1) MAANA YA IMANI
1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Waebrania 11:1
Amplified Bible (Hebrews 11:1)
Now faith is the assurance (title deed, confirmation) of things hoped for (divinely guaranteed), and the evidence of things not seen [the conviction of their reality—faith comprehends as fact what cannot be experienced by the physical senses].
>> IMANI NI KULE KUWA NA UHAKIKA MOYONI MWAKO(rohoni mwako) WA MAMBO YALE YOTE UNAYOYATARAJIA KATIKA MUNGU; NI KULE KUWA NA USHAHIDI MOYONI MWAKO WA MAMBO YALE YASIYOONEKANA!! YAANI.,
>> NI ULE "UHAKIKA" WA MATARAJIO YAKO YOTE KATIKA MUNGU: UHAKIKA WA KUWA NAYO, UHAKIKA WA KUYAPATA, UHAKIKA WA KUJA KWA HAYO UNAYOYATARAJIA, UHAKIKA WA KUTENDEWA NA MUNGU, UHAKIKA WA KUTETEWA, UHAKIKA WA ULINZI, UHAKIKA WA KUFAULU, UHAKIKA WA KUPATA FAIDA, UHAKIKA WA KUPATA MTOTO, UHAKIKA WA KUOA, UHAKIKA WA KUOLEWA, UHAKIKA WA KUKAMILISHA KAZI ALIYOKUPA BWANA, UHAKIKA WA BADILIKO LA TABIA ZAKO, ZA MUMEO, ZA MKEO, ZA NDUGUZO, ZA WANAO, UHAKIKA WA KUPONA, UHAKIKA WA KUPATA CHANZO CHA MAPATO, UHAKIKA WA [ NINI UNATARAJIA KATIKA MUNGU??!!]
A) KWENYE SEHEMU HII YA KWANZA YA TAFSIRI HII NENO KUU NI UHAKIKA!!
>> UKIAMINI UNAKUWA NA UHAKIKA HATA KAMA MAMBO YANAONEKANA KUKWAMA, KUHARIBIKA, KUWA MAGUMU, KUCHELEWA, AU MAUMIVU KUONGEZEKA, N.K HAYA YOTE LAZIMA YAJE ILI KUIJARIBU NA KUIPIMA IMANI YAKO KAMA BADO UNA UHAKIKA AU LA!!
>> UKIPOTEZA UHAKIKA HOFU INAINGIA, WOGA UNAINGIA, WASIWASI UNAINGIA, KUSUMBUKA KUNAINGIA, KUBABAIKA KUNAINGIA, KUHANGAIKA KUNAINGIA, PAPARA INAINGIA, KUJIPIGANIA KIBINADAMU KUNAINGIA, N.K.
>> MUNGU AMETULETEA IMANI YA YESU ILI TUWE NA UHAKIKA WA KESHO YETU KATIKA MAISHA
>> LAKINI PIA IMANI INATUONDOA KWENYE KUANGALIA HALI NGUMU AU MAZINGIRA MAGUMU TULIYOMO, NA KUTUFUMBUA MACHO YA KUTAZAMA NA KUYAONA YASIYOKUWEPO SASA LAKINI HAKIKA NI YETU NA YANAKUJA!!
B) SEHEMU YA PILI YA TAFSIRI YA ANDIKO LETU NI KULE KUWA NA USHAHIDI (EVIDENCE)AU HATI MILIKI (TITLE DEED) MOYONI MWAKO YA MAMBO YALE YASIYOONEKANA BADO!!
>> HAYAONEKANI LAKINI WEWE UNAYO TAYARI, HAYAONEKANI LAKINI TAYARI NI YAKO WEWE!! HAPA IMANI INAKUINGIZA KWENYE UMILIKI WA VISIVYOONEKANA NA VISIVYOKUWEPO BADO KWA JINSI YA MWILI!!
