MAPATO, MATUMIZI, NA UMILIKI WA MALI NA FEDHA KWENYE NDOA PAMOJA NA USAIDIZI WA MKE





MAPATO, MATUMIZI, NA UMILIKI WA MALI NA FEDHA KWENYE NDOA PAMOJA NA USAIDIZI WA MKE

UTANGULIZI

Hapo mwanzo Mungu aliumba ndoa, yaani mtu mume na mtu mke,

4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 

Mathayo 19:4

Kisha Mungu aliwabarikia akisema; "Genesis 1:28

[28]And God blessed them, and God said unto them, Be fruitful, and multiply, and replenish the earth, and subdue it: and have dominion over the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over every living thing that moveth upon the earth. 

Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

1) MUNGU ALIWABARIKI (GOD BLESSED THEM)

2) MUNGU HAKUMBARIKI MWANAMUME PEKE YAKE WALA MWANAMKE PEKE YAKE!

3) BARAKA ALIZOZITAMKA MUNGU NI BARAKA ZA PAMOJA ( CORPORATE BLESSINGS)

4) BARAKA HIZI ZA NDOA ZILIBEBA KUSUDI LA MUNGU DUNIANI KUPITIA NDOA YAO

5) MAKUSUDI NA MPANGO WA MUNGU DUNIANI NI MAKUBWA KULIKO MUME PEKE YAKE AU MKE PEKE YAKE, NA NDIYO MAANA MUNGU AKAWABARIKIA......!!

6) BARAKA HIZI ZA NDOA NI BARAKA ZA MUNGU KWA MATAIFA YA ULIMWENGU NA VIZAZI VIJAVYO VILIVYO VIUNONI MWA WANANDOA!!

7) BARAKA HIZI ZINAHITAJI WAWILI HAWA AMBAO SI WAWILI TENA BALI NI MMOJA MAANA WAMEKUWA MWILI MMOJA!!

8) ANGUKO LIMEJARIBU KUUGAWANYA MWILI MMOJA NA KUUTENGANISHA ILI KUVURUGA KULE "KUWA KWAO MMOJA" (ONENESS) ILI KUMUONDOA MUNGU KATIKATI YAO MAANA UTENGANO SI MPANGO WALA MAKUSUDI YAKE!!!

9) NDICHO ALICHOFANYA MWANAMKE ALIPODANGANYWA, AKAAMUA KIVYAKE PEKE YAKE, PASIPO KUMSHIRIKISHA MUMEWE, KUTWAA KATIKA YALE MATUNDA WALIYOKATAZWA, AKAYALA!!

>> KWENYE NDOA TAKATIFU KILA ANACHOTENDA MWANANDOA HUWA KINAJULIKANA NA MWENZAKE KWA KUWA,

1) WALISHIRIKISHANA, 

2) WALIJADILIANA, 

3) WAKAKUBALIANA, 

4) NA SASA MUME AU MKE KULE ALIKO ANATEKELEZA YALE WALIYOKUBALIANA!! >> HIVI  NDIVYO MUNGU ANAVYOTAKA IWE KWENYE NDOA ZOTE ZILIZOUMBWA NA YEYE!!

>> MWANAMKE ALIFANYA MAAMUZI YANAYOHUSU NDOA PASIPO KUMSHIRIKISHA KIONGOZI WAKE, MUMEWE ADAMU, ALIYE KICHWA, KWA KUWA YEYE NI MSAIDIZI, NA HIVYO KUASI MAMLAKA YA MUME, AMBAYO ILIMAANISHA ALIBATILISHA NENO LA MUNGU LILILOMWEKA KWENYE NAFASI YA MSAIDIZI NA KUTENDA KAMA YUKO PEKE YAKE KWENYE NDOA NA KANA KWAMBA YEYE NDIYE KIONGOZI PEKEE!! MWANAMKE ALIMUASI MUNGU!!!

>> BAADA YA KUMUASI MUNGU AKAJA KWA MUMEWE KUMSHAWISHI NAYE AASI KAMA YEYE!! NA MUMEWE NAYE AKARIDHIA UASI ULE, YEYE ALIYE KICHWA, NAYE AKALA, WAKAANGUKA WOTE WAWILI DHAMBINI, NA VIZAZI VYOTE VIKAANGUKA DHAMBINI VIUNONI MWAO!!!

