UTAKATIFU KWENYE PESA-SEHEMU YA KWANZA
Biblia inasema, "15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu."(1 Petro 1:15-16)
>> "...........IWENI WATAKATIFU KATIKA MWENENDO WENU WOTE"
>> Biblia inakutaka wewe uliyeokoka, ukajazwa Roho Mtakatifu, kisha unaishi na kuenenda kwa huyo Roho, na unaishi hivyo kwa kulitenda na kuliishi Neno lake, kwamba UWE MTAKATIFU KWENYE MWENENDO WAKO WOTE KUHUSU PESA NA MAENEO MENGINE YOTE YA MAISHA YAKO!! HAPA NINANENA KWA HABARI YA PESA!!! UTAKATIFU KWENYE MAMBO YOTE YA PESA!! (HOLINESS IN ALL MONEY MATTERS) Katika hili tutatazama:
1) MAWAZO YASIYO SAHIHI KUHUSU PESA (ERRONEOUS THOUGHTS ABOUT MONEY)
2) MIPANGO, NIA, NA MAKUSUDI YASIYO SAHIHI KUHUSU PESA
3) HISIA ZISIZO SAHIHI KUHUSU PESA
1) MAWAZO YASIYO SAHIHI KUHUSU PESA
>> Katika hili tunasema 'siyo sahihi' kwa sababu hayapatani na Kweli! Mawazo yasiyopatana na kweli hayawezi kuwa matakatifu, bali yanakuwa ni mawazo maovu! Kweli ni Neno la Mungu (Yohana17:17) Kumbuka mawazo yamo nafsini, na mtu ni roho mwenye nafsi anayeishi kwenye mwili!! roho ina nafsi!! Mawazo hutoka kwenye roho!!
"7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai."
Mwanzo 2:7
>> Mungu alipotia roho ndani ya ule mwili, ndipo mtu huyo akawa nafsi hai!! Hivyo mtu ni roho mwenye nafsi hai!! Nafsi ina mawazo/ fikra/akili + nia/makusudi/mapenzi + hisia.
Tutakuwa tunaweka andiko ambalo linabeba mawazo na mapenzi ya Mungu na hapo hapo tutakuwa tunaeleza mawazo na fikra zisizo sahihi na za uongo zilizo kinyume na kweli zinazopelekea mtu aliyenazo kuwa na mwenendo wa uovu kwenye eneo husika!!
1) FEDHA NI JAWABU LA MAMBO YOTE
Ecclesiastes 10:19
[19]A feast is made for laughter, and wine maketh merry: but money answereth all things.
Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.
>> Fedha ni jawabu la mambo yote YANAYOHITAJI KUNUNUA!! Usimwambie Mungu akufungulie milango halafu ukaishia hapo huku una uwezo wa kumsaidia: Proverbs 3:28
"[28]Say not unto thy neighbour, Go, and come again, and to morrow I will give; when thou hast it by thee.
Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe."
>> Mpe fedha, mlipie ada, mnunulie kiwanja, mjengee nyumba, mnunulie anachokihitaji, msaidie kifedha!! Msomeshe, mfungulie mradi au kampuni, mnunulie shamba, trekta, mbolea, madawa, n.k. TATUA MATATIZO YAKE YA KIFEDHA YA SASA NA YA BAADAE!! Na namna bora ya kumsaidia kifedha ni kumpa CHANZO CHA MAPATO CHAKE MWENYEWE!! MUNGU HAKUKUBARIKI KIPESA ILI UTENGENEZE GHALA ILI UJAZE MIPESA, BALI ALIKUBARIKI NA ATAKUBARIKI KIPESA ILI UWE BARAKA KIPESA KWA MWILI WA KRISTO, UFALME WA MUNGU, NA KWA WATU WOTE WENGINE!! "2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;"
Mwanzo 12:2
>> MUNGU AMEKUSUDIA KUPITISHA PESA KWAKO KUSAIDIA MASKINI NA WAHITAJI SIKUZOTE NDANI NA NJE YA MWILI WA KRISTO, NA KUUJENGA UFALME WAKE!!!