>> HAPA IMANI INAKUINGIZA KATIKA HALI YA [HUNA- UNAVYO] YAANI, UNAVYO VYOTE USIVYOKUWANAVYO KWA KUWA UMEAMINI!! UNA KAZI UKIWA HUNA KAZI, UNA HELA UKIWA MASKINI, UMEPONA UKIWA UNAUGUA NA MAUMIVU UNAYO AU DAKTARI KAKUPIMA NA KASEMA UNA HIKI AU KILE, LAKINI WEWE UMEPONA KWA KUWA UNAMILIKI UPONYAJI USIOONEKANA KWA MACHO BADO, UMEFANIKIWA UKIWA MASKINI BADO, UMEJENGA NYUMBA UKIWA UNADAIWA KODI KWENYE VYUMBA VIWILI ULIVYOPANGA, MUMEO AU MKEO AMEOKOKA AKIWA MLEVI AU MGOMVI BADO, WANAO NI WACHA MUNGU WAKIWA WAASI BADO, UMEFANIKIWA UKIWA UNASHINDWA BADO, UNAWEZA UKIWA HUWEZI BADO KWA KUWA UMEAMINI, MAMBO NI MEPESI YAKIWA MAGUMU BADO, N.K.
>> KWA HIYO IMANI INAKUPA UHAKIKA WA MATARAJIO YAKO YOTE NA HATI MILIKI AU USHAHIDI WA KUWA NAVYO AMA UMILIKI WA VYOTE VISIVYOONEKANA BADO
>> IMANI INAKUUNGANISHA NA KESHO YAKO KATIKA MUNGU NA KUKUFANYA UIONE KAMA MUNGU ANAVYOIONA KWA KUWA UMEIONA KWA MACHO YA NENO LA MUNGU!! NENO LA MUNGU LINAKUFUMBUA MACHO SABA YA MUNGU MOYONI MWAKO
Zekaria 4:10
[10]Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya BWANA; yapiga mbio huko na huko duniani mwote.
For who hath despised the day of small things? for they shall rejoice, and shall see the plummet in the hand of Zerubbabel with those seven; they are the eyes of the LORD, which run to and fro through the whole earth.
2) UMUHIMU WA KUSIMAMIA IMANI ULIYONAYO
>> Kabla ya kusema lolote hapa nikumbushe kwamba;
Warumi 10:17
[17]Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
So then faith cometh by hearing, and hearing by the word of God.
>> Imani chanzo chake ni kusikia; na huko kusikia huja kwa neno la Kristo!! Imani inatoka wapi? Imani inazaliwaje?
1) IMANI INATOKANA NA KUSIKIA
2) LAZIMA ULISIKIE NENO LA MUNGU MOYONI MWAKO
3) HAPO NDIPO TUNASEMA UMEAMINI, MAANA IMANI IMEZALIWA NDANI YAKO!
4) PASIPO NENO LA KRISTO AMBALO NDILO NENO LA MUNGU, HAKUNA IMANI INAYOWEZA KUZALIWA NDANI YAKO!!
Ezekieli 2:2
[2]Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami.
And the spirit entered into me when he spake unto me, and set me upon my feet, that I heard him that spake unto me.
1) Mungu anaposema nawe neno lake
2) Huwa roho ya hilo neno inakuingia rohoni(moyoni) mwako
3) Hiyo roho ya hilo neno ulilolisikia ndiyo inayokufungua masikio yaliyo ndani yako
4) Ndipo unamsikia Yeye aliyesema nawe moyoni mwako(rohoni mwako) Mungu ni Roho nawe unamsikia kwa roho yako!!
5) Kuamini maana yake umemsikia Mungu sauti yake kupitia ile roho ya lile neno iliyokuingia na kuzaa imani ndani yako
>> Imani inakuunganisha na Mungu katika roho, kwa sababu roho yako inaungana na roho ya Neno ambaye ni Mungu
Imani = roho yako + roho ya Neno na nguvu zake!!