>> UASI WA MWANADAMU NA ANGUKO LAKE LILITOKEA KWENYE NDOA NA LINAWEZA KUITWA: 1) HAWA KIVYAKE PASIPO MUMEWE (EVE ON HER OWN WITHOUT HER HUSBAND), NA KISHA 2) ADAMU KURIDHIA UASI WA MKEWE NA KUSHIRIKI (ADAMU SANCTIONING HIS WIFE'S REBELLION AND EVENTUALLY PARTICIPATING IN IT)

>> Ni maamuzi na mambo mangapi umeyafanya wewe mwanamke kivyako pasipo kumshirikisha, wala kumwambia, wala kumjulisha, wala kutaka ridhaa ya mumeo wala maoni yake??!! HUU NI UASI KWAKO HAIJALISHI WEWE NI NANI NA UKO WAPI!!! UNAJIAMULIA TU MAMBO NA HATA MUMEO AKIKATAA UNALAZIMISHA, UNABISHA, UNAGOMBANA, UNALALAMIKA, UNALAUMU, UNAKOSOA, UNALETA TAABU KWA MUMEO!! NYOKA AMEKUTUMA KUHARIBU NDOA NA KUSUDI LA MUNGU KWENYE NDOA HIYO, KAMA ALIVYOFANYA HAWA MAMA YAKO!!

>> NI MARA NGAPI WEWE MUME UMERIDHIA MAAMUZI MABOVU NA MIPANGO MIBOVU YA MKEO AMBAYO HATA HAKUKUSHIRIKISHA LAKINI UKAIBARIKI NA KULETA MIPANGO YA SHETANI KWENYE  NDOA YENU??!! 

>> NDOA HII ITALETA ULIMWENGUNI WATOTO WAASI AKINA KAINI, WATAKAOLETA TAIFA NA KIZAZI CHA UASI NA UKAIDI, NA UBISHI, NA KIBURI, NA JEURI, NA DHARAU, NA MAJIVUNO, NA UCHUNGU, NA CHUKI, NA UGOMVI, NA UADUI, NA MAUTI!


KANUNI YA UTENDAJI KWENYE NDOA 

Genesis 1:28

[28]And God blessed them, and God said unto them, Be fruitful, and multiply, and replenish the earth, and subdue it: and have dominion over the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over every living thing that moveth upon the earth. 

Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

>> HAYA YOTE YALIKUWA WAYAFANYE KWA PAMOJA KILA MMOJA KWA NAFASI YAKE ALIYOWEKWA!


MUME:

>> MUME POPOTE ALIPO YUPO KWA AJILI YA MKE WAKE(FOR HIS WIFE), NA KWA NIABA YA MKE WAKE!!(ON HIS WIFE'S BEHALF)

>> KWA AJILI YA MKE ILI KUTIMIZA ANDIKO; "33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe."

1 Wakorintho 7:33

>> KWA NIABA YA MKE KWA KUWA HAWA NI MWILI MMOJA!! MUME ANATENDA HUKU NA MKE ANATENDA KULE LAKINI NI KATIKA KUTIMIZA MAPENZI YA MUNGU KWAO!!


MKE:

>> MKE POPOTE ALIPO YUPO KWA AJILI YA MUMEWE, NA PIA KWA NIABA YA MUMEWE!! IMEANDIKWA PIA "........YEYE ALIYEOLEWA HUJISHUGHULISHA NA MAMBO YA DUNIA HII JINSI ATAKAVYOMPENDEZA MUMEWE!!" (1Kor7:34b)

>> KAMA WANANDOA HAWAISHI NA KUENENDA KWA KANUNI HII HAWAWEZI KUMPENDEZA MUNGU WALA KUTIMIZA MAKUSUDI, MIPANGO,  NA MAPENZI YAKE!! 

>> HII INAITWA KANUNI YA KUWA PAMOJA NA KUWAKILISHANA KATIKA YOTE, MAHALI POTE, NA SIKUZOTE!! (THE MARITAL PRINCIPLE OF TOGETHERNESS AND MUTUAL REPRESENTATION IN EVERYTHING, ALWAYS, AND EVERYWHERE) LAITI HAWA ANGEZINGATIA KANUNI HII ASINGEIAMINI ILE roho ILIYOMLETEA MAWAZO NA ELIMU MPYA ILIYOJIINUA KINYUME NA ELIMU YA MUNGU ALIYOKUWA NAYO KUTOKA KWA MUMEWE. BADALA YAKE ANGEMSHIRIKISHA KWANZA MUMEWE KABLA YA KUFANYA MAAMUZI AU ANGEUKATAA MOJA KWA MOJA ULE USHAURI WA NYOKA KWA KUWA ULIKUWA KINYUME  NA MUNGU!!


