JE! NI MIMI??!! HAPANA SI MIMI!!
1) 20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Wagalatia 2:20
>> SIYO MIMI NINAYEISHI BALI YESU NDIYE ANAYEISHI NDANI YANGU!!
2) KAMA SI MIMI NINAYEISHI NDANI YANGU, MIMI MWENYEWE NIKO WAPI?
1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
Wakolosai 3:1
2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.
Wakolosai 3:2
3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. [Berean Standard Bible
For you died, and your life is now hidden with Christ in God.]
Wakolosai 3:3
4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.
Wakolosai 3:4
>> MIMI NILIKUFA NA MAISHA YANGU(UHAI WANGU) YAMEFICHWA PAMOJA NA KRISTO KATIKA MUNGU
>> NILIKUFA LAKINI NIKO HAI NDANI YAKE KRISTO
3) NI NANI SASA ANAYETENDA KAZI NDANI YANGU?
"13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema."
Wafilipi 2:13
Amplified Bible(Phillipians 2:13)
"For it is [not your strength, but it is] God who is effectively at work in you, both to will and to work [that is, strengthening, energizing, and creating in you the longing and the ability to fulfill your purpose] for His good pleasure."
>> SI TU KWAMBA MUNGU NDIYE ANAYEISHI NDANI YANGU, BALI PIA YEYE NDIYE ANAYEZITENDA KAZI ZOTE NDANI YANGU SAWASAWA NA KUSUDI LAKE JEMA!! YAANI, MUNGU YUMO NDANI YANGU ILI KULITIMIZA KUSUDI LAKE JEMA!! (GOD LIVES IN ME FOR THIS ONE SOLE AIM: TO FULFIL HIS PURPOSES FOR ME AND THE WHOLE WORLD THROUGH ME)
>> WAJIBU WANGU NI UPI? NI KUMWAMINI, KUMTUMAINI, NA KUNYENYEKEA CHINI YA MKONO WAKE HODARI ILI YEYE AWE NA UHURU WA KUTENDA ALITAKALO NDANI YANGU NA PIA KUPITIA MIMI!! (KUNYENYEKEA HUKU NI KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YA ROHO WAKE, NENO LAKE, NA NGUVU ZAKE)
>> HAMNA WAJIBU MWINGINE MKUBWA NA WA MUHIMU KULIKO HUU KWA MWAMINI KATIKA ZAMA HIZI ZA KUONGOZWA NA ROHO WA YESU!!
>> Wanafunzi wa Yesu walidhani wanaweza kufanya kitu fulani ili kuzitenda kazi za Mungu walizomwona Yesu akizitenda na wakamwuliza:
John 6:28
[28]Then said they unto him, What shall we do, that we might work the works of God?
Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?
>> TUFANYE NINI YESU ILI TUPATE KUZITENDA KAZI ZA MUNGU??!! YAANI, TUAMBIE SISI YESU KAMA KUNA TUNACHOWEZA KUKIFANYA ILI KUZITENDA KAZI ZA MUNGU (IS THERE ANYTHING WE CAN DO TO WORK THE WORKS OF GOD THAT WE SEE YOU DOING?)
>> SWALI HILI PENGINE MWANAFUNZI WA YESU LEO UNGEULIZWA UNGEKUWA NA MAJIBU MENGI!! FANYA HIVI, FANYA VILE N.K.!!! LAKINI YESU ALIWAJIBU:
John 6:29
[29]Jesus answered and said unto them, This is the work of God, that ye believe on him whom he hath sent.
Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.
>> HAKUWAJIBU KWAMBA FANYENI HIVI AU FANYENI VILE
>> BALI ALIWAPA TAFSIRI YA KAZI YA MUNGU!!(definition of God’s work)
>> YESU ALIWAONYESHA KAZI YA MUNGU NI IPI!!
>> HII INA MAANA WALIULIZA WASICHOKIJUA!!! HAWAKUIJUA KAZI YA MUNGU WALA KAZI ZA MUNGU!!
>> UNAPODHANI KUNA KITU UNAWEZA KUKIFANYA ILI KUZITENDA KAZI ZA MUNGU UNAONYESHA HUIJUI BADO KAZI YA MUNGU NA WALA HAUJAUJUA WAJIBU WAKO MKUU NDANI YA YESU!!
*KAZI YA MUNGU*
"Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye."
