KUTOWEZA KWAKO KUFANYA NENO LOLOTE

 


1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 

Yohana 15:1


2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 

Yohana 15:2


3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 

Yohana 15:3


4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 

Yohana 15:4


5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 

Yohana 15:5


6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 

Yohana 15:6


7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 

Yohana 15:7


8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 

Yohana 15:8


>> MST 5C ".......MAANA PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI KUFANYA NENO LOLOTE."

Swali la haraka ni hili: Hatuwezi kufanya neno lolote??!!! Neno lipi??!! Na kwa nini hatuwezi??!! Ukisoma fungu hili la maandiko utaona kuwa Bwana wetu Yesu anaongelea suala muhimu la kiroho la KUMZALIA MUNGU MATUNDA!! (Fruitfulness in the Lord) Kwenye mstari wa 8 anasema kama hauzai matunda wewe si mwanafunzi wake!! KAMA UNAFUNDISHWA NA YESU LAZIMA UTAZAA MATUNDA KUONYESHA UMEFUNDISHIKA! Maana Aliyekuumba hashindwi kukufundisha wewe aliyekupa roho alipokuumba, ukaanguka dhambini, na kisha kukuzaa mara ya pili roho yako, na kisha akakupa Roho wake Mtakatifu ili uwe ndani yake na Yeye awe ndani yako!! Yesu ni mwalimu asiyeshindwa!! Ukifaulu shule yake ndipo UNAMZALIA MATUNDA na kuzidi kufanya hivyo kadiri unavyozidi kufundishwa naye na kuyapokea na kuyatenda yote akufundishayo! Sasa kumzalia Mungu matunda ni jambo la roho na nafsi yako!!! Siyo jambo la mwili!!! Neno la Mungu ndilo maisha yetu tuaminio. Yesu Kristo ni Neno la Mungu aliyekuja kwetu kwenye mwili! Akaishi kwetu nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba amejaa neema na kweli (Yohana 1:1,14) Maisha aliyoyaishi Yesu kwenye mwili ni maisha ya Neno la Mungu ambayo ndiyo maisha yetu watoto wa Mungu. Maisha ya Neno ndiyo maisha ya Mungu maana imeandikwa, "Naye Neno alikuwa Mungu" (Yohana 1:1c) Maisha ya Mwana wa Mungu ni yale yale ya Mungu mwenyewe kwa kuwa Yesu ni Mungu kwenye mwili (1 Timotheo 3:16)


16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu. 

1 Timotheo 3:16

>> Mara moja Mungu ametuonyesha YEYE MWENYEWE ANAISHIJE KWENYE MWILI ILI TUFUATE MFANO WAKE NA TUISHI KAMA YEYE! Ila hatuwezi kuishi kama Yeye mpaka;

1) KWANZA TUZALIWE MARA YA PILI roho zetu (Yohana 3:6)

2) KISHA TUANZE NA KUENDELEA MAISHA YA KUJIFUNZA NENO LAKE ILI TUPATE KUUKULIA WOKOVU KWA HILO (1Petro 2:2), NA KUJITAKASA ILI TUMZALIE MATUNDA!!

3) TUNAPOMZALIA MATUNDA TUNAFANANA NAYE YESU NA KUENENDA VILE VILE KAMA YEYE MWENYEWE ALIVYOENENDA (1 Yohana 2:6), NA HIVYO KUYAFANYA MAPENZI YOTE YA MUNGU YALIYOMO KWENYE NENO LAKE

>> HAPA KWENYE HILI LA PILI NA LA TATU NDIPO YESU ANASEMA"PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI KUFANYA NENO LOLOTE!!" (Yohana 15:5c)

