KWA NINI NISUBIRI KATIKA MAUMIVU?
“Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, 2tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. 3Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.” (Ebrania 12:1-3)
Katika hali ya kujikana, kubeba msalaba wako kila siku, na kumfuata Yesu, Biblia inatuagiza,
1)TUWEKE KANDO KILA MZIGO MZITO
2)PIA TUWEKE KANDO KILA DHAMBI ILE ITUZINGAYO UPESI
3)ILI TUWEZE KUPIGA MBIO KWA SABURI KATIKA ‘MASHINDANO YALE YA IMANI’ YALIYOWEKWA MBELE YETU;
“Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu” (Yd 1:3)
-Kila mzigo mzito na Kila dhambi ile ituzingayo kwa upesi ni maeneo mawili ya udhaifu ya kila mtoto wa Mungu anayevipiga vita vizuri vya imani, na amemwamini Mungu kwa mambo mbalimbali, na anamngojea Mungu adhihirishe majibu yake /baraka zake ambazo tayari amezipokea na anazimiliki kwa imani!!! Huyu anazo haja alizomwomba Mungu (1 Yoh 5:14-15), na alipoomba katika kusali kwake aliamini kuwa anapokea, na yote aliyokuwa anayaombea yakawa yake (Mk 11:24); Naye tayari amekwishahamisha milima yote katika maisha yake (Mk11:23), amekwishatumia mamlaka ya mwamini katika kuharibu, kung’oa, kuangamiza, kubomoa, kufunga na kufungua, kujenga na kupanda!!! (Mt 18:18, Yer 1:10). Mkristo huyu amevaa silaha zote za Mungu (Efe 6:11) na anakabiliwa na changamoto moja tu! KUNGOJEA WAKATI WA BWANA!!! Wakati wa Bwana ni lini sasa?! Maana wakati tunangojea, mazingira yetu na hali zetu za maisha bado hazijabadilika kwa macho ya mwilini!!! Hali zile ngumu, mbaya, zinazoumiza, zinazosumbua, zinazoudhi, zinazochukiza, zinazochosha, tusizozitaka, n.k. bado zipo!!! Ila sisi katika hali yetu ya kiroho tuliyofikia hatuzioni, bali tunamuona Bwana/ tunaona ahadi zilizotimizwa/tunaona Neno lililotimizwa/ tunamwona Mungu aliyetutendea!!! Shetani atatuletea mazingira magumu na mabaya yote anayoweza ili tusimwangalie Yesu halafu tuanze kuzama kama Petro!!!
LAKINI KWA NINI NITESEKE NA NIUMIE?! (MAUMIVU YANA FAIDA GANI?)
Kule kuanguka dhambini kwa mwanadamu kulisababisha mwanadamu awe chini ya nguvu, mamlaka na utawala wa shetani roho, nafsi na mwili!!! Kuokoka maaana yake tumekombolewa kutoka katika nguvu za giza, na kuhamishwa na kuingizwa katika ufalme wa Mungu! (Kol 1:13-14). Tulisamehewa dhambi zetu na kukombolewa kutoka katika ufalme wa giza na nguvu zake zote!!! Yesu alivumilia taabu, shida, adha, mateso, maumivu, aibu, dharau, kukataliwa, machubuko, vidonda, kuonewa, n.k kwa ajili yetu!!! MWILI WA MWANADAMU HAUTAKI MATESO!! WALA HAUTAKI MAUMIVU!!! SEMBUSE KUTESWA KWA AJILI YA MWINGINE!!! Hii ndiyo maana Yesu aliomba “ikiwezekana Baba uniepushe na kikombe hiki, walakini si kama nitakavyo mimi bali utakavyo wewe” !!!(Mt 26:39,42) YAKO MATAKWA YA MWILI na pia yako MATAKWA YA MUNGU!!! Kwa kuwa mwanadamu ni mbinafsi hapendi kuteseka yeye mwenyewe binafsi wala kwa ajili ya mwingine! Sisi tuliookoka kwa upendo mwingi tunaombwa kushiriki mateso ya Kristo ili kushiriki baraka ya msalaba ambayo ni kuteswa, kufa, na kufufuka kwake Yesu NDANI YETU SISI “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake;” (Efe 1:29)
WOKOVU UNA KUMWAMINI YESU, NA PIA KUTESWA KWA AJILI YA YESU!!!
