPOKEA WAKATI ULE ULE ULIPOKUWA UKIWAOMBEA!! ULIPOKEA BADILIKO LAO LA TABIA NA MWENENDO NDANI YA KRISTO YESU KATIKA ROHO MTAKATIFU!!
"16 Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena."
2 Wakorintho 5:16
>> HATUMJUI MTU AWAYE YOTE KWA JINSI YA MWILI
>> YAANI, HATUMTAMBUI NA KUMFAHAMU NA KUMJUA KWA VILE ALIVYO NA ANAVYOTENDA AU ANAVYOONEKANA SASA KWA JINSI YA MWILI, BALI TUNAMWONA KATIKA ROHO KAMA MTU TOFAUTI, ALIYEBADILIKA, NA ANAYEENENDA KATIKA KWELI. MAANA TUMEAMINI MAMBO YALIYO MEMA KUMHUSU YEYE!! TUNA TAARIFA ZA MBINGUNI KUMHUSU YEYE, AMBAZO NI TAARIFA ZA UPENDO!! ZILIZOTUFUNGUA MACHO YA UPENDO!! HATUNYOOSHI KIDOLE WALA KUHUKUMU!! TUNAUJUA MWISHO TANGU MWANZO MAANA ROHO NA NENO LAKE AMETUFUMBUA MACHO KUUJUA MWISHO TANGU MWANZO!! ANANIA ALIPOTOKA KUONGEA NA YESU, MOYONI MWAKE ALIKUWA ANAJUA SAULI AMEOKOKA, NA NI CHOMBO KITEULE CHA MUNGU!! ALIBEBA HUKUMU YA HAKI!!
>> KAMA KWELI UMEOMBA NA KUAMINI LAZIMA KAULI NA MTAZAMO WAKO KUHUSU WATU WALIVYO LEO, HALI ZILIVYO SASA NA MAMBO YALIVYO SASA VITABADILIKA!!! MAANA UMEOMBA, UMEAMINI, UMEPOKEA, UMESHUKURU, NA SASA UNAKIRI/UNASHUHUDIA/ UNATAMKA/ UNATANGAZA/ NA UNANENA "YALE MAJIBU YA NENO" ULIYOYAPOKEA TAYARI WAKATI ULE ULE ULIPOKUWA UKIOMBA NA KUSALI KAMA MAANDIKO YANENAVYO:
"24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu."
Marko 11:24
>> NA TENA;
"14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
1 Yohana 5:14
"15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba."
1 Yohana 5:15
>> KAMA UNAYAJUA KWELI MAPENZI YA MUNGU KWENYE NENO LAKE, PALE UNAPOONA WATU KWA NJE WANATENDA NA KUENENDA KINYUME NA NENO AU KWELI HIYO, JE! UNAUGUA, NA KULIA, NA KUOMBOLEZA KWA AJILI YAO??!! AU UNAANZA KUSEMA HAWA NI WATENDA DHAMBI AMBAO HAWATAINGIA MBINGUNI??!! KAMA HAUWALILII WEWE NI MUOVU ZAIDI KULIKO WAO MAANA UNAWAFUNGIA MLANGO WA MBINGUNI KWA CHUKI NA UBINAFSI WAKO BADALA YA HURUMA NA UPENDO WA KRISTO!
>> LAZIMA, KAMA KWELI UNAAMINI,
1) UWAONE WASIOOKOKA WAKIWA WAMEOKOKA
2) WANAOUGUA WAKIWA WAMEPONA
3) MASKINI WAKIWA MATAJIRI
4) DHAIFU WA IMANI WAKIWA NA IMANI THABITI NA IMARA KWA KRISTO
5) WALIORUDI NYUMA NA KUPOA WAKIWA WAMETUBU NA KUREJEA KWA YESU NA WAKIWA MOTO NDANI YAKE!!
6) WASIOJAZWA ROHO WAKIWA WAMEJAZWA ROHO MTAKATIFU NA IMANI
7) WALIO TASA KIROHO NA WALIODUMAA WAKIWA WANAMZALIA MUNGU MATUNDA NA WAMEJAA ROHO NA WANAKUA KIROHO
8) WALIO MABAHILI NA WACHOYO WAKIWA WAKARIMU NA WATOAJI HODARI WALIOJITOA NA KUJIWEKA WAKFU KWA BWANA!!
