1) DHAMBI KWENYE BIBLIA
1) KUTOMWAMINI YESU NDIYO DHAMBI
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yohana 3:16
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
Yohana 3:18
>> ASIYEMWAMINI YESU NDIYE TAYARI YUKO CHINI YA HUKUMU YA MUNGU
2) KUASI KWELI/ NENO AU SHERIA YA MUNGU NI DHAMBI
1 Yohana 3:4
[4]Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
Whosoever committeth sin transgresseth also the law: for sin is the transgression of the law.
>> YESU AMETUPA AMRI MPYA YA AGANO JIPYA YA UPENDO (YOHANA 13:34-35)
>> KUTOISHI KWA UPENDO WA KRISTO NI DHAMBI
>> UKISEMA HII NI DHAMBI ONYESHA ANDIKO LILILOKATALIWA AU AMBALO ALIYETENDA DHAMBI HAJALITII AU AMELIKATAA NA KULIASI
3) TENDO LOLOTE LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI
Warumi 14:23
[23]Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
And he that doubteth is damned if he eat, because he eateth not of faith: for whatsoever is not of faith is sin.
>> UKIFANYA TENDO LOLOTE, LAKINI SI KWA IMANI, UNATENDA DHAMBI
>> KWA KUWA MWENYE HAKI (MTAKATIFU) ANAISHI KWA IMANI
>> KUISHI KWA IMANI NI KUISHI KWA KILA NENO LA MUNGU NDANI YA YESU
Mathayo 4:4
[4]Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
But he answered and said, It is written, Man shall not live by bread alone, but by every word that proceedeth out of the mouth of God.
>> "....KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU!!"
>> UKISEMA AMETENDA DHAMBI ONYESHA ANDIKO ALILOLIKATAA NA ASILOLITAKA KABISA KULITENDA. KWAMBA ANDIKO LINASEMA HIVI LAKINI YEYE ANANG'ANG'ANIA KUTENDA KINYUME CHAKE!!! AU AMETENDA KINYUME CHAKE!!
4) KUTOTENDA MEMA AMBAYO UNAJUA KUWA NI MEMA, NA UNATAKIWA KUYATENDA, LAKINI BADO HUYATENDI HIYO NI DHAMBI
Yakobo 4:17
[17]Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.
Therefore to him that knoweth to do good, and doeth it not, to him it is sin.
>> KUTOTOA, KUTOSAIDIA, KUTOSAMEHE, KUTOOMBEA, KUTOHURUMIA, KUHUKUMU HUKUMU YA MACHO, KUWEKA UCHUNGU MOYONI, KUTOPELEKA HABARI NJEMA, KUTOPENDA, KUTOSEMA KWELI, KUTOFUNDISHA, N.K. HAYA NI MFANO TU!! LOLOTE JEMA, LOLOTE LA KUFAA, LOLOTE LENYE MANUFAA, LOLOTE LA KUPENDEZA, LOLOTE LENYE KUFAIDIA, LOLOTE LA KUTIA MOYO, LOLOTE LA KUJENGA, LOLOTE LA KUFARIJI, LOLOTE LA KUONYA, LOLOTE LA KUKEMEA, LOLOTE LA KUKARIPIA, LOLOTE LA KUHUISHA, LOLOTE LA KUREJEZA, LOLOTE ZURI, LOLOTE LILILO LA KWELI, LOLOTE LA HAKI, LOLOTE LA KUMFAA, N.K. N.K. AMBALO HULITENDI WAKATI UNATAKIWA KULITENDA, HIYO NI DHAMBI!!
5) LOLOTE LISILO LA HAKI NI DHAMBI
17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
1 Yohana 5:17
>> HAKI NI KUTOKUWA NA HATIA MBELE ZA MUNGU MOYONI MWAKO (ROHONI MWAKO), KINYWANI MWAKO (MANENO YA KINYWA CHAKO), NA MATENDO YAKO
>> HAKI NI UTAKATIFU, USAFI, NA UCHAJI MUNGU ULIOKUBALIWA NA MUNGU MWENYEWE UNAOTOKANA NA UTII WAKO WA KWELI KUTOKA MOYONI MPAKA NJE KWENYE UTENDAJI WA MAISHA YA KILA SIKU!!
