NURU KAZI YAKE NI KUFUKUZA NA KUONDOA GIZA!!!

>> UKIMWONA MKRISTO, MTUMISHI, MCHUNGAJI, MTUME, AU YEYOTE ANAONGELEA HABARI ZA KWAMBA ZAMANI KANISA LILIKUWA BORA ZAIDI KULIKO LEO, AU MTU ANAYETAMANI MAISHA YA ZAMANI KWA KUWA YALIKUWA BORA ZAIDI KULIKO MAISHA YA LEO, AU ANAYEDAI HUDUMA YAKE ZAMANI ILIKUWA BORA ZAIDI ZAIDI KULIKO LEO, HUYO HANA NURU, NI KIPOFU, AMEPOTEZA MWELEKEO, AMEACHA KUENENDA KATIKA UPENDO, ANA WAZIMU WA KULAUMU NA KUKOSOA KOSOA NA KUHUKUMU WENGINE!! KWA NINI ULALAMIKIE AU UNUNG'UNIKIE GIZA WAKATI WEWE NI NURU???!!! UMEWAHI KUONA NURU INAYOLALAMIKA KWAMBA GIZA LIMEZIDI SIKU ZA MWISHO!!! NURU YENYEWE HUWA INANG'AA TU NA GIZA HUWA LINAKIMBIA SIKUZOTE!!! WALALAMIKAJI NDIO WALE WASIO NA NURU MIOYONI MWAO YA KUFUKUZA GIZA!!! WAMERUDI NYUMA!!! WAMEPOA NA KUWA BARIDI, WAMEKUWA VUVU VUGU!! WAMEUACHA UPENDO WA KWANZA!!! WANAHANGAIKIA NA KUSHUGHULIKIA NA KUYATAFUTA MAMBO YANAYOHARIBIKA YA DUNIA HII TU AMBAYO NI YA ZIADA, HUKU WAMEUPA UFALME WA MUNGU KISOGO KINYUME NA MAANDIKO!! (MATHAYO 6:33) ISAYA ALISEMA WAZIWAZI 

"1 Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia."

Isaya 60:1

>> UKIMFUATA YESU HAUWEZI KWENDA GIZANI BALI UNAKUWA NA NURU YA UZIMA John 8:12

[12]Then spake Jesus again unto them, saying, I am the light of the world: he that followeth me shall not walk in darkness, but shall have the light of life. 

Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima."

"2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako."

Isaya 60:2

>> GIZA LAZIMA LIIFUNIKE DUNIA KATIKA SIKU ZA MWISHO!! UNASHANGAA NINI GIZA KUZIDI??!! GIZA LAZIMA LIZIDI ILI MUNGU AZIDI KUTUKUZWA KUPITIA ILE NURU YAKE YA UTUKUFU!!!

3 Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako. 

Isaya 60:3

>> ISAYA ANASEMA MATAIFA WATAIJILIA NURU YAKO WEWE!!! KAMA HAWAJI KWAKO INA MAANA WEWE HUNA NURU YA MUNGU YA WAO KUIFUATA!!!

>> HATA WADUDU HUTOKA VICHAKANI KUIFUATA NURU YA ASILI

>> KAMA UNA NURU LAZIMA DUNIA ILIYOMO GIZANI IJE KWAKO KUIFUATA NURU YAKO!!

>> WASIO NA NURU NDIO WALE AMBAO SIKU ZOTE WANATAZAMA VIBANZI KWENYE MACHO YA WENGINE HUKU BORITI ZILIZOMO KWENYE MACHO YAO HAWAZIANGALII WALA KUZISHUGHULIKIA!! YESU ALIWAITA HAWA WANAFIKI!!! (MATHAYO 7:1-5) USIWE MNAFIKI!!! MBINGUNI HAWAINGII WANAFIKI!!!

Manabii Isaya na Mika kwa nyakati tofauti walitabiri vile ambavyo WATU WA MATAIFA WATAIJIA NURU YAKO MAKUNDI MAKUNDI (KAMA UNAYO!!)

"1 Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. 

Mika 4:1

2 Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu. 

Mika 4:2

3 Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. 

Mika 4:3

[SOMA PIA ISAYA 2:1-4]

>> KAMA HII HAITOKEI KWAKO AU KWENYE HUDUMA YAKO WEWE BADO HAUJAWA NURU YA ULIMWENGU

>> NI WAKATI WA KUFUMBA KINYWA NA KUANZA KUMTAFUTA MUNGU

>> NI WAKATI WA KUACHA MALALAMIKO NA MANUNG'UNIKO NA KUJAA ROHO NA NENO, KUJAA BABA NA MWANA!!!

>> Neno la Mungu ni roho na pia ni uzima! The word of God is spirit and it is life!! (Yohana 6:63) MAISHA YA KRISTO YALIYOMO KWENYE NENO LAKE NDIYO NURU AMBAYO DUNIA ILIYOMO GIZANI INAITAFUTA ILI IWEZE KUJA NURUNI NA KUTIWA NURU "KWAKO WEWE" (THE LIFE OF CHRIST THAT'S IN THE WORD IS THE LIGHT(Yohana 1:1-4) THE WORLD IS LOOKING FOR!!)

NI WAKATI WA KAZI!!

 Hii ni kwa sababu Mungu mwenyewe amesema;

11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. 

Yeremia 29:11

JEREMIAH 29:11 ( TAFSIRI KADHAA)

New International Version (NIV)

For I know the plans I have for you,” declares the LORD, “plans to prosper you and not to harm you, plans to give you hope and a future.

