HAKI NA USAWA KWENYE NDOA

 


HAKI NA USAWA KWENYE NDOA


Biblia inasema kwenye kitabu cha Mwanzo:

■ 26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 

Mwanzo 1:26

27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 

Mwanzo 1:27

>> MWANAMUME NA MWANAMKE WOTE WAKO SAWA KWA MAANA WAMEUMBWA KWA SURA NA MFANO WA MUNGU KIROHO

>> KIMAUMBILE WAKO TOFAUTI ( physically, biologically, physiologically)

>> MWANAMUME SIYO BORA KULIKO MWANAMKE NA MWANAMKE SIYO BORA KULIKO MWANAMUME 

■ 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. 

Mwanzo 1:28

>> HAKUNA MWENYE HAKI ZAIDI YA UMILIKI MALI NA BARAKA ZOTE ZA NDOA NA FAMILIA KULIKO MWINGINE KWENYE NDOA!! MUNGU ALIWABARIKIA.....! HAKUMBARIKIA MUME AU MKE PEKE YAKE!! HIVYO MKE NA MUME WANA HAKI SAWA YA UMILIKI KWENYE NDOA!! WANAMILIKI KWA PAMOJA!! NA HII NDIYO HAKI YA MUNGU, NJE YA HAPO NI UOVU, UBINAFSI, TAMAA, NA UCHOYO!!


>> HAKUNA USAWA WA MAJUKUMU KWENYE NDOA 

■18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. 

Mwanzo 2:18

>> MKE KUMSAIDIA MUME NDO HAKI!! MKE KUMTAWALA MUME AU KUTAKA USAWA WA MAAMUZI AU KUTAKA UONGOZI MBELE YA MUME SIYO HAKI, BALI NI UOVU!! MKE KUKAA KWENYE NAFASI YA USAIDIZI HIYO NDIYO HAKI YA MUNGU NA TOFAUTI NA HAPO NI UOVU!!


■ 25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 

Waefeso 5:25


28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 

Waefeso 5:28

>> MUME KUMPENDA MKEWE KAMA MWILI WAKE MWENYEWE NA KUYATOA MAISHA YAKE KWA AJILI YAKE NI HAKI MBELE ZA MUNGU, KINYUME NA HAPO NI KUUKANA NA KUUKATAA WAJIBU WAKO KAMA MUME, NA HIYO SIYO HAKI MBELE ZA MUNGU, NI UOVU!!


■ Ephesians 5:22-23

[22]Wives, submit yourselves unto your own husbands, as unto the Lord. 

Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

[23]For the husband is the head of the wife, even as Christ is the head of the church: and he is the saviour of the body. 

Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

>> MKE KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YA MUME NA KUMTII KATIKA MAMBO YOTE KAMA KUMTII BWANA NI HAKI MBELE ZA MUNGU!! KINYUME NA HAPO HUO NI UOVU NA UASI!! MKE KUWA NA ELIMU KUBWA KULIKO MUME AU KUWA NA FEDHA NYINGI KULIKO MUME SIYO TIKETI YA KUASI MAMLAKA YA MUME!! HIYO SIYO HAKI NI UOVU!! NILIWEKE HILI SAWA HIVI:

1) Mke na  vyovyote vile alivyo anabaki ni msaidizi wa mumewe!! Haijalishi amesoma vipi au ana cheo kipi duniani, MKE NI MSAIDIZI WA  MUMEWE AMBAYE NDIYE KICHWA CHA MKEWE!! Kinyume na hapo hiyo ni roho ya shetani inayomfanya mke ajione anafaa kumuongoza mumewe au yuko juu ya mumewe!!

