Hebu tuendelee kutazama mawazo ya Mungu kuhusu pesa ili tujue mapenzi yake ni yapi na tuweze kuyafanya!!
6) USIJIWEKEE AKIBA HAPA DUNIANI, WEKA AKIBA MBINGUNI
>> Kama kweli wewe umeokoka na ni mtoto wa Mungu, hapa duniani siyo kwako na unapita tu kama msafiri na mpitaji kama maandiko yasemavyo.
17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
1 Petro 1:17
20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
Wafilipi 3:20
Phillipians 3:20 (New Living Translation)
But we are citizens of heaven, where the Lord Jesus Christ lives. And we are eagerly waiting for him to return as our Savior.
>> MTAKATIFU ULIYE MTOTO WA MUNGU KWELI HAPA DUNIANI SIYO KWAKO, KWA MAANA WEWE SASA NI RAIA WA MBINGUNI!! HAPA UNAPITA TU, NA DUNIA HII INAPITA TU NAYO, "Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele."
1 Yohana 2:17
>> USILOWEE UGENINI MPAKA UKAJISAHAU WEWE UPO HAPA KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU TU, NA MAISHA YAKO HALISI YATAFUNULIWA BAADAE YESU ATAKAPOFUNULIWA!!
2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. (1 Yohana 3:2)
Tena,
3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. (Wakolosai 3:3)
4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. (Wakolosai 3:4)
>> Hivyo hatuweki hazina hapa kwa sababu siyo kwetu!! Hatuwekezi ugenini!! Wapi unaweka hazina yako hiyo inaonyesha tumaini lako liko wapi!! Walio wa mbinguni wanaweka hazina mbinguni!!
>> Walio wa dunia wanatafuta ya dunia sikuzote na kuweka hazina zao duniani:
"18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
Wafilipi 3:18
19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani."
Wafilipi 3:19
[New International Version
Their destiny is destruction, their god is their stomach, and their glory is in their shame. Their mind is set on earthly things.
New Living Translation
They are headed for destruction. Their god is their appetite, they brag about shameful things, and they think only about this life here on earth.]
>> Dunia hii na kila kilichomo vitaharibiwa!! Na wote walioipenda dunia hii na kujiwekea hazina zao hapa duniani nao wataharibiwa!! Kwa kuwa wao walichagua kuishi maisha yenye kuharibika na kuweka tumaini kwenye vitu vinavyoharibika!! Tubu na kisha uhamishie hazina zako zote mbinguni!! Uanze kuishi maisha ya imani na kumtumainia Mungu asiyeharibika!!
>> Sababu nyingine muhimu kwa nini hatuweki hazina duniani hapa ni hii:
19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
Mathayo 6:19
>> HAZINA ZA DUNIANI HAZIKO SALAMA KAMA UNAVYODHANI, NA HIVYO ZAWEZA KUPOTEA AU KUHARIBIKA WAKATI WOWOTE KWA SABABU MBALIMBALI
20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
Mathayo 6:20
>> HAKUNA ANAYEWEZA KUIBA AU KUHARIBU MBINGUNI KAMWE!!
21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Mathayo 6:21
>> MWISHO HAPA ALIYEUUMBA MOYO (ALIYEIUMBA roho) ANAJUA KWAMBA MOYO WAKO MWANADAMU SIKUZOTE UNAKUWEPO PALE ULIPOWEKA HAZINA YAKO!! UKIJIWEKEA HAZINA DUNIANI MOYO WAKO PIA UNAKUWEPO DUNIANI, NA KAMWE HAUWEZI KUWA KWA MUNGU MBINGUNI!! HIVYO HUWEZI KUMWABUDU MUNGU KWA USAFI NA UNYOFU KATIKA ROHO NA KWELI!! UNAWEZA KUMWACHIA GARI MUOSHA .MAGARI ALIOSHE UKAENDA MBALI KUNYWA SUPU, LAKINI MULE KWENYE GARI MKIWA NA MILIONI 40, HAUENDI KOKOTE!!! GARI LITAOSHWA NA WEWE UPO PALE PALE KUHAKIKISHA USALAMA WA FEDHA YAKO!! KWA NINI? KWA SABABU MOYO WAKO UKO KWENYE ILE HAZINA YAKO NA HUJISIKII AMANI KUIACHA GARINI NA MUOSHA MAGARI! UKIWEKA HAZINA DUNIANI, TUMAINI LAKO LINAHAMIA KWENYE HAZINA HIYO!! HUWEZI KUMTUMAINI MUNGU UKIWEKA HAZINA DUNIANI!!
21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Mathayo 6:21
7) MTINDO WA KUJIWEKEA HAZINA MBINGUNI NI KUTAWANYA NA SIYO KUKUSANYA
Proverbs 11:24
>>New Living Translation
"Give freely and become more wealthy; be stingy and lose everything."
>>English Standard Version
"One gives freely, yet grows all the richer; another withholds what he should give, and only suffers want."
