UBINAFSI NA CHUKI

                                          Corrie ten Boom Quote: Forgiveness is the key that unlocks the door of  resentment and the handcuffs of hatred. It is a power that breaks the  chains of bitterness and the shackles

[DHAMBI MOYONI= UBINAFSI + CHUKI]
A: UBINAFSI
Moyo uliojaa ubinafsi una:
1) roho ya kiburi (spirit of pride)
2) roho ya ubishi ( spirit of stubbornness)
3) roho ya ukaidi (spirit of obstinacy)
4) roho ya jeuri ( spirit of rudeness)
5) roho ya dharau (spirit of contempt)
6) roho ya majivuno ( spirit of arrogance)
>> moyo wa namna hii hupelekea mtu kutafuta, SIKUZOTE, faida yake, manufaa yake, mafanikio yake, heshima yake, shukrani zake, sifa zake, utukufu wake, kibali chake, NA KILA KITU KINACHOMHUSU YEYE KWANZA, NA SIYO WEWE AU MWINGINE YEYOTE!!! Mtu wa namna hii SIKUZOTE hujihesabia haki, hujitetea, hujifikiria yeye kwanza, hujiinua, hujitanguliza, huringa, hujionyesha, hupenda na hutafuta sifa za watu, heshima za watu, shukrani za watu, na utukufu wa watu, hukandamiza wengine, hudhulumu wengine, huburuza wengine, hupunja wengine, huwatumia wengine kwa faida yake, hupenda na hutaka kuwa wa kwanza, hupenda Na hutaka kushindana na wengine, hupenda na hutaka kuwashinda wengine, hupenda na hutaka kuwazidi wengine, hupenda na hutafuta kuonewa wivu, kustaajabiwa, na hata kusujudiwa na wengine! Mtu wa namna hii hapendi na hataki KUZIDIWA NA YEYOTE NA KUSHINDWA NA YEYOTE MAANA ANAAMINI YEYE NI BORA ZAIDI YA WENGINE WOTE, HATA WEWE UKIWEMO!! Mtu wa namna hii hupenda kujilinganisha na wengine na kujipima nao!! AKIWA NA MALI, ELIMU, CHEO, AU PESA NA MAFANIKIO YOYOTE HUJIONA BORA KULIKO WOTE ALIOWAZIDI! NA WALE WALIOMZIDI HUWA NA WIVU NAO NA KUTAMANI KILA WALICHONACHO!!
AKITUMIWA KWA VIPAWA NA KARAMA ZA KIROHO, HUJIVUNA NA KUJIONA BORA KULIKO WOTE. WASIOTUMIKA HIJVYO!! AKITUMIWA NA MUNGU KWA ISHARA, MAAJABU, NA MIUJIZA HUJIONA NI KWA SABABU YEYE NI WA KIROHO ZAIDI KULIKO WENGINE, MTAKATIFU ZAIDI KULIKO WENGINE, NA AKIENDELEA HIVI HUJA KUDHANI NI UPAKO WAKE NA NGUVU ZAKE YEYE ZINAZOTENDA NA HUJIONA KAMA mungu mtu!! Mbinafsi hupenda kubishana na kushindana!! Mbinafsi hapendi, hakubali, na hataki kushindwa!! Huwa anajivunia