2) Suala la kusema mke ana hela kuliko mume NI UOVU WA KUZIMU UNAOPINGANA NA KWELI!! MKE HANA HELA ZAKE MWENYEWE WALA MUME HANA HELA ZAKE MWENYEWE!! KULE KUSEMA MKE ANA HELA KULIKO MUMEWE HUKO NI KUONGEA KAMA SHETANI!! IWE NI  MSHAHARA KAZINI AU PATO LA BIASHARA FEDHA YOTE NI YA NDOA NA FAMILIA!! MKE ANAINGIZA FEDHA NA MUME HALIKADHALIKA, LAKINI WANACHOKIPATA NI CHETU! HAKUNA FEDHA YA MUME AU FEDHA YA MKE!! SHETANI AMEFAULU SANA KUINGIZA roho HII CHAFU NA FIKRA ZAKE POTOFU NA KUVURUGA HATA KUVUNJA NDOA ZA WATAKATIFU NA WATU WENGINE!! UMILIKI WA PAMOJA (JOINT OWNERSHIP) WA MKE NA MUME NDIYO HAKI MBELE ZA MUNGU!! HIVYO WEWE MUME USIJIONE FEDHA NA MALI NI ZAKO NA MKEO UKAMFANYA NI MTUMWA AU OMBAOMBA, AU UKAWEKA MASHARTI KIBAO YA KUTOA HELA KWAKE!! MPE HELA!! MZAWADIE HELA!! MZAWADIE MIRADI YA KUINGIZA HELA!! UNAWEZA KUMWACHIA MAPATO YA MIKONO YAKE AYATUMIE ATAKAVYO KWA UPENDO, LAKINI SIYO KWAMBA HIYO NDIYO KANUNI YA UMILIKI KWENYE NDOA!!


■ 28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 

Waefeso 5:28


29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. 

Waefeso 5:29

>> MUME KUMLISHA NA KUMTUNZA MKEWE NI HAKI MBELE ZA MUNGU: NA NI HAKI YA MKE KULISHWA NA KUTUNZWA NA MUMEWE!! KINYUME NA HAPO HUO NI UOVU!!


■1 Corinthians 11:9

[9]Neither was the man created for the woman; but the woman for the man. 

Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.

>> THE WOMAN WAS CREATED FOR THE MAN (MWANAMKE ALIUMBWA KWA AJILI YA MWANAMUME)

>> MWANAMKE KUJUA, KUTAMBUA, KUKUBALI, NA KUENENDA KAMA MALI YA MUMEWE NI HAKI MBELE ZA MUNGU!!! MWANAMKE ANAYELITAMBUA HILI ANAKUWA SIKUZOTE "ANAPATIKANA (AVAILABLE)KUMHUDUMIA NA KUTIMIZA WAJIBU WAKE KWA MUMEWE"!!! >> UTUMISHI WA KWANZA WA MKE NI KWA MUMEWE!! MKE HAWEZI KUMTUMIKIA BWANA YESU HUKU NYUMBANI AMEKATAA, AMESUSA, AMEZIRA, NA HATIMIZI MAJUKUMU YAKE NA WAJIBU WAKE KWA MUMEWE!! AKIFANYA HIVYO ANAKUWA MNAFIKI NA ANAYEFANYA MACHUKIZO MBELE ZA MUNGU!! 

>> MSAIDIZI HUWA A) ANASHAURI, B) ANAPOKEA MAAGIZO NA MAELEKEZO YA MUME NA KUYATEKELEZA, NA SIYO KUBISHANA, KULALAMIKA, KUGOMBANA, KUWEKA UCHUNGU, CHUKI,UADUI, NA VISASI MOYONI, HUKU MBELE ZA WATU UNAONEKANA UKO SAWA!! HUU NI UOVU MKUU!!! JAMII YA LEO IMEVAMIWA SANA KWENYE NDOA!! 


■ 3 Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. 

1 Wakorintho 7:3


4 Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. 

1 Wakorintho 7:4


5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. 

1 Wakorintho 7:5

>> MKE NA MUME LAZIMA WAISHI PAMOJA NA KULALA KITANDA KIMOJA NA KILA MMOJA LAZIMA AMPE MWENZAKE HAKI YAKE!! NA KWAMBA HAKUNA MWENYE MAMLAKA JUU YA MWILI WAKE YEYE MWENYEWE!! MUME ANA HAKI NA MAMLAKA JUU YA MWILI WA MKEWE: NA MKE ANA HAKI NA MAMLAKA JUU YA MWILI WA MUMEWE! HAWA NI MWILI MMOJA!!