FEDHA, MAPATO, NA MATUMIZI KWENYE NDOA 

>> Mpaka hapa ni kama somo limeisha baada ya kueleza kanuni inayotawala utendaji wa mambo yote kwenye ndoa!Nataka ieleweke kwamba tunaongelea ndoa takatifu ambapo wanandoa wameokoka kweli kweli, wamejazwa Roho Mtakatifu, na wanamzalia Mungu matunda kwa kuwa wanaongozwa na Roho Mtakatifu!! Yaani, wanaishi kwa kulitenda Neno la Mungu (Yakobo 1:22), na kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu (Mathayo 4:4)!! Hivyo "KILA WALIFANYALO WANALIFANYA KWA MOYO KAMA KWA BWANA NA SIYO KWA MWANADAMU, WAKIJUA KWAMBA WATAPOKEA KWA BWANA UJIRA WA URITHI, MAANA WANAMTUMIKIA BWANA KRISTO!!" (WAKOLOSAI 3:23-24)

>> HIVYO INGAWA MUME YUKO "BIZE" KUMPENDEZA MKEWE, NA MKE NAYE YUKO "BIZE" KUMPENDEZA MUMEWE, HAKIKA WAKO "BIZE" KUMPENDEZA MUNGU KWA KUMTUMIKIA BWANA NA MWOKOZI WETU YESU KRISTO!! MUME AU MKE HANA UTUMISHI WOWOTE UNAOKUBALIKA KWA MUNGU KAMA HAISHI KWA NIABA YA, NA KWA FAIDA NA MANUFAA YA MWENZI WAKE!! NA HII NDIYO NDOA TAKATIFU!! SASA KAMA HIVI NDIVYO ILIVYO MKE AU MUME ANAANZAJE KUSEMA HII NI FEDHA YANGU AU MALI YANGU???!!! WAMEPOKEA VYOTE KAMA BARAKA YA MUNGU ILI IWASAIDIE KATIKA KUTIMIZA MIPANGO NA MAKUSUDI YA MUNGU KWAO!! NDOA TAKATIFU HAINA UBINAFSI KWA KUWA WANAZINGATIA HILI: 


24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake. 

1 Wakorintho 10:24


1 CORINTHIANS 10:24 TAFSIRI KADHAA TOFAUTI 

Berean Standard Bible

No one should seek his own good, but the good of others.


Christian Standard Bible

No one is to seek his own good, but the good of the other person


King James Bible

Let no man seek his own, but every man another's wealth.


New King James Version

Let no one seek his own, but each one the other’s well-being.


New American Standard Bible

No one is to seek his own advantage, but rather that of his neighbor.

>> HII NDIYO KANUNI KUU YA KIMAANDIKO YA UPENDO (THE CHIEF PRINCIPLE OF LOVE): "KUTAFUTA FAIDA, MANUFAA, RAHA, AMANI, USTAWI, MAFANIKIO, UTAMU, USHINDI, FURAHA, MEMA, MAZURI, NA KILA NENO JEMA LA MWINGINE, WENGINE, AMA MWENZAKO!!"

>> HII NDIYO NDOA ILIYOJAA UPENDO WA KRISTO, HII NDIYO NDOA ILIYOJAA YESU, HII NDIYO NDOA ILIYOJAA ROHO MTAKATIFU, HII NDIYO NDOA ILIYOJAA UTUKUFU WA MUNGU, AMBAPO YESU PEKEE ANATUKUZWA NA KUINULIWA!! 

>> KAZI AU  BIASHARA AU HUDUMA ZINATOKA KWA YESU!! IBRAHIMU, ISAKA, NA YAKOBO WALITAJIRISHWA NA YESU; AYUBU ALITAJIRISHWA NA YESU; MFALME SELEMANI ALITAJIRISHWA NA YESU; DAUDI BABA YAKE ALITAJIRISHWA NA YESU; N.K. N.K.

>> NA SISI TUAMINIO TUMETAJIRISHWA NA YESU: 

1) Mithali 10:22

"[22]Baraka ya BWANA hutajirisha, 

Wala hachanganyi huzuni nayo. 

The blessing of the LORD, it maketh rich, and he addeth no sorrow with it."

>> BARAKA YAKE BWANA MUNGU MWENYEZI NDANI YAKE KRISTO YESU IMETUTAJIRISHA KWA UTAJIRI USIOPIMIKA WA KRISTO YESU (UTAJIRI UNAOONEKANA NA USIOONEKANA, UNAOHARIBIKA NA USIOHARIBIKA)

2) "3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;"

Waefeso 1:3

>> TUMEBARIKIWA KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE KRISTO YESU, AMBAZO ZIMETUTAJIRISHA KWA UTAJIRI WOTE WA ROHONI NDANI YAKE KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU!!