>> Ukiamini huwezi kushindwa, ukiamini huwezi kuchoka, ukiamini huwezi kuogopa, ukiamini unafanana na Yesu ambaye ni Neno Aliye Hai mwenye uzima wa milele!!
>> Imani inakuunganisha na Uungu wa Mungu, na nguvu zake, na utukufu wake!!
3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
2 Petro 1:3
4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
2 Petro 1:4
>> IMANI INAKUWEKA KWENYE DARAJA LA UUNGU NA UTUKUFU WAKE AMBAPO HAKUNA LISILOWEZEKANA KWAKO TENA!!
23 Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.
Marko 9:23
>> HUU NDIO UMUHIMU MKUU WA KUSIMAMIA IMANI YAKO ULIYONAYO
☆☆☆KUSIMAMA KWAKO KWA IMANI KUNAKUFANYA UWE MSHINDI JUU YA ULIMWENGU NA JUU YA MKUU WA ULIMWENGU HUU☆☆☆
A) USHINDI DHIDI YA ULIMWENGU
1 Yohana 5:4
[4]Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
For whatsoever is born of God overcometh the world: and this is the victory that overcometh the world, even our faith.
>> HUKU NDIKO KUSHINDA KUUSHINDAKO ULIMWENGU HIYO IMANI YETU!!
B) USHINDI DHIDI YA MKUU WA ULIMWENGU HUU ( SHETANI)
John 14:30
[30]Hereafter I will not talk much with you: for the prince of this world cometh, and hath nothing in me.
Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.
YOHANA 14:30 (TAFSIRI KADHAA)
New International Version
"I will not say much more to you, for the prince of this world is coming. He has no hold over me,"
New Living Translation
“I don’t have much more time to talk to you, because the ruler of this world approaches. He has no power over me,"
English Standard Version
"I will no longer talk much with you, for the ruler of this world is coming. He has no claim on me"
>> UKISIMAMA KWA IMANI MKUU WA ULIMWENGU HUU HAKUWEZI KWENYE ENEO LOLOTE WALA MITEGO NA HILA ZAKE ZOTE HAZIWEZI KUFUA DAFU KWAKO!!
>> YAANI, MIFUMO YOTE YA UOVU YA ULIMWENGU HUU YA KIFEDHA, KIBIASHARA, KIUCHUMI, KIIMANI, KIUTAWALA NA KISERIKALI, KIUTAMADUNI, KISIASA, KIMADHEHEBU, N.K. HAIWEZI KUKUNASA WALA KUKUSHINDA!!!
Warumi 11:19-21
[19]Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi.
Thou wilt say then, The branches were broken off, that I might be graffed in.
[20]Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.
Well; because of unbelief they were broken off, and thou standest by faith. Be not highminded, but fear:
[21]Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.
For if God spared not the natural branches, take heed lest he also spare not thee.
>> USIPOSIMAMIA IMANI YAKO LAZIMA UTAKATWA KUTOKA KWENYE MWILI WA KRISTO!! KWA MAANA PASIPO IMANI HAIWEZEKANI KUMPENDEZA MUNGU (WAEBRANIA 11:6)
3) MAJARIBU YA IMANI TUNAYOYAPITIA
Biblia inasema,
"6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
1 Petro 1:6
7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo."
1 Petro 1:7
>> MAJARIBU YA NAMNA MBALIMBALI ANAYOYAPITIA MTAKATIFU KATIKA NYAKATI MBALIMBALI ZA MAISHA YAKE, HUWA YANARUHUSIWA KWA LENGO LA KUIJARIBU IMANI YAKE!!
1) Kwamba ni kweli unaamini?
2) Kama kweli unaamini hebu tuone katika hili utasemaje!! (maneno ya kinywa chako)
- kama unasema umepona hebu tulete maumivu au dalili, za ugonjwa ili tuone utasemaje!! Shetani ndiye mjaribu!!