>> TABIA YA MKE KUISHI KIGOMA NA MUME KUISHI MSUMBIJI SIYO HAKI MBELE ZA MUNGU, NA PIA NI KUNYIMANA HAKI ZAO!! MUME ANAMNYIMA MKE HAKI YAKE, NA MKE ANAMNYIMA MUME HAKI YAKE!! LOLOTE LISILO LA HAKI NI DHAMBI (1 YOHANA 5:17)

>> JAMBO LINGINE HAPA NI KWAMBA KWA KUNYIMANA HAKI MKE NA MUME SHETANI ANAPATA NAFASI NA KUINGIA: ANGUKO LA UZINZI LINAFUATA HARAKA MAANA WOTE WANAPINGANA NA  KWELI NA HAWANA NEEMA YA MUNGU!! KUMBUKA:

2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. 

1 Wakorintho 7:2

>> MUNGU ALIWEKA NDOA KAMA SULUHISHO LA UZINZI!! MKE NA MUME KUAMBATANA NA KUWA MWILI MMOJA NDIYO HAKI MBELE ZA MUNGU NA MBELE ZAO WENYEWE KWA WENYEWE! HAPA MKE NA MUME WANA HAKI SAWA KIMAANDIKO!! MASUALA YA KUGOMBANA HALAFU MNALETEANA "USINIGUSE" HUO NI UOVU AMBAO USIPOTUBIWA JEHANAMU HAIEPUKIKI!! SIYO TU TOBA BALI NA MATENGENEZO NA KUFANYA YAKUPASAYO!!


HAKI??!!

>> UTII WA KWELI NDIYO HAKI, NA NDIO UTAKATIFU WA WANANDOA!!

>> MWENYE HAKI MBELE ZA MUNGU NI YEYE ANAYEAMINI KWA KULIISHI NENO LA MUNGU 

>> MUME AKIITII KWELI YOTE KUHUSU MUME KWENYE MAANDIKO HIYO NDO HAKI YAKE, NAYE HUHESABIWA HAKI! NA KAMWE HAWEZI KUMTENDEA NENO BAYA MKEWE MAANA ANAMPENDA KATIKA KWELI!!


■ 7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. 

Warumi 13:7


8 Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. 

Warumi 13:8


9 Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Warumi 13:9


10 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria. 

Warumi 13:10

>> ANAANZA KWENYE MSTARI WA SABA: "WAPENI WATU WOTE HAKI ZAO!!"

- Ukiwapa watu wote haki zao, hiyo ndiyo haki; na huko ndiko kutenda haki!!

- Ukifanya hivyo ndipo Mungu naye atakupa haki zako kwa kipimo kilichojaa, kushindiliwa, kusukwa-sukwa hata kumwagika!! Ukipanda haki hupelekea kuvuna haki!!

>> MST 10 UNASEMA PENDO HALIMFANYII JIRANI NENO BAYA!! PENDO LA MUNGU NDANI YAKO HALIMFANYII MUMEO AU MKEO NENO BAYA!! HIYO NDIYO HAKI!! KWA HILI MUME NA MKE WANA HAKI SAWA, NA WOTE WAWILI:

1) WANAPASWA KUAMINI ILI WAHESABIWE HAKI;

2) WANATAKIWA KUTENDA HAKI KWA NJIA YA KULITENDA NENO ILI WAMPENDEZE MUNGU

3) WANATAKIWA KUTENDEANA HAKI WAO KWA WAO 

>> HUWEZI KUMPENDA MKEO AU MUMEO HALAFU, ukamdhulumu, ukamdanganya, ukamdharau, ukampunja, ukamchukia, ukamsusa, ukaweka uadui naye moyoni mwako, ukagombana naye na kutomsamehe, ukaishi naye mkiwa na uadui usioisha, ukamshitaki mahakamani, ukamuaibisha, ukamtenda mabaya ya aina yoyote, ukamwacha au kudai talaka, n.k. MAANA PENDO HALIMFANYII JIRANI NENO BAYA!! PENDANENI! HIYO NDIYO HAKI!!!