>> "Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji."(Mithali 11:24)
>> WALIO WA MBINGUNI MIOYO YAO IKO MBINGUNI WANAKOWEKA HAZINA ZAO SIKUZOTE KWA BIDII KWA KUTENDA MEMA!! FEDHA KWAO NI ZANA (TOOL) YA KUTENDEA MEMA, NA SIYO VINGINEVYO!! WANAITAFUTA FEDHA KWA BIDII ZOTE, KWA AKILI ZOTE, NA KWA NGUVU ZOTE, ILI WAITUMIE KUTENDA MEMA!! MEMA CHUMBANI, MEMA NYUMBANI, MEMA MTAANI, MEMA KANISANI, MEMA KAZINI, MEMA KILA MAHALI SIKUZOTE
14 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
Tito 2:14
10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Waefeso 2:10
>> UNAJIWEKEA HAZINA MBINGUNI KWA KUTOA NA KUTOA NA KUTOA, KUSAIDIA, KUSAIDIA, NA KUSAIDIA MASKINI NA WAHITAJI WOTE, SIKUZOTE, KUHURUMIA NA KUHURUMIA NA KUHURUMIA MASKINI NA WAHITAJI KILA UPATAPO NAFASI!! KIRIMU KANA KWAMBA UMEPEWA NAFASI HIYO MOJA TU YA KUTENDA MEMA HALAFU UONDOKE DUNIANI!!! UTOAJI WA NAMNA HII UNAHARIBU SANA UFALME WA GIZA NA KUENEZA, KUIMARISHA, NA KUJENGA UFALME WA MUNGU!! FEDHA, MALI, NA UTAJIRI NI ZANA ZA KUTENDEA MEMA KWENYE MWILI WA KRISTO, NA UFALME WAKE KIUJUMLA!! UTOAJI WA NAMNA HII NI DALILI MUHIMU YA MOYO ULIO KWA BABA USIOTEGEMEA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI!!!
>> UPANDE WA PILI WA SHILINGI UNAONEKANA KWENYE ANDIKO LETU:
"Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji."(Mithali 11:24)
>> YULE ANAYETAWANYA MUNGU HUMUONGEZEA ZAIDI ILI AZIDI KUTAWANYA AMA KUPANDA MBEGU ZA UPENDO WA MUNGU
6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
2 Wakorintho 9:6
7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
2 Wakorintho 9:7
8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
2 Wakorintho 9:8
9 kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.
2 Wakorintho 9:9
10 Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;
2 Wakorintho 9:10
11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.
2 Wakorintho 9:11
>> KILA FEDHA NI MBEGU YA KUPANDA ZAIDI (KUTENDA MEMA) NA NDIYO MAANA MTOTO WA MUNGU KWELI KWELI NI TAJIRI WA MATENDO MEMA!!
>> LAKINI WALE WENGINE NI MABAHILI, WACHOYO, NA WENYE TAMAA AMBAO SIKUZOTE HAWATOSHEKI NA KILA WANACHOPATA!! KWA KUWA MIOYO YAO IKO KWENYE VITU VINAVYOHARIBIKA HAWA HAWAWEZI KAMWE KUTAWANYA!!!
>> DUNIA HII NA WATENDA DHAMBI WAKE WABINAFSI NA WACHOYO "INAKUSANYA", HUKU WATAKATIFU WATOTO WA MUNGU WAO "WANATAWANYA!!!"
>> WALE WANAOKUSANYA SIKUZOTE NI WAHITAJI NA KAMWE HAWATOSHEKI NA WALA HAWAPATI UTOSHELEVU (CONTENTMENT) KWENYE YOTE WAYAFANYAYO, MAANA HAWANA MUNGU MIOYONI MWAO!! WANAMILIKI PESA NA MALI LAKINI HAWANA AMANI NA FURAHA NA UTOSHELEVU WA KWELI UNAOPATIKANA KWA YESU PEKEE!! UKWELI HAWA BADO NI MASKINI MNO MAANA MUNGU HAYUPO PAMOJA NAO KWA KUWA HAWAMWAMINI WALA HAWAMTUMAINI!! HAWA WAPO MAKANISANI KAMA HAWA HAPA:
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
Ufunuo wa Yohana 3:15
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
Ufunuo wa Yohana 3:16
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
Ufunuo wa Yohana 3:17
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
Ufunuo wa Yohana 3:18
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
Ufunuo wa Yohana 3:19
>> BIBLIA INASEMA UNAJIONA TAJIRI KWA SABABU YA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI, LAKINI KUMBE MUNGU ANAKUONA WEWE NI 1) MASKINI, 2) KIPOFU, 3) UCHI, 4) MNYONGE, NA 5) MWENYE MASHAKA KATIKA ROHO!!! UNAHITAJI KUOKOKA; NA KAMA ULIOKOKA UNAHITAJI KUJAZWA ROHO MTAKATIFU; NA KAMA ULIJAZWA ROHO MTAKATIFU UNAHITAJI KUTUBIA TAMAA NA IBADA YAKO YA SANAMU ILI UTAKASIKE, NAYE ROHO AKUONGOZE HATUA ZAKO KWENYE NENO LAKE, KULIISHI NA KULITENDA KWA NGUVU NA UWEZA WAKE!! TUBU, MAANA YESU YUKO NJE YA MOYO WAKO ANABISHA HODI!! UMEMSUKUMA NJE UKAUJAZA MOYO WAKO SANAMU PESA, MALI, NA UTAJIRI,
8) KAMA UMEJALIWA NEEMA YA KUMILIKI FEDHA, MALI, NA UTAJIRI HAYA HAPA NI MAAGIZO NANE KWAKO YA KUYAZINGATIA SANA KAMA UNATAKA KUURITHI UZIMA WA MILELE ( soma somo hili>> https://spiritbrideministries.blogspot.com/2023/05/maagizo-nane-kwa-matajiri-waliookoka.html)
Tutaendelea tukijaliwa, bado mengi ya kusema!