- kama unasema umebarikiwa hebu tulete dhiki, shida, uhitaji, kupungukiwa, kuishiwa, n.k. ili tuone utasemaje!!
>> UNASEMA NINI? UNAKIRI NINI? UNATAMKA NINI? NA UNAONGEA NINI PALE MAMBO YANAPOONEKANA KUHARIBIKA, AU KWENDA KINYUME NAWE, AU KUKWAMA, AU KUVURUGIKA?
Biblia inasema,
Warumi 10:10
[10]Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
For with the heart man believeth unto righteousness; and with the mouth confession is made unto salvation.
>> KWA MOYO MTU HUAMINI NA KWA KINYWA MTU HUKIRI!! IMANI MOYONI, UKIRI KINYWANI!!
Na maandiko yanasema kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake (Mathayo 12:34)
>> KINYWA CHA MTAKATIFU KINATAKIWA KUKIRI, KUTAMKA, KUONGEA, KUSEMA, KUTANGAZA, KUAMURU, NA KUSHUHUDIA LILE NENO ULILOLIAMINI MOYONI MWAKO, NA SIYO HALI MBAYA ZA UZIONAZO, MAZINGIRA MAGUMU ULIYOMO, MAUMIVU ULIYONAYO, UVIMBE AU NGOZI ILIYOHARIBIKA ULIYONAYO, UPINZANI UNAOKUKABILI, MATESO UNAYOYAPITIA, N.K.
>> HUWEZI KAMWE KUSEMA HIVI KAMA HUJAAMINI KWA KUWA LILE NENO HALIMO MOYONI MWAKO!! TULISEMA UKIAMINI, LILE NENO ULILOLIAMINI LINAKAA NDANI YAKO KAMA roho! NA HIVYO KINYWA CHAKO HUONGEA NENO LA IMANI ILIYOMO MOYONI MWAKO!
Bwana wetu Yesu Alimshinda shetani namna hii: KILA ALIPOLETA JARIBU ALIMWAMBIA, "IMEANDIKWA!!"
1) 4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Mathayo 4:4
2) 7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Mathayo 4:7
3) 10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Mathayo 4:10
>> KILA NENO ALILOLISEMA YESU KUMSHINDA SHETANI LILIKUWA LIMEANDIKWA SI TU KWENYE GOMBO LA CHUO BALI KWENYE KIBAO CHA MOYO WAKE KWA MOTO WA ROHO MTAKATIFU, NALO LILITOKA KAMA UPANGA WA MOTO AMBAO NI SILAHA YA KUMSHINDA SHETANI (Efe 6:10-17)
>> NA KWA WEWE UAMINIYE NI VIVYO HIVYO PIA!! LILE NENO LITOKALO KWA IMANI KINYWANI MWAKO NI MOTO WA ROHO MTAKATIFU!!
>> USHINDI DHIDI YA SHETANI KWENYE MAJARIBU UNATAKA IMANI ILIYO HAI!!
>> LAKINI SI IMANI PEKE YAKE!!
11 Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho;
Waebrania 6:11
12 ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.
Waebrania 6:12
13 Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,
Waebrania 6:13
14 akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza.
Waebrania 6:14
15 Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.
Waebrania 6:15
>> MST WA 12: KURITHI AHADI KUNAHITAJI IMANI NA UVUMILIVU
>> MST WA 15: IBRAHIMU ALIIPATA ILE AHADI KWA IMANI NA UVUMILIVU
HII NDIYO KANUNI YA USHINDI YA KIBIBLIA: IMANI + UVUMILIVU
[KUPOKEA AHADI ZA MUNGU = IMANI + UVUMILIVU ]
>> UKIKOSA IMANI HALAFU UKAKOSA UVUMILIVU UTAHAHA KUTOKA KWA MTUME HUYU HADI MTUME HUYU, NABII HUYU HADI NABII YULE, KANISA HILI HADI KANISA LILE, LAKINI HUTAPOKEA KUTOKA KWA MUNGU BALI UTAINGIWA NA roho zidanganyazo NA KUZIDI KUHARIBIKIWA!!