>> HAUWEZI KUMZALIA MUNGU MATUNDA KWA KUFUNGA SANA, KUTOA SANA, KUJITAHIDI SANA, KUSUMBUKA SANA, KWA JUHUDI ZAKO NYINGI SANA, N.K. WAKRISTO WENGI WENYE NIA NJEMA NA WATUMISHI PIA WAMESHINDWA KUELEWA NINI BWANA ANATAKA NA NINI ANAMAANISHA HAPA, NA MATOKEO YAKE WAMEJIKUTA WAKIISHI KWENYE WOKOVU FULANI WA MATENDO NA SHERIA HIVI (LEGALISTIC CHRISTIANITY) USIOJIKITA KWENYE USHIRIKA WA KINA NA WA NDANI NA BWANA WETU YESU KWA ROHO WAKE MTAKATIFU!! WOKOVU WA SHERIA UNAJIKITA KWENYE KUTIMIZA "DUTY" TU ("JUKUMU") PEKE YAKE!! YAANI, MFANO NI MTEULE ANAJIONA NI MTAKATIFU AKISHATOA ZAKA TU BASI AMEMALIZA! ANACHOFANYA NA FEDHA ILIYOBAKI HAKINA UHUSIANO NA YESU!! MTEULE AKISHAFUNGA SIKU THELATHINI TAYARI AMETIMIZA JUKUMU LAKE MAISHA MENGINE YAENDELEE!! MTEULE AKIISHA CHANGIA FEDHA ZA UJENZI TAYARI AMETIMIZA JUKUMU LAKE! MTEULE HUYU UTAKATIFU KWAKE UNAPATIKANA KWA MATENDO HAYA YA KIROHO AYATENDAYO!! LAKINI KULE KUFANANA NA YESU HAKUPO!! KULE KUWA NA USHIRIKA NA BABA NA MWANA KWA ROHO MTAKATIFU HAKUPO!! KULE KUMJUA KIBINAFSI YESU KAMA RAFIKI HAKUPO!! KULE KUONGEA NA YESU, KUTEMBEA NA YESU, KUSHIRIKIANA NA YESU, URAFIKI NA YESU, HAMNA!! NA HIVYO MTEULE ANAJIKUTA HAMZALII MUNGU MATUNDA!! BWANA YESU HAKUJA KUTUTUMA TU FANYA HIVI, FANYA VILE, TOA, N.K. BALI ALIKUJA AKAE NDANI YETU NA SISI NDANI YAKE, ILI SISI NA YEYE TUWE MMOJA! ALISEMA KWENYE YOHANA SURA YA 15 KWAMBA YEYE NI MZABIBU WA KWELI NA SISI TU MATAWI YAKE!! TAWI NA MZABIBU NI KITU KIMOJA!! HILI NI TAWI LA MZABIBU, NA MATUNDA YA KWELI YANAKAA KWENYE TAWI. MATUNDA HAYA HAYAPATIKANI KWA NJIA NYINGINE YOYOTE ISIPOKUWA NI KWA HILI TAWI KUBAKI KUWA TAWI LA MZABIBU NA KUENDELEA KUNYONYA NA KULA UNONO WA SHINA LA MZABIBU!! TAWI HALIHANGAIKI KUKATAA UNONO WA SHINA ILI LIZAE MATUNDA!! TAWI HALIHITAJI KUTUMWA KWENYE MAJUKUMU YA KIROHO ILI LIZAE MATUNDA!! TAWI HALIHITAJI JITIHADA NA JUHUDI ZOZOTE ZA KIROHO ILI LIZAE MATUNDA!! TAWI LINAHITAJI TU KUBAKI NDANI YA MZABIBU ILI LIZAE MATUNDA!!! KWA KUBAKI NDANI YA MZABIBU NDIPO MZABIBU UNAFANYA KAZI YOTE YA KULILISHA TAWI UNONO KUTOKA KWENYE MIZIZI, SHINA, NA MAGAMBA MPAKA TAWI LINAZAA MATUNDA!! MATUNDA HAYO NDIO UTAKATIFU WA BWANA YESU UNAONEKANA SASA KWENYE MAISHA YA MTAKATIFU!! HILI NI JAMBO LA NDANI KATI YA ROHO WA KWELI NA roho yako mtakatifu iliyozaliwa mara ya pili. 

