"John 15:5
[5]I am the vine, ye are the branches: He that abideth in me, and I in him, the same bringeth forth much fruit: for without me ye can do nothing.
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote."
>> "...........PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI KUFANYA NENO LOLOTE!!!"
Bwana YESU alikuwa anaongelea suala la kumzalia MUNGU;
1) matunda ya haki (Wafilipi 1:11)
2) tunda ya nuru (Waefeso 5:9)
3) tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23)
4) matunda yapasayo toba (Luka 3:7-9)
5) matunda mazuri ( Mathayo 3:8,10, 7:14, 16-20)
>> NAMNA YA KUMZALIA MATUNDA NI KWA KUKAA NDANI YAKE!! UNAKAAJE NDANI YAKE??!!
Yohana anasema, "1 John 4:13
[13]Hereby know we that we dwell in him, and he in us, because he hath given us of his Spirit.
Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake."
>> UNAPOOKOKA NA KISHA UKABATIZWA KWA JINA LA YESU KWENYE MAJI MENGI, NA KISHA KUPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU KAMA ASEMAVYO PETRO KWENYE MATENDO 2:38 NDIPO UNAKUWA UMEUNGWA NA BWANA YESU NA KUWA ROHO MOJA NAYE (1 KOR 6:17). YAANI, WEWE UNAKUWA MMOJA NA YEYE KATIKA ROHO (ONE WITH HIM IN SPIRIT) HII INA MAANA YEYE YUMO NDANI YAKO NA WEWE UMO NDANI YAKE!!! YEYE NI MZABIBU NA WEWE NI TAWI! TAWI NA MTI NI KITU KIMOJA, HALIKADHALIKA ROHO YAKE NA roho YAKO NI MMOJA SASA!! Huu ni zaidi ya umoja maana mmekuwa mmoja au roho moja ama mmoja katika roho!! HAPA NDIPO ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE ANAPOTENDA KAZI NDANI YAKO KUKUWEZESHA roho YAKO kuenenda sawasawa NA NENO LA KRISTO lilivyo na pia lisemavyo!! Huu ndio usaidizi WA ROHO kwa roho yako [KUPITIA IMANI YAKO ILIYO HAI KWA YESU KRISTO, NENO LA MUNGU] KINACHOTAKIWA UPANDE WAKO WEWE NI " KUAMINI TU"(ONLY BELIEVE) NA UTENDAJI WOTE MUACHIE YEYE!! HII NDIYO MAANA YA KUAMINI NA KUPEWA NEEMA YAKE! UNAPOAMINI KAZI YOTE INAKUWA NI YA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAKO KULITENDA NA KULITIMIZA NENO KATIKA MUUNGANIKO NA roho yako (in oneness with your spirit) YAANI;
>> YEYE AKITENDA NAWE UMETENDA KWA KUWA ANATENDA NDANI YAKO AU ANATENDA KUPITIA WEWE!!
>> YEYE AKINENA NAWE UMENENA KWA KUWA NI YEYE ANAYENENA NDANI YAKO AU ANAYENENA KUPITIA WEWE
Philippians 2:13
"[13]For it is God which worketh in you both to will and to do of his good pleasure.
Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema."
>> MUNGU NDIYE ANAYETENDA KAZI NDANI YAKO, NA SIYO WEWE
>> ROHO MTAKATIFU NDIYE ATENDAYE KAZI NDANI YAKO NA SIYO WEWE
>> MUNGU NDIYE ANAYETENDA KAZI NDANI YAKO KWA ROHO WAKE NA NGUVU ZAKE, NA SIYO WEWE
>> MUNGU NDIYE ANAYETAKA NA ANAYEPENDA KUTENDA KAZI NDANI YAKO AU KUPITIA WEWE, NA SIYO WEWE!
>> JUKUMU LAKO PEKEE NI KUAMINI NA KUNYENYEKEA CHINI YA MKONO WAKE HODARI NA WENYE NGUVU, YAANI, KUJINYENYEKEZA CHINI YA UONGOZI WA ROHO WAKE MTAKATIFU ILI AKUONGOZE (WARUMI 8:14) HATUA ZAKO KWA NENO LAKE (ZABURI 119:133) ILI UENENDE KATIKA UTAKATIFU, HAKI, NA KWELI!!!
>> UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU KWAKO NI KUPITIA roho yako ILIYOZALIWA MARA YA PILI KWA ROHO HUYO HUYO NA NENO LAKE TAKATIFU ULILOLIAMINI!!