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
Yakobo 1:6
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
Yakobo 1:7
8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.
Yakobo 1:8
>> UNAOMBA SANA LAKINI HUOMBI KWA IMANI
4) KUJIBIWA MAOMBI YA IMANI
>> BWANA WETU YESU KRISTO AMETUPATIA KANUNI YA IMANI AMBAYO, TUKIITUMIA VEMA ITAKIWAVYO, TUNAWEZA KUPOKEA KILA TUKIOMBACHO KWAKE AU KWA JINA LAKE!! Biblia inasema,
Marko 11:24
[24]Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Therefore I say unto you, What things soever ye desire, when ye pray, believe that ye receive them, and ye shall have them.
>> KANUNI YA MAANDIKO: " YOYOTE MYAOMBAYO, MNAPOSALI, AMININI KWAMBA MNAYAPOKEA, NDIPO YATAKUWA YENU."
1) UNAPOKUWA MBELE ZA MUNGU KWENYE SALA ZAKO UKIOMBA
2) LAZIMA UAMINI KWAMBA, YALE YOTE UNAYOYAPELEKA MBELE ZAKE, UNAYAPOKEA WAKATI ULE ULE UNAPOSALI UKIOMBA!! YAANI, MAJIBU UNAYAPOKEA PALE PALE NA WAKATI ULE ULE WA SALA ZAKO NA MAOMBI!!
3) UKIAMINI UMEPOKEA NDIPO YOTE ULIYOYAOMBA YATAKUWA YAKO!!
>> HII INA MAANA KWA SISI TUAMINIO TUNAPOKWENDA MBELE ZA MUNGU KUSALI NA KUOMBA, HUWA TUNAKWENDA KUPOKEA HAJA ZOTE ZA MIOYO YETU
>> HIVYO TUTAMALIZA SALA NA MAOMBI YETU KWA KUMSHUKURU MUNGU KWAMBA TUMEPOKEA HAJA ZOTE ZA MIOYO YETU!!
>> HII MAANA YAKE USIPOPOKEA WAKATI WA KUSALI NA KUOMBA HAUTAPOKEA TENA KWA KUWA UMEVUNJA KANUNI KUU YA IMANI YA KUPOKELEA HAJA ZA MOYO WAKO KUTOKA KWA MUNGU!!
KWA NINI IKO HIVI?
>> NI KWA SABABU MUNGU ALISHASEMA TANGU ZAMANI KWAMBA;
"Isaya 65:24
[24]Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.
And it shall come to pass, that before they call, I will answer; and while they are yet speaking, I will hear."
1) MUNGU ANATUJIBU WATOTO WAKE HATA KABLA HATUJAOMBA
2) NA TUNAPOKUWA KATIKA KUNENA MBELE ZAKE KWENYE SALA NA MAOMBI ANATUSIKIA!!
INAKUWAJE HII?!
>> KWANZA AMESEMA ANAJUA TUNAYOYAHITAJI HATA KABLA HATUJAMWOMBA (MATHAYO 6:8)
>> PILI, ROHO WAKE ANATUONGOZA KWENYE KUOMBA SAWASAWA NA ANAVYOTAKA NA ANAVYOPENDA YEYE, HIVYO KUJIBIWA NA KUPOKEA KWETU KUTOKA KWAKE NI UHAKIKA TANGU KABLA HATA HATUJAZALIWA!! TULIOOKOKA TUMEJIBIWA MAOMBI YETU!! TUMEJIBIWA HATA KABLA HATUJAOMBA!! NDIYO MAANA TUNAPOKUWA TUNAOMBA TUKISALI ANATUSIKIA!!
>> KANUNI HII YA KIMAANDIKO IMETHIBITISHWA NA ROHO MTAKATIFU KIMAANDIKO HAPA:
1 Yohana 5:14-15
[14]Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
And this is the confidence that we have in him, that, if we ask any thing according to his will, he heareth us:
[15]Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.