Paulo anaandika,
“tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; 10ILI NIMJUE YEYE, na UWEZA WA KUFUFUKA KWAKE, na USHIRIKA WA MATESO YAKE, NIKIFANANISHWA NA KUFA KWAKE; 11ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu (resurrection of the dead).” (Flp 3:9-11)
-PAULO ANATAMANI SANA AONEKANE KATIKA KRISTO AKIWA NA HAKI ILE ITOKAYO KWA MUNGU IPATIKANAYO KWA IMANI YA KRISTO YESU
-ILI AMJUE YESU, NA UWEZA WA KUFUFUKA KWAKE YESU, NA USHIRIKA WA MATESO YAKE, AKIFANANISHWA NA KUFA KWAKE, ILI AWEZE, KWA NJIA YOYOTE, KUFIKILIA UFUFUO WA WAFU/KIYAMA YA WAFU
Uweza wa kufufuka kwake Yesu ndio ule ule unaotufufua sisi tulioamini kutoka kwenye mauti ya kiroho na kutufanya kuwa hai ndani ya Yesu! Na ndio uweza huo huo uliomwezesha Yesu kuishi kwa ushindi dhidi ya dhambi na mauti!!! Hizi ni nguvu za Mungu ambazo alitembea nazo Yesu hapa duniani kwa Roho Mtakatifu! Nguvu hizi pia zinapatikana kwako kwa Roho yuleyule wa Yesu pale unapomwamini Yeye, ukabatizwa, na kupata ondoleo la dhambi, na kisha kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu (Mdo 2:38-39)! Nguvu hizi zilimfunika Yesu alipouendea msalaba na kumpa kushinda ule udhaifu wa mwili; na sisi zinatupa kushinda kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi ili tuweze kupiga mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu! (Waebrania 12:1)
Unapokuwa unamngojea Bwana katika hali ya mateso na maumivu pasipo kuacha Imani wala kumwacha Yesu, unasababisha nguvu zilezile kujaa ndani yako na kukuinua juu ya udhaifu wote wa kibinadamu, na hivyo kukuvika uungu wa Yesu unaokuweka katika daraja moja na Yesu kwa habari ya nguvu za Mungu! Bwana wetu Yesu alining’inia masaa matatu juu ya msalaba akiwa ana maumivu makali, huku akivuja damu, huku akikejeliwa vikali! ILE ILIWAKILISHA HALI YA KUTOWEZA KUFANYA LOLOTE (HELPLESSNESS) YA MWANADAMU ANAYETESEKA! YAANI, UNAUMIA, UNATESEKA NA HAUNA UNALOWEZA KUFANYA, NA WALA HAUJUI HALI HIYO ITAISHA LINI?! Yesu alipitia hali hiyo ngumu wanayopitia wanadamu ili aje AWATOE WANADAMU WOTE WANAOMWAMINI KUTOKA KATIKA HALI HIYO NGUMU INAYOTESA NA KUUMIZA!!! NA WALA SI HIVYO TU BALI PIA AJE KUWASAIDIA, KWA KUWATIA NGUVU ZA KUSHINDA, WATAKATIFU WANAOPITIA MAJARIBU MBALIMBALI YA IMANI YENYE KUUMIZA NA KUHUZUNISHA.
