UTAKATIFU KWENYE PESA-SEHEMU YA TATU
Kwenye sehemu hii ya tatu tutaangalia, tukijaliwa, watu hawa watatu kwenye Biblia:1)TAJIRI ÀLIYEUKOSA UFALME WA MUNGU (Marko 10:17-25)
2) TAJIRI MPUMBAVU ALIYEISHIA KUZIMU (Luka 12: 15-21)
3) ZAKAYO TAJIRI ALIYEJIWEKEA HAZINA MBINGUNI ( Luka 19:1-10)
MFANO WA KWANZA
1) TAJIRI ÀLIYEUKOSA UFALME WA MUNGU (Marko 10:17-25)
17 Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?
Marko 10:17
18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.
Marko 10:18
19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.
Marko 10:19
20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.
Marko 10:20
21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Marko 10:21
22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Marko 10:22
23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Marko 10:23
24 Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Marko 10:24
25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Marko 10:25
>> MTU HUYU TAJIRI ALIKUWA NA MALI NYINGI
>> LAKINI PIA ALIKUWA MWENYE KUZISHIKA AMRI KUMI NA TORATI YA MUSA TANGU UTOTONI
>> LAKINI HAKUWA NA UZIMA WA MILELE, MAANA ALIMUULIZA YESU AFANYE NINI ILI APATE KUURITHI UZIMA WA MILELE! (ETERNAL LIFE) UZIMA WA MILELE NI MAISHA YA MILELE YASIYOHARIBIKA NA YASIYO NA MWISHO!! NI DHAHIRI MAISHA ALIYOYALETA YESU HAYAMO KWENYE WINGI WA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI ULIONAO!! ( LUKA 12:15)
>> MAISHA HUJAYAPATA WALA KUYAPATIA KAMA ULICHONACHO NI WINGI TU WA FEDHA, MALI, NA VITU PEKE YAKE BILA YESU! NA UKIWA NA YESU MOYONI MWAKO UTAISHI MAISHA MENGINE TOFAUTI KWENYE MALENGO YA UTAFUTAJI, UMILIKI, NA MATUMIZI YA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI ULIVYOAMINIWA UWAKILI!
>> MTU HUYU TAJIRI ALIPOJIELEZA KUWA AMEZISHIKA AMRI KUMI TANGU UTOTONI NDIPO YESU ALIMWAMBIA BADO AMEPUNGUKIWA NA NENO MOJA!! YAANI, HILO LILILOPUNGUA NDILO LILILOKUWA LIMESABABISHA ASIWE NA MAISHA YA MILELE (UZIMA WA MILELE) YA YESU KRISTO KUTOKA KWA BABA WA MBINGUNI!! YESU ALIMWAMBIA ILI AKAMILIKE KWA KUWA NA UZIMA WA MILELE,
MST 21
a) AKAUZE VYOTE ALIVYONAVYO
b) KISHA AKAWAPE FEDHA ZA MAUZO HAYO MASKINI
c) NDIPO ATAKUWA NA HAZINA MBINGUNI
D) KISHA AJE AMFUATE YESU
>> KIUFUPI YESU ALIMTAKA AFANYE TENDO LA IMANI ILI AJITAKASE MOYO WAKE NA KUACHANA NA SANAMU FEDHA, MALI, NA UTAJIRI ZILIZOKUWA ZIMEJAA MOYONI MWAKE!
>> YESU ALITAKA KUMFUNDISHA MAISHA MAPYA YA KUMWAMINI NA KUMTUMAINIA YESU TU PEKE YAKE
>> YESU ALITAKA KUMFUNDISHA JINSI YA KUJITAJIRISHA MBINGUNI KWA KUTAWANYA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI DUNIANI KWA KUWAPA MASKINI NA HIVYO KUMKOPESHA MUNGU KAMA MAANDIKO YANENAVYO (MITHALI 19:17)
>> ISITOSHE ANGEMTII YESU ANGEPOTEZA VINAVYOHARIBIKA NA VYA HAPA NA KISHA ANGEPEWA VYA MILELE, VISIVYOHARIBIKA VYA KUTOKA MBINGUNI!! NA ZAIDI, MUNGU ANGEMLIPA SAWASAWA NA LUKA 6:38!! LAKINI MOYO WAKE USIO SAFI ULIMWONGOZA KUKATAA YOTE HAYA NA UZIMA WA MILELE (MAISHA YA MILELE) ( MARKO 10:23) AKACHAGUA MAUTI NA UHARIBIFU!! IBADA YA SANAMU HIZI "PESA" "MALI" NA "UTAJIRI" ITAKUPELEKA JEHANAMU USIPOTUBU NA KUREJEA KWA YESU AKUPE MAISHA YA KWELI YASIYO NA UHARIBIFU!!
