MPENDE HIVI....WAPENDE HIVI!!

             1 John 4 8 Love Does Not Know God Powerpoint Church Sermon | PowerPoint  Slide Presentation Sample | Slide PPT | Template Presentation

MPENDE……..WAPENDE………!!!

Kila mmoja anapenda kupendwa kiasili! Lakini tunatakiwa pia kupenda! Wengine husema mpende akupendaye! Lakini Biblia inasemaje kuhusu upendo? Inaposema mpende au wapende inamaanisha nini? Hapa siongelei upendo wa kibinadamu ambao ni rahisi kugeuka kuwa chuki wakati wowote! Naongelea upendo wa Mungu aliyetuumba maana imeandikwa;

“Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.” (1 Yoh 4:8)

-KAMA HAUPENDI KATIKA KWELI, WEWE HAUMJUI MUNGU KWA MUJIBU WA BIBLIA

-KWA MAANA MUNGU NI UPENDO!

Mungu ni Upendo! Kwa hiyo imetupasa kupenda kwa namna ya Mungu kwa maana huo ndio upendo halisi, na kama hauna upendo huu HAUWEZI KUPENDA KIKWELIKWELI! Huo unaouita upendo sio wa kweli kwa maana unategemea mazingira na hali fulani fulani za kibinadamu na za kidunia ambazo zikibadilika upendo huo huo unaweza kugeuka kuwa chuki na uadui! Na hii inasababishwa na dhambi ambayo sikuzote asili yake na tabia yake ni ubinafsi. Ubinafsi ni dhambi, ubinafsi ni chanzo cha dhambi, ubinafsi ni asili ya dhambi, ubinafsi ni sifa ya dhambi, ubinafsi ni tabia ya dhambi, ubinafsi ni kiini cha dhambi, ubinafsi na dhambi ni mmoja, (selfishness and sin are one) dhambi inatenda kazi kibinafsi sikuzote; UPENDO WA MUNGU HAUNA HATA CHEMBE YA UBINAFSI! (LOVE IS COMPLETELY UNSELFISH)

TABIA KUU YA UPENDO WA MUNGU

Tabia kuu ya upendo wa Mungu ni KUWAPENDA MAADUI. Biblia inasema,

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yoh 3:16)

-Mungu aliupenda ulimwengu ulioasi, yaani, alitupenda wanadamu tuliomwasi.

-Tulipoasi tulikuwa maadui zake mioyoni mwetu, kwenye akili zetu, na kwenye maisha yetu yote ya kila siku.

COLOSSIANS 1:21

New International Version
Once you were alienated from God and were enemies in your minds because of your evil behavior.”

New Living Translation
This includes you who were once far away from God. You were his enemies, separated from him by your evil thoughts and actions.”

“Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; (Kol 1:21)

>> Tulikuwa mbali sana na Mungu, tulikuwa maadui zake tukiwa tumetengwa naye kwa sababu ya mawazo na matendo yetu maovu! Mungu ni Mtakatifu na dhambi ni chukizo kwake! Ukitenda dhambi unakuwa unapinga moja kwa moja utakatifu wa Mungu kwa matendo yako maovu, na hivyo unakuwa adui yake. Sasa sisi tulikuwa hivyo na hukumu ya haki tuliyostahili ni kifo mara mbili! 1) Yaani, kifo cha kiroho hapa duniani na kisha, 2) Mauti ya milele/adhabu ya milele/kutengwa na Mungu milele jehanamu, kama ukifa ungali mwenye dhambi!! Kama wewe ni mtenda dhambi tayari umekufa kiroho hapa duniani;

“Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; 2ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme a uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;” (Efe 2:1-2)

-Waefeso walikuwa wamekufa kwa sababu ya MAKOSA NA DHAMBI ZAO mbele za Mungu kama vile wewe ulivyo sasa! Utakapomwamini Yesu atakusamehe na kukuondolea dhambi zako zote na hivyo kukufanya uwe hai pamoja naye kwa kuwa amekupatanisha na Mungu wako na kukukirimia uzima wake wa milele!