Pale msalabani kwa Yesu imeandikwa,
45Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. 46Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?(Mathayo 27:45-46)
……MUNGU WANGU, MUNGU WANGU, MBONA UMENIACHA?! Ni kana kwamba Yesu alikuwa peke yake, siyo?! Pia ni kana kwamba Mungu alikuwa amemuacha, siyo?! Haya mawili;
1) KUONA MUNGU AMEKUACHA PEKE YAKO KWENYE MATESO NA MAUMIVU
2) KWAMBA UKO PEKE YAKO KWENYE HALI NGUMU UNAZOPITIA
Na pia kwamba,
3) MUNGU AMESHINDWA KUKUTETEA
4) MUNGU HAJALI SHIDA NA MAUMIVU YAKO
5) KWAMBA MUNGU NI MKATILI NA HAKUPENDI
HAYA HUWA NI MAWAZO AMBAYO SHETANI HUWA ANAYALETA KAMA MAFURIKO, AU UPEPO WA KISULISULI WAKATI WA TAABU YAKO ILI AKUFARAKANISHE NA MUNGU MOJA KWA MOJA! AKIFANIKIWA KUKUPATA UTAKUWA UMEJENGA KUMCHUKIA MUNGU NA KUMUONA NDIYE SABABU YA MATESO YAKO! NA PIA UTAWACHUKIA WANADAMU NA KUWAONA HAWAKUJALI NA HAWANA UPENDO! SHETANI ATAKUWA AMEINGIA MOYONI MWAKO KUPITIA CHUKI ILI AENDELEE KUKUTUMIKISHA KWENYE DHAMBI ZINGINE MPAKA AFANIKIWE KUKUPELEKA JEHANAMU USIPOTUBU NA KUREJEA KWA MUNGU ALIYE HAI!!!
Hayo mawazo anayoleta shetani hapo juu wakati wa maumivu, taabu na mateso huwa yanakubalika sana kwa mwanadamu anayeufuata mwili!!!
“Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. 6Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. 7Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.” (Rum 8:5-8)
KUUFUATA MWILI NA KUYAFIKIRI MAMBO YA MWILI KUNA MAANA YA KUYAPA NAFASI MOYONI NA MAISHANI MWAKO YALE MAWAZO ANAYOLETA SHETANI, KUHUSU MAUMIVU NA MATESO YAKO, YALIYO KINYUME NA KWELI!!!
-TUMESOMA HAPA JUU KWAMBA NIA YA MWILI/MAWAZO YA MWILI NI UADUI JUU YA MUNGU (HOSTILE TO GOD)
-MWILI/UTU WA KALE/UTU WA DHAMBI HAUWEZI NA HAUTAKI KUMTII MUNGU
-USHIRIKA WA MATESO YA KRISTO UNAKUFUNGULIA MLANGO WA KUONDOA UADUI HUO WA SIRI MOYONI ILI UZIDI KUTAKASIKA NA KUWA NA MOYO SAFI
-USHIRIKA WA MATESO YA KRISTO UNAONEKANA NI MATESO NA MAUMIVU KWA SABABU UNAKUPELEKA KINYUME NA WEWE MWENYEWE! FAHARI YAKO, FURAHA YAKO, MAPENZI YAKO, MATAKWA YAKO, NIA YA MOYO WAKO, MALENGO YAKO N.K YALE YASIYOPATANA NA MIPANGO/NIA/MATAKWA/MAKUSUDI NA MALENGO YA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU!!!
-USHIRIKA WA MATESO YA KRISTO UNABADILISHA MOYO WAKO, MAWAZO YAKO, MANENO YAKO, NA MATENDO YAKO ILI YOTE YAPATANE NA KWELI NA HIVYO KUZIDI KUFANANA NA YESU!!!
“Maana hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli” (2 Kor 13:8)
-ASILI YA MWANADAMU ILIBADILIKA NA KUWA YENYE KUASI (SINFUL/REBELLIOUS NATURE)
-ROHO YA UASI ILIMWINGIA NA KUENDELEA KUMTAWALA MWANADAMU TANGU MIMBA KUTUNGWA MPAKA MTOTO KUZALIWA
“Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu;
Mama yangu alinichukua mimba hatiani.” (Zab 51:5)
-HATUZALIWI NA DHAMBI, BALI TUNAZALIWA NA ASILI YA DHAMBI INAYOTUPELEKEA KUANZA KUTENDA DHAMBI BILA KUSOMEA WALA KUFUNDISHWA PALE TU UNAPOFIKIA KUPAMBANUA MEMA NA MABAYA! HII HAIJALISHI UMEZALIWA KWENYE DINI AU DHEHEBU GANI!!!
Biblia inafundisha kwamba sisi tulioamini, tukaokoka, tulisulubiwa pamoja na Kristo, tukazikwa pamoja naye, na kisha tukafufuliwa pamoja naye.
“Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; 6mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena” (Rum 6:5-6)
-UTU WETU WA KALE ULISULUBIWA PAMOJA NAYE, NA MWILI WA DHAMBI UKABATILIKA NA HIVYO HATUTUMIKII DHAMBI TENA
-TUKAUNGANIKA NAYE KWA MFANO WA MAUTI YAKE NA KUZIKWA PAMOJA NAYE
-TUKAUNGANIKA PAMOJA NAYE KATIKA MFANO WA KUFUFUKA KWAKE
Tulisulubiwa pamoja na Yesu, tukafa pamoja naye, tukazikwa pamoja naye, na kisha tukafufuliwa pamoja naye KWA IMANI! Na hili ndilo lilikuwa kusudi la Yesu kuvaa mwili ili amweke huru mwanadamu mwenye mwili kutoka katika utumwa wa dhambi!!! YESU ALIMUDU HAYA WAKATI HUO KWA NGUVU ZA MUNGU! NA SISI TUNAMUDU HAYA WAKATI HUU KWA NGUVU HIZO HIZO ZA MUNGU TUKIWA NA YESU HUYO HUYO!!! TULISOMA ANDIKO PALE MWANZO KABISA KWAMBA YESU ALIIDHARAU AIBU NA KUUSTAHIMILI MSALABA
Waebrania 12:2
“tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.”
YESU ALIIDHARAU AIBU NA KUUSTAHIMILI MSALABA KWA AJILI YETU!! IMETUPASA NA SISI KUIDHARAU AIBU NA KUSTAHIMILI MISALABA YETU WENYEWE KWA AJILI YA YESU (Lk 9:23);
Yesu alikuja ili kututoa kwenye ubinadamu na kutuingiza kwenye uungu! Yaani, alikuja kutukirimia uungu sisi tunaomwamini yeye kama Bwana na Mwokozi wetu!
“Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2 Pet 1:4)
-AMETUKIRIMIA AHADI KUBWA MNO NA ZA THAMANI
-ILI KWAMBA KWA HIZO TUPATE KUWA WASHIRIKA WA TABIA YA UUNGU
-HII INAPATANA NA MAANDIKO KAMA MWANDISHI WA ZABURI ALIVYOANDIKA;
“Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.” (Zab 82:6)
WANA WA MUNGU NDANI YA KRISTO NI MIUNGU! WANAENENDA KATIKA UWEZA WA UUNGU!!!
Na inawezekana kuenenda hivyo kwa sababu hawaufuati mwili bali Roho! Wanaenenda kwa Roho na wala hawawezi kamwe kuzitimiza tamaa za mwili (Gal 5:16) Ule uadui wa asili umeondolewa, wametakasika, wako safi roho, nafsi na mwili! Ni lazima ieleweke kwamba TUMESAMEHEWA NA SASA TUNATAKASWA ILI KUZAA MATUNDA YA TOBA NA MSAMAHA! KWAMBA TUWEZE KUENENDA KATIKA KWELI SIKUZOTE ZA MAISHA YETU!!! Ule uadui wa mwili na mawazo yake ndio kikwazo cha kuuona utukufu wa Mungu kupitia ishara, maajabu na miujiza kwa jina la Yesu! KULE KUPITIA MAUMIVU KWA MUDA USIOJULIKANA KWAMBA LINI YATAKOMA HALI UKIMNG’ANG’ANIA YESU KUNAVUNJA VIKWAZO VYOTE VYA MWILI, DUNIA NA SHETANI NA KURUHUSU KUJAZWA ROHO ZAIDI
Jinsi mwili unavyozidi kumezwa na Roho kwa kuuvua utu wa kale na kuvaa utu mpya ndivyo mwamini anavyozidi kujaa Yesu na kuenenda kwa Roho yuleyule wa Kristo! Na hivyo kuenenda kwa nguvu zilezile za Kristo!!! Inasemekana no pain, no gain! (yaani, hamna kuumia, hamna kupata faida); Vivyo hivyo kiroho kama hamna maumivu hamna kupata faida za kiroho kama maandiko haya hapa chini yanavyoonyesha! Yasome kwa umakini ujifunze wewe mwenyewe faida zinazotokana na shida, adha, mateso na maumivu!