23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
Marko 10:23
>> MSTARI WA 23 UNAONYESHA KWAMBA NI NGUMU SANA, NI SHIDA KWELI KWELI KWA ["WENYE KUTEGEMEA MALI"] KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU!! KWENYE UFALME WA MUNGU WANAINGIA WALE WENYE KUMTEGEMEA MUNGU PEKE YAKE!! MATAJIRI KARIBU WOTE WANATEGEMEA MALI ZAO, PESA ZAO, NA UTAJIRI WAO!! HAWAWEZI KUMTEGEMEA MUNGU MAANA HAWAMWAMINI!! HAWAWEZI KUINGIA MPAKA WATUBU NA KUBADILIKA KABISA KAMA ZAKAYO ALIVYOFANYA (TUTALITAZAMA HILI HAPO MBELE)
25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Marko 10:25
>> YESU AMBAYE KWA NJIA YAKE NA KWA AJILI YAKE MOYO AMA ROHO ILIUMBWA (WAKOLOSAI 1:16) ANASEMA NI RAHISI NGAMIA (MFANO TEMBO KWA HUKU KWETU AU TWIGA) KUPENYA KAMA UZI KWENYE TUNDU LA SINDANO KULIKO TAJIRI KUINGIA KWENYE UFALME WA MUNGU!! NI DHAHIRI KWA ANDIKO HILI KWAMBA HILO NI JAMBO LISILOWEZEKANA!!
>> SASA NA WEWE UNAYEUGUA, UNAYESUMBUKA, UNAYETESEKA, UNAYECHANGANYIKIWA, UNAYEUMIA, UNAYEHANGAIKA, USIYE NA AMANI, UNAYEKOSA RAHA, UNAYEGOMBANA NA MKEO/ MUMEO, UNAYEDAIANA MPAKA MAHAKAMANI NA NDUGU KWENYE MWILI WA KRISTO, UNAYEVUNJA MAHUSIANO, UNAYEDHULUMU, UNAYEPOKEA RUSHWA, UNAYEDANGANYA, UNAYEJITENGA NA MASKINI NA WAHITAJI, ETI KWA KUTAKA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI, AU KWA KUWA FEDHA HAMNA KWA SASA, NI DHAHIRI ZIKIJA HIZO PESA UTAJIWEKEA HAZINA HAPA DUNIANI NA SIYO MBINGUNI KWA KUWA HATA SASA HUMTEGEMEI MUNGU, NA NDIYO MAANA HUNA AMANI YA YESU MOYONI MWAKO!! IMEANDIKWA,
Isaiah 26:3
[3]Thou wilt keep him in perfect peace, whose mind is stayed on thee: because he trusteth in thee.
Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
>> KWA WANAOMTEGEMEA NA KUMTUMAINI BWANA WAO WANA AMANI TELE SIKUZOTE VIKIWEPO AU VISIPOKUWEPO, VIKIWA VINGI AU VICHACHE, WAKISHIBA AU WAKIONA NJAA, WAKIVAA AU WAKIWA HAWANA NGUO, N.K. MAANA WANA UHAKIKA VYOTE HIVYO VINAKUJA KWA WAKATI ULIOAMURIWA, NA MUNGU ANASHUGHULIKIA MAMBO YAO YOTE KILA IITWAPO SASA!! HAWAYUMBISHWI WALA KUTETEMESHWA NA MABADILIKO YA HALI AU MAZINGIRA, WALA HAWAOGOPI CHOCHOTE!!
MFANO WA PILI
2) TAJIRI MPUMBAVU ALIYEISHIA KUZIMU (Luka 12: 15-21)
15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
Luka 12:15
16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
Luka 12:16
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
Luka 12:17
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
Luka 12:18
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
Luka 12:19
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
Luka 12:20
21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.
Luka 12:21
>> NIMESHASEMA NA SASA NARUDIA KWELI HII: MAISHA YA MILELE SIYO MAISHA YA KUHARIBIKA! YAKO MAISHA YA MWILI HUU NA MAISHA YA roho ZETU!! SISI NI roho, TUNA NAFSI, NA TUNAISHI KWENYE MWILI!! PAULO ALISEMA DAMU NA NYAMA HAVIWEZI KUURITHI UFALME WA MUNGU:
1 Corinthians 15:50
[50]Now this I say, brethren, that flesh and blood cannot inherit the kingdom of God; neither doth corruption inherit incorruption.
Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika.