SASA MUNGU ALITUPENDA TUKIWA MAADUI, NA TUKIWA WAFU KWA SABABU YA DHAMBI NA MAKOSA YETU! ALITUPENDA TULIPOKUWA MAADUI ZAKE!

“Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; ……………” (Rum 5:10)

>>YAANI, MUNGU ALIMTOA MWANAWE PEKEE AFE KWA AJILI YA DHAMBI ZA ADUI ZAKE ILI AWAPATANISHE NA NAFSI YAKE!!!(2 Kor 5:19)

>>YAANI, BADALA YA KUTUANGAMIZA KAMA ILIVYOSTAHILI AKAAMUA KUTUSAMEHE NA KUTUOKOA NA ADHABU YA MILELE KWA KUMTOA YESU KRISTO KAMA SADAKA PEKEE YA DHAMBI YA MILELE ILI AFANYE UPATANISHO NA SISI TUSIHUKUMIWE KWA DHAMBI ZETU!!

>>YAANI, MAKOSA TUMEFANYA SISI KINYUME NA YEYE; DHAMBI TUMETENDA SISI KINYUME NA YEYE; TUMEMFANYIA KIBURI, JEURI, UKAIDI, DHARAU, UBISHI, MAJIVUNO NA CHUKI; LAKINI YEYE NDIYE ALIYEMTOA MWANAWE PEKEE AFE KWA AJILI YA DHAMBI ZETU NA KUTUPATANISHA! NA HUU NDIO UPENDO NA NDIYO MAANA AKATUAGIZA KWAMBA:

>> UPENDO NI SAFI NA MTAKATIFU (LOVE IS PURE AND HOLY) DHAMBI NI OVU NA BINAFSI (SIN IS EVIL AND SELFISH); MUNGU ASINGEKUWA MTAKATIFU TUNGEANGAMIA NA WALA ASINGETUTENDEA MEMA WALA ASINGETUOKOA KWA KUTUSAMEHE DHAMBI ZETU NA KUTUPA UZIMA WA MILELE; UKIWA MUOVU NA MTENDA DHAMBI HUWEZI KULITENDA FUNGU LA MAANDIKO LIFUATALO, MAANA UTAONA NI UPUUZI USIOWEZEKANA KUTENDEKA; ILE ASILI YA UOVU NA DHAMBI YA UBINAFSI INA VAZI LA CHUKI, AMBAO NI UCHUNGU MOYONI; UCHUNGU MOYONI NI KUTOSAMEHE, NI KISASI, NI UBAYA ULIOHIFADHIWA MOYONI. UPENDO HAUNA CHUKI, UPENDO HAUNA UCHUNGU MOYONI, UPENDO UNASAMEHE, UPENDO HAUTAFUTI MAMBO YAKE YENYEWE. Biblia inasema,

“27 Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, 28wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. 29Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. 30Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. 31Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo. 32Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao. 33Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. 34Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile. 35Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu. 36Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.” (Luka 6;27-36)

WAPENDE ADUI ZAKO

▪ WATENDEE MEMA WALE WANAOKUCHUKIA

▪ WABARIKI WALE WANAOKULAANI

▪ WAOMBEE WALE WANAOKUONEA

▪ AKUPIGAYE SHAVU MOJA MGEUZIE LA PILI (USISHINDANE NA MWOVU WALA USIPIGANE KIMWILI)

▪ AKUNYANG’ANYAYE JOHO LAKO USIMZUILIE NA KANZU

▪ AKUNYANG’ANYAYE VITU VYAKO USITAKE AKURUDISHIE

▪ VILE UNAVYOTAKA WATU WAKUTENDEE WATENDEE WEWE HIVYO SIKUZOTE

Kama haufanyi haya, hutaki kuyafanya haya, unaona hayawezekani kabisa haya kutendeka, n.k. je! una tofauti gani na mtenda dhambi ambaye;

HUWAPENDA WALE TU WAMPENDAO NA KUWACHUKIA ADUI ZAKE?