>> " NINAIJUA MIPANGO NILIYONAYO KWA AJILI YAKO", ASEMA BWANA, NI MIPANGO YA KUKUFANIKISHA (MIPANGO YA MAFANIKIO YAKO) NA SIYO MIPANGO YA KUKUDHURU (AU KUKULETEA MADHARA), NI MIPANGO YA KUKUPA WEWE TUMAINI NA KESHO BORA."

New Living Translation (NLT)

For I know the plans I have for you,” says the LORD. “They are plans for good and not for disaster, to give you a future and a hope.

>> "NINAIJUA MIOANGO NILIYONAYO KWA AJILI YAKO," ASEMA BWANA. NI MIPANGO YA MEMA (KUKULETEA NA KUKUTENDEA MEMA) NA SIYO MIPANGO YA (KUKULETEA) MAJANGA, BALI NI MIPANGO YA KUKUPA WEWE KESHO NA TUMAINI BORA."

English Standard Version (ESV)

For I know the plans I have for you, declares the LORD, plans for welfare and not for evil, to give you a future and a hope. 

KWA MAANA NINAIJUA MIPANGO NILIYONAYO KWA AJILI YAKO, ASEMA BWANA, NI MIPANGO YA MAFANIKIO NA FURAHA NA SIYO MIPANGO YA MABAYA, BALI NI KUKUPA KESHO NA TUMAINI BORA.

>> NENO HILI NI KUKUHUSU WEWE NA NYUMBA YAKO (MKEO/MUMEO, WANAO, WAZAZI WAKO, NDUGUZO), KAZI YA MIKONO YAKO, HUDUMA YAKO, AFYA YAKO, MASOMO YAKO, UTUMISHI WAKO, KANISA LA KRISTO, TAIFA LAKO, N.K.

>> NENO HILI NI DIRA NA TAA INAYOKUONGOZA KUELEKEA KESHO YAKO KAMA ALIVYOIKUSUDIA MUNGU

>> NENO HILI LINAHUSU MPANGO NA MAKUSUDI YA MUNGU MAISHANI MWAKO, KWENYE MAISHA YA KANISA, KWENYE UHAI WA TAIFA, N.K.

>> NENO HILI NI NURU ING'ARAYO MAHALI PENYE GIZA NA KUKUWEZESHA KUTEMBEA KATIKA NURU YA UTUKUFU WA MUNGU

19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. 

2 Petro 1:19

>> UKITEMBEA KWENYE MPANGO NA KUSUDI LA MUNGU LAZIMA UTAKUTANA NA GIZA

>> HII NDIYO KUSEMA KUNA GIZA LIMEFUNIKA MEMA ALIYOKUKUSUDIA MUNGU YAWE YAKO KATIKA KAZI, HUDUMA, NA MAISHA YAKO YA KIROHO

>> LAKINI BIBLIA INASEMA;

John 1:4-5

[4]In him was life; and the life was the light of men. 

Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

[5]And the light shineth in darkness; and the darkness comprehended it not. 

Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.

>> NDANI YAKE NENO LA MUNGU NDIMO MNA MAISHA/UZIMA; NA MAISHA HAYO YA NENO NDIYO NURU YA WATU; NA NURU HII NDIYO ILE ING'ARAYO GIZANI; NA GIZA LOLOTE HALIIWEZI NURU KAMWE!!

>> NENO LA MUNGU NDANI YAKO NI UZIMA NA NI MAISHA YAKO: MAISHA HAYO NDIYO NURU YA ULIMWENGU!! ILI KUTEMBEA KATIKA NURU YA UTUKUFU WA MUNGU, NI LAZIMA UJAE NENO LA MUNGU MOYONI AU ROHONI MWAKO AMBALO UMELIAMINI!!!

>> HII NURU YA UZIMA AU NURU YA MAISHA YA NENO LILILOMO NDANI YAKO NDIYO INAYOKUWEZESHA KUTEMBEA KATIKA NJIA YA UTAKATIFU!! NA NDIYO NURU INAYOYATIA MACHO YAKO YA MOYONI NURU!! NDIPOSA UNAWEZESHWA, KWA NEEMA YAKE, KUONA GIZANI!!

>> MWENYE KUONA GIZANI HAANGALII MMOMONYOKO WA MAADILI LEO, KUPOA KWA UPENDO WA WENGI, UHARIBIFU WA SHETANI KWENYE FAMILIA, TAIFA, AU KANISA LILILOMPA IBILISI NAFASI!! KIUFUPI ALIYETIWA NURU, HAONI GIZA, HATAZAMI GIZA, HATISHWI NA GIZA, HAOGOPI GIZA, HAOGOPESHWI NA GIZA, HAONGEI KUGOKANA NA GIZA LILILOPO, HATOI HUKUMU KUTOKANA NA GIZA LILILOTANDA, HAKATISHWI TAMAA NA KUVUNJWA MOYO WALA HAFADHAISHWI NA GIZA LOLOTE KWENYE NDOA YAKE, KWA WANAWE, KWA WASHIRIKA WAKE, KWENYE TAIFA LAKE, KWENYE FAMILIA YAKE, KAZI YA MIKONO YAKE NA HUDUMA YAKE!!! KWA SABABU YEYE MWENYEWE NDIYE NURU YA ULIMWENGU!!!

14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. 

Mathayo 5:14

15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. 

Mathayo 5:15

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post