>> FEDHA SIYO JAWABU LA MAMBO YA KIROHO (SPIRITUALLY), KIAKILI (MENTALLY), NA KIHISIA (EMOTIONALLY)
>> USIONE UMEBARIKIWA KIPESA UKAJIONA HAUMHITAJI MUNGU TENA, AMA HAUHITAJI TENA USHIRIKA NA MWILI WA KRISTO, AU HAUMHITAJI MUMEO/ MKEO TENA!!! FEDHA HIYO IMEKUSUDIWA UITUMIE KUUTUMIKIA NA KUUHUDUMIA MWILI WA KRISTO, KUIPELEKA INJILI YA YESU, KUUJENGA UFALME WA MUNGU, NA KUTENDA MEMA UKIANZIA CHUMBANI KWAKO NA NYUMBANI MWAKO. KAMA HAUTENDI MEMA KWA MKEO/MUMEO KWANZA, NA KISHA KWA WATU WA NYUMBANI MWAKO, HUKO KWINGINE KOTE UNATENDA DHAMBI YA UNAFIKI NA UDANGANYIFU!! UKIJIONA UNA FEDHA NYINGI ZA ZIADA ZISIZO NA KAZI. BADO HUJAJUA MAJUKUMU YAKO YA KIFEDHA KWENYE UFALME WA MUNGU, MAANA NI MENGI MNO KIASI KWAMBA FEDHA INAYOHITAJIKA NI NYINGI MNO LAKINI IMEKWAMA KWA WALE WAABUDU SANAMU, WALIOJIVUNA, WANAOTUMAINIA FEDHA, NA WANAOWEKA HAZINA DUNIANI!!!! MKUMBUKE TAJIRI MPUMBAVU (LUKA 12:15-21)
2) MAISHA YA MTU (UZIMA WA MTU) HAYAMO KWENYE WINGI WA VITU ALIVYONAVYO
Luke 12:15
"[15]And he said unto them, Take heed, and beware of covetousness: for a man's life consisteth not in the abundance of the things which he possesseth.
Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo."
>> KWA KUDHANI MAISHA, YAANI, USALAMA NA UHAKIKA WA MAISHA, YAMO KWENYE WINGI WA VITU ANAVYOVIMILIKI (ZIKIWEMO FEDHA), MWANADAMU ASIYEMWAMINI WALA KUMTUMAINI MUNGU AMEKUWA AKIPIGA MBIO SIKU ZAKE ZOTE ILI KUKUSANYA, KURUNDIKA, NA KULIMBIKIZA FEDHA NA MALI KAMA ALIVYOFANYA HUYU TAJIRI MPUMBAVU (LUKA 12:15-21): ALIPOMALIZA KULIMBIKIZA NA KUDHANI KUWA KILICHOBAKI SASA NI KUTUMBUA NA "KULA BATA" (KAMA WANAVYOSEMA LEO) USIKU ULE AKAAMBIWA NA MUNGU,
Luke 12:20
"[20]But God said unto him, Thou fool, this night thy soul shall be required of thee: then whose shall those things be, which thou hast provided?
Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?"
>> ALIKUWA AMEPOTOKA KWENYE FIKRA, AKILI, NA MAWAZO YAKE KUHUSU PESA NA MALI! MTIZAMO WAKE ULIKUWA POTOFU!! TAMAA ILIMPOFUSHA ASIONE NINI ALIKUWA ANATAKIWA KUFANYA!! HAKUWA NA "AKILI" ITOKAYO KWA MUNGU KUPITIA NENO LAKE LILILO HAI (YESU)!! AKAFA, AKAANGAMIA, NA MALI NA FEDHA ALIZOZIKUSANYA WAKALA WENGINE!!
18 Nami nikaichukia kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo chini ya jua; maana sina budi kumwachia yeye atakayenifuata.
Mhubiri 2:18
19 Naye ni nani ajuaye kama huyo atakuwa mwenye hekima au mpumbavu? Hata hivyo atatawala juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo, ambamo ndani yake mimi nimeonyesha hekima chini ya jua. Hayo nayo ni ubatili.
Mhubiri 2:19
>> MAISHA TELE NA UZIMA TELE YAKO KWA YESU ALIYEFUFUKA KUTOKA KWA WAFU (YOHANA 10:10)
>> UKIDHANI FEDHA TU INATOSHA UMEDANGANYIKA!! UKIFIKIRI KWAMBA UKIPATA FEDHA UNAZOZITAKA SANA UMEYAPATIA MAISHA, UMEDANGANYIKA!!
UZIMA AU MAISHA YAKO KWA ROHO MTAKATIFU!!!
John 6:63
[63]It is the spirit that quickeneth; the flesh profiteth nothing: the words that I speak unto you, they are spirit, and they are life.