nguvu na uweza wake wa kibinadamu!! Mbinafsi sikuzote anajiona yuko sahihi na wewe au mwingine yeyote amekosea! UBINAFSI KWENYE NDOA UNALETA MAUMIVU, MISUGUANO, MAGOMVI, MIVUTANO, NA KUPELEKEA KUACHANA!! MUME NA MKE WAKIWA WABINAFSI HUWA HAMNA SULUHU KWENYE NDOA NA MWISHO NI KUFARAKANA!! Ubinafsi ni sumu kuu ya kuua mahusiano! MBINAFSI HAWEZI KUMUABUDU MUNGU WALA KUMPENDA MAANA HANA UNYENYEKEVU UNAOTAKIWA MBELE ZA MUNGU, NA HAWEZI KUTAFUTA SIFA, SHUKRANI, HESHIMA, NA UTUKUFU WA MUNGU MAANA YEYE MBINAFSI ANAYATAKA YEYE HAYA YOTE! Mbinafsi akija Kanisani au akijidai ameokoka ni kwa sababu anatafuta faida yake!! Na kamwe hatafuti faida na manufaa ya Kristo au mwanadamu au kanisa Bali faida yake! Mbinafsi hawezi kumcha Mungu na kamwe hana uzima wa milele!! UBINAFSI NI KINYUME CHA UPENDO WA MUNGU!! YAANI, MBINAFSI HANA NA KAMWE HAWEZI KUWA NA UPENDO WA MUNGU NA WANADAMU!! Mbinafsi hapendi na hataki kuonywa wala kukaripiwa! Akionywa Na kukaripiwa hukasirika, hununa, na kuzira! Dhambi imo moyoni mwake na zile roho sita za shetani tulizoanza nazo huwa hazipendi kusemwa semwa!! ( kiburi, ubishi, ukaidi, jeuri, dharau, na majivuno)! Nazo ndizo zinazounda MOYO MGUMU AU MOYO WA JIWE usio na toba wala unyenyekevu!! Mbinafsi sikuzote huwa anaona makosa na mapungufu ya wengine, na kamwe haoni wala hayatazami ya kwake!! Mbinafsi ni hushughulika na vibanzi tu vya wengine huku boriti aliyonayo haishughulikii wala kuigusa kamwe!! Mbinafsi anapenda kuwatendea wengine yale asiyopenda kutendewa yeye mwenyewe. Mbinafsi hupenda na hutaka kupokea tu zaidi kuliko kutoa!! Mbinafsi HAKUJALI WEWE KAMWE ILI MRADI MAMBO YAKE YANAMWENDEA VEMA!! Mbinafsi atakutumia na kukuacha peke yako akishakufanikisha jambo lake. Mbinafsi akija kwako ni kwa sababu anatafuta faida fulani, na hivyo uhusiano wake huwa sio wa kweli kutoka moyoni!! Kwenye ndoa mke mbinafsi ana roho ya Delila wa Samsoni, na mume mbinafsi ana roho ya Mfalme Ahasuero wa Vashti malkia!! Mfalme Selemani alioa wake wengi kwa kuongozwa na tamaa za kibinafsi!! MBINAFSI ANATAWALIWA NA TAMAA ISIYOISHA
  Mungu aliwaua Anania na Safira (Matendo 5:1-11) KUONDOA UBINAFSI KANISANI KWENYE KANISA AMBALO HALIKUWA NA UBINAFSI WOWOTE!!

