UTAKATIFU NI KWA NEEMA SI KWA MATENDO

1) Hauwi mtakatifu kwa KUTENDA MEMA, bali UNATENDA MEMA KWA KUWA WEWE NI MTAKATIFU! 

2) Hauwi mtakatifu KWA KUSALI NA KUOMBA bali UNASALI NA KUOMBA KWA KUWA NI MTAKATIFU!

3) Hauwi mtakatifu KWA KUFUNGA NA KUOMBA bali UNAFANYA HAYO KWA KUWA U MTAKATIFU!

4) Hauwi mtakatifu KWA MATENDO MEMA NA YA HAKI YOYOTE UYATENDAYO, bali UNATENDA HAYO YOTE UKIWA TAYARI NI MTAKATIFU!!

5) Hauwi mwema KWA KUTENDA MEMA, BALI UNATENDA MEMA KWA KUWA TAYARI U MWEMA!!!

>> UTAKATIFU HAUTAFUTWI KWA MATENDO, BALI UTAKATIFU UNATOKANA NA 

1) KUMWAMINI YESU

2) KUOSHWA NA DAMU YA YESU

3) KUHESABIWA HAKI KWA IMANI KATIKA DAMU YA YESU

4) KUWA NA ROHO MPYA NA MOYO MPYA KUTOKA KWA YESU, KUPITIA IMANI YAKO KWAKE, KULIKOKUFANYA UWE KIUMBE KIPYA 

5) KUISHI NA KUENENDA KWA IMANI YA YESU, KUNAKOKUFANYA UISHI KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU (Mathayo 4:4)

6) KATIKA KUISHI HUKO UNAKUWA UNAENENDA KWA ROHO NA NGUVU ZAKE SAWASAWA NA NENO LA KRISTO, AMBAYO NDIYO NEEMA YA KRISTO (Tito 2:11-12)

Titus 2:11-12

"[11]For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men, 

Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;

[12]Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly, in this present world; 

nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;"

7) UNAKUWA MTAKATIFU KWA NEEMA YA KRISTO, INAYOKUWEZESHA KUISHI SAWASAWA NA NENO LA MUNGU LOTE!!! YAANI, UNAPEWA NEEMA YA KULITENDA NENO (Yakobo 1:19-25)

>> UTAKATIFU WA KWELI NI ULE UNAOTOKANA NA VILE ULIVYO MBELE ZA MUNGU (MTAKATIFU KATIKA ROHO NA NAFSI YAKO); NA SIYO VILE UTENDAVYO AU UFANYAVYO!! Maana watenda dhambi wengi sana leo wanafunga na kuomba, wanatoa mno sadaka, wanatenda mema, wanasoma Biblia na hata kusomea vyuo vya Biblia! wanafanya huduma kwa jina la Yesu, wanafundisha na kuhubiri, wanasaidia maskini na wahitaji, wanaimba nyimbo za Injili, huingia makanisani kwa uaminifu, wana vyeo makanisani, wanatoa pepo, wanatoa unabii, na kufanya miujiza pia, n.k. LAKINI HAWAYATENDI MAPENZI YA MUNGU!! Maana ukitenda mema yoooote huku moyo wako haujabadilika, au haujazitubia na kuziacha dhambi zako, au hauishi kwa Imani ya Yesu, yaani, hauishi kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu; BADO MATENDO YAKO MEMA HAYAKUFANYI UWE MTAKATIFU AU MWENYE HAKI MBELE ZA MUNGU!! Lakini mbele za wanadamu UTAKUWA MTU MZURI NA MWEMA SANA!!


Titus 3:3-5

[3]For we ourselves also were sometimes foolish, disobedient, deceived, serving divers lusts and pleasures, living in malice and envy, hateful, and hating one another. 

Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.

[4]But after that the kindness and love of God our Saviour toward man appeared, 

Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;

[5]Not by works of righteousness which we have done, but according to his mercy he saved us, by the washing of regeneration, and renewing of the Holy Ghost; 

si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;


Ephesians 2:8-10

[8]For by grace are ye saved through faith; and that not of yourselves: it is the gift of God: 

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

[9]Not of works, lest any man should boast. 

wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

[10]For we are his workmanship, created in Christ Jesus unto good works, which God hath before ordained that we should walk in them. 

Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. Umoja katika Kristo

>> MATENDO MEMA YENYEWE YALISHAANDALIWA TANGU KABLA HUJAZALIWA, ILI UJE UYATENDE NDANI YA KRISTO KWA NEEMA YAKE!!! NDIYO MAANA KUJISIFU AU KUJIVUNA KWA KUTENDA MEMA NI UOVU KWA KUWA SI WEWE UNAYETENDA HAYO BALI MUNGU NDIYE AYATENDAYE HAYO KWA NEEMA YAKE NDANI YAKO!


"Philippians 2:13

[13]For it is God which worketh in you both to will and to do of his good pleasure. 

Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema."

1) MUNGU, KWA ROHO WAKE, NDIYE ANAYEKUPA "KUTAKA", NA 2) PIA NDIYE ANAYEKUPA "KUTENDA" KWA NGUVU ZAKE!!


Imeandikwa kwenye Zecharia, "Zechariah 4:6

[6]Then he answered and spake unto me, saying, This is the word of the LORD unto Zerubbabel, saying, Not by might, nor by power, but by my spirit, saith the LORD of hosts. 

Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi."

>> MAPENZI YA MUNGU YOTE HUTENDWA KWA ROHO MTAKATIFU 

NA NGUVU ZAKE SIKUZOTE, NA MAHALI POTE, NA WALA,  ".........SI KWA UWEZA WAKO, NA WALA SI KWA NGUVU ZAKO!!" 

>> Mwanadamu huwa anajivunia nguvu za pesa, elimu, cheo, mali, madaraka, akiba benki, watu anaowategemea, n.k.

>> Lakini pia mwanadamu hujivunia kufunga na kuomba, kutenda mema, kusaidia, kujitoa, n.k.

>> HAYA YOTE YANA FAIDA KWAKO MWANADAMU NA WALA SI MUNGU!!! LAKINI MAPENZI YA MUNGU HUTENDWA NA ROHO WA MUNGU KWA NGUVU ZA MUNGU NDANI YAKE AAMINIYE!

Mapenzi ya Mungu = Roho Mtakatifu + Nguvu Zake= Neema ya Kristo

Bwana wetu Yesu mwenyewe ndiye aliyeifunua neema hii kwetu sisi tunaomwamini, maana aliishi na kuenenda kwa neema hiyo!


Acts 10:38/Matendo 10:38

[38]How God anointed Jesus of Nazareth with the Holy Ghost and with power: who went about doing good, and healing all that were oppressed of the devil; for God was with him. 

habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.

>> YESU ALITIWA MAFUTA KWA = ROHO MTAKATIFU NA + NGUVU ZAKE!!, 

1) AKAUFUNUA UTAKATIFU WA MUNGU AMBAO NI UTUKUFU WA PENDO LAKE

2) AKAUFUNUA UPENDO WA MUNGU AMBAO NI UTUKUFU WA UTAKATIFU WAKE

3) AKAUDHIHIRISHA UTUKUFU WAKE AMBAO NDIO UTAKATIFU WA PENDO LAKE!!


John 1:14/Yohana 1:14

[14]And the Word was made flesh, and dwelt among us, (and we beheld his glory, the glory as of the only begotten of the Father,) full of grace and truth. 

Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.


>> NEEMA YA KRISTO NDIYO MAFUTA YAKE KWETU!! (1 Yohana 2:20,27)

>> Neema hii, siyo tu inaokoa, lakini pia inafundisha!!!


Titus 2:11-12

[11]For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men, 

Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;

[12]Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly, in this present world; 

nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;

>> Na yale mafuta yake, yaani, Roho Mtakatifu na Nguvu zake, nayo yanafundisha!!


John 14:26

[26]But the Comforter, which is the Holy Ghost, whom the Father will send in my name, he shall teach you all things, and bring all things to your remembrance, whatsoever I have said unto you. 

Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Na tena,


1 John 2:27

[27]But the anointing which ye have received of him abideth in you, and ye need not that any man teach you: but as the same anointing teacheth you of all things, and is truth, and is no lie, and even as it hath taught you, ye shall abide in him. 

Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.


>> Neema au mafuta yake yanafundisha kuliishi neno la Mungu na kulitenda! Yanafundisha utii, unyenyekevu, Kicho, utakatifu, upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, uaminifu, fadhili, upole, kiasi, hekima, ufahamu, maarifa, kicho, shauri, uweza (nguvu), ufunuo, unyoofu, usafi, n k. Haya yote na mengine mengi yasiyohesabika, yanazaliwa mioyoni mwetu kadiri tunavyoliamini na kulitenda neno lake!! Roho na Nguvu zake hutuwezesha sisi tuaminio kutenda sawasawa na kweli ilivyo!! Hutuwezesha kumuabudu Mungu katika Roho na Kweli, na kuyatenda mapenzi yake yote!!!

>> Neema ya Kristo, siyo tu inatuwezesha kuishi maisha matakatifu bali pita INATUTENGENEZA TUFANANE NA KRISTO YESU BWANA WETU


1 Corinthians 15:10

[10]But by the grace of God I am what I am: and his grace which was bestowed upon me was not in vain; but I laboured more abundantly than they all: yet not I, but the grace of God which was with me. 

Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.


1) NEEMA YAKE INATUFANYA TUWE WATAKAKATIFU (it makes us holy)

2) KISHA NEEMA HIYO INATUWEZESHA KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU YOTE KATIKA ROHO, NAFSI, NA MWILI PIA! 

>> Wasioamini hutenda dhambi wanapojaribu kumpendeza 

Mungu kimwili pasipo neema yake!! Pasipo neema ya Kristo usijaribu kumpendeza Mungu!!!


Isaiah 64:6

[6]But we are all as an unclean thing, and all our righteousnesses are as filthy rags; and we all do fade as a leaf; and our iniquities, like the wind, have taken us away. 

Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.


>> VUA KWANZA VAZI LAKO CHAFU KWA KUOKOKA, UVAE VAZI SAFI, ILI SASA UKATENDE MEMA KAMA WAEFESO 2:10 isemavyo!!!


Ephesians 2:8-10

[8]For by grace are ye saved through faith; and that not of yourselves: it is the gift of God: 

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

[9]Not of works, lest any man should boast. 

wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

[10]For we are his workmanship, created in Christ Jesus unto good works, which God hath before ordained that we should walk in them. 

Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.


>> KAMA KWELI UMEOKOKA HUWEZI KUJISIFU KWA KUTENDA MEMA AU KUJIVUNA!! MAANA MATENDO MEMA HAYO YALISHAANDALIWA TANGU KABLA HUJAZALIWA ILI KWAMBA UJE UYATENDE NDANI YA YESU KRISTO KWA NEEMA YAKE!!


UTAKATIFU SI KWA MATENDO BALI NI KWA NEEMA YAKE BWANA WETU YESU KRISTO!!! UTII NAO NI NEEMA YAKE!! SHUKURU, NYENYEKEA, NA OGOPA NA KUTETEMEKA KWAMBA AMEKUJALIA KUTII!! USIJIVUNE NA KUJIHESABIA HAKI KAMA MAFARISAYO!!


9 Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. 

Luka 18:9


10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. 

Luka 18:10


11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. 

Luka 18:11


12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. 

Luka 18:12


13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. 

Luka 18:13


14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. 

Luka 18:14


FARISAYO ALIDHANI UTAKATIFU NI KWA MATENDO!! HAKUWAHI KUIJUA NEEMA IOKOAYO NA IWEZESHAYO YA YESU KRISTO!! UTAKATIFU NI KWA NEEMA NA SIYO MATENDO!!