▪ HUWATENDEA MEMA WALE TU WAMTENDEAO MEMA YEYE?

▪ HUKOPESHA WATU HUKU AKITUMAINI KULIPWA?

▪ HUWALAANI WANAOMLAANI?

▪ AKINYANG’ANYWA KITU ANADAI/ANAGOMBANA/ANAJIPIGANIA/ANAJITETEA?

▪ HAWEZI KAMWE KUWATENDEA MEMA WANAOMCHUKIA?

▪ HAWEZI KAMWE KUWAOMBEA WANAOMUONEA?

▪ AKIPIGWA NAYE HURUDISHIA NA KUPIGANA?

Bali kama kweli wewe una upendo wa Mungu ndani yako utatii na kutenda hivi;

“……. Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.” (MST 35)

KAMA HAUFANYI HIVI WEWE SI MWANA WA MUNGU KWA MAANA UPENDO WA MUNGU HAUMO NDANI YAKO

UKISOMA KWA UMAKINI MAANDIKO HAYA UTAONA KWAMBA UPENDO HAUNA CHEMBE YA UBINAFSI BALI SIKUZOTE UNATAFUTA FAIDA YA MWINGINE/WENGINE, NA SIYO FAIDA BINAFSI!!! YESU ALIDHIHIRISHWA ILI AONDOE DHAMBI NA UBINAFSI WOTE MAISHANI MWAKO KAMA UKIMWAMINI.

“Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake” (1 Kor 10:24)

1 Cor 10:24

New International Version
No one should seek their own good, but the good of others.


New Living Translation
Don’t be concerned for your own good but for the good of others.

English Standard Version
Let no one seek his own good, but the good of his neighbor.”

>>MTU MWENYE UPENDO WA MUNGU HATAFUTI FAIDA YAKE BALI FAIDA YA WENGINE/MEMA YA WENGINE KWA KUWA HAMNA CHEMBE YA UBINAFSI NDANI YAKE

“Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe. 3Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi” (Rum 15:2-3)

2Each of us should please his neighbor for his good, to build him up. 3For even Christ did not please Himself, but as it is written: “The insults of those who insult You have fallen on Me.” (Rom 15:2-3)

YESU HAKUISHI KWA AJILI YA NAFSI YAKE MWENYEWE BALI KWA AJILI YA ULIMWENGU WOTE; NDIYO MAANA YOHANA MBATIZAJI ALIMSHUHUDIA AKISEMA “…., TAZAMA MWANAKONDOO WA MUNGU AICHUKUAYE DHAMBI YA ULIMWENGU!” (Yoh 1:29) NA HIVYO WOTE WALIO WA KRISTO HAWAISHI KWA AJILI YA NAFSI ZAO WENYEWE BALI KWA AJILI YA YESU (2 Kor 5:15). Kuishi kwa ajili ya Yesu ni kuishi kwa ajili ya mwili wa Kristo (Kanisa), na kwa ajili ya wanadamu wote waliopotea! Ni kuishi kwa ajili ya malengo, nia, makusudi, matakwa, mipango, madhumuni, maslahi, faida na mapenzi ya KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU! Hayo ndiyo maisha ya Upendo wa Mungu maana Yesu Kristo ndiye upendo wa Mungu kwa wanadamu katika mwili!! YESU NI UPENDO WA MUNGU NA KUMPOKEA YEYE AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO NI KUPOKEA PENDO LA MUNGU BABA YETU WA MBINGUNI!

“Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu ye yote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenipeleka.” (Yoh 13:20)

-NAYE ANIPOKEAYE MIMI AMPOKEA YEYE ALIYENIPELEKA!!!