>> Muunganiko huu wa tawi na mzabibu ndio huu hapa kwenye Wakorintho wa Kwanza sura ya sita;


1 Corinthians 6:17

[17]But he that is joined unto the Lord is one spirit. 

Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.


>> Muunganiko huu ndio msingi wa kumzalia Mungu matunda na wala si bidii au jitihada yako yoyote ya kimwili!! Mzabibu hapa ni Roho wa Kweli Aliye Mtakatifu, Na tawi hapa ni roho yako iliyozaliwa mara ya pili!! Yaani,

-Uzaaji matunda= Roho wa Kweli + roho yako iliyozaliwa mara ya pili

-Uzaaji matunda (fruitfulness) = Roho + roho

>> Siri ya uzaaji matunda iko kwenye huu muunganiko ambapo inazaliwa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo kwa wateule wake tuliomwamini!! Mzabibu na tawi haviko kwenye umoja (unity) bali mzabibu na tawi ni mmoja!! i.e. mzabibu + tawi lake = mti mmoja [1+1=1]

>> Unapokuwa roho moja na Bwana Yesu maana yake wewe na Yesu mmekuwa MMOJA katika roho, au mmekuwa roho moja!! Muunganiko huu unatokea pale unapopokea kipawa cha Roho Mtakatifu!!( Matendo 2:38-39)

>> Kwa kujazwa Roho Mtakatifu unakuwa umeunganishwa Na Bwana Yesu katika roho, na hivyo sasa wewe ni roho moja naye, au ni mmoja na Yeye!! Muunganiko huu ndio maandiko yanausema hapa:


21 That they all may be one; as thou, Father, art in me, and I in thee, that they also may be one in us: that the world may believe that thou hast sent me. 

John 17:21

[Ili kwamba wawe mmoja; kawa vile wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, Na wao pia wawe mmoja ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki kwamba wewe ndiwe uliyenituma].

1) Baba, (Roho) ndani ya Mwana, (Neno)

2) Na Neno (Mwana), ndani ya Baba ( Roho))

3) Kanisa/Watakatifu, ndani ya Roho Mtakatifu na Neno lake (Baba na Mwana)

4) Huu sio umoja (unity) Bali huu ni muunganiko (oneness)

5) Mapenzi na mpango wa Mungu kwa Agano Jipya ni huu: KANISA KUWA MMOJA NA BABA NA MWANA!! KANISA KUWA MMOJA NA ROHO NA NENO LAKE!!

>> Roho Mtakatifu + roho yako iliyozaliwa mara ya pili + nguvu zake = MAISHA YA KRISTO NDANI YA KANISA

>> HAPA NDIPO PENYE KUZAA MATUNDA KWA MWANAFUNZI WA YESU KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE KUPITIA IMANI YAKO KWA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WAKO

>> JE! WEWE UNAWEZA KUZAA MATUNDA WEWE MWENYEWE??!! HAPANA!!

>> JE! TUNDA LA ROHO SIYO UTAKATIFU WA KRISTO YESU BWANA WETU??!! HAKIKA NDIO UTAKATIFU WAKE HUO!!

>> JE! NI WEWE UNAJIPA HUO KWA JUHUDI, NGUVU, UWEZA, BIDII, NA KUTAKA KWAKO SANA??!! HAPANA!!!

>> JE! SI ROHO MTAKATIFU ANAKUSAIDIA NA KUKUWEZESHA KWA UWEZO WOTE KUZAA MATUNDA HAYO? NDIYO!!

>> JE! NGUVU ZA KUZAA NI ZAKO WEWE AU NI ZA ROHO MTAKATIFU? NI ZA ROHO!!!

>> NI IPI BASI SEHEMU YAKO WEWE MWAMINI??!! NI KUAMINI NENO LAKE NA KUNYENYEKEA CHINI YA MKONO WAKE HODARI USIOSHINDWA NA USIOPUNGUKIWA CHOCHOTE SIKU ZOTE ILI AKUTENGENEZE, AKUIMARISHE, AKUTIE NGUVU, NA KUKUTHIBITISHA, (FAITH AND YIELDING/SUBMITTING TO THE HOLY GHOST) UKIZINGATIA YEYE MWENYEWE AMESEMA KUWA ALISHAANZA KAZI NDANI YAKO, NA HATA SASA BADO ANAENDELEA NA KAZI HIYO AMBAYO LAZIMA ATAIKAMILISHA YOTE KWA WAKATI WAKE!


