LENGO SAHIHI LA KUTOA
|
B |
iblia inasema,
1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
Mwanzo 12:1
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
Mwanzo 12:2
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Mwanzo 12:3
Mungu alimbariki Ibrahimu ILI NAYE AWE BARAKA KWA MATAIFA YOTE YA DUNIA! Huu ndio mpango wa Mungu kwa wanadamu wote! Yaani, Mungu amekusudia kufikisha baraka zake zote kwa ulimwengu kupitia wanadamu WANAOMWAMINI NA WANAOMPENDA KWA DHATI NA KUMTII!! Baraka ya Ibrahimu imeufikia ulimwengu wote leo kupitia Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wa dunia yote! (Wagalatia 3:9,13-14)
>> WENGI HUJIZUILIA BARAKA ZAO PALE WANAPOANZA KUBARIKIWA KWA KURUHUSU ZILE BARAKA "KUINGIA MIOYONI MWAO" NA HATIMAYE KUJA KUWA SANAMU AU miungu MBELE ZA MUNGU!! Yaani, upendo wao unahamia kwa "Isaka" na kuhama kutoka kwa "aliyemtoa Isaka!" Wengi mioyo yao imehamia kwenye fedha zao, vyeo, mke, mume, watoto, mali, utajiri, upako, miujiza, ishara, maajabu, huduma, mafanikio, kazi za mikono, n.k. NA KUMWACHA MUNGU; hivyo wamejivuna, wamejikweza, wamejiinua, wamependa sifa za wanadamu zaidi, wamependa zaidi umaarufu wao binafsi, wameingiwa na tamaa ya fedha, mali, utajiri, ulafi, uzinzi, wamejiona miungu watu, wamejidhania wameshafika au wameshafuzu tayari, wamewadharau wengine na kuwashusha, wamejiona bora zaidi, wamejiona wa kiroho zaidi, wamejilinganisha, wamehamisha tumaini lao na kuliweka kwa wanadamu, kwa kazi, kwa huduma, kwa washirika, n.k. NA SIYO MUNGU TENA: wengine wamejiona kuwa ni badala ya Mungu, hivyo wamependa kuogopwa, kutetemekewa, na hata kusujudiwa!! Kiburi kimeingia na kuwapoteza njia! Wamefuata njia zao wenyewe, wamebuni mafundisho yao wenyewe kinyume na kweli, n.k. UOVU UMEWATEKA NA KUWATAWALA! Laiti wangejinyenyekeza kwa Mungu, wakiwa wamejaa hofu na kutetemeka, na kumshukuru, kumwinua, na kumpa sifa zote, shukrani zote, heshima zote, na utukufu wote Mungu, wakimtumainia, na kumtegemea neema yake na rehema zake, pengine wangekuwa salama!!
UTOAJI WA KIBINAFSI (SELFISH GIVING)
|
S |
hida moja kubwa sana ni UTOAJI WA KIBINAFSI (SELFISH GIVING)!! Wengi hutoa kwa malengo ya kibinafsi!! Wengi hutoa ili wapate!! Hili siyo lengo wala mpango wa Mungu kibiblia!! Mungu amekubariki wewe mtoto wa Mungu kwa baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho ndani yake Kristo Yesu (Efe 1:3) Katika baraka hizo kuna:
1) Baraka ya Utoaji: ambayo ni roho ya utoaji, au neema ya utoaji; hii ni baraka ya Mungu inayokuwezesha KUTOA AU KUPANDA MBEGU sawasawa na Neno la Mungu! Hii maana yake umebarikiwa kwa moyo wa utoaji wa Yesu ili UTOE KWA UPENDO na kudumu katika kutenda mema, kama maandiko yasemavyo, mema ambayo Mungu alishayaandaa tangu kabla wewe hujazaliwa, kwamba uje kuyatenda (Efe 2:10) Unatoa kwa msukumo wa roho ya utoaji iliyomo ndani yako! Unatoa kwa msukumo wa ndani na siyo msukumo wa nje! Unatoa kwa kuwa umebarikiwa!! Lengo, na msukumo, na nia ya roho ya utoaji, NI KUTOA SIYO KUPOKEA, na ndiyo maana imeandikwa "Ni heri kutoa kuliko kupokea" (Matendo 20:35) Moyo wa utoaji wa Yesu ndani yako UNA UPENDO NA HURUMA ZA YESU, na lengo lake ni kuhurumia na kusaidia; kuhurumia na kuinua; kuhurumia na kufariji; kuhurumia na kufadhili; kuhurumia na kuokoa; kuhurumia na kufaidia: Yaani, kuondoa shida, taabu, adha, upungufu, uhitaji, mateso, huzuni, fadhaa, kuchanganyikiwa, aibu, maumivu, umaskini, na yote kama hayo, kwa maskini na wahitaji wote, mahali pote, sikuzote. Utoaji wa Upendo unagusa, unaganga, unatibu, unafariji, unatia moyo, na kuburudisha mioyo!! UTOAJI ULIO BARAKA UNAELEKEZA HURUMA ZAKE KWA ANAYEPOKEA ILI KUMTOA MAHALI PA GIZA, PA UCHUNGU, PA KUISHIWA, PA KUHANGAIKA, PA KUTESEKA, PA KUFADHAIKA, PA KUHUZUNIKA, PA KUDHARAULIKA, PA KUKOSA MSAADA, PA UHITAJI, N.K.