-TUNAJUA KWAMBA ALIYEMPELEKA YESU NI UPENDO (1 Yoh 4:8)

-HIVYO AMPOKEAYE YESU ANAMPOKEA UPENDO MWENYEWE, YAANI, ANAPOKEA UPENDO WA MUNGU MOYONI MWAKE, ILI KWA HUO AWEZE KUWAPENDA WANADAMU

Sasa upendo wa Mungu una tabia zake ambazo ziko wazi kabisa na ukiwa nazo utajua kama unapenda ama unachukia!! Moyo wa mwanadamu awaye yote ama una upendo wa Mungu ama una chuki ya shetani, ingawa chuki hii inaweza kufichwa na upendo unaoitwa wa kibinadamu! Hili ni jina jingine zuri la chuki!!! Kwa nini? Tazama tabia za upendo hapa uelewe! KUMPENDA/KUWAPENDA NI NINI? Kabla sijaweka andiko hapa nikukumbushe kwamba tumeshaona kwamba

-KUWAPENDA WAKUPENDAO TU NI TABIA YA WENYE DHAMBI

-KUWAPENDA WAKUPENDAO TU NI UBINAFSI NA DHAMBI

-UPENDO HUTAFUTA SIKUZOTE FAIDA, MAFANIKIO, FURAHA, AMANI, MEMA, AFYA, USHINDI, N.K VYA WENGINE

-MWENYE UPENDO HAISHI KWA AJILI YA FAIDA YAKE TU BINAFSI KAMWE

-UPENDO UNAFURAHIA KUHUDUMIA, KUTUMIKIA, NA KUTENDEA MEMA WENGINE.

-UTOSHELEVU NA KURIDHIKA KWA UPENDO NI KATIKA KUTOSHELEZA NA KURIDHISHA WENGINE

NA UPENDO SIKUZOTE NA WAKATI WOTE CHANZO NA ASILI YAKE NI NENO NA AMRI ZA MUNGU;

“Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” (Yoh 14:21)

-UKIWA NA AMRI ZA MUNGU NA KUZISHIKA WEWE NDIWE UMPENDAYE YESU (UPENDO)

-UKILIPENDA PENDO LAKE NAYE ATAKUPENDA NA KUJIDHIHIRISHA (MANIFEST/REVEAL) KWAKO

-UTALIJUA NA KULIDHIHIRISHA PENDO LA MUNGU KWA ULIMWENGU

“Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.” (Yoh 14:23)

-IKIWA UNALISHIKA NENO LA MUNGU BASI KWELI WEWE UNAMPENDA YESU

-HII INAMAANISHA UNALIPENDA PENDO LA MUNGU

-KWA KUWA MUNGU NI UPENDO UKIFANYA HIVYO MUNGU NA NENO LAKE ATAKUJA KWAKO NA KUFANYA MAKAO YAKE NDANI YAKO

-NDIPOSA UTAKUWA UMEJAA UPENDO WA MUNGU

TABIA ZA UPENDO

“4Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8Upendo haupungui neno wakati wo wote” (1 Kor 13:4-8)

1) UPENDO HUVUMILIA/LOVE IS PATIENT

-Unayempenda utamvumilia! Siyo akifanya kosa dogo tu umevunja mahusiano! Hata akifanya makosa mara kwa mara bado utamvumilia! Kuna tofauti ya kumwamini na kumvumilia! Mara ngapi na wapi umeshindwa kuvumilia na kujaa ghadhabu na hasira na kuchukua maamuzi yasiyo na faida yoyote kwa ulioshindwa kuwavumilia bali hasara na maumivu??!! JE! UNAMPENDA….UNAWAPENDA HIVYO?

2) UPENDO HUFADHILI/LOVE IS KIND

-Upendo wa Mungu una tabia ya kufadhili wengine bila kujali kama unawajua ama la!

“What is the meaning of kind person?

These words and phrases refer to people who are generous, helpful, and who think of other people's feelings. One of the most common words for this is kind. Kind can be used of people or of their actions.”