Sasa wewe unayejiona ni mtakatifu kuliko wale wasiofunga kama wewe,  mtakatifu kuliko wale wasiotoa kama wewe, mtakatifu kuliko wale wasiosali na kuomba kama wewe, mtakatifu kuliko wale wasiohudhuria ibada kama wewe, mtakatifu kuliko wale wasiotoa michango ya ujenzi,harusi, misiba, n.k. kuliko wewe, mtakatifu kuliko 1) WALE WASIOFANYA MEMA YALE UYAFANYAYO WEWE, 2) WASIOBARIKIWA KAMA ETI ULIVYOBARIKIWA WEWE, 3) WASIOTUMIWA NA MUNGU KAMA WEWE, 4) WASIO NA HUDUMA KUBWA KULIKO HIYO ULIYONAYO, 5) WASIOABUDU PALE UNAPOABUDU WEWE, 6) WASIO KWENYE KUSANYIKO LENYE JINA KAMA JINA LA KUSANYIKO LAKO MFANO PENTECOASTAL........! ASSEMBLIES OF .........! AU SIJUI MINISTRY GANI, AU SIJUI HUKO KWENYE HUDUMA YA MTUME AU NABII GANI SIJUI N.K. JINSI GANI UMEDANGANYIKA!! JINSI GANI UNAISHI KWA MATENDO YA SHERIA NA SIYO NEEMA!! JINSI GANI UMEJIVUNA!!! JINSI GANI UMEPOTEA!! JINSI GANI UMEPOTOKA!! JINSI GANI UKO MWILINI!! HUJAIJUA NEEMA YA BWANA YESU BADO!! NA HUJAJUA KWAMBA VYOVYOTE VILE ULIVYO LEO, AU CHOCHOTE ULICHOKIFANYA AU UNACHOKIFANYA, AMA UNACHOKIMILIKI NI KWA NEEMA YAKE TU NA SI KWA UWEZO WALA NGUVU ZAKO! BALI NI KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE!!


Ecclesiastes 9:11

"[11]I returned, and saw under the sun, that the race is not to the swift, nor the battle to the strong, neither yet bread to the wise, nor yet riches to men of understanding, nor yet favour to men of skill; but time and chance happeneth to them all. 

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote."


>> NEEMA YA KRISTO INAPATIKANA KWA WOTE AMBAO WAKO TAYARI KUAMINI NA KUNYENYEKEA CHINI YA MKONO WAKE HODARI!!!


1 Peter 5:5-6

[5]Likewise, ye younger, submit yourselves unto the elder. Yea, all of you be subject one to another, and be clothed with humility: for God resisteth the proud, and giveth grace to the humble. 

Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.

[6]Humble yourselves therefore under the mighty hand of God, that he may exalt you in due time: 

Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;

>> NEEMA YAKE HUWAPA WANYENYEKEVU AMBAO WAKO TAYARI KUMWAMINI, KUMTEGEMEA, NA KUMTUMAINIA YEYE TU PEKE YAKE HADI MWISHO, AU IKIBIDI HADI KUFA!!!


Philippians 2:8-9

[8]And being found in fashion as a man, he humbled himself, and became obedient unto death, even the death of the cross. 

tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

[9]Wherefore God also hath highly exalted him, and given him a name which is above every name: 

Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;


NJIA YA KUINULIWA NI KUJISHUSHA NA KUJIDHILI!! KADIRI UNAVYOINULIWA NDIVYO UNAVYOJIDHILI NA KUJISHUSHA NA KUNYENYEKEA CHINI YA MKONO WAKE NA SI "MKONO WA MWILI!"

>> NGUVU ZA ROHO NI NGUVU ZA NENO AMBALO NI ROHO NA UZIMA/MAISHA NDANI YA WANYENYEKEVU WAKE WALIOAMINI!


Isaiah 57:15

[15]For thus saith the high and lofty One that inhabiteth eternity, whose name is Holy; I dwell in the high and holy place, with him also that is of a contrite and humble spirit, to revive the spirit of the humble, and to revive the heart of the contrite ones. 

Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.

>> HII NDIYO SIFA KUU YA WALE AMBAO MUNGU ATAWATUMIA KUWAFUFUA (REVIVE) WENGINE KWENYE UAMSHO WA SIKU ZA MWISHO! ATAWAJAZA NEEMA YAKE ILI WAYAFANYE MAPENZI YAKE YOTE KWA SIFA, SHUKRANI, HESHIMA, NA UTUKUFU WA JINA LAKE "YESU"

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post