>> UTOAJI ULIO BARAKA UNATATUA MATATIZO NA KULETA MAJIBU PALE YALIPOKOSEKANA KIROHO, KIAKILI, KIHISIA, KIMWILI, KIFEDHA, KIMALI NA VITU, NA KIJAMII; NA KULETA SULUHISHO LA KUDUMU.
>> BARAKA YA UTOAJI NI PROBLEM-SOLVER NA SOLUTION-GIVER,[INATATUA MATATIZO NA KUTOA SULUHISHO]; NA KAMWE HAITAFUTI FAIDA BINAFSI!! ALIYEBARIKIWA KWA MOYO WA KUTOA AMETOSHEKA NA KURIDHIKA NA MUNGU!! AMEJITOSHELEZA KATIKA MUNGU!! ANA VYOTE, NA SI MHITAJI, MAANA MOYO WAKE UMEJAA MUNGU, NDANI YAKE YESU KRISTO, BWANA NA MWOKOZI WETU!!
>> ALIYEBARIKIWA KWA ROHO YA UTOAJI HATAFUTI BARAKA MAANA YEYE AMESHABARIKIWA NA HIVYO YEYE NI BARAKA KWA ULIMWENGU (HE WHO IS BLESSED SEEKETH NOT BLESSINGS, FOR HE IS A BLESSING ALREADY! HE SEEKETH TO BLESS AND NOT TO BE BLESSED!!) YAANI, YEYE ANATAFUTA KUBARIKI NA SI KUBARIKIWA!! WANAOTAFUTA KUBARIKIWA HUDHIHIRISHA WASIVYOELEWA MPANGO WA MUNGU, AU MIOYO YAO WASIVYO NA BARAKA YA UTOAJI!! Agano Jipya la Damu ya Yesu ni Agano la Baraka Zote za Kiroho Kwa Wamwaminio Yesu!! Wamebarikiwa, hawatafuti baraka! Hawatafuti KUBARIKIWA bali wanatafuta KUBARIKI! Wao ni watoaji (GIVERS) na siyo wapokeaji (RECEIVERS)! Biblia inasema,
1) 6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. (2 Wakorintho 9:6)
>> HAPA BIBLIA IMEWEKA KANUNI NA SIYO KIWANGO
>> HII NI KANUNI YA KWANZA YA UWIANO WA KUTOA NA KUPOKEA, KUPANDA NA KUVUNA!!
2) 7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. (2 Wakorintho 9:7)
>> KANUNI YA PILI YA UTOAJI INAHUSU "MOYO UNAOTOA" Mungu hataki na wala hapendezwi na KUTOA KWA LAZIMA AU KWA KUTISHWA KWA NAMNA YOYOTE!!
>> KANUNI HII INATAKA "UTOE KWA MOYO WA HIYARI au MOYO WA KUPENDA!!! Huu ni UTOAJI WA UPENDO AMBAPO UNATOA KWA KADIRI UNAVYOMPENDA MUNGU NA MWANADAMU!! YAANI, UTOAJI WAKO UELEZEE UPENDO WAKO ULIONAO HATA UKATOA! YEYE AMETUPA KIELELEZO KWAMBA "Aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." (Yoh 3:16)
>> MUNGU ALITOA KWA UPENDO KWA FAIDA YETU SISI TULIOUPOKEA UPENDO HUO MIOYONI MWETU
-Unapotoa kwa upendo NI KWA FAIDA YA UNAOWAPA! YAANI, UNAWABARIKI! UNAFANYIKA BARAKA KWAO!! HAUTOI ILI UBARIKIWE!! (huu ni utoaji wa watenda dhambi walio wabinafsi) UNATOA KUBARIKI MAANA WEWE NI BARAKA TAYARI KWA KUWA UNAZO TAYARI BARAKA ZOTE!! KUTOA KWAKO NI KUWA BARAKA KWA UNAOWAPA! UNAWABARIKI KWA KUWA UMEBARIKIWA!!