-Upendo wa Mungu una tabia ya kujali sana hisia za wengine na huwatendea mema kwa ukarimu, hupenda kusaidia wengine naturally (kiasilia)

- Upendo wa Mungu hujali shida za wengine na kuzitatua bila hata kuombwa bali kwa sababu ile asili yake haiwezi kutosaidia wakati msaada huo unahitajika! JE! UNAMPENDA?......UNAWAPENDA HIVYO?

- Upendo una macho ya kuona uhitaji pale ulipo na unapohitajika

3) UPENDO HAUHUSUDU/LOVE DOES NOT ENVY

-Upendo wa Mungu hauhusudu mtu awaye yote! Kuhusudu ni kuonea wivu au kuonea kijicho! Ukiwa mbinafsi na mchoyo na mwenye tamaa au mwenye kijicho huwezi kupenda mafanikio ya wengine-maadui au marafiki; lakini upendo wa Mungu ukiwa nao moyoni mwako hauwezi kumuonea wivu mtu yeyote, hata akiwa mkeo au mumeo. Kwa sababu wewe unamtegemea Mungu aliyekupa huyo, unamuombea, na unajua kwamba Mungu anamlinda dhidi ya vishawishi vyote na uovu wa kila namna, na kwamba kila aendako yuko katika mikono salama. Kwa sababu pia unamwamini Mungu kwa ajili yake katika maeneo yote ya maisha yake! Wivu ni tabia ya dhambi na siyo utakatifu wa Kristo hata kidogo! Unaruhusiwa tu kuwa na wivu wa Bwana. JE! UNAMPENDA?.....UNAWAPENDA HIVYO?

4) UPENDO HAUTAKABARI/LOVE DOES NOT BOAST/IS NOT PROUD

-Upendo hautakabari kamwe! Kutakabari ni kujivuna na kuwa proud ni kujionea fahari na kujisifia MAFANIKIO YAKO, UWEZO WAKO, NGUVU ZAKO, NA MALI ZAKO (your achievements, abilities and possessions)

-Mtenda dhambi hupenda kujisifia na pia kujivuna mbele ya wanadamu wenzake ama kwa sauti ama kwa kimyakimya moyoni na mawazoni mwake! Hujipima na kujilinganisha na wengine na huwadharau na kuwashusha chini wale wote ambao;

>> anaona amewazidi uwezo au akili au kipawa

>> anaona hawana fedha, mali na utajiri alionao

>> anaona hawajafikia mafanikio aliyoyafikia maishani mwake

>> anaona hawawezi kufanya yale aliyoyafanya au anayoweza kuyafanya.

Yeye hujiweka kwenye daraja la juu kimaisha kutokana na mambo ya muda mfupi tu yanayoharibika na yasiyodumu ya hapa duniani; Yaani, hujiona bora zaidi kuliko wao kwa sababu hizi dhaifu. Hii ni  tofauti na Yesu aliyekuwa na ambaye bado a) anajua yote, b) anaweza yote, c) anamiliki yote, lakini wala HAJIVUNI NA HAMDHARAU MTU AWAYE YOTE. Na alipokuwa hapa kwenye mwili alijifanya mtumwa na kuwatumikia wanadamu ambao walikuwa ni adui zake;

“ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;” (Flp 2:6-7)

6Though he was God,a

he did not think of equality with God

as something to cling to.

7Instead, he gave up his divine privilegesb;

he took the humble position of a slavec

and was born as a human being.” (Phillipians 2:6-7)

-ALIKUWA NI MUNGU

-HAKUJIVUNIA KULE KUWA SAWA NA MUNGU KAMA KITU CHA KUJIVUNIA AMA KUKIONEA FAHARI

-BADALA YAKE ALIACHA HAKI NA STAHILI ZAKE ZOTE ZA KIMUNGU NA UTUKUFU

-KISHA AKATWAA NAFASI YA CHINI KWA UNYENYEKEVU YA KUWA MTUMWA,

-AKAISHI KAMA MWANADAMU WA KAWAIDA AKIWATUMIKIA SAWASAWA NA MAPENZI YA BABA YAKE

Mwenye dhambi unajivunia pesa, kazi, cheo, elimu, mali, utajiri, uwezo wako, nguvu zako n.k

Unajivunia

>>mambo uliyoyafanya

>>mambo unayoweza kuyafanya

>>vitu ulivyonavyo n.k

UPENDO WA MUNGU HAUTAKABARI!!!