1) “ Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.” (Ayu 23:10)
2) “Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuru ya mateso” (Isa 48:10)
3) “Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu, Hapo ningalipotea katika taabu zangu.” (Zab 119:92)
4) “Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA humponya nayo yote.” (Zab 34:19)
5) “Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.” (Mith 24:10)
6) “Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; 4atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu. 5Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo. 6Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi. 7) Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.” (2 Kor 1:3-7)
8) “Wakakubali maneno yake; nao walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha wakawaacha waende zao. 41Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo. 42Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.” (Mdo 5:40-42)
9) “3Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu. 4Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi; 5tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana,
Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana,
Wala usizimie moyo ukikemewa naye;
6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi,
Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
7Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? 8Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? 10Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. 11Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. 12Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, 13mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.” (Ebrania 12:3-13)
-KURUDIWA NI FUNGU LA WOTE
-KAMA HAUNA KURUDIWA NI MWANA HARAMU WEWE
-NI BORA SANA KUJITIA CHINI YA BABA WA ROHO ZETU ILI TUPATE KUISHI (ABUNDANT LIFE)
-BABA YETU WA MBINGUNI HUTURUDI KWA FAIDA YA ROHO ZETU ILI TUPATE KUSHIRIKI UTAKATIFU WAKE
-WAKATI WA KUPITA/MATESO/DHIKI HAUONEKANI KUWA NI KITU CHA FURAHA BALI HUZUNI
-BAADAE WATAKATIFU HUZOEZWA NA HIYO “ADHABU”NA KUWALETEA MATUNDA YA HAKI YENYE AMANI (UZAAJI MATUNDA HUPATIKANA)
-HIVYO UNATAKIWA KUJITOA KWA BABA YAKO KWA NJIA YA USHIRIKA WA MATESO YA KRISTO ILI KILA KILICHO LEGELEGE/POOZA/KIGONJWA/KIWETE KIPATE KUPONYWA!!!
KULE KUSEMA ADHABU NI KWA SABABU MWILI UNATAFSIRI YALE USIYOYATAKA YANAYOENDELEA KUWA NI “ADHABU”, LAKINI UKWELI HUWA NI MATIBABU YA KIROHO YANAYOTUPONYA NA KUTUTAKASA, NA KUTUFANYA WATAKATIFU/WASIO NA UCHUNGU, WALA UGONJWA, WALA UDHAIFU!!!
10) 2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. (Yak 1:2-4)
-HESABU KUWA NI FURAHA TUPU UNAPOANGUKIA KATIKA MAJARIBU YA NAMNA MBALIMBALI
-HAPA INAYOJARIBIWA NI IMANI YAKO YA THAMANI SANA
-KUJARIBIWA HUKO NA KUVUMILIA HUZAA SABURI (UWEZO WA KUVUMILIA NA KUNGOJEA KATIKA HALI YA MAUMIVU NA MATESO BILA KUCHOKA WALA KUKATA TAMAA AU KURUDI NYUMA)
-SABURI INAKUPELEKEA KUWA MKAMILIFU: YAANI, UNAKUWA MKAMILIFU NA MTIMILIFU USIYEPUNGUKIWA NENO LOLOTE!!!-perfect and entire always wanting nothing;hamna kupungukiwa kiroho, kiakili, kihisia, kimwili n.k –no lack, no want!! LAKINI NI KUPITIA SABURI!!! KWA NJIA YA KUVUMILIA MAJARIBU YA IMANI!!!