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
>> YESU NI ROHO ANAYEHUISHA (QUICKENING SPIRIT/ SPIRIT OF LIFE)
1 Corinthians 15:45
[45]And so it is written, The first man Adam was made a living soul; the last Adam was made a quickening spirit.
Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.
>> MAISHA YAKO KWENYE NENO LA KRISTO!! UKILIAMINI UTAKUWA HAI!!
John 1:1,3-4
"[1]In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
[3]All things were made by him; and without him was not any thing made that was made.
Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
[4]In him was life; and the life was the light of men.
Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu."
>> MAISHA YA MTAKATIFU YAMO NDANI YAKE NENO LA UZIMA!! MAISHA YA MTEULE NI MAISHA YA KRISTO YESU YA NENO ALIYOYAISHI YEYE MWENYEWE KWENYE MWILI!!
>> INJILI YA YESU ILILETA AMA ILIFUNUA MAISHA NA KUTOHARIBIKA (LIFE AND IMMORTALITY)
"2 Timothy 1:10
[10]But is now made manifest by the appearing of our Saviour Jesus Christ, who hath abolished death, and hath brought life and immortality to light through the gospel:
na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;"
>> BILA YESU UNAWEZA KUMILIKI PESA YOTE YA DUNIA LAKINI HAITAKUSAIDIA KITU MAANA UTAIACHA NA KUANGAMIA MILELE!! Hii ndiyo maana Yesu alisema,
Matthew 16:26
[26]For what is a man profited, if he shall gain the whole world, and lose his own soul? or what shall a man give in exchange for his soul?
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
>> KABLA YA FEDHA AU PESA JIFIKIRIE WEWE MWENYEWE NAFSI YAKO KWANZA!! YESU ANA HAJA NA WEWE!! YEYE ALIKUJA KUKUTAFUTA WEWE ULIYEPOTELEA KWENYE IBADA YA SANAMU AU mungu PESA, ILI AKUOKOE (Luka 19:10)
>> WEWE MWINGINE UMO KANISANI LAKINI BADO NI MWABUDU SANAMU PESA, NA NDIYO MAANA BADO UNADHULUMU PESA, UNATAPELI FEDHA, UNAPOKEA RUSHWA, UNATANGATANGA HUKO NA HUKO KUVUNJIWA LAANA YA UMASKINI, UNAKWENDA KUTABIRIWA KWA MANABII WAKO, UNAITHAMINI PESA KULIKO MAMBO YA MUNGU, N.K. UNAPENDA FEDHA KULIKO MUNGU NA WANADAMU!! NA WALA HUMTAKI MUNGU BALI UNATAKA TU AKUBARIKI KIFEDHA!!
3) MPENDA FEDHA KAMWE HAUTASHIBA FEDHA
"Ecclesiastes 5:10
New International Version
Whoever loves money never has enough; whoever loves wealth is never satisfied with their income. This too is meaningless.
Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba nyongeza. Hayo pia ni ubatili."
>> Ndugu mpendwa mchungaji, usipowajua watu wa namna hii utashangaa unasema weeeee lakini hawabadiliki! Mbio zao siyo ndani ya Yesu ili kumjua zaidi Yesu, kumpendeza zaidi Yesu, kufanana zaidi na Yesu, na kumtumikia zaidi Yesu; BALI HAWA MBIO ZAO NI KUPATA FEDHA ZAIDI NA ZAIDI! NA KADIRI WANAVYOZIPATA NDIVYO WANAVYOZITAKA ZAIDI NA ZAIDI MAANA KAMWE HAWATOSHEKI! HAWA WANAPENDA FEDHA NA MALI KULIKO YESU!! HAWAWEZI KUJALI MAMBO YA YESU KUTOKA MIOYONI MWAO!! HAWATOSHEKI NA FEDHA WALA MALI ZINAZOONGEZEKA! HAWA HAWATATOSHEKA MPAKA WATUBU DHAMBI ZAO NA KUFUNGULIWA KWENYE KIFUNGO CHA TAMAA ZAO!!
>> HUJAWAHI KUONA KANISANI WATU WANAONEKANA MATAJIRI AU WANAZO LAKINI SIYO WATOAJI KABISA??!! WALA SIYO WASAIDIAJI??!! WALA HAWATOI MPAKA IPIGWE BARAGUMU??!! FEDHA IMO MOYONI!!! FEDHA HATA IKIONGEZEKA HAIWATOSHI KAMWE!! ONGEZEKO LA MALI HALIWATOSHI PIA!!!