Linganisha maandiko haya!!
>> 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Malaki 3:10
>> LETE ZAKA KAMILI GHALANI /KIWEMO CHAKULA NYUMBANI MWANGU/NITAWAFUNGULIA MADIRISHA YA MBINGUNI/NITAWAMWAGIENI BARAKA!!!........!
>> HII NI BARAKA YENYE SHARTI (CONDITIONAL BLESSING): ILI UBARIKIWE LAZIMA ULETE ZAKA KAMILI! BARAKA HII INATEGEMEA "MATENDO YAKO" YAANI, KULETA ZAKA KAMILI GHALANI! SHARTI LA BARAKA HIZI NI "TENDO LA NJE" (EXTERNAL ACT) AMBALO LAZIMA ULITENDE KWANZA ILI UIRITHI HIYO BARAKA!
>> NA PIA BARAKA HII IMEWEKEWA KIWANGO, YAANI ASILIMIA KUMI (10%)
Linganisha na maandiko yafuatayo:
"3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;" (Waefeso 1:3)
>> HIZI NI BARAKA ZA AGANO JIPYA LA DAMU YA YESU AMBAPO KITENDO CHA WEWE KUMWAMINI YESU, KUOKOKA, NA KUWA NDANI YAKE, KINAKUFANYA WEWE UWE UMEBARIKIWA TAYARI KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE YESU!!
>> HAPA UMEBARIKIWA TAYARI KWA BARAKA ZOTE KABLA HATA HUJATENDA LOLOTE!! UMEBARIKIWA KUPITIA IMANI YAKO KWA YESU!! BARAKA YA IBRAHIMU IMEKUFIKIA MTOTO WA MUNGU KWA NJIA YA YESU KRISTO!!
5 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Mwanzo 15:5
6 Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Mwanzo 15:6
NA HAPA PAULO ANASEMA;
"6 Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.” (Gal 3:6)
>> IBRAHIMU ALIMWAMINI MUNGU AKAHESABIWA HAKI, NA AKABARIKIWA KWA NJIA YA IMANI YAKE!
>> LEO UKIMWAMINI YESU UNABARIKIWA KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE YESU KRISTO, MAANA WEWE TAYARI NI MTOTO WA MUNGU! BARAKA ZOTE ALIZOKUWA NAZO YESU NI ZAKO NDANI YAKE! KULE KUSEMA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KUNAMAANISHA HAMNA BARAKA KATIKA BIBLIA ALIYOIBAKISHA AMBAYO SIYO YAKO!! BARAKA ZAKO NI ZA KIROHO KWANZA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, KISHA ZITAKUWA BARAKA ZA KIAKILI, KIHISIA, KIMWILI, KIFEDHA, KIMALI NA VITU, NA MWISHO KIJAMII!
>> KULE KUSEMA BARAKA ZOTE ZA ROHONI KUMEONDOA LAANA ZOTE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE KRISTO YESU BWANA WETU! HAMNA LAANA NDANI YA YESU!!
>> UPENDO WA MUNGU NDIO UNAOTUBIDIISHA KUTENDA MEMA, KUPANDA MBEGU ZA UPENDO, NA KUTOA KWA UPENDO NA HURUMA ZA KRISTO!!
KUJIZUILIA BARAKA??!!
>> Wakristo wengi wamejizuilia baraka zao kwa sababu zifuatazo:
1) Ubinafsi unaozaa ubahili, na uchoyo, na umimi!
2) Kupanda mbegu na kutenda mema kwa kutafuta faida binafsi
3) Kulimbikiza fedha, mali, na vitu, na kujiwekea hazina hapa duniani BADALA YA KUJIWEKEA HAZINA MBIGUNI! (Mt 6:19-21)
>>Ibrahimu aliahidiwa mtoto ambaye alimngojea kwa miaka 25! Isaka alikuwa "mwana wa ahadi!", lakini Mungu alimuomba Ibrahimu amtoe Isaka "sadaka ya kuteketezwa!!" Yaani, aliombwa KUITOA SADAKA BARAKA ALIYOAHIDIWA, NA KUINGOJEA SANA, NA KUVUMILIA MENGI, NA KUPITIA MAJARIBU MENGI, KWA AJILI YAKE!! ALIPOSHINDA JARIBIO (TEST) HILO, MUNGU ALILIFANYA IMARA AGANO LAKE NA IBRAHIMU KWA KIAPO, KWAMBA LAZIMA AHADI YAKE ITIMIE KWA IBRAHIMU!! NA IBRAHIMU AKAITWA BABA WA IMANI, CHEO CHA KIROHO ALICHOPEWA KUTOKANA NA IMANI ALIYOKUWA NAYO, NA KICHO CHAKE KWA MUNGU!!!