KATIKA UKAMILIFU HUU SHETANI HANA CHA KUKURINGISHIA WALA KUKUSHAWISHI NACHO CHA DUNIA HII CHOCHOTE!! Si fedha, si cheo, si mali, si umaarufu, si sifa, si shukrani, si utukufu, si makwazo(haukwaziki kwa lolote!), si digrii, si ajira, n.k YAANI,
A B
-KUWA NAVYO = KUTOKUWA NAVYO
-KUMILIKI = KUTOMILIKI
-KUISHIWA = KUWA NA VINGI
-KUPATA = KUKOSA
-KUTENDEWA = KUTOTENDEWA
-KUPEWA = KUTOPEWA
-KUOA = KUTOOA
-KUWA NA PESA = KUTOKUWA NA PESA N.K
- A=B
A-NI UPANDE WA MWILINI/MATARAJIO YA MWILI
B-MATARAJIO YA MWILINI HAYAKWENDA ULIVYOTARAJIA
CHOCHOTE CHA DUNIA HII, LOLOTE LA DUNIA HII, YOYOTE YA DUNIA HII, ZOZOTE ZA DUNIA HII, KOKOTE KWA DUNIA HII, YEYOTE WA DUNIA HII, VYOVYOTE VYA DUNIA HII, POPOTE PA DUNIA HII, YOTE YA DUNIA HII, WOTE WA DUNIA HII, ZOTE ZA DUNIA HII, HAYANA ATHARI ZOZOTE KWANGU MIMI KWA WINGI AU UCHACHE WAKE, KUWEPO AU KUTOKUWEKO KWAKE, KUPATA AU KUKOSA KWAKE, KUFANIKIWA AU KUTOFANIKIWA KWAKE N.K BALI YESU TU PEKE YAKE NDO HAJA YANGU, UTOSHELEVU WANGU, HITAJI LANGU NA KILA KITU KWANGU!!!
Hii ndiyo maana ikaandikwa;
>> “Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana; 30na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu. 31Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.” (1 Kor 7:29-31)
>> “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele” (1 Yoh 2:15-17)
-UPENDO WA MUNGU MOYONI MWAKO USIWE NA MSHINDANI YEYOTE
-YESU ANATAKA MOYO WAKO WOTE
SABABU KUU KWA NINI MAUMIVU YANARUHUSIWA NI KWAMBA MOYO WAKO BADO UKO KWENYE VITU/WATU/HALI/MAZINGIRA YA DUNIA HII NA BWANA YESU ANAKUONGOZA KWA UPENDO UMPE MOYO WAKO WOTE!!!ANAPOVIONDOA KWA MUDA UNAUMIA!!! ANAPOONEKANA KUVICHELEWESHA, UNAUMIA!!!VIKIONDOKA MOYONI MWAKO HAUUMII TENA!KUTOUMIA NI ISHARA KWAMBA UMEPONA, UMEWEKWA HURU, UMEKOMBOLEWA KUTOKA KWENYE IBADA YA SANAMU NA TAMAA ZA KIDUNIA, NA MOYO WAKO UKO IMARA UKIMTUMAINI BWANA PASIPO KUJALI UNA FEDHA AU HUNA, UNA KAZI AU UMEFUKUZWA, UMEKUBALIWA AU UMEKATALIWA, UMEFAULU AU UMEFELI, UMESHINDA AU UMESHINDWA, UNAVYO AU HUNA, UNA VINGI AU VICHACHE, UMEHESHIMIWA AU UMEDHARAULIWA, UMESHIBA AU UNA NJAA N.K. KUTOUMIA TENA UNAPOPITIA HALI AU MAZINGIRA YA KUUMIZA WAKATI UNAPOMNGOJEA BWANA NI ISHARA KWAMBA KAZI YA MSALABA IMEKAMILIKA NDANI YAKO; UMEUSULUBISHA MWILI PAMOJA NA TAMAA ZAKE MBAYA NA MAWAZO YAKE MABAYA, UMEZIFIA TAMAA ZA DHAMBI, NA UMEFUFULIWA PAMOJA NA KRISTO KWA NGUVU ZA MUNGU NA SASA UNAENENDA KATIKA MAISHA MAPYA YALIYO HURU MBALI NA TAMAA ZA KIMWILI NA ZA KIDUNIA. UNAPOKUWA BADO NA VITU MOYONI HUWEZI KUISHI KWA AJILI YA YESU KRISTO PEKE YAKE.
“tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao” (2 Kor 5:15)
New
Living Translation
He died for everyone so that those who receive his new life will no longer live
for themselves. Instead, they will live for Christ, who died and was raised for
them. (2 Cor 5:15)