WANAENDESHWA NA TAMAA ISIYOSHIBA INAYOWAVUTA KUZIMU!!!
6 Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
1 Timotheo 6:6
7 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;
1 Timotheo 6:7
8 ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.
1 Timotheo 6:8
9 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
1 Timotheo 6:9
10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
1 Timotheo 6:10
11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.
1 Timotheo 6:11
>> FEDHA NA MALI SIYO TATIZO ILA TAMAA YA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI NI roho za shetani!! Ndoa zimevurugwa na hata kuvunjika, wateule wamesalitiana, wamefarakana, wamepelekana mahakamani, huduma zimeyumba hata kufa, migogoro ya uongozi haiishi, n.k. kwa SABABU YA WAABUDU SANAMU WAPENDA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI!!! HAWA HAWANA YESU MIOYONI MWAO HATA KAMA WANAITWA WATUMISHI, AU WAMO MAKANISANI MIAKA MINGI, AU NI VIONGOZI, WOTE NI WAOVU AMBAO WASIPOTUBU NA KUMGEUKIA BWANA WATAANGAMIA WOTE MILELE!!
5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.
Waebrania 13:5
New International Version
Keep your lives free from the love of money and be content with what you have, because God has said, “Never will I leave you; never will I forsake you.”
>> WENGINE WANAPENDA FEDHA KULIKO WAUME/WAKE ZAO, WATOTO WAO, NDUGU ZAO, WATEULE WATAKATIFU WENZAO, NA HATA YESU MWENYEWE!!! FEDHA YAO NI YAO WAO TU, LAKINI YAKO NI YAO PIA!! AKITAKIWA KUSAIDIA ANAJITETEA KUWA ANA MAJUKUMU MEEENGI YA KIFEDHA NA HIVYO HAWEZI KUSAIDIA!!! ( ingawa anaweza kusaidia!!)
>> MPENDA FEDHA ANAUMIA SANA HISIA ZAKE ANAPOTAKIWA AU KULAZIMIKA KUTOA PESA, IWE NI NYUMBANI, KAZINI, KANISANI, AU POPOTE!! MAANA KWA KUWA PESA HAIMTOSHI SIKUZOTE YEYE HUWA ANATAKA IINGIE TU ISITOKE!!! AU IINGIE KUMI ITOKE MOJA AU PUNGUFU YA MOJA!! Mpenda pesa ni mbahili, mchoyo, mlafi, na mwenye tamaa!
4) MKOPESHE MUNGU USIMKOPESHE MWANADAMU
Proverbs 19:17
[17]He that hath pity upon the poor lendeth unto the LORD; and that which he hath given will he pay him again.
Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.
>> WAPENDA FEDHA WOTE HAWAISHI KWA IMANI WALA HAWAWEZI KUMTEGEMEA MUNGU MIOYONI WAO
>> Hii ndiyo maana huwa wakitoa fedha kumkopesha mtu yeyote huwa ni wenye kudai sana!! Maana tumaini lao lipo kwenye fedha na siyo Mungu
>> LAKINI ANDIKO LINASEMA UKIMHURUMIA MASKINI UNAMKOPESHA MUNGU!! NAYE MUNGU ATAKULIPA KWA TENDO LAKO JEMA!! KUMBE MUNGU ANATUBARIKI KWA FEDHA NA MALI ILI TUZITUMIE KUTENDA MEMA!!! NA MTINDO WA KIFALME (ROYAL STYLE) NI KUMKOPESHA MUNGU BABA YETU WA MBINGUNI!!! TUMEOKOLEWA KWA NEEMA ILI TUDUMU KATIKA MATENDO MEMA SIKUZOTE ZA MAISHA YETU!!
8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
Waefeso 2:8
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Waefeso 2:9
10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Waefeso 2:10
MST WA 10:
>>TULIUMBWA MARA YA PILI NDANI YA KRISTO YESU ILI TUTENDE MEMA!!!
>> MEMA AMBAYO TOKEA KABLA HATUJAZALIWA MUNGU ALISHAYATENGENEZA ILI SISI TUJE TUENENDE NAYO NDANI YA YESU!!
>> MEMA HAYO TUNAYAFANYA KWA BIDII NA JUHUDI ZOTE KADIRI YA NEEMA YAKE ANAYOTUJALIA, NA HIVYO HATUWEZI KAMWE KUJISIFU MAANA,
Philippians 2:13
[13]For it is God which worketh in you both to will and to do of his good pleasure.
Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
>> NI MUNGU ATENDAYE KAZI HIZO NJEMA NDANI YETU
>> YEYE ANATUPA KUTAKA (TO WILL) NA KISHA ANATUWEZESHA KUTENDA (TO DO)
>> HIVYO TUNATENDA SAWASAWA NA MAKUSUDI NA MAPENZI YAKE
>> NDIYO MAANA ANAHITAJI MOYO SAFI ULIOOSHWA KWA DAMU YAKE, NA UNAOENDELEA KUTAKASWA NA KWELI YAKE (NENO LAKE!) WATAKATIFU WA NAMNA HII WANAMTII KWENYE MAMBO YOTE!! HAWAMZUILII ISAKA WAO ASICHINJWE!!!
>> UKIMKOPESHA MUNGU YEYE HUWA ANALIPA HIVI:
Luke 6:38
[38]Give, and it shall be given unto you; good measure, pressed down, and shaken together, and running over, shall men give into your bosom. For with the same measure that ye mete withal it shall be measured to you again.
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
>> UNAAMINI HAYA??!!
5) USIKOPESHE WANADAMU FEDHA KWA RIBA NA FAIDA, AMA UTAZIACHA AU ZITAKUACHA
"8 Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini"
Mithali 28:8
>> HII INAONYESHA WAZIWAZI KWAMBA ANAYEKOPESHA WANADAMU NA KUWATIA UTUMWANI HANA HURUMA ZA YESU!! NA HII NDIYO MAANA MUNGU ANAMPENDA YULE ANAYEWAHURUMIA MASKINI MAANA MOYO WENYE HURUMA NI WA MUNGU, NA MOYO USIO NA HURUMA NI WA SHETANI!!
>> ANAYEJIKUSANYIA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI KWA KUKOPESHA WATU AJUE ANAMKUSANYIA TU YULE MWENYE KUMKOPESHA MUNGU KWA KUWAHURUMIA MASKINI NA WAHITAJI!!
>> BWANA WETU YESU ALISEMA,
34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.
Luka 6:34
35 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.
Luka 6:35
36 Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
Luka 6:36
>> HAKUNA THAWABU YA KUKOPESHA NA KISHA KUTUMAINI KULIPWA
>> THAWABU IPO KWENYE KUKOPESHA NA KUTOTARAJIA KULIPWA!!
>> ASIYETARAJIA KULIPWA HAWEZI KUDAI MPAKA KUBURUZA ANAOWADAI MAHAKAMANI AU KUGOMBANA NAO MPAKA KUVUNJA MAHUSIANO NAO!! HII NI MATOKEO YA KUABUDU SANAMU PESA!!
>> BAADA YA KUSISITIZA KUTOTUMAINI KULIPWA, HAPA ANASISITIZA IWENI NA HURUMA KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
>> HII INA MAANA KAMA MUNGU NI BABA YAKO KWELI, HUWEZI KUKOSA KUWAHURUMIA MASKINI NA WAHITAJI, (KUMKOPESHA BWANA) YAANI, HUWEZI KUFANYA HILI:
Proverbs 22:7
[7]The rich ruleth over the poor, and the borrower is servant to the lender.
Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.
>> HUWEZI KUMTAWALA MASKINI KWA MIKOPO YAKO INAYOMTIA KWENYE UTUMWA WA MADENI!! HUU NI UOVU NA NI roho YA UKANDAMIZAJI (spirit of oppression) KUTOKA KWA SHETANI!!
>> UNAPOMKOPESHA BWANA HUPOTEZI BALI UNAKUWA UMEWEKA AKIBA KWAKE!! NAYE AMESEMA HAPO JUU KWAMBA THAWABU YAKO ITAKUWA NYINGI NAWE UTAKUWA MWANA WA MUNGU KWELI KWELI!! NA MWISHO KABISA AKAONYESHA INAVYOTAKIWA KUFANYWA:
Luke 6:38
[38]Give, and it shall be given unto you; good measure, pressed down, and shaken together, and running over, shall men give into your bosom. For with the same measure that ye mete withal it shall be measured to you again.
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
>> HIVI NDIVYO ANAVYOLIPA WANAOMKOPESHA YEYE
Tukutane sehemu ya pili
Tags
MAHUBIRI