>> MWENYE HAKI HAPENDELEI, HADHULUMU, HASINGIZII, HAHUKUMU KWA MACHO AU KWA KUSIKIA, HASENGENYI, HANYIMI AMA KUZUIA ISIVYO HAKI, HAFANYI UZEMBE, HATEGEI, HAMVUNJII HESHIMA MWINGINE, HAKOSI KUWA NA ADABU INAVYOMPASA, HAKOSI KUTIMIZA WAJIBU WAKE KWA MUNGU, KWA MUME, KWA MKE, KWA WATOTO, KWA WAZAZI, NA KWA ULIMWENGU, HAPENDELEI, HAVUNJI AHADI AU MAAGANO, HACHUKII WENGINE, HADHARAU MTU YEYOTE, HANYOOSHEI VIDOLE WENGINE, HAMZUILII MEMA YEYOTE MWINGINE, HAMUWAZII VIBAYA MWINGINE, HAMZUNGUMZII VIBAYA MWINGINE, WALA HAMTENDEI MABAYA MENGINE, BALI HUMTENDEA SAWASAWA NA KWELI ILIVYO (NENO LINAVYOTAKA), HAMTAKII MABAYA MWINGINE, ANAOMBEA NA KULIA MBELE ZA MUNGU ZAIDI KULIKO KUZUNGUMZIA MABAYA YA WENGINE AU WENGINE WALIVYOANGUKA!! N.K.
>> LOLOTE LISILO LA HAKI NI DHAMBI!!
>> KUTOFUATA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU NI DHAMBI!! NI KUKATAA MAMLAKA YA MUNGU NA KRISTO WAKE KWAKO!!
>> HAPA NAMALIZIA KWA KUSEMA:
Proverbs 17:15
[15]He that justifieth the wicked, and he that condemneth the just, even they both are abomination to the LORD.
Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
>> ASEMAYE MTAKATIFU NI MTENDA DHAMBI, NA MTENDA DHAMBI NI MTAKATIFU, WOTE WAWILI NI CHUKIZO KWA MUNGU
>> ILI UWE SALAMA ZINGATIA HILI:
Isaya 11:2-3
"[2]Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;
And the spirit of the LORD shall rest upon him, the spirit of wisdom and understanding, the spirit of counsel and might, the spirit of knowledge and of the fear of the LORD;
[3]na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;
And shall make him of quick understanding in the fear of the LORD: and he shall not judge after the sight of his eyes, neither reprove after the hearing of his ears:"
1) ALIYEJAA ROHO MTAKATIFU NA IMANI ANA MACHO SABA YA ROHONI NA KAMWE,
2) HATOI HUKUMU KWA KUZINGATIA YALE AYAONAYO KWA MACHO AU YALE AYASIKIAYO KWA MASIKIO!! USITUMIE MACHO NA MASIKIO YA NJE KUTOA HUKUMU, TUMIA MACHO NA MASIKIO YA NDANI KUTOA HUKUMU YA HAKI!!
3) CHUNGA KINYWA CHAKO JINSI UNAVYOWAONGELEA WATAKATIFU KWENYE MWILI WA KRISTO (UNAVYOLIONGELEA KANISA!!)
2) MUNGU ANAITAZAMAJE DHAMBI?
>> MUNGU HASUBIRI KUONA TENDO LA NJE NDIPO AONE KWAMBA DHAMBI IMETENDWA!!
>> MUNGU HASUBIRI UTAMKE MANENO KWA KINYWA CHAKO ILI ASIKIE KWAMBA UMETAMKA UOVU
1 Samweli 16:7
"[7]Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.
But the LORD said unto Samuel, Look not on his countenance, or on the height of his stature; because I have refused him: for the LORD seeth not as man seeth; for man looketh on the outward appearance, but the LORD looketh on the heart."
>> MUNGU HUUTAZAMA MOYO!! <<
>> HII INAMAANISHA MUNGU HUWA ANAIONA DHAMBI MOYONI!!
>> KULE KUIONA DHAMBI MOYONI KUNAMAANISHA HUWA ANAIONA ILE roho ya dhambi MOYONI!!
>> roho huwa ina nafsi!! Yaani, mawazo/fikra, nia/mapenzi, na hisia (mind+will+emotions)
>> hivyo Mungu huwa anayasikia mawazo ya siri ya kila roho ya mwanadamu!! Daudi alisema,
Psalm 66:18
GOD'S WORD® Translation
"If I had thought about doing anything sinful, the Lord would not have listened [to me]."
"18 Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia."