Upendo wa Mungu UKO KINYUME NA UBINAFSI NA ULILETWA KWETU ILI KUONDOA UBINAFSI MIOYONI MWETU!!

1 John 3:16 (New International Version)

This is how we know what love is: Jesus Christ laid down his life for us. And we ought to lay down our lives for our brothers and sisters.

16 Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. 

1 Yohana 3:16

>> TUMEUJUA UPENDO; TULIUONA

 UPENDO PALE YESU ALIPOUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YETU

>> KWA HIVYO, NA SISI TUKIWA NA UPENDO HUO HUO MIOYONI MWETU, IMETUPASA NA SISI KUUTOA UHAI WETU KWA AJILI YA HAO NDUGU ZETU (KWA AJILI YA KANISA, AMBALO NI MWILI WA KRISTO)

>> ANAPOSEMA ' IMETUPASA' ANAMAANISHA NI LAZIMA, AMA TUNALAZIMIKA NA SISI KUUTOA UHAI WETU KWA AJILI YA NDUGU ZETU KATIKA MWILI WA KRISTO!! UKIUTOA UHAI WAKO KWA AJILI YA NDUGU ZAKO, HAKUNA KITU CHOCHOTE AMBACHO UTAWEZA KUWAZUILIA, AU KUWANYIMA, AMA KUTOWAPA!!! MAANA UMEJITOA WEWE MWENYEWE UHAI WAKO KWA AJILI YAO, UMEJITOA VYOTE VILE ULIVYO KWA AJILI YAO, NA VYOTE ULIVYONAVYO KWA AJILI YAO!! HAUNA CHAKO TENA KWA KUWA WEWE NA VYOTE ULIVYONAVYO NI MALI YAO!! KILA MMOJA KWENYE MWILI WA KRISTO AKIFANYA HIVI HAIWEZEKANI PAKAWEPO UHITAJI WA AINA YOYOTE KANISANI, KIROHO (SPIRITUALLY), KIAKILI (MENTALLY), KIHISIA (EMOTIONALLY), KIMWILI (PHYSICALLY), KIFEDHA (FINANCIALLY), KIMALI NA VITU (MATERIALLY), NA KIJAMII (SOCIALLY)

>> UHITAJI KANISANI NI ZAO LA UBINAFSI KANISANI, NA UBINAFSI KANISANI NI ZAO LA KUKOSEKANA UPENDO WA MUNGU KANISANI

1 John 5:2

[2]By this we know that we love the children of God, when we love God, and keep his commandments. 

Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.

>> YAANI, KAMA KWELI UNAMPENDA MUNGU, NA KUZISHIKA AMRI ZAKE, LAZIMA UTAWAPENDA WATOTO WA MUNGU!! UPENDO WAKO KWA MUNGU UNAONEKANA PALE UNAPOWAPENDA WATOTO WA MUNGU!! NA HII NDIYO AMRI MPYA YA AGANO JIPYA!! HII SIYO MOJA YA ZILE AMRI KUU MBILI ZA UPENDO ZA TORATI, BALI NI AMRI MPYA!! NAYO NI:

34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. 

Yohana 13:34

>> WATOTO WA MUNGU, WATAKATIFU, WALIO WA- KRISTO, WAMEAGIZWA KUPENDANA WAO KWA WAO, VILE VILE KAMA KRISTO ALIVYOWAPENDA!! YAANI, KILA MMOJA IMEMPASA KUUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YA NDUGU ZAKE (1 YOHANA 3:16)

12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. (Yohana 15:12)

13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. (Yohana 15:13)

14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. (Yohana 15:14)

35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.(Yohana 13:35)

>> PALE KILA MKRISTO MTAKATIFU KWENYE MWILI WA KRISTO ATAKAPOUTOA UHAI WAKE KWA AJILI YA WENGINE KWENYE MWILI, NDIPO DUNIA ITAONA, NA KUTAMBUA, NA KUFAHAMU, NA KUJUA KWAMBA HUU WANAOUONA NDIO UPENDO HALISI WA KRISTO!! KAMA DUNIA INAYOLIZUNGUKA KANISA NYUMBANI, MTAANI, KAZINI, KWENYE BIASHARA, N.K. HAIWEZI KUSHUHUDIA UPENDO ULE ULE WA KRISTO KANISANI MIONGONI MWA NDUGU KATIKA KRISTO, NI DHAHIRI KANISA HILO LINAVUNJA AMRI MPYA YA YESU, NA HIYO INAMAANISHA UBINAFSI UMO KANISANI!!! JE! USHUHUDA WA JAMII INAYOKUZUNGUKA NI UPI? JE! JAMII HIYO INAONA NA KUKIRI KWAMBA HAKIKA MNAPENDANA NA NI WANAFUNZI WA YESU KWELI KWELI!!

24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake. 

(1 Wakorintho 10:24)

Na tena,

3 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. 

Wafilipi 2:3

4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

 Wafilipi 2:4

5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;

 Wafilipi 2:5

DHAMBI MOYONI = UBINAFSI + CHUKI

Tukutane kwenye CHUKI!!!

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post