9) WALIO TASA WAKIWA WANALEA WATOTO WENGI WA KIKE NA KIUME
10) VIPOFU WAKIWA WANAONA, VIZIWI WAKIWA WANASIKIA, VIWETE WANA RUKARUKA, MABUBU WAKISEMA, WAFU WAKIFUFUKA, KANISA LISILOONGEZEKA LIKIWA LIMEJAA KIASI CHA WATEULE KUTOENEA NDANI YAKE, N.K.
- HII NDIYO HUKUMU YA HAKI YA MTU ANAYEAMINI!! HUKUMU YA MACHO NI DHAMBI KWA KUWA IMEANDIKWA,
Proverbs 17:15
"[15]He that justifieth the wicked, and he that condemneth the just, even they both are abomination to the LORD.
Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA."
>> PETRO ALIWAITA WATU WA MATAIFA " NAJISI" (MATENDO YA MITUME 10:9-15), NA BWANA YESU AKAMKEMEA,
"15 Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi."
Matendo ya Mitume 10:15
>> KWA NENO HILO PETRO ALIINGIA KWA WATU WA MATAIFA AKINA KORNELIO NA KULA NAO, NAO WAKAOKOKA, NA KUPOKEA PIA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU, NA KISHA WAKABATIZWA WOTE!!
>> PETRO ALIINGIA NYUMBANI MWA KORNELIO AKIWA MWENYE HUKUMU YA HAKI BAADA YA KUSIKIA KWA YESU!! VINGINEVYO ASINGEKWENDA KAMWE KWA WATU WA MATAIFA KUHUBIRI HABARI NJEMA!!!
>> USIWAITE WATAKATIFU NI WATENDA DHAMBI, NA USIWAITE WATENDA DHAMBI KUWA NI WENYE HAKI, HUO WOTE NI UOVU MBELE ZA MUNGU!!
>> USIHUKUMU HUKUMU YA MACHO HUO NAO NI UOVU MBELE ZA MUNGU!!
>> USIWAFUNGIE WATU MILANGO YA MBINGUNI KWA KUSEMA HAWATOINGIA HUMO KWA SABABU YA KUZIFUATA AKILI ZAKO NA MACHO NA MASIKIO YAKO, HUO NAO NI UOVU, MAANA UNAJIFUNGIA MWENYEWE MILANGO YA MBINGUNI KWA KUJIFANYA HAKIMU,
11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
Yakobo 4:11
12 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?
Yakobo 4:12
>> WEWE UMEWEKWA UWE KUHANI KWA MUNGU NDANI YA KRISTO YESU,
5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
1 Petro 2:5
7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
1 Petro 2:7
9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
1 Petro 2:9
>> KAMA KUHANI NENDA MBELE ZA MUNGU NA UTIMIZE MAJUKUMU YAKO YA KIKUHANI!! WAOMBEE HAO WOTE UNAOWAONA NI WATENDA DHAMBI AMBAO UNADAI HAWATAINGIA MBINGUNI!! TUBU KWANZA KWA KUHUKUMU NA KISHA UWAOMBEE KWA MACHOZI!! KAMA HUWEZI KUWAOMBEA NA KUMWAMINI MUNGU KWA AJILI YA MKEO, MUMEO, WANAO, NDUGUZO NA WALE WA MUMEO NA MKEO, MAJIRANI, KAZINI KWAKO, WASHIRIKA WAKO, SHULENI NA CHUONI KWAKO, KANISANI KWAKO, MWILI WA KRISTO NA TAIFA LAKO, WEWE NI MTENDA DHAMBI MTOA VIBANZI ASIYESHUGHULIKA NA BORITI MACHONI MWAKO MWENYEWE!! TUBU USIJEANGAMIA!!
"7 Lakini mimi, nitamtazamia Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.
Mika 7:7
8 Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, Bwana atakuwa nuru kwangu.
Mika 7:8
9 Nitaivumilia ghadhabu ya Bwana, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea teto langu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.
Mika 7:9
10 Ndipo adui yangu ataliona jambo hilo, na aibu itamfunika, yeye aliyeniambia, Yuko wapi Bwana, Mungu wako? Macho yangu yatamtazama; sasa atakanyagwa kama matope ya njia kuu."
Mika 7:10
Tags
MAFUNDISHO