Philippians 1:6

[6]Being confident of this very thing, that he which hath begun a good work in you will perform it until the day of Jesus Christ: 

Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;

NA TENA HAPA ANASEMA:


Philippians 2:13

[13]For it is God which worketh in you both to will and to do of his good pleasure. 

Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.

>> MUNGU NDIYE ANAYETENDA KAZI NDANI YAKO KWA ROHO WAKE ALIYEMO NDANI YAKO, NA SI WEWE HATA KIDOGO!! WEWE KAZI YAKO NI KUUFUNGUA MOYO WAKO, KULIPOKEA NENO, KUOMBA REHEMA NA NEEMA ZAKE ILI KULIISHI, NA KUMWACHA ROHO MTAKATIFU AFANYE KAZI YAKE NDANI YAKO HALI UKIMWAMINI NA KUMTUMAINIA KABISA, NA KUTOZITUMAINIA AKILI NA NGUVU ZAKO WALA JUHUDI NA JITIHADA ZAKO!! UKIKUMBUKA KWAMBA IMEANDIKWA, SI KWA NGUVU ZAKO WALA UWEZA WAKO BALI NI KWA ROHO MTAKATIFU (ZECHARIA 4:6) 

>> UTAKATIFU SIYO ZAO LA JASHO LAKO, AU KUJITESA KWAKO, AU BIDII YAKO YOYOTE YA KIMWILI!!

>> UTAKATIFU NI ZAO LA IMANI, UTII, NA UNYENYEKEVU WAKO ULIOKIRIMIWA KWA NEEMA PIA. VITU VYA MUNGU VINAZALIWA NDANI YAKO KWA KAZI YA ROHO MTAKATIFU, NA NDIYO MAANA PAULO AKAWEKA OMBI HILI KWA KANISA KUJIOMBEA NA KUOMBEANA,


14 Kwa hiyo nampigia Baba magoti, 

Waefeso 3:14


15 ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, 

Waefeso 3:15


16 awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. 

Waefeso 3:16

>> NEEMA YA KRISTO MAANA YAKE ROHO MTAKATIFU ANATENDA KAZI NDANI YAKO, KWA NGUVU ZAKE, KUKUFANYA UWE IMARA KATIKA NEEMA YAKE, KATIKA UTU WAKO WA NDANI!! UNADHANI ZAO MOJAWAPO NI LIPI ISIPOKUWA NI MAISHA YA UTAKATIFU??!! ILI ROHO MTAKATIFU ATENDE KAZI HIYO LAZIMA UAMINI HILO ANDIKO, UOMBE, UAMINI KWAMBA AMEKUSIKIA NA AMEANZA KAZI HIYO, NA UANZE KUSHUKURU HALI UKIMTUMAINI YEYE ATIMIZE NA KUKAMILISHA KAZI YAKE!! KUNA NINI UWEZACHO KUFANYA ZAIDI YA HAPO??!!

Paulo anauliza,

7 Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? 

1 Wakorintho 4:7

>> UNA NINI WEWE CHA KIROHO USICHOKIPOKEA??!!

>> NA KAMA ULIPOKEA UTAJISIFIA NINI KANA KWAMBA HUKUPOKEA??!!

>> KAMA UTAKATIFU UNGEPATIKANA KWA MATENDO UNGEJIVUNA SANA WEWE NA KUJIONA NI MTAKATIFU KULIKO WENGINE!!!