5) UPENDO WA MUNGU HAUKOSI KUWA NA ADABU/LOVE IS NOT RUDE

-Upendo wa Mungu haukosi kuwa na adabu, yaani, hauna jeuri! Mwenye dhambi hana adabu na huwavunjia watu heshima! Ana tabia ya kujibu watu kwa mkato, wala hajali hisia za wale anaoongea nao, na hivyo anaropoka jibu lolote limjialo, na wala haonyeshi heshima wala adabu katika kuongea au kutenda kwake; jeuri ni roho ya shetani! Ni roho ya uasi na kutotii mamlaka wala kuheshimu wanaostahili heshima. Kinyume cha jeuri ni politeness; mwenye jeuri hajali na huwa anawapuuza wale anaowafanyia jeuri, na hata wakiumizwa hisia zao hiyo haimshughulishi yeye! JE! UNAMPENDA?......UNAWAPENDA HIVYO?

6) UPENDO HAUTAUFUTI MAMBO YAKE/LOVE IS NOT SELF-SEEKING

Hili tumeshaliangalia huko nyuma jinsi ambavyo upendo HAUTAFUTI MAMBO YAKE BINAFSI bali hutafuta faida ya wengine!

“Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. 4Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.” (Flp 2:3-4)

UPENDO HAUANGALII MAMBO YAKE MWENYEWE, BALI HUANGALIA MAMBO YA WENGINE; YAANI, MATAKWA, MASLAHI NA FAIDA YA WENGINE! UPENDO HAUISHII KWENYE NGAZI YA FAMILIA TU BALI HUVUKA HAPO NA KUWA MTUMWA NA MTUMISHI WA WENGINE KWA AJILI YA KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WETU. Kama unampenda utatafuta faida yake, utaangalia maslahi yake, utazingatia ustawi wake kimwili na kiroho, utajali matakwa yake n.k.  JE! UNAMPENDA?.........UNAWAPENDA HIVYO?

 

 

7) UPENDO HAUONI UCHUNGU/LOVE IS NOT EASILY ANGERED

-Uchungu moyoni ni kisasi kisicholipwa bado! Yaani, unakuwa umehifadhi hasira moyoni mwako, na hasira hiyo inahifadhiwa kama chuki!! Unayempenda haumkasirikii haraka! Na Neno la Mungu limeagiza,

“Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;” (Yak 1:19)

>> UNAYEMPENDA UNAMTHAMINI NA UNAMTANGULIZA, NA UNAMHESABU KUWA YEYE NI BORA KULIKO NAFSI YAKO; HIVYO UNAMSIKILIZA NA WALA HAUWI NA HARAKA YA KUTAKA KUSEMA WEWE KABLA YEYE HAJASEMA. Biblia inasema,

“Yeye ajibuye kabla hajasikia,

Ni upumbavu na aibu kwake.” (Mithali 18:14)

>>UPENDO UNA BUSARA HIVYO, HUKU CHUKI NI UPUMBAVU MOYONI KAMA ILIVYOANDIKWA KWAMBA HASIRA HUKAA KIFUANI MWA MPUMBAVU

MUNGU WA UPENDO ANASEMA UWE MWEPESI WA KUSIKIA, BALI SI MWEPESI WA KUSEMA; WALA KUKASIRIKA! Upendo si mwepesi wa hasira! Kama wewe ni mwepesi kukasirika ina maana moyoni mwako hauna upendo wa Mungu!

“Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako,

Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.” (Mhu 7:9)

UNAYEMKASIRIKIA HARAKA HARAKA HAUMPENDI KWA KUWA UPENDO SI MWEPESI WA HASIRA. JE! UNAMPENDA?.......UNAWAPENDA HIVYO?