YAANI, HAYA MAISHA YA KULA, KUNYWA, KUVAA, KULALA, KUAMKA, KUINGIA, KUTOKA, KWENDA, KURUDI, KUNUNUA, KUUZA, KUOA, KUOLEWA, N.K. HAYAWEZI KUURITHI UFALME WA MUNGU!! MAISHA HALISI YA MTOTO WA MUNGU NI YALE YALIYOANDIKWA!! MTOTO WA MUNGU:
1) ANAPOSEMA ANASEMA NENO LILILOANDIKWA
2) ANAPOTAFAKARI ANATAFAKARI NENO LILILOANDIKWA,
3) ANAPOTENDA ANALITENDA NENO LILILOANDIKWA
4) ANAPOFANIKIWA MAANA YAKE MAANDIKO YAMETIMIA MAISHANI MWAKE!!
>> MAISHA NA HUDUMA YAKE NI KULITENDA NENO LA MUNGU KWA JINA LA YESU!!
4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Mathayo ⚃
>> UKIACHA NENO LA MUNGU KWA SABABU YA YALE MAISHA YANAYOHARIBIKA UKAANZA KUTOSAMEHE, KUSUSA, KUZIRA, KUJAA UCHUNGU, KUJIVUNA, KUSHINDANA, KUJIKWEZA, KUTAMANI, KUTENDA KWA KIBURI, UBISHI, UKAIDI, JEURI, DHARAU, MAJUVUNO, UADUI, DHULUMA, UDANGANYIFU, UONGO, ULAFI, ULEVI, UZINZI, TALAKA, KUPELEKANA NDUGU MAHAKAMANI, N.K. HUU NI USHAHIDI WA KUFA KIROHO!!! INJILI YA YESU ILILETA MAMBO MAWILI:
2 Timothy 1:10
[10]But is now made manifest by the appearing of our Saviour Jesus Christ, who hath abolished death, and hath brought life and immortality to light through the gospel:
na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;
1) LIFE (MAISHA/UZIMA) NA 2) IMMORTALITY (KUTOHARIBIKA)
>> MAISHA YA MTOTO WA MUNGU YAMO KWENYE NENO
John 1:1,4
[1]In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
[4]In him was life; and the life was the light of men.
Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
>> MAISHA YAMO KWENYE NENO LA KRISTO!!! KULITENDA NENO NDIKO KUISHI, NA KUTOLITENDA NENO NI MAUTI!!!
>> MAISHA YAKO KWA HUYO ROHO WA NENO AU ROHO WA UZIMA/MAISHA (SPIRIT OF LIFE)
John 6:63 New Living Translation
The Spirit alone gives eternal life. Human effort accomplishes nothing. And the very words I have spoken to you are spirit and life.
63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Yohana 6:63
>> HUYU ROHO WA UZIMA au ROHO WA MAISHA NDIYE ATUPAYE UHAI/UZIMA/MAISHA YA MILELE YASIYOHARIBIKA TUNAPOLIAMINI NA KULITENDA NENO!!
>> MAISHA YETU YAKO KWA ROHO NA NENO LAKE, YAANI, KWA BABA NA MWANA, NA SIYO KWENYE FEDHA NYIIII GI, MAGARI MEEENGI, MAJUMBA MEEENGII, MASHAMBA MEEEÈNGI, VIWANDA VIIIIINGI, DHAHABU NYIIIIINGI, MADINI MEEEEEENGI, N.K. ULIVYOVIKUSANYA NA KUVIRUNDIKA DUNIANI (UMEJIWEKEA HAZINA)!!! KULIMBIKIZIA NI ULAFI!! NI TAMAA!! NI UMASKINI KIROHO, NI KUKOSA MAVAZI YA WOKOVU, NI UPOFU KIROHO, NI KUTUMAINIA USALAMA AU ULINZI DANGANYIFU, NI KUKOSA MSAADA WA MUNGU NA KUWA MASHAKANI WAKATI WOTE!!! (UFUNUO 3:15-19)
>> TAJIRI HUYU ALIDANGANYIKA KWAMBA SASA AMEYAPATIA MAISHA KWA KURUNDIKA MAZAO YAKE GHALANI, NA KUSEMA SASA NI KULA, KUNYWA, NA KUFURAHI KWA MIAKA MINGI INAYOFUATA!! UNAWEKA HAZINA DUNIANI HAPA UKIWA NA MAWAZO YALE YALE POTOFU KAMA HUYU TAJIRI!! YEYE ALIKUFA NA KUPOTEA, NA WEWE UTAKUFA NA KUPOTEA USIPOTUBU NA KUMWAMINI YESU!!! NA KISHA UKAANZA KUWEKA HAZINA MBINGUNI KWA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI ULIONAO:
Kumbuka,
Proverbs 11:4
[4]Riches profit not in the day of wrath: but righteousness delivereth from death.
Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti.