>> LAKINI BARAKA HIZI MUNGU ANAZIPITISHIA KWENYE NDOA TAKATIFU!!!

1) BARAKA ZOTE ZA ROHONI (ALL SPIRITUAL BLESSINGS)

2) BARAKA ZOTE ZA KIAKILI (ALL MENTAL BLESSINGS)

3) BARAKA ZOTE ZA KIHISIA (ALL EMOTIONAL BLESSINGS)

4) BARAKA ZOTE ZA KIMWILI (ALL PHYSICAL BLESSINGS)

5) BARAKA ZOTE ZA KIFEDHA (ALL FINANCIAL BLESSINGS)

6) BARAKA ZOTE ZA MALI NA VITU(ALL MATERIAL BLESSINGS)

7) BARAKA ZOTE ZA KIJAMII (ALL SOCIAL BLESSINGS)

>> HIZI BARAKA NI ZA NDOA NA FAMILIA!!


>> KAMA MKE AU MUME ULIINGIA KWENYE NDOA UKIWA NA BAADHI YA BARAKA HIZI UJUE UTATAKIWA KUZIWEKA WAKFU KWA AJILI YA NDOA NA FAMILIA AMBAYO NI MISINGI MIWILI YA KANISA LA NYUMBANI!!

[KANISA LA NYUMBANI = KANISA LA NDOA + KANISA LA FAMILIA ]

1) KANISA LA NDOA LINA MUME NA MKE

2) KANISA LA FAMILIA LINA BABA, MAMA, NA WATOTO (NDUGU, MARAFIKI, MAJIRANI, N.K.WANAKARIBISHWA PIA)

3) KANISA LA MAHALI PAMOJA NI MKUSANYIKO WA MAKANISA YA NYUMBANI AMBAYO YAKO TAYARI NA YALE YAJAYO KUPITIA WALE WANAOOKOLEWA MMOJA MMOJA AMBAO NYUMBA ZAO PIA LAZIMA ZITAOKOKA KAMA WAKIDUMU KATIKA IMANI KAMA ILIVYOANDIKWA, 


Matendo ya Mitume 16:30-31

[30]kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? 

And brought them out, and said, Sirs, what must I do to be saved?

[31]Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. 

And they said, Believe on the Lord Jesus Christ, and thou shalt be saved, and thy house.

>> MWAMINI BWANA YESU NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO!!

>> ANGUKO LILITOKEA KWENYE NDOA NA KUATHIRI FAMILIA!! NYUMBA YA ADAMU ILIANGUKA BUSTANINI EDENI! KAINI AKAMUUA ABEL!! BWANA YESU LEO ANAOKOA TENA NYUMBA NA FAMILIA ZETU ILI MAKUSUDI NA MIPANGO YA MUNGU KUPITIA NDOA IENDELEE!! NAAM, MWAMINI BWANA YESU NAWE UTAOKOKA PAMOJA NA NYUMBA YAKO!! MUME OKOKA NAWE UTAOKOA NYUMBA YAKO! MKE OKOKA NAWE UTAOKOA NYUMBA YAKO! MTOTO OKOKA NAWE UTAOKOA NYUMBA YAKO!! AIBU YAKO WEWE ULIYEOKOKA HALAFU UNALETA MIGOGORO KWENYE NDOA NA KUMPA IBILISI NAFASI MOYONI MWAKO,  AKILINI MWAKO, NA KUVURUGA NDOA, ILI KUMUONDOA MUNGU KWENYE NDOA, KWA LENGO LA KUMPA SHETANI NDOA NA FAMILIA HIYO ILI WATENDA DHAMBI WAONGEZEKE DUNIANI KUPITIA WEWE!!! TUBU DELILA!! TUBU NABALI!! TUBU YEZEBELI!! TUBU AHABU!!


1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. 

Isaya 38:1

>> TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO MAANA UTAKUFA NA WALA HUTAMWONA MUNGU!!!

>> UMEVUNJA NDOA HALAFU UNAJIONA SALAMA??!! UNAHALALISHA HASIRA ZAKO ZA KIPEPO, HUKUSOMA?

Yakobo 1:19-20

[19]Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika; 

Wherefore, my beloved brethren, let every man be swift to hear, slow to speak, slow to wrath:

[20]kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu. 

For the wrath of man worketh not the righteousness of God.

>> HASIRA YA MWANADAMU KAMWE HAITENDI HAKI YA MUNGU!! NA PIA IMENENWA,

1 Yohana 5:17

[17]Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti. 

All unrighteousness is sin: and there is a sin not unto death.