8) UPENDO HAUHESABU MABAYA/LOVE KEEPS NO RECORD OF WRONGS

-Ili usiweke kumbukumbu ya mabaya ni lazima uwe na moyo wa kusamehe na kuachilia na kisha kusahau kama vile Mungu anavyotusamehe dhambi zetu tunapookoka, na kisha hakumbuki tena dhambi hizo (Ebrania 10:17).

-Kama unampenda au unawapenda utasamehe makosa yake/yao

-Kama unampenda au unawapenda utasamehe na kisha kuachilia makosa yake/yao

-Ukiachilia makosa hayo yatoke moyoni mwako ndipo itakuwa rahisi kusahau mabaya uliyotendewa

-Ndiposa utaweza kutokuwa na kumbukumbu yoyote ya mabaya uliyotendewa

-mtenda dhambi huweka kumbukumbu ya mabaya moyoni mwake na hivyo huwa na uchungu sikuzote maana hajasamehe/hawezi kusamehe/hataki kusamehe

-UKIWEMO UPENDO MOYONI MWAKO HAULIMBIKIZI MABAYA ULIYOTENDEWA MOYONI MWAKO, CHUKI HUWEKA KUMBUKUMBU YA MABAYA ULIYOTENDEWA SIKU NYINGI, MIEZI MINGI NA HATA MIAKA MINGI ILIYOPITA. JE UNAMPENDA?.....UNAWAPENDA HIVYO?

9) UPENDO HAUFURAHII UDHALIMU BALI HUFURAHI PAMOJA NA KWELI/LOVE DOES NOT DELIGHT IN EVIL BUT REJOICES WITH THE TRUTH

-Upendo haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli, upendo huchukia uovu bali huwapenda waovu! Upendo haufurahii uovu ama udhalimu! Kupenda siyo kuridhia uovu au kuruhusu uovu ushamiri, bali upendo hujitenga na uovu, hukataa uovu, huchukia uovu, hukemea uovu, huwa kinyume na uovu, hupinga uovu n.k

-Mtenda dhambi huachilia uovu, hushiriki uovu, hunyamazia uovu, huruhusu uovu, hachukui hatua dhidi ya uovu n.k

-Upendo haufurahii uovu/udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli na hivyo, kama andiko lisemavyo,

“Maana hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli” (2 Kor 13:8)

-Kutenda kinyume na kweli ni uovu; na kutenda sawasawa na kweli ni haki mbele za Mungu; Upendo wa Mungu ni kweli!

-Je! Unatenda sawasawa na Neno la Mungu katika kila jambo? Yaani, je! Huwa unajiuliza, ‘Neno la Mungu linasemaje kabla hujatenda lolote au kabla hujafanya maamuzi yoyote?

-Je! Unazingatia Neno la Mungu katika mahusiano yako yote? Yaani, kabla hujamtendea mtu jambo au kumsemesha, unazingatia kwamba umtendee sawasawa na Neno lisemavyo? Vinginevyo utakuwa unatenda udhalimu kila siku maana unatenda kinyume na kweli! Neno la Mungu ndiyo kweli (Yoh 17:17) JE! UNAMPENDA................UNAWAPENDA HIVYO?

10) UPENDO HUVUMILIA YOTE; HUAMINI YOTE; HUTUMAINI YOTE; HUSTAHIMILI YOTE

-Upendo ni tiba ya uhakika kwenye mahusiano yote yanayolegalega au yanayotaka kuvunjika, na hata yaliyokwisha kuvunjika tayari; maana WENYEWE HUVUMILIA YOTE; mtenda dhambi huwa anachagua mambo ya kuvumilia na mengine anasema hili siwezi hata kidogo kulivumilia; lakini Mungu anasema upendo HUVUMILIA YOTE! Kama unampenda au unawapenda inakupasa KUVUMILIA YOTE!!!