1 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
Mwanzo 22:1
2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
Mwanzo 22:2
3 Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.
Mwanzo 22:3
4 Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake, akapaona mahali pakali mbali.
Mwanzo 22:4
5 Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena.
Mwanzo 22:5
6 Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja. (Mwanzo 22:6)
9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
Mwanzo 22:9
10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.
Mwanzo 22:10
11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
Mwanzo 22:11
12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
Mwanzo 22:12
13 Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
Mwanzo 22:13
14 Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,kama watu wasemavyo hata leo,Katika mlima wa BWANA itapatikana.
Mwanzo 22:14
15 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni
Mwanzo 22:15
16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
Mwanzo 22:16
17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
Mwanzo 22:17
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu. Mwanzo 22:18
>> MOYO WA IBRAHIMU UNGEHAMIA KWA ISAKA ASINGEFAULU JARIBIO LILE, MAANA ANGELIMZUILIA MUNGU ISAKA NA KUKOSA BARAKA YA MUNGU!!
"8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;"
2 Wakorintho 9:8
>> UKIISHA KUTOA KWA MOYO WA KUPENDA AU MOYO WA UKUNJUFU, AU UKIISHA KUPANDA KWA UKARIMU, Biblia inasema,
1) MUNGU AWEZA KUKUJAZA KILA NEEMA KWA WINGI- HII NI BARAKA YA UTELE (BLESSING OF ABUNDANCE!)
2) ILI UKIWA NA RIDHIKI ZA KILA NAMNA SIKUZOTE(BLESSING OF WEALTH AND RICHES):[ 2 KOR 9:8 ]
New International Version (2 Cor 9:8)
And God is able to bless you abundantly, so that in all things at all times, having all that you need, you will abound in every good work.
[NA MUNGU AWEZA KUKUBARIKI KWA BARAKA TELE, ILI KATIKA MAMBO YOTE NA SIKUZOTE, UKIWA NA KILA UNACHOKIHITAJI, UPATE KUZIDI SANA KATIKA KILA TENDO JEMA!!]
>> UMEBARIKIWA ILI UWE BARAKA KWA WENGINE! UTELE WA BARAKA ULIZOAMINIWA UWAKILI NI KWA LENGO LA KUKUFANYA UWE TAJIRI WA MATENDO MEMA! UTAJIRI WA AGANO JIPYA NI UTAJIRI WA MATENDO MEMA! KILA NEEMA ULIYOKIRIMIWA NA BWANA WETU YESU NI KWA AJILI YA KUTENDEA MEMA NA KAMWE SIYO KWA AJILI YA KUJILIMBIKIZIA NA KUJIWEKEA HAZINA HAPA DUNIANI, BALI NI KWA AJILI YA KUJIWEKEA HAZINA MBINGUNI!! (Mathayo 6:19-21)
>> Iko wazi kwa andiko hili kwamba
A) HAKUNA BARAKA AMBAYO MUNGU AMEISAZA HAJAKUPA!!
B) AMEKUBARIKI KWA UTELE WOTE WA VITU VYOTE
C) MATOKEO YAKE UNA KILA UNACHOKIHITAJI
D) LENGO NI ILI UPATE SASA KUZIDI KATIKA KILA TENDO JEMA!!
Hii kwenye D ni eneo la WEWE KUWA BARAKA KWA WENGINE WOTE, HUSUSANI WALE WAAMINIO (GAL 6:9-10)
>> Unaweza kuona hapa kwamba HATUTOI NDANI YA YESU, HUKU TUMEJENGA GHALA LA KURUNDIKA NA KUKUSANYA MAVUNO BAADA YA KUPANDA!! Hiyo isingetutofautisha na Tajiri Mpumbavu (Luka 12:15-21)! Anaitwa mpumbavu kwa sababu "ALIJIWEKEA NAFSI YAKE AKIBA HAPA DUNIANI, ASIJITAJIRISHE KWA MUNGU" (Lk 12:21) SISI TUNATOA NA KUTENDA MEMA KAMA NAMNA YA KUJIWEKEA HAZINA MBINGUNI NA HIVYO KUJITAJIRISHA KATIKA MUNGU (Mt 6:19-21) TULIOBARIKIWA KWA MIOYO YA UTOAJI TUNATOA, TUNAPANDA MBEGU, NA
KUTENDA MEMA KAMA KUWEKEZA KATIKA MUNGU maana Yesu alishasema HAZINA/AKIBA YAKO ILIPO NDIPO UTAKAPOKUWAPO NA MOYO WAKO (MT 6:21)
>> Ni dhahiri ukianza kupokea baraka halafu ukasahau kwamba unatakiwa kuwa baraka kwa wengine LAZIMA UTAWEKA HAZINA DUNIANI NA MOYO WAKO KUMWACHA MUNGU!!