<> MALI HAZITAKUEPUSHA NA GHADHABU YA MUNGU
>> MATAJIRI-MASKINI WENGI WAMEJAA MAKANISANI NA ULIMWENGUNI!! TAJIRI WA VITU VINAVYOHARIBIKA VYA KIDUNIA LA MASKINI KWA MUNGU!!! HAWA WOTE HAWAWEZI KUINGIA MBINGUNI WASIPOTUBU "TOBA YA ZAKAYO"
3) ZAKAYO TAJIRI ALIYEJIWEKEA HAZINA MBINGUNI ( Luka 19:1-10)
1 Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake.
Luka 19:1
2 Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri.
Luka 19:2
3 Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo.
Luka 19:3
4 Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile.
Luka 19:4
5 Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako.
Luka 19:5
7 Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi.
Luka 19:7
8 Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.
Luka 19:8
9 Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu.
Luka 19:9
10 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.
Luka 19:10
>> ZAKAYO ALIKUWA NI MTOZA USHURU ANAYETAMBULIKA KWENYE JAMII YAKE KAMA MTENDA DHAMBI, TAJIRI ALIYEDHULUMU WATU, ALIYEONEA WATU, NA KUJITAJIRISHA!!
>> ALIKUWA AMESIKIA HABARI ZA YESU, NA MOYONI MWAKE ALIKUWA ANATAKA 1KUMWONA YESU NI MTU WA NAMNA GANI!!
>> ALIPOSIKIA YESU ATAPITA NJIA ILE ALIWAHI KUPANDA MKUYU ILI AWEZE KUMWONA YESU MAANA ALIKUWA NI MFUPI NA ASINGEWEZA KUMWONA YESU KWA SABABU YA UMATI WA WATU!!
>> YESU ALIPOFIKA PALE ALISIMAMA NA KUMWAMBIA ZAKAYO ASHUKE MAANA ALIKUWA AMEAZIMIA KUSHINDA NYUMBANI MWA ZAKAYO
>> WATU WAKAWA WANANUNG'UNIKA KWAMBA YESU AMEINGIA NYUMBANI MWA MTU MWENYE DHAMBI
>> ZAKAYO, KATIKA UWEPO WA MUNGU ULE, MOYO WAKE UKIMSHTAKI KWA SABABU YA DHAMBI ZAKE, AKASEMA:
"8 Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne." (Luka 19:8)
1) NUSU YA MALI YANGU NAWAPA MASKINI
2) NA KILA NILIYEMNYANG'ANYA AU KUMDHULUMU NAMRUDISHIA MARA NNE!!
>> ZAKAYO ALIGUSWA MOYO WAKE NA MUNGU, AKAJUTIA DHAMBI ZAKE, AKATUBU NA KUMWAMINI YESU, NA KISHA KUFANYA MALIPIZI PIA KWA WALE ALIOWADHULUMU!! HUU ULIKUWA NI USHAHIDI KWAMBA MOYO WAKE ULIKUWA UMEBADILIKA!! MAANA MATAJIRI HAWAPENDI KUTOA MALI ZAO KWA KIWANGO CHA ZAKAYO!!
>> ZAKAYO ALIKUWA ANAJI-"MASKINISHA" ILI KUJITAJIRISHA!!!
>> ZAKAYO ALIKUWA ANAWEKA HAZINA MBINGUNI NA HIVYO ALIKUWA AMEHAMISHA MOYO WAKE KUTOKA KWENYE SANAMU PESA, MALI, NA UTAJIRI, NA KUUWEKA MOYO HUO KWA MUNGU ALIYEMTUMAINI SASA!! AMEMWAMINI YESU SASA! ANA MOYO SAFI SASA!! HAABUDU TENA SANAMU SASA! ANAWAHURUMIA NA KUWASAIDIA MASKINI NA WAHITAJI SASA!! ANACHUKIA UOVU SASA!! ZAKAYO AMEKUWA KIUMBE KIPYA!!
>> ZAKAYO NI MWANADAMU KAMA WEWE, NA HIVYO HUTAKUWA NA UDHURU SIKU YA HUKUMU USIPOTUBU!!
1 Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia.
Yakobo 5:1
2 Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo.
Yakobo 5:2
3 Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho.
Yakobo 5:3
4 Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.
Yakobo 5:4
5 Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.
Yakobo 5:5
6 Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.
Yakobo 5:6
>> USIWE TAJIRI MUOVU MWABUDU SANAMU!! JIFUNZE KWA AYUBU, ZAKAYO, NA KORNELIO (MATENDO YA MITUME SURA YA KUMI!!)
>> RUDIA KUSOMA MAAGIZO NANE KWA MATAJIRI WALIOOKOKA ( NAKILI LINK HII: https://spiritbrideministries.blogspot.com/2023/05/maagizo-nane-kwa-matajiri-waliookoka.html)