-Neema ya Mungu ya kuvumilia ipo! Mungu ametoa mwaliko wa wewe kukikaribia kiti cha neema kwa ujasiri wote ili upewe rehema na kupata neema ya kukusaidia wakati wa uhitaji (Ebrania 4:16)

-Hii ndiyo maana ikaandikwa si kwa uwezo wala nguvu bali ni kwa Roho Mtakatifu (Zech 4:6), na tena, Mungu ndiye atendaye kazi ndani yetu kutaka kwetu na kutenda kwetu kwa kulitimiza kusudi lake jema (Flp 2:13); na ndiyo maana ikaandikwa, Yote yawezekana kwake yeye aaminiye (Mk 9:23). Na pia, nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu (Flp 4:13)! Hivyo kama unamwamini na kumpenda Yesu UNAWEZA  KUVUMILIA YOTE, KUAMINI YOTE, KUTUMAINI YOTE NA KUSTAHIMILI YOTE!!! Hii inamaanisha,

-kamwe haukati tamaa wala kuvunjika moyo na kurudi nyuma, bali UNAVUMILIA YOTE

-kamwe hauachi KUAMINI kwa ajili ya umpendaye ama uwapendao popote walipo nyumbani, kazini, shuleni, chuoni, hekaluni n.k bali UNAAMINI YOTE.

-kamwe haupotezi MATUMAINI juu ya yeye umpendaye au hao uwapendao bali UNATUMAINI YOTE.

-kamwe haurudi nyuma wala hauchoki bali UNASTAHIMILI YOTE, SIKUZOTE, MAHALI POTE!

KWA MST HUU PEKE YAKE HAKUNA KINACHOSHINDIKANA NA HAKUNA UHUSIANO MGUMU KUIMARIKA UNAPOLEGALEGA AU KUKARIBIA KUVUNJIKA! WALA HAKUNA UHUSIANO ULIOVUNJIKA UNAOSHINDIKANA KUTENGENEZWA Unahitaji tu kujaa upendo wa Mungu moyoni mwako! JE! UNAMPENDA?........UNAWAPENDA HIVYO?

 

11) UPENDO HAUPUNGUI NENO WAKATI WOWOTE/LOVE NEVER FAILS

-Upendo wa Mungu KAMWE HAUSHINDWI, HAUJAWAHI KUSHINDWA NA HAUTASHINDWA MILELE YOTE!

-UKIWA NA UPENDO WA MUNGU MOYONI MWAKO WEWE NI MSHINDI SIKUZOTE KAMWE TULIVYOONA HAPO JUU!!

-UPENDO WA MUNGU NI MWAROBAINI WA TALAKA! PENYE UPENDO WA MUNGU HAMNA TALAKA NA MAHUSIANO YOTE;

>>HUPENDWA

>>HUTHAMINIWA

>>HUHESHIMIWA

>>HULINDWA

>>HUIMARISHWA NA PIA

>>HUJENGWA

PENDO LA MUNGU LINAANZIA KWENYE MATENDO YA MITUME 2:38-39

“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie” (Mdo 2:38-39)

KWA KUPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU UNAKUWA UMETIMIZA WARUMI 5:5

“5na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi” (Rum 5:5)

PENDO LA MUNGU LIMEKWISHAKUMIMINWA MIOYONI MWETU NA ROHO MTAKATIFU TULIYEPEWA SISI!!! ROHO MTAKATIFU NDIYE ATAKUWEZESHA KUPENDA KWA UPENDO WA MUNGU KUPITIA IMANI YAKO ILIYO HAI  KWA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU.

 KUMBUKA:

IMANI YA YESU SIKUZOTE INATENDA KAZI KWA UPENDO (WAGALATIA 5:6); HII MAANA YAKE NGUVU YA IMANI NI UPENDO; NA PASIPO KUWA NA PENDO LA MUNGU MOYONI MWAKO HUWEZI KUMWAMINI MUNGU; YESU NDIYE PENDO LA MUNGU BABA YETU NDANI YA MIOYO YETU!

 

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post