>> Roho Mtakatifu alinena kwa kalamu ya Paulo:
"17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha." (1 Timotheo 6:17)
"18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;" (1 Timotheo 6:18)
"19 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli."
(1 Timotheo 6:19)
Matajiri wote wa ulimwengu huu;
A) WASIJIVUNE
B) WASIUTUMAINIE UTAJIRI USIO WA KUTUMAINIKA
C) WAMTUMAINI MUNGU ATUPAYE VITU VYOTE TUVITUMIE KWA FURAHA
D) WATENDE MEMA
E) WAWE MATAJIRI KWA KUTENDA MEMA
F) WAWE NA UTAYARI WA KUTOA MALI ZAO (UKARIMU)
G) WAWE NA UTAYARI WA KUGAWANA MALI ZAO NA WENGINE NA KUSHIRIKIANA NAO KWA MOYO
>> KWA KUFANYA MAMBO HAYA SABA AMBAYO NI MAAGIZO YA ROHO MTAKATIFU,
E) WANAKUWA WANAJIWEKEA HAZINA NZURI KWA MUNGU KWA AJILI YA KESHO YAO HAPA NA MBINGUNI PIA, ILI WAPATE UZIMA WA MILELE WA KWELI!
>>SASA PALE KWENYE NAMBA TANO (E) ANAAGIZA BWANA KWAMBA WAWE MATAJIRI KWA KUTENDA MEMA (MATAJIRI WA MATENDO MEMA) KAMA YESU ALIVYOKUWA, NA PIA ALIVYO LEO NDANI YA WOTE WANAOENENDA KATIKA UPENDO WA MUNGU KAMA ALIVYOAGIZA KWENYE NENO LAKE:
"16 Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa Yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu, imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.” (1 Yohana 3:16)
“9 kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.” (2 Wakorintho 9:9)
10 Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu; (2 Wakorintho 9:10)
1) MUNGU ANAPOANZA KUDHIHIRISHA BARAKA ZAKE KWAKO HIZO NI "MBEGU ZA KUPANDA"!! ANAKUPA MBEGU ILI UKAZIPANDE SHAMBANI MWAKE!! SHAMBA LA MUNGU NI ULIMWENGU,
Matthew 13:38
"[38]The field is the world; the good seed are the children of the kingdom; but the tares are the children of the wicked one;
lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;"
2) UKIMALIZA MBEGU ALIZOKUPA KUZIPANDA ATAKUPA MBEGU ZAIDI, NAYE ATAZIZIDISHA SANA ILI UZIDI KUZIPANDA
3) HUWEZI KUWA TAJIRI WA MEMA USIPOKUWA MPANDA MBEGU!! UTAJIRI WA MEMA UNAZALIWA NA UPANDAJI MBEGU USIOKOMA SIKUZOTE, WAKATI WOTE, MAHALI POTE, KATIKA MAZINGIRA YOTE, NA HALI ZOTE!!
4) TAJIRI KATIKA UFALME WA MUNGU NI YULE ALIYEPANDA, NA ANAYEENDELEA KUPANDA, MBEGU ZA UPENDO ZA KILA AINA KATIKA SHAMBA LA BWANA AMBALO NI ULIMWENGU!!
>> UTAKAPOBADILIKA MOYO NA KUANZA KUTAFUTA BARAKA WAKATI UMESHABARIKIWA TAYARI, HAPO HAPO MUNGU NAYE ANAACHA KUZILETA NA KUZIDHIHIRISHA BARAKA ZAKE KWAKO!! BADILIKA MTAZAMO WAKO, BADILIKA MOYO WAKO, TUBU MGEUKIE BWANA ILI UPOKEE BARAKA ZA KWELI ZA MUNGU!! NA KISHA UWE BARAKA KWA WENGINE!!
UBARIKIWE KWA FUNDISHO HILO NALO LIKUPE MOYO SAHIHI NA MTAZAMO SAHIHI WA UTOAJI, NA UKATOKE KWENYE UOVU WA UBINAFSI, UCHOYO, NA TAMAA. UBARIKIWE!!