>> IMANI AMEIANZISHA YESU, NA NEEMA NI YAKE YESU UNAYOPEWA KUPITIA IMANI HIYO, ROHO NI WAKE, NGUVU NI ZAKE, NENO NI LAKE, roho YAKO ILIYOZALIWA MARA YA PILI NI YAKE (YAANI, WEWE NI WAKE), NA CHOCHOTE ULICHONACHO KIMETOKA KWAKE, LOLOTE ULIFANYALO UNALIFANYA KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE!! KAMA HUJUI HAYA JIFUNZE ILI UANZE URAFIKI NA USHIRIKA NA YESU, ILI UIJUE NEEMA YAKE, HALAFU


1) UWE HODARI KATIKA NEEMA


2 Timothy 2:1

[1]Thou therefore, my son, be strong in the grace that is in Christ Jesus. 

Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.


2) UKUE KATIKA NEEMA HIYO


2 Peter 3:18

[18]But grow in grace, and in the knowledge of our Lord and Saviour Jesus Christ. To him be glory both now and for ever. Amen. 

Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.

3) NEEMA HIYO IENDELEE KUKUFUNDISHA


11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 

Tito 2:11


12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 

Tito 2:12


13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 

Tito 2:13



>> KAMA WEWE UNAUTAFUTA UTAKATIFU KWA MATENDO YAKO YA HAKI INA MAANA BADO UKO KWENYE WOKOVU WA SHERIA WA KUTIMIZA MAJUKUMU TU BASI!! YAANI, UKIISHA FANYA YALE UYAFANYAO TAYARI WEWE NI MTAKATIFU!!! UKIISHAFUNGA WEWE NI MTAKATIFU,(wasiofunga wote ni watenda dhambi) UKIISHA TOA WEWE NI MTAKATIFU, (wasiotoa wote ni watenda dhambi), UKIISHA OMBA WEWE NI MTAKATIFU,(wasioomba wote siyo watakatifu) UKIISHATOA SADAKA WEWE NI MTAKATIFU, ( wasiotoa wote ni watenda dhambi), UKISHAWAHI IBADANI WEWE NI MTAKATIFU (wasiowahi wote ni watenda dhambi), UKISHAHUDHURIA MKESHA WEWE NI MTAKATIFU (wasiohudhuria mkesha wote ni watenda dhambi), n.k.

>> Unamaanisha kwamba kwenye kusanyiko lako siku Yesu akirudi atakuta wateule wote kama ni kwenye mkesha wapo wote pale, kama ni ibadani wapo wote pale, kama ni matoleo fulani wametoa wote, NA KWA SABABU HIYO NI WATAKATIFU WATAKAONYAKULIWA??!! n.k.?! HAPANA!!! WATANYAKULIWA WALIOOKOLEWA KWA NEEMA, NA WANAOISHI NA KUENENDA KWA NEEMA HIYO KUPITIA IMANI YAO ILIYO HAI KWA YESU KRISTO POPOTE WALIPO!! HII YAKO NI AINA YA WOKOVU WA SHERIA NA MATENDO AMBAPO WATU HAWAMJUI YESU KABISA KIBINAFSI KATIKA ROHO (THEY HAVE NO INTIMACY WITH JESUS) KWA KUWA WANAELEKEZWA NA KUFUNDISHWA ZAIDI SI KUELEKEA KWA ROHO NA NENO LAKE, BALI KUTEKELEZA MAAGIZO, TARATIBU, SHERIA, NA MAELEKEZO YA NJE ZAIDI!! MTU AKITOKA KUSHUHUDIA ANAJIONA AMEKUWA MTAKATIFU ZAIDI!! SIKILIZA! HAYA YOTE NI MAZURI NA TUNAYAFANYA SI KWA NGUVU NA UWEZA WA KIBINADAMU, BALI KWA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE (YAANI, KWA NEEMA YAKE) NA HIVYO HATUWEZI KUJIVUNA WALA KUJISIFU BALI TUNAZIDI KUSHUKURU NA KUNYENYEKEA, NA KUZIDI KUWAOMBEA NDUGU ZETU KATIKA BWANA REHEMA NA NEEMA KWA MUJIBU WA WAEBRANIA 4:16 ILI NAO WAONGEZEWE REHEMA NA NEEMA YAKE. MARA NYINGI PAULO AMEKUWA AKITOA SALAMU HII!!