And if we know that he hear us, whatsoever we ask, we know that we have the petitions that we desired of him.
1) TUNA UJASIRI MKUBWA TUNAPOKWENDA MBELE ZA MUNGU BABA YETU KWA JINA LAKE YESU KRISTO BWANA WETU
2) HII NI KWA SABABU TUNAKWENDA KUOMBA KATIKA KUSALI KWETU SAWASAWA NA MAPENZI YAKE KWA KUSAIDIWA NA ROHO WAKE ALIYETUPA!!
26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Warumi 8:26
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Warumi 8:27
>> KWA NINI TUSIWE NA UJASIRI WAKATI ROHO ANATUOMBEA VILE APENDAVYO MUNGU NA HIVYO KUWA NA UHAKIKA WA KUPOKEA KILA TUKIOMBACHO??!!
A) 1 YOHANA 5:14
>> TUNAOMBA SAWASAWA NA MAPENZI YAKE NA YEYE ANATUSIKIA
B) 1 YOHANA 5:15
>> TUNAJUA KWAMBA ANATUSIKIA NA HIVYO TUNAJUA KWAMBA TUNAZO ZILE HAJA TULIZOMWOMBA
C) TUNASHUKURU NA KUONDOKA TUKIWA NA KILA HAJA TULIYOMWOMBA!!
>> KUOMBA HUKU KWA IMANI NDIKO KUNAKOTUPATIA HAJA NA MAHITAJI YETU YOTE, NA NDIKO KUNAKOONDOA UHITAJI MAISHANI MWETU!!
1) Zaburi 23:1
[1]BWANA ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
(A Psalm of David.) The LORD is my shepherd; I shall not want.
>> SIPUNGUKIWI WALA SIHITAJI MAANA NINAZO HAJA ZOTE NILIZOOMBA!!
2) Zaburi 34:9-10
[9]Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake,
Yaani, wamchao hawahitaji kitu.
O fear the LORD, ye his saints: for there is no want to them that fear him.
[10]Wana-simba hutindikiwa, huona njaa;
Bali wamtafutao BWANA hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.
The young lions do lack, and suffer hunger: but they that seek the LORD shall not want any good thing.
>> SIHITAJI KITU CHOCHOTE KILICHO CHEMA MAANA NAMCHA NA KUMTAFUTA BWANA SIKUZOTE (NATAFUTA YALE YALIYO JUU, YASIYOHARIBIKA, ALIKO KRISTO, AMEKETI MKONO WA KUUME WA MUNGU (WAKOLOSAI 3:1-4)
>> HATA WATOTO WA SIMBA HUISHIWA LAKINI MIMI SIISHIWI MAANA NIMEOMBA NA KUMWAMINI BWANA WETU YESU!!
>> JE! BADO UNASUBIRI MAJIBU??!! BILA SHAKA HAUAMINI!!
>> LAZIMA UAMINI HIVI ILI UWE NA MSINGI IMARA WA KUISHINDANIA IMANI YAKO TAKATIFU SANA (YUDA MST 3) MAANA KUSHINDANA KWAKO SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME, MAMLAKA, WAKUU WA GIZA, NA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO (WAEFESO 6:12)
>> KWA SABABU KILA UNACHOSEMA, UNACHOKIRI, UNACHOTAMKA, UNACHOTANGAZA, NA UNACHOSHUKURU KWA IMANI KWAMBA UNACHO, SHETANI ATAKUPINGA SANA KWA KULETA KINYUME CHAKE!!
● ATALETA UMASKINI KINYUME NA UTAJIRI
● ATALETA UHITAJI, KUPUNGUKIWA, NA KUISHIWA, KINYUME NA UTELE
● ATALETA DALILI ZA MAGONJWA NA MAUMIVU, KINYUME NA UPONYAJI NA AFYA
● ATALETA TABIA ZA HOVYO KINYUME NA KWELI KWA MKEO, MUMEO, WANAO, NA KANISANI KINYUME NA UTAKATIFU, KICHO, UNYENYEKEVU, HAKI, NA KWELI!!