Zaburi 66:18
>> MUNGU ANAYASIKIA MAWAZO MAOVU NA MABAYA KABLA HUJATAMKA LOLOTE
>> roho huwa inaongea na kurusha mawazo yake wakati wote, kwa nguvu za hiyo roho ( upako)
>> ni kama jiwe la urania linalotoa (emit) miali wakati wote!!
>> ukiona mawazo mabaya yamekuja kwako kama "flash"( akilini mwako) ujue kuna hiyo roho yenye hayo mawazo karibu inakurushia!! Ukiwa muovu utayapokea moyoni (rohoni) mwako kama receiver- kipokeleo
>> KWA HIYO DHAMBI MUNGU ANAIONA IKIWA HAIJAZUNGUMZA WALA KUTENDA BADO
>> HALIKADHALIKA MTU WA ROHONI!!
2 Wakorintho 5:16
"[16]Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.
Wherefore henceforth know we no man after the flesh: yea, though we have known Christ after the flesh, yet now henceforth know we him no more."
>> HATUMJUI NA HATUTAKIWI KUMJUA MTU AWAYE YOTE KWA JINSI YA MWILI!!
>> DAUDI ALIKUWA NA ILE roho ya uzinzi SIKUZOTE MPAKA ALIPOANGUKA DHAMBINI NDIPO HATA YEYE MWENYEWE AKAJUA KUWA UOVU ULIKUWEMO NDANI YAKE (TOBA YA DAUDI ZABURI 51:5)
>> YESU ALITUSAMEHE NA KUTUONDOLEA DHAMBI MIOYONI MWETU, KISHA AMETUPA NENO LAKE ILI LITUTAKASE (YOHANA 17:17) MAISHANI MWETU BAADA YA KUMWAMINI!! NENO LAKE NDILO LINALOBADILI FIKRA ZETU, MAWAZO YETU, NIA ZETU, MAKUSUDIO YETU, MIPANGO YETU, MAAZIMIO YETU, MAPENZI YETU, NA HATA HISIA ZETU!! NENO LINATUTAKASA ROHO ZETU, NAFSI ZETU, NA MIILI YETU!!
>> MUNGU NI ROHO NA NDIYO MAANA ANASHUGHULIKA NA SISI KATIKA ROHO!! NENO LAKE NI ROHO NA PIA NI MAISHA YETU NA UZIMA WETU (YOHANA 6:63)
>> WOTE TULIOOKOKA TUKO KWENYE MADARASA TOFAUTI TOFAUTI YA SHULE YA UTAKASO! MWALIMU WETU NI ROHO MTAKATIFU! MTAALA WETU NI BIBLIA TAKATIFU!! MITIHANI YETU NI MAJARIBU! SHULE YA UTAKASO NDIYO SHULE YA UTAKATIFU!!
>> WALIO MADARASA YA JUU YA UTAKASO HUWA WANA WAJIBU WA KUWAOMBEA, KUWAFUNDISHA, KUWASAIDIA, KUWAHURUMIA, KUWAPENDA, KUCHUKULIANA NAO, KUWACHUKULIA MIZIGO YAO, KUWAJENGA, KUWAIMARISHA, KUWATIA MOYO, NA KUWAFARIJI WALE WALIOMO KWENYE MADARASA YA CHINI AMBAYO WAO WAMEYAVUKA!!
2 Wakorintho 1:3-7
"[3]Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;
Blessed be God, even the Father of our Lord Jesus Christ, the Father of mercies, and the God of all comfort;
[4]atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.
Who comforteth us in all our tribulation, that we may be able to comfort them which are in any trouble, by the comfort wherewith we ourselves are comforted of God.
[5]Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo.
For as the sufferings of Christ abound in us, so our consolation also aboundeth by Christ.
[6]Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi.
And whether we be afflicted, it is for your consolation and salvation, which is effectual in the enduring of the same sufferings which we also suffer: or whether we be comforted, it is for your consolation and salvation.
[7]Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.
And our hope of you is steadfast, knowing, that as ye are partakers of the sufferings, so shall ye be also of the consolation."
>> KUTOFANYA HAYA KUNAONYESHA HAUJAELIMIKA(HAUJATAKASIKA) AU SIYO MWANAFUNZI WA YESU KWELI KWELI, AMA HAUJAOKOKA BALI NI PANDO LA ADUI KANISANI!!