>> KUAMINI NI KULIKUBALI NA KULIPOKEA NENO LA MUNGU ROHONI MWAKO, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA NA NGUVU ZAKE ILI LIKUONGOZE, LIKUFUNDISHE, LIKUELEKEZE, LIKUONYE, LIKUTAKASE, LIKUHEKIMISHE, LIKUFAHAMISHE, LIKUPE AKILI, LIKUFUNULIE, N.K. KWA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YAKO
>> PASIPO NENO LAKE, NA ROHO WAKE, NA NGUVU ZAKE, roho yako peke yake haiwezi KUFANYA NENO LOLOTE LA KUMPENDEZA MUNGU. YAANI, HAUWEZI KUYAFANYA MAPENZI YAKE YALIYOMO KWENYE NENO LAKE!!
>> KWA MUJIBU WA YOHANA 15:1-8 HAUWEZI KUMZALIA MUNGU MATUNDA PASIPO MKONO WAKE YEYE MWENYEWE KUKUSAIDIA!! NA MUNGU KWA KULIJUA HILO AMETUPATIA MSAADA SISI TUAMINIO!!
"7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu."
Yohana 16:7
-Hauwezi kusamehe atakavyo na apendavyo Mungu pasipo nguvu ya kusamehe kutoka kwa roho ya kusamehe!!
-Hauwezi kutoa atakavyo na apendavyo Mungu pasipo nguvu ya kutoa kutoka kwa roho ya kutoa!!
- Hauwezi kuimba atakavyo na apendavyo Mungu pasipo nguvu ya kuimba itokayo kwa roho ya uimbaji!!
- Hauwezi kuomba atakavyo na apendavyo Mungu pasipo nguvu ya kuomba itokayo kwa roho ya kuomba!!
- Hauwezi kushauri atakavyo na apendavyo Mungu pasipo nguvu ya kushauri itokayo kwa roho ya kushauri!!
- Hauwezi kufundisha apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya kufundisha itokayo kwa roho ya kufundisha
- Hauwezi kuhubiri apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya kuhubiri itokayo kwa roho ya kuhubiri!!
- Hauwezi kujitakasa vile apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya utakaso kutoka kwa roho ya utakaso!!
- Hauwezi kujikana vile apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya kujikana kutoka kwa roho ya kujikana
- Hauwezi kutii vile apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya kutii kutoka kwa roho ya UTII
- Hauwezi kumcha Mungu vile apendavyo na atakavyo pasipo nguvu ya kumcha Mungu kutoka kwa roho ya kumcha Mungu
- Hauwezi kunyenyekea kwa Mungu vile apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya unyenyekevu kutoka kwa roho ya unyenyekevu!
- Hauwezi kusimamia vile apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya kusimamia itokayo kwa roho ya kusimamia
- Hauwezi kufariji vile apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya kufariji itokayo kwa roho ya faraja
- Hauwezi kujenga au kutia moyo vile apendavyo Mungu au atakavyo Mungu pasipo nguvu ya kujenga au kutia moyo itokayo kwa roho ya kujenga na ya kutia moyo
- Hauwezi kuhudumu vile apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya kuhudumu itokayo kwa roho ya hiyo huduma
- Hauwezi kuchunga kanisa vile apendavyo na atakavyo Mungu pasipo nguvu ya uchungaji itokayo kwa roho ya uchungaji
- HUWEZI KUFANYA LOLOTE LIMPENDEZALO NA ALITAKALO MUNGU PASIPO NGUVU YA MUNGU ITOKAYO KWA ROHO WA MUNGU!!!
>> Hiyo roho ya neno na nguvu zake zitokazo kwa Roho Mtakatifu NDIYO NEEMA YA KRISTO
>> UNAPOLIAMINI NENO LA KRISTO, MUNGU ANAKUPA NEEMA YAKE KUKUWEZESHA KULIISHI NA KULITENDA HILO NENO
>> YAANI, ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE ANATENDA KAZI NDANI YAKO NA KUPITIA WEWE KULITENDA NENO NDANI YAKO
>> HUWEZI KAMWE KUFANYA NENO LOLOTE JEMA PASIPO MSAADA WAKE YEYE MWENYEWE YESU!!
" 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake huyo huzaa sana; maana PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI KUFANYA NENO LOLOTE."
Yohana 15:5
>> HAUWEZI KUISHI MAISHA MATAKATIFU PASIPO NEEMA YANGU
>> HAUWEZI KUKUA KIROHO PASIPO NEEMA YANGU
>> HAUWEZI KUENENDA KWA ROHO PASIPO NEEMA YANGU
NA HII NDIYO NEEMA YANGU: "......SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI NI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA WA MAJESHI" (ZECHARIA 4:6)