>> MAAMUZI ULIYOYAFANYA KWA HASIRA NI DHAMBI!! UMETENDA DHAMBI!! HALAFU UTAJITETEA KUWA "SI HUYO MKE WANGU......!!!" "SI HUYO MUME WANGU....!!" HAUNA TOFAUTI YOYOTE NA WALE WALIOSEMA: " NYOKA ALINIDANGANYA...! HUYO MWANAMKE ULIYENIPA NDIYE ALIYESABABISHA NIMPIGE, NIMWACHE.....!" UNAJITETEA BADALA YA KUTUBU NA KUMREJEA ULIYEMWACHA!! SIKILIZA NENO LA BWANA EWE UNAYESHUPAZA SHINGO:



Ezekieli 18:31

[31]Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli? 

Cast away from you all your transgressions, whereby ye have transgressed; and make you a new heart and a new spirit: for why will ye die, O house of Israel?

>> TUNAPOINENA KWELI HIVI NI KWA UPENDO ILI KUKUSAIDIA KUREJEA!! UTAKUWA NI KIUMBE WA AJABU USIYETAKA KUTUBU NA UNAYEING'ANG'ANIA JEHANAMU!!! UKILIACHA NENO UMEMUACHA YESU!! USITAFUTE KUONEKANA MZURI KWA WANADAMU, HAMNA ATAKAYEKUTETEA SIKU YA GHADHABU!! HAO NDUGU ULIOWARUHUSU KUVURUGA NDOA HAWATAKUTETEA, HIZO HASIRA NA UCHUNGU NA UADUI NA UGOMVI NI MAPEPO YATAKAYOING'ANG'ANIA roho YAKO UKIFA, KUWA WEWE NI MALI YAO! WAKATI HUO UMESHAPOTEZA NAFASI YA KUTUBU!! FEDHA UNAZOZIKIMBIZA LEO HAZITAKUWEPO, BOSI MWAJIRI ULIYEKUWA UNAMWOGOPA KULIKO MUNGU KWA KUWA ULIKUWA UNAABUDU SANAMU PESA HATAKUWEPO KUKUTETEA, WACHUNGAJI NA MAASKOFU WALIOKUDANGANYA NA KUFUMBIA MACHO UOVU WAKO KWA SABABU YA SADAKA ZAKO HUTAWAONA!!! SHETANI ANAKUPOFUSHA KWA KIBURI CHA UZIMA HUKU ANAWINDA roho YAKO!! TUBU UPATE KUPONA!! TENGENEZA MAMBO YA  NYUMBA YAKO!!


USAIDIZI WA MKE 

18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. 

Mwanzo 2:18

USAIDIZI WA MWANAMKE NI KWENYE MAENEO HAYA SABA

1) USAIDIZI WA KIROHO (SPIRITUAL HELP)

2) USAIDIZI WA KIAKILI (MENTAL HELP)

3)USAIDIZI WA KIHISIA (EMOTIONAL HELP)

4) USAIDIZI WA KIMWILI (PHYSICAL HELP)

5) USAIDIZI WA KIFEDHA (FINANCIAL HELP)

6) USAIDIZI WA MALI NA VITU ( MATERIAL HELP)

7) USAIDIZI WA KIJAMII ( SOCIAL HELP)

>> SITAINGIA KWA KINA KWA KILA ENEO MOJA MOJA MAANA HAYA NI MASOMO MENGINE SABA MAREFU!!

>> LILE NENO "KUSAIDIA" LINA MAANA WEWE KICHWA UNAHITAJI MSAADA WAKE KWENYE MAENEO HAYO YOTE NA KWAMBA BILA YEYE ADUI LAZIMA ATAKUSHINDA! HALIKADHALIKA NA YEYE ANAHITAJI MSAADA WAKO KWENYE MAENEO HAYO YOTE, NA PASIPO WEWE YEYE HAWEZI KITU! MUHIMU NI KWAMBA NGUVU YENU KAMA MWILI MMOJA NI KUBWA MNO ISIYOWEZA KUSHINDWA KAMWE (SPIRITUAL COUPLES ARE INVINCIBLE) KAMA MAANDIKO YASEMAVYO:


Mhubiri 4:9-12

[9]Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; 

Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. 

Two are better than one; because they have a good reward for their labour.

[10]Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! 

For if they fall, the one will lift up his fellow: but woe to him that is alone when he falleth; for he hath not another to help him up.

[11]Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? 

Again, if two lie together, then they have heat: but how can one be warm alone?

[12]Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi. 

And if one prevail against him, two shall withstand him; and a threefold cord is not quickly broken.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post