1) 4 kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu. 

Tito 1:4


2) 3 Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. 

Filemoni 1:3


3) 24 Wasalimuni wote wenye kuwaongoza, na watakatifu wote; hao walio wa Italia wanawasalimu. 

Waebrania 13:24


4) 25 Neema na iwe nanyi nyote. 

Waebrania 13:25


5) 2 kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. 

2 Timotheo 1:2


6) 18 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. 

2 Wathesalonike 3:18


7) 14 Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. 

2 Wakorintho 13:14


Soma nyaraka za Paulo zote utakuta karibu kote anafungua na salamu hii na kufunga nayo salamu hii ya baraka!! ANAWATAKIA WATAKATIFU BARAKA HIZI ZA REHEMA, NEEMA, NA AMANI ZIKAE KWAO SIKUZOTE NA PIA ZIONGEZWE KWAO!! PAULO ANAJUA MAISHA YA KRISTO NDANI YAO WANAISHI KWA NEEMA YAKE KRISTO KUPITIA IMANI YAO KWAKE!! NA YOTE WAYATENDAYO SI KWA UWEZA WALA NGUVU ZAO BALI NI KWA ROHO WA KRISTO ALIYEMO NDANI YAO!! PAULO AKILITAMBUA HILI ANASEMA,


10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami. 

1 Wakorintho 15:10


1) KWA NEEMA YA KRISTO AMEKUWA VILE ALIVYO!! YUKOJE??!! NI MTAKATIFU, MCHA MUNGU, MNYENYEKEVU, AMEJAA UPENDO, MTIIFU, N.K. NEEMA YA KRISTO IMEMFANYA AMA IMEMTENGENEZA AWE MTAKATIFU!! PAULO ALIJUA SIRI YA UTAKATIFU KWA NEEMA NA REHEMA ZA BWANA YESU, N.K.

2) NEEMA HIYO HIYO ILIMFANYA PIA AZIDI SANA KUFANYA KAZI KUPITA MITUME WOTE WALIOMTANGULIA!! NA ANAKIRI HARAKA "....WALA SI MIMI. BALI NI NEEMA YA MUNGU PAMOJA NAMI." NEEMA GANI? UWEPO WA MUNGU NA NGUVU ZAKE NDANI YAKE, KWA ROHO MTAKATIFU WA NEEMA!!!

>> ANDIKO HILI LINAONYESHA NEEMA YA KRISTO 1) ILIMTENGENEZA PAULO AWE VILE ALIVYO, NA 2) PIA ILIMUWEZESHA ATENDE KAZI KUPITA MITUME WOTE WALIOMTANGULIA!! ANASISITIZA KUWA SI YEYE BALI NI NEEMA YA MUNGU NDANI YA KRISTO!! UKIENENDA KWENYE WOKOVU KWA MATENDO YA SHERIA HUWEZI KUZAA MATUNDA, HUWEZI KUKUA KIROHO, UTACHOKA HUKO MBELE MAANA UNATUMIA NGUVU NYINGI, UTAJIVUNA UKIFANIKIWA, UTAJILINGANISHA NA WENGINE UKIWAHESHIMU UNAOONA WAMEKUZIDI NA KUWASHUSHA HAUL UKIWADHARAU UNAOONA UMEWAZIDI, UTADUMAA NA KUSHINDWA KUZAA, HUWEZI KUWA NA USHIRIKA WA KINA NA WA NDANI KABISA NA ROHO MTAKATIFU, NA NENO LA MUNGU KWAKO LITAKUWA,


10 Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo. 

Isaya 28:10


13 Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa. 

Isaya 28:13


NIMALIZIE KWA NENO HILI (INGAWA BADO NINAYO MENGI YA KUSEMA)


4 Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. 

Wagalatia 5:4


5 Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. 

Wagalatia 5:5


6 Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo. 

Wagalatia 5:6


Mungu akuzidishie neema, rehema, na amani kwa Kristo Yesu Bwana Na Mwokozi wetu!! AMEN HALELUYA!

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post