>> KAZI YA MUNGU NI KUMWAMINI YESU ALIYETUMWA NA BABA!!
KWA NINI KUAMINI NI KAZI?
KWA SABABU KUAMINI KUNAKUPATIA NEEMA YA MUNGU INAYOKUWEZESHA KUYATENDA MAPENZI YAKE YOTE POPOTE ULIPO KATIKA LOLOTE ULIFANYALO!!!
- KUNA NEEMA IOKOAYO, na
- KUNA NEEMA IFUNDISHAYO KUYATENDA YOTE YALE YAMPENDEZAYO MUNGU (TITO 2:11-13),
- YESU ALIIANZISHA IMANI HII TAKATIFU SANA KWA LENGO LA KUTUPATIA NEEMA YAKE ILI, KWA HIYO, TUPATE KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU YOTE YALIYOMO KWENYE NENO LAKE!!! NEEMA MAANA YAKE NI HII:
Zechariah 4:6
[6]Then he answered and spake unto me, saying, This is the word of the LORD unto Zerubbabel, saying, Not by might, nor by power, but by my spirit, saith the LORD of hosts.
"Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi."
>> "SI KWA UWEZO WAKO WALA NGUVU ZAKO, BALI NI KWA ROHO MTAKATIFU"
>> HAIWI KWA ROHO MTAKATIFU PASIPO NGUVU ZAKE (MATENDO YA MITUME 1:8)
NEEMA = (ROHO MTAKATIFU + NGUVU ZAKE) NDANI YA MWAMINI!!
Maandiko yanasema, "1 Corinthians 6:17
"[17]But he that is joined unto the Lord is one spirit.
Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye."
[New International Version
But whoever is united with the Lord is one with him in spirit.
New Living Translation
But the person who is joined to the Lord is one spirit with him.]
>> KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NI KUUNGWA NA BWANA YESU KATIKA ROHO NA KUWA ROHO MOJA NAYE!! Yaani, roho yako iliyozaliwa mara ya pili inaunganika na Roho wa Kristo Aliye Mtakatifu, i.e. roho yako + Roho Mtakatifu
>> Hivyo,
Neema ya Kristo kwako uaminiye = roho yako + (Roho Mtakatifu + Nguvu zake)
[ Neema ndani yako=Roho + roho + nguvu za Roho]]
>> Hii inatafsiri andiko kwamba "si kwa uweza wala nguvu bali ni kwa Roho yangu, asema Bwana wa Majeshi"(Zech 4:6)
>> Na pia inaeleza andiko "kwamba Mungu ndiye atendaye kazi ndani yangu, kutaka kwangu na kutenda kwangu kwa kulitimiza kusudi lake jema"(Flp 2:13)
>> Inaeleza pia kwamba, "Yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye" (1 Kor 6:17)
>> Kuwa roho moja na Bwana Yesu ni mfano wa kuunganisha waya wako wa umeme kwenye "grid" kuu ya taifa inayosafirisha umeme mkubwa kiasi kwamba ule umeme mkubwa sasa unapita kwenye waya wako na kuleta matokeo!!!
>> Kuunganika na Bwana na kuwa roho moja naye ni kuunganika na Roho wa Bwana na nguvu zake na kisha Bwana mwenyewe kutenda kazi ndani yako kutaka kwako na kutenda kwako kwa kulitimiza kusudi lake jema!! (Flp 2:13)
>> Unaweza kuona hapa kwamba si wewe bali Bwana ndani yako!! Si nguvu zako bali nguvu zake ndani yako!! Si uweza wako bali uweza wake ndani yako!! Si hekima yako bali hekima yake ndani yako!! n.k. Si wewe bali Bwana mwenyewe ndani yako!! NA HII NDIYO NEEMA!! NEEMA YAKE NDIYO INAYOZITENDA KAZI ZAKE NDANI YAKO KWA KUPITIA ROHO HUYU WA NEEMA TULIYEPEWA!! Wewe unaweza kufanya nini??!! Yesu alisema,
"John 15:5
[5]I am the vine, ye are the branches: He that abideth in me, and I in him, the same bringeth forth much fruit: for without me ye can do nothing.
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote."
>> PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI KUFANYA NENO LOLOTE!!! WEWE HUWEZI KUFANYA NENO LOLOTE PASIPO YESU!! YAANI, PASIPO NEEMA YAKE, PASIPO ROHO WAKE MTAKATIFU, HUWEZI KUFANYA LOLOTE LA KUMPENDEZA AMA KUMPA MUNGU UTUKUFU!! UNAWEZA KUFANYA YOTE ISIPOKUWA MAPENZI YA MUNGU USIPOKUWA NA ROHO WAKE MTAKATIFU!!
>> MUNGU AMEMTUMA YESU ULIMWENGUNI KUTULETEA NEEMA TELE ILI TUWEZE KUENENDA KATIKA KWELI YAKE YOTE KWA NJIA YA KUMWAMINI YEYE TU!!
John 1:17
[17]For the law was given by Moses, but grace and truth came by Jesus Christ.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
>> KUAMINI NI KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU
>> KUAMINI NI KUMPENDEZA MUNGU KATIKA YALE YOTE UYAFANYAYO
>> KUAMINI NI KURUHUSU NGUVU ZA MUNGU ZITIRIRIKE (FLOW) KUTOKA MBINGUNI HADI NDANI YAKO NA KISHA KWENDA KWA WENGINE KUPITIA WEWE, KATIKA KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU ULIMWENGUNI!!!
>> KUAMINI NI KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YA ROHO WA KRISTO, NA NENO LAKE, NA NGUVU ZAKE, NA UTENDAJI WA MAPENZI YAKE!!
>> KUAMINI NI KULITENDA NENO LA KRISTO SAWASAWA NA KUSUDI NA MPANGO WA MUNGU KWA NGUVU NA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU
>> HII NDIYO MAANA YESU ALISEMA:
"Yohana 6:29
[29]Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.
Jesus answered and said unto them, This is the work of God, that ye believe on him whom he hath sent."
>> HII NDIYO KAZI YA MUNGU, MMWAMINI YEYE ALIYETUMWA NA YEYE!!
>> WAJIBU WAKO NI KUAMINI! JUKUMU LAKO NI KUAMINI!! UNACHOTAKIWA KUKIFANYA NI KUAMINI!! HII NDIYO KAZI YA MUNGU!! WALE WANAOTAFUTA WAFANYE NINI ILI KUZITENDA KAZI ZA MUNGU HUWA HAWAWEZI KAMWE KUZITENDA MAANA WANAJIVUNIA NGUVU NA UWEZA WAO WENYEWE NA SIYO NEEMA YA MUNGU!! HAWAWEZI KUWA NA NEEMA HIYO KWA KUWA HAWAJAJUA KUWA KUMWAMINI YESU NDIYO KAZI YA MUNGU!!!
*PAULO*
Nimalize kwa kumuelezea Paulo na neema aliyopewa na Bwana: Paulo alisema:
1 Wakorintho 15:10
"[10]Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
But by the grace of God I am what I am: and his grace which was bestowed upon me was not in vain; but I laboured more abundantly than they all: yet not I, but the grace of God which was with me."
1) NEEMA YA MUNGU NDIYO ILIYOMTENGENEZA PAULO AWE VILE ALIVYOKUWA
2) NEEMA HIYO NDIYO ILIYOMWEZESHA KUFANYA KAZI KUPITA MITUME WOTE WALIOMTANGULIA
3) LAKINI ANASEMA, SI YEYE BALI NI NEEMA YA MUNGU PAMOJA NAYE!!
>> IMANI YA YESU (GAL 2:20) ILIMPELEKEA PAULO KUPEWA NEEMA HII YA AJABU ILIYOMTENGENEZA NA KUMWEZESHA KUZITENDA KAZI ZAKE BWANA WETU YESU KRISTO!!
>> PAULO ANASEMA HAIKUWA KWA NGUVU NA UWEZA WAKE YEYE, WALA HAIKUWA YEYE BALI NI NEEMA YA BWANA YESU NAYE!!
5 Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
1 Petro 5:5
>> MUNGU HUWAPA WANYENYEKEVU NEEMA
>> WANYENYEKEVU WANAOJUA KWAMBA HAWAWEZI CHOCHOTE PASIPO YESU, NA HIVYO WAKO TAYARI KILA MARA KUJA KWA YESU KUOMBA REHEMA NA NEEMA
Hebrews 4:16
"[16]Let us therefore come boldly unto the throne of grace, that we may obtain mercy, and find grace to help in time of need.
Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji."
>> NEEMA YAKE KRISTO YATUTOSHA!!!