HAWA MANABII WAKO WA UONGO WATAKUPELEKA JEHANAMU USIPOTUBU!

 


1) Matthew 7:15-16

[15]Beware of false prophets, which come to you in sheep's clothing, but inwardly they are ravening wolves. 

Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

[16]Ye shall know them by their fruits. Do men gather grapes of thorns, or figs of thistles? 

Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

2) 20 Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. 

Kumbukumbu la Torati 18:20

21 Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana? 

Kumbukumbu la Torati 18:21

22 Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope 

Kumbukumbu la Torati 18:22


3) 1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 

Kumbukumbu la Torati 13:1

2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 

Kumbukumbu la Torati 13:2

3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 

Kumbukumbu la Torati 13:3

4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye. 

Kumbukumbu la Torati 13:4

5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako. 

Kumbukumbu la Torati 13:5

Biblia inasema;

1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. 

2 Petro 2:1

2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. 

2 Petro 2:2

3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii. 

2 Petro 2:3

4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu; 

2 Petro 2:4

5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu; 

2 Petro 2:5

6 tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya; 

2 Petro 2:6

7 akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu; 

2 Petro 2:7

8 maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria; 

2 Petro 2:8

9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu; 

2 Petro 2:9

10 na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka. 

2 Petro 2:10

11 Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa malaika ambao ni wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele za Bwana. 

2 Petro 2:11

12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao; 

2 Petro 2:12

13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi; 

2 Petro 2:13

14 wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana; 

2 Petro 2:14

15 wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu; 

2 Petro 2:15

16 lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule. 

2 Petro 2:16

17 Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa. 

2 Petro 2:17

18 Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu; 

2 Petro 2:18

19 wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule. 

2 Petro 2:19

20 Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. 

2 Petro 2:20

21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa. 

2 Petro 2:21

22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni. 

2 Petro 2:22

Imeandikwa pia:

21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 

Mathayo 7:21


22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 

Mathayo 7:22


23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. 

Mathayo 7:23


HAWA:

1)WALITOA UNABII KWA USAHIHI KWA JINA LA YESU

2) WALITOA PEPO KWA JINA LA YESU

3) WALIFANYA MIUJIZA KWA JINA LA YESU

>> LAKINI YESU ATAWAAMBIA A) "SIKUWAHI KUWAJUA NINYI", B) "ONDOKENI KWANGU WATENDA MAOVU NINYI!!" 

>> UNADHANI HAWA WATAKATALIWA PEKE YAO??!! HUKUSOMA?


Matthew 15:14

[14]Let them alone: they be blind leaders of the blind. And if the blind lead the blind, both shall fall into the ditch. 

Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

>> NA WEWE UNAPIGA MBIO KUTOKA NABII HUYU HADI YULE, NA KUOMBEWA NA KUTABIRIWA, NA KUFUATA MIUJIZA: OLE WAKO!!!! WEWE NA MANABII WAKO MTAELEKEA SHIMONI USIPOTUBU!!

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post