*UTAJIRI WA KWELI NI WA MOYONI*
*2 Corinthians 9:6-8*
"6Remember this: Whoever sows sparingly will also reap sparingly, and whoever sows generously will also reap generously. 7Each of you should give what you have decided in your heart to give, not reluctantly or under compulsion, for God loves a cheerful giver. 8And God is able to bless you abundantly, so that in all things at all times, having all that you need, you will abound in every good work."
2 Wakorintho 9:6-8
"6Kumbuka hili: Yeye apandaye kwa ubahili (au unyimivu) naye atavuna kwa unyimivu, Naye yote apandaye kwa ukarimu ( utele) naye atavuna kwa utele pia. 7 Kila mmoja wenu atoe kama alivyokusudia moyoni mwake kutoa, siyo kana kwamba kwa kulazimishwa, au si kwa moyo wa kupenda, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu na wa kupenda. 8 Na Mungu anaweza kukubariki kwa vingi sana ( kukutajirisha), ili kwamba katika mambo yote na sikuzote, ukiwa na kila unachokihitaji kwa wingi, upate kutenda kila tendo jema ( kutenda mema) kwa wingi kila mahali."
Mungu hajakubariki ili uwe mbinafsi na ujione bora kwa kuwa umebarikiwa kuliko wengine!! Waovu na watenda dhambi ndio wanaojivuna, wanaojikweza, na kuwadharau wasio navyo, na kuwabagua na kujitenga nao!! ALIYEBARIKIWA ANA HURUMA NA UPENDO WA MUNGU, NI MKARIMU NA MTOAJI SANA SANA SIKUZOTE, MAHALI POTE, WAKATI WOTE, HACHAGUI WALA HABAGUI, HACHOKI WALA HAACHI KUTENDA MEMA!! FEDHA NA MALI ZAKE NI KWA AJILI YA UTUMISHI HUU WA KUKIRIMU NA KUSAIDIA WENGINE!!! YEYE ANAJIWEKEA HAZINA MBINGUNI!!
17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. (1 Timotheo 6:17)
18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;
1 Timotheo 6:18
19 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli. (1 Timotheo 6:19)
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. (Ufunuo wa Yohana 3:17)
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. (Ufunuo wa Yohana 3:18)
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
Ufunuo wa Yohana 3:19
Luke 18:25
[25]For it is easier for a camel to go through a needle's eye, than for a rich man to enter into the kingdom of God.
Kwa maana ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
KWA NINI?☝️☝️☝️👉👇SOMA JIBU
Psalms 62:10
[10]Trust not in oppression, and become not vain in robbery: if riches increase, set not your heart upon them.
Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang’anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
>> TATIZO NI MALI, FEDHA, NA UTAJIRI KUINGIA MOYONI, NA KUMWONDOA MUNGU MOYONI HUMO
>> NI MATAJIRI WANGAPI AMBAO MALI HAZIMO MIOYONI MWAO??!!🙇🏻♂️
>> MATAJIRI WASIO NA MALI MOYONI HUWA HAWALIMBIKIZI WALA KUJIKUSANYIA UTAJIRI, BALI HUTAWANYA!
24 Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
Mithali 11:24
>> TAWANYA UONGEZEWE, ZUIA/NYIMA/KUWA BAHILI/ KUWA MCHOYO/LIMBIKIZA UMKOSE MUNGU MAANA UNAABUDU SANAMU NA mungu PESA!!
>> HAYA NI MAKUNDI MAWILI YA WANADAMU! 1) WABINAFSI/WACHOYO/WABAHILI, 2) WAKARIMU/WENYE HURUMA/ WATOAJI!! WA KWANZA HUWEKA HAZINA DUNIANI, WA PILI HUWEKA HAZINA ZAO MBINGUNI
19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; (Mathayo 6:19)
20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
Mathayo 6:20
21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Mathayo 6:21
>> HAZINA AU AKIBA YAKO YA THAMANI ILIPO NDIPO NA MOYO WAKO ULIPO!! UKIWEKA HAZINA DUNIANI MOYO WAKO UTAKUWA DUNIANI, NA KAMWE HAUWEZI KUWA KWA MUNGU JUU!!
MOYO WAKO UKIWA DUNIANI KWENYE HAZINA YAKO INAMAANISHA UNAPENDA, NA KUTHAMINI, NA KUZITEGEMEA FEDHA, MALI, NA UTAJIRI WAKO KULIKO MUNGU!! UTAINGIAJE MBINGUNI WAKATI UNAABUDU SANAMU!!! MOYO WAKO UTAJAA MAOVU MENGI "
10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi."
1 Timotheo 6:10
Luke 16:13 New International Version
“No one can serve two masters. Either you will hate the one and love the other, or you will be devoted to the one and despise the other. You cannot serve both God and money.”
13 Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Luka 16:13
UPENDO WA MOYO HAUWEZI KUGAWANYIKA!!! AMA UMPENDE MUNGU KWA MOYO WAKO WOTE, AMA UPENDE KINGINE AU MWINGINE!!! USIJIDANGANYE!!
6 Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. (1 Timotheo 6:6)
7 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;
(1 Timotheo 6:7)
8 ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. (1 Timotheo 6:8)
9 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. (1 Timotheo 6:9)
Psalms 49:16-17
[16]Be not thou afraid when one is made rich, when the glory of his house is increased;
Usiogope mtu atakapopata utajiri, Na fahari ya nyumba yake itakapozidi.
[17]For when he dieth he shall carry nothing away: his glory shall not descend after him.
Maana atakapokufa hatachukua cho chote; Utukufu wake hautashuka ukimfuata.
4 Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.
Mithali 23:4
5 Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.
Mithali 23:5
41 Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.
Marko 12:41
42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.
Marko 12:42
43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;
Marko 12:43
44 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
Marko 12:44
>> MUNGU HAANGALII UNACHOTOA LAKINI ZAIDI SANA HUTAZAMA MOYO UNAOTOA
[2]And I will make of thee a great nation, and I will bless thee, and make thy name great; and thou shalt be a blessing:
nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
>> LENGO LA WEWE KUBARIKIWA NI ILI UWE BARAKA KWA KANISA NA KWA ULIMWENGU WOTE
>> HAUBARIKIWI ILI UJENGE GHALA NA KISHA KUZIHIFADHI BARAKA HIZO ILI ULE NA KUNYWA MILELE! HUU NI UCHOYO, UBAHILI, TAMAA, NA UBINAFSI WA SHETANI