>> WATAKATIFU WANAPENDANA NA KUTENDA MAMBO YOTE KWA UPENDO!(1 KOR 16:14) WANAJITAHIDI SIKUZOTE KUUHIFADHI UMOJA WA ROHO KATIKA KIFUNGO CHA AMANI!!( Efe 4:3), WANAUMIA NA WANAOUMIA NA WANALIA NA WANAOLIA! WANAUGUA NA KUOMBOLEZA KWA AJILI YA WACHANGA ILI WASIPOTEE AU KURUDI NYUMA AU KUANGUKA WAKATI WA MAJARIBU AU WASIPOTOSHWE!! PAMOJA NA KUWAOMBEA WATAKATIFU WENGINE WOTE!!
>> KWA NINI NINASEMA HAYA YOTE? IMEANDIKWA,
Wafilipi 1:6
[6]Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;
Being confident of this very thing, that he which hath begun a good work in you will perform it until the day of Jesus Christ:
>> MUNGU AMEANZA KAZI NJEMA NDANI YA KILA ALIYEOKOKA!! KUMTAKASA ROHO, NAFSI, NA MWILI; NA KUMSAIDIA KUKUA KIROHO KATIKA MAENEO YOTE MPAKA AFIKIE UKAMILIFU NA UTIMILIFU WA KRISTO!!!
"15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo."
Waefeso 4:15
>> HII KAZI LAZIMA ITAKAMILIKA, NA KAMWE HAITAKWAMA MAANA ANAYEIFANYA NI BWANA MWENYEWE NDANI YA MTAKATIFU WAKE KWA ROHO WAKE!! PAULO ALIIJUA VEMA KAZI HII KAMA MZAZI KIROHO, MWALIMU, NA MLEZI!! AKATUFUNDISHA TUOMBEANE ILI KAZI HII NJEMA IKAMILIKE NDANI YA KILA MMOJA WETU KWA MAOMBI HAYA;
"14 Kwa hiyo nampigia Baba magoti,
Waefeso 3:14
15 ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa,
Waefeso 3:15
16 awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.
Waefeso 3:16
17 Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;
Waefeso 3:17
18 ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina;
Waefeso 3:18
19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu."
Waefeso 3:19
>> 20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
Waefeso 3:20
>> SASA WEWE NI MFARIJI, MWALIMU, MUONYAJI, MTIA MOYO, AU HAKIMU?
>> JE! UNAZINGATIA HAO UNAOWAHUDUMIA WAKO DARASA GANI KATIKA KRISTO?
>> KUNA WENGI WAKO HIVI AU VILE LEO LAKINI KESHO WATAKUWA WAMEBADILIKA BAADA YA KUKUA KATIKA NEEMA NA KATIKA KUMJUA YESU KRISTO (2 PETRO 3:18)
>> ULIPOKUWA MADARASA YA AWALI NDANI YA KRISTO NI MAMBO MANGAPI ULIKUWA HUYAWEZI LAKINI LEO UNAYAWEZA??!! ULIKUWA HUYAFANYI LAKINI LEO UNAYAFANYA??!! AU ULIKUWA UNAYAFANYA LAKINI LEO HUYAFANYI??!! N.K.
>> KANISA LA KRISTO HALIKO CHINI YA SHERIA, MAANA NGUVU YA DHAMBI NI SHERIA!!
1 Wakorintho 15:56
[56]Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
The sting of death is sin; and the strength of sin is the law.
>> LAKINI WATAKATIFU HAWAKO CHINI YA SHERIA BALI CHINI YA NEEMA
Warumi 6:14
[14]Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.
For sin shall not have dominion over you: for ye are not under the law, but under grace.
>> DHAMBI HAIWEZI KUMTAWALA MTAKATIFU MAANA HAYUKO CHINI YA SHERIA!! KANISA LA KRISTO HALIKO CHINI YA SHERIA!!
9 akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,
1 Timotheo 1:9
10 na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;
1 Timotheo 1:10
11 kama vile ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu ahimidiwaye, niliyowekewa amana.
1 Timotheo 1:11
>> MTU WA HAKI NI YEYE ALIYEOKOKA NA ANAYEISHI KWA IMANI YA YESU!!
●●● TUJIEPUSHE NA WOKOVU WA SHERIA UNAOWARUDISHA WATAKATIFU DHAMBINI ●●●
>> KWA MAANA NGUVU YA DHAMBI NI TORATI AU SHERIA!!