● ATALETA DALILI ZOTE ZA KUSHINDWA KINYUME NA MIPENYO ( BREAK-THROUGHS)
● ATALETA UKAME KIROHO KINYUME NA BUBUJIKO LA ROHO NA MMWAGIKO WA ROHO MTAKATIFU
● ATALETA KUKATALIWA BADALA YA KUKUBALIWA, KUSAHAULIWA BADALA YA KUKUMBUKWA, MKWAMO BADALA LA MWENDELEZO, MAMBO KUHARIBIKA BADALA YA MAMBO KUNYOOKA, GIZA BADALA YA NURU, UASI BADALA YA UTII, KUCHUKIWA BADALA YA KUPENDWA, N.K.
>> HAPA NDIPO PENYE VITA VYA KIROHO MAANA IBILISI ANATAKA KUKUNYANG'ANYA KILE ULICHONACHO TAYARI!!
● ATATAKA KUKUONYESHA KUWA HUNA NA KWAMBA UTAPATA SIKU ISIYO NA JINA ILI KUKUCHOSHA NA KUKUKATISHA TAMAA!!
>> VAA SILAHA ZOTE UPAMBANE BILA KUSAHAU,
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Waefeso 6:16
>> NGAO YA IMANI, NGAO YA IMANI, NGAO YA IMANI
>> HII ITAKUKINGA NA MISHALE YENYE KUJERUHI, KUUMIZA, NA KUDHURU, YA SHETANI!!!
10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
Waefeso 6:10
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Waefeso 6:11
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Waefeso 6:12
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Waefeso 6:13
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
Waefeso 6:14
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
Waefeso 6:15
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Waefeso 6:16
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
Waefeso 6:17
18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Waefeso 6:18
5) JINSI YA KUOMBA
●1 Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.
Luka 11:1
>> MWANAFUNZI HUYU ALIMWOMBA YESU AWAFUNDIASHE JINSI YA KUSALI:
>> INAYOFUATA HAPA NI PRAYER SKELETON ( MUUNDO AU MFANO WA AU MIFUPA YA MAOMBI) AMBAYO INATAKIWA KUJAZIA NYAMA
● 2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]
Luka 11:2
>> MAOMBI YANAPELEKWA KWA BABA YETU WA MBINGUNI KWA JINA LA YESU
>> YESU NI JINA LA BABA YETU LINALOTAKIWA KUTUKUZWA NA KUINULIWA UNAPOANZA MAOMBI YAKO. HII NI HATUA YA KUMTUKUZA MUNGU NA BWANA WETU YESU KWA WEMA WAKE WA AJABU NA UPENDO WAKE MKUU KWETU!!
>> BAADA YA HAPO UNAINGIA KWENYE MAMBO YANAYOHUSU UFALME WAKE HAPA ULIMWENGUNI, KWENYE MAISHA YAKO KILA SIKU, NA TAIFA LAKO!!
>> KISHA UNAINGIA KWENYE ENEO LA MAPENZI YAKE KUFANYIKA HAPA DUNIANI KAMA ILIVYO MBINGUNI
>> MAOMBI HAYA YAMEKWISHA KUJIBIWA MAANA YAMEGUSA MPANGO NA MAKUSUDI YA MUNGU KWAKO, KWA KANISA, NA ULIMWENGUNI!!
●3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
Luka 11:3
>> HILI NI ENEO LA KUMTWIKA MUNGU FADHAA ZAKO ZOTE KAMA ANDIKO LISEMAVYO, "6 Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
1 Petro 5:6
7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu."