- MUME NA MKE WANA HAKI SAWA MBELE ZA MUNGU: HAKI ILE ITOKAYO KATIKA IMANI, NA KUDHIHIRISHWA KWA UTII WA KWELI MAISHANI MWAO!!

>> MAJUKUMU YAO YAMETOFAUTIANA MAANA MUME NI KICHWA CHA MKEWE NA MKE NI MSAIDIZI WA MUMEWE! HII NDIYO HAKI MBELE ZA MUNGU 

>> LOLOTE LISILO LA HAKI MBELE ZA MUNGU NI DHAMBI NA UOVU HATA KAMA WANADAMU WANASEMA NI HAKI ZA BINADAMU!!


■17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti. 

1 Yohana 5:17

>> KIBIBLIA HAKUNA KITU KINACHOITWA HAKI KAMA NI KINYUME NA KWELI!! HAKI YA KUTENDA DHAMBI???!!! HUO NI UOVU MKUBWA!!! USIITE DHAMBI HAKI!!! HAKI KIBIBLIA INAENDANA NA USAFI WA MOYO!! WENYE MOYO SAFI NDIO WENYE HAKI NA WANAOTENDA HAKI DUNIANI, KWA KUWA WANAENENDA KATIKA KWELI YOTE KWA HUYO ROHO WA KWELI AKAAYE NDANI YETU!!

>> HAKI YA MUNGU IKIWEPO KWENYE NDOA NA NDANI YA MIOYO YA WANANDOA HAKUNA TALAKA WALA KUACHANA!! UPENDO WA MUNGU UKIWEMO MOYONI HAMNA TALAKA WALA KUACHANA!! UOVU NA UCHAFU UKIINGIA MOYONI NDOA ZINAVUNJIKA!!

>> Ukimpenda utamsamehe saba mara sabini, utamvumilia, utachukuliana naye, utamwombea kwa machozi mbele za Mungu, utamlinda, utamheshimu, utamtendea mema, utaiheshimu ndoa, utamsitiri wingi wa uovu wake (1 Petro 4:8) na siyo kumuaibisha na kumdhalilisha kwa watu wakiwemo nduguzo na wapendwa kanisani, utamtetea, utampigania, utaubeba udhaifu wake, utamwezesha, utamthamini, utajivunia yeye, utamsifu, utamshukuru, utamtanguliza, utamtendea mema, utajitahidi kumfurahisha na mengi kama haya!! Utazingatia maandiko haya:


33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe. 

1 Wakorintho 7:33


34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe. 

1 Wakorintho 7:34


>> LAZIMA UJISHUGHULISHE (YOU MUST BE BUSY) NA MAMBO YA DUNIA HII, JINSI GANI UTAMPENDEZA MKEO/MUMEO!!


1 CORINTHIANS 7:33 ( THE HUSBAND)

New International Version

But a married man is concerned about the affairs of this world—how he can please his wife—


New Living Translation

But a married man has to think about his earthly responsibilities and how to please his wife.


English Standard Version

But the married man is anxious about worldly things, how to please his wife,


Berean Standard Bible

But the married man is concerned about the affairs of this world, how he can please his wife,


1 CORINTHIANS 7:34 ( THE WIFE)

New International Version

"..................But a married woman is concerned about the affairs of this world—how she can please her husband."


New Living Translation

".......................But a married woman has to think about her earthly responsibilities and how to please her husband."


English Standard Version

"...............But the married woman is anxious about worldly things, how to please her husband."


Berean Standard Bible

"...............But the married woman is concerned about the affairs of this world, how she can please her husband."

34 "..................... Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe."

1 Wakorintho 7:34


>> HII NDIYO HAKI MBELE ZA MUNGU

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post