1 Petro 5:7
>> NI ENEO LA KUPELEKA HAJA ZAKO ZA SIKU KWA SIKU MBELE ZAKE ( WAEFESO 4:4-6)
>> MUNGU ANAJALI SANA MAISHA YAKO NA ANATAKA UMWAMBIE! UJUE KWAMBA YEYE NI BABA YAKO ANAYEKUPENDA NA ANAYESHUGHULIKA SANA NA MAISHA YAKO. ANAPENDA USHIRIKA NA WEWE! ANATAKA SANA URAFIKI NA WEWE! SEMEZANA NAYE MARA KWA MARA ĶWENYE KUOMBA KWAKO.
● 4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].
Luka 11:4
>> HII NI KANUNI YA KUTUBU NA KUJITAKASA MBELE ZA MUNGU MTAKATIFU!! LAZIMA UWE UMESAMEHE VINGINEVYO HAUTASAMEHEWA KAMWE!!( KWA KUWA NA WEWE PIA UNAWAKOSEA WENGINE NA MUNGU PIA) KUTOSAMEHE NI KIKWAZO CHA MAOMBI KIKUU!! MOYO WENYE UCHUNGU HAUWEZI KUOMBA!! UCHUNGU NI CHUKI, NI UADUI, NI MAUTI!!
● 5 Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu,
Luka 11:5
6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake;
Luka 11:6
7 na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?
Luka 11:7
8 Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.
Luka 11:8
>> MSTARI WA 5-8 UNAFUNUA KANUNI YA KUOMBA PASIPO KUKATA TAMAA AMA KUOMBA KWA KUNG'ANG'ANIA MPAKA UPATE AU UPOKEE UNACHOKITAKA!! MUNGU ANAPENDA IMANI YENYE UBISHI (STUBBORN FAITH) ISIYOKATA TAMAA WALA ISIYOKUBALI JIBU LA HAPANA! MAANA KAMA UNAYAJUA MAPENZI YA MUNGU KIUHAKIKA KUPITIA NENO LAKE HAKUNA SABABU KWA NINI USIPOKEE HAJA YA MOYO WAKO!! UNA SABABU YA KUNG'ANG'ANIA MPAKA MWISHO KAMA HUU MFANO UNAVYOELEZA!!
● 9 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
Luka 11:9
>> OMBA! KAMA HUONI, TAFUTA! KAMA HUONI, BISHA!!
>> KUNA UTAKAVYOVIPATA UKIOMBA; KUNA UTAKAVYOVIPATA KWA KUVITAFUTA; NA KUNA UTAKAVYOVIPATA KWA KUBISHA!!
>> WENGI HAWAELEWI KWA NINI HUWA HAWAPATI WAYATAKAYO, LAKINI NI KWA SABABU YA KUKATA TAMAA MAPEMA AMA KUVUNJIKA MOYO!!
● 10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Luka 11:10
>> HILI NI HAKIKISHO LA KUPOKEA HAJA ZA MOYO WAKO KUPITIA NGAZI HIZI TATU ZA MAOMBI
● 11 Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
Luka 11:11
12 Au akimwomba yai, atampa nge?
Luka 11:12
>> MISTARI YA 11 NA 12 ANAKUELEZA KWAMBA UKIOMBA ROHO MTAKATIFU MUNGU ATAKUPA ILI AKUSAIDIE KUOMBA SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU
●13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
Luka 11:13
>> OMBA ROHO MTAKATIFU NA UTAPEWA!! OMBA NA MUNGU ATAKUPA ROHO MTAKATIFU!! ROHO MTAKATIFU NDIYE ANAYEKUFUNDISHA:
1) JINSI YA KUOMBA
2) LINI UOMBE
3) NINI UKIOMBEE, NAYE ATAKUKUMBUSHA MAANDIKO YA KUTUMIA KWENYE MAOMBI
4) KIVIPI UKIOMBEE
5) KWA NINI UOMBE
6) UOMBE KWA MUDA GANI
7) NA KUOMBA KWA SIFA, SHUKRANI, HESHIMA, NA UTUKUFU WA MUNGU!!