YE HAVE NOT BECAUSE YE ASK NOT (HAMNA KITU KWA KUWA HAMWOMBI)


YE HAVE NOT BECAUSE YE ASK NOT! (HAMNA KITU KWA KUWA HAMWOMBI)


James 4:2 (KJV)" Ye lust, and have not: ye kill, and desire to have, and cannot obtain: ye fight and war, yet ye have not, because ye ask not."[2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!]
Yakobo 4:2
>> Kwa mujibu wa andiko hili  CHOCHOTE AMBACHO HUNA NI KWA SABABU HUOMBI!!! Kuna mahitaji ya kiroho (spiritual), kiakili (mental), kihisia (emotional), kimwili (physical), kifedha (financial), kimali na vitu ( material), na kijamii (social). CHOCHOTE AU LOLOTE AMBALO HUNA KATI YA HAYA NI KWA KUWA HUOMBI!!

NI NANI AWEZAYE AU ASTAHILIYE KUMWOMBA MUNGU?

John 9:31 "Now we know that God heareth not sinners: but if any man be a worshipper of God, and doeth his will, him he heareth." [ 31 Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. ]
Yohana 9:31
>> MTENDA DHAMBI HAWEZI KUMWOMBA MUNGU MAOMBI YAKE NA SALA ZAKE ZOTE HAZIMFIKII MUNGU MASIKIONI MWAKE KWA KUWA HATAKI KUZISIKIA!!! DHAMBI ZAKO MTENDA DHAMBI ZIMEKUFARAKANISHA NA MUNGU NA HATAKI KUKUSIKILIZA!

1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
Isaya 59:1

2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
Isaya 59:2
>> MTENDA DHAMBI UNAPOSALI NA KUOMBA NA HATA KUFUNGA UNAJIDANGANYA MAANA MUNGU HAKUSIKII NA WALA HAJISHUGHULISHI NA HAYO UNAYOMWOMBA! HIVYO SHETANI ANA UHURU, HAKI, MAMLAKA, NA UHALALI WA KUKUTESA NA KUKULETEA MABAYA YOTE VILE APENDAVYO!!
>> Lakini mtu akiwa ni mcha Mungu na mwenye kuyafanya mapenzi yake, MUNGU HUMSIKIA HUYO!! Biblia inaeleza kumcha Mungu ni kupi!
13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Mithali 8:13
>> Tazama wewe unavyopenda uovu na kuutenda!! Unajivuna, unasengenya, unajiinua, unajikweza, unajiona bora kuliko wengine, ni mbishi, mgomvi, u mwenye uchungu, hautaki kusamehe, haupendi suluhu, umejaa lawama, ni mkosoaji sikuzote, ni mwenye kunyooshea vidole wengine sikuzote, huna adabu wala heshima kwa watumishi wa Mungu na watoto wengine wa Mungu, umejaa mashindano, unapenda kusambaza na kueneza habari mbaya za wengine, ni mchoyo, mbahili, mwenye tamaa ya pesa na mali, unapenda umaarufu na sifa kuliko Yesu, huna toba na hivyo hutubii maovu yako huku ukijihesabia haki, sikuzote unataka kutoa vibanzi vya wengine na boriti yako hutaki kuitoa, unawatendea wengine vile ambavyo wewe hupendi kutendewa, umejaa ubinafsi na umimi, hauheshimu ndoa yako, unatoka nje ya ndoa yako, haumheshimu wala kumtii mumeo, haumpendi wala kumtunza mkeo, mwenendo wako kwenye ndoa ni aibu kusema nje, umemtenda kwa hiyana mke wa ujana wako kwa kumpa talaka au kumwacha tu na huyo uliye naye sasa si mkeo, na huyo uliye naye sasa si mumeo, n.k. UKIWA NI MTENDA DHAMBI SI SALA NA MAOMBI YAKO TU MUNGU HAYASIKILIZI, BALI HATA SADAKA ZAKO NI CHUKIZO KWAKE!!

22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
1 Samweli 15:22

23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
1 Samweli 15:23

HAPA TENA;

13 Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.
Isaya 1:13
>> MATOLEO YAKO MTENDA DHAMBI NI BATILI
>> KUSHEHEREKEA KWAKO MWEZI MPYA NA SABATO ZAKO UNAZOZISHIKA NI MACHUKIZO KWA MUNGU
>> MAKUTANO YENU NA IBADA ZENU WATENDA DHAMBI MUNGU AMEZIKATAA!!
>> UVUMBA MNAOFUKIZA KWENYE MADHABAHU ZENU NI MACHUKIZO KWA MUNGU!!

27 Sadaka ya wasio haki ni chukizo; Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!
Mithali 21:27
ASIYE HAKI NI WEWE USIYEMWAMINI YESU NA HIVYO HUJAOKOKA!!

8 Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.
Mithali 15:8
>> MTU MBAYA NI WEWE MTENDA DHAMBI MWENYE roho YA SHETANI NDANI YAKO
>> MTU MNYOOFU NI YULE MWENYE HAKI ALIYEMWAMINI YESU MA ANAYEISHI KWA IMANI TAKATIFU YA YESU!!!
>> MTAKATIFU NI YULE ALIYEOKOKA BAADA YA KUMWAMINI YESU NA KUOSHWA DHAMBI ZAKE KWA DAMU YAKE HUYU YESU; NA SASA ANAISHI KWA IMANI YA YESU AKIONGOZWA NA ROHO WA YESU ALIYE MTAKATIFU AMBAYE ANAMWEZESHA KUISHI MAISHA MATAKATIFU KWA NGUVU ZA ROHO HUYU MTAKATIFU WA KRISTO!! HUYU AKIOMBA ANASIKIWA!! SALA ZAKE NA SADAKA ZAKE ZOTE NI MANUKATO NZURI MBELE YA KITI CHA ENZI MBINGUNI!!

8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
Ufunuo wa Yohana 5:8

>> NIMALIZIE HAPA KWAMBA " MUNGU HUWA ANASIKIA MAOMBI YA WATAKATIFU TU PEKE YAO"!!
>> KAMA WEWE SIYO MTAKATIFU BASI NI MTENDA DHAMBI
>> NA KAMA WEWE NI MTENDA BASI U MALI YA SHETANI

8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
1 Yohana 3:8
>> KAMA HUTATUBU UTAISHIA HAPA ATAKAPOISHIA SHETANI ALIYEKUDANGANYA UKANG'ANG'ANIA DHEHEBU AU DINI YA MAPOKEO KUTOKA KWA WAZAZI NA KUKATAA KUZALIWA MARA YA PILI (YOHANA 3:3-7 & TITO 3:3-7)

10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Ufunuo wa Yohana 20:10

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
Ufunuo wa Yohana 20:12

15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Ufunuo wa Yohana 20:15
>> UKIOKOKA JINA LAKO LINAANDIKWA KWENYE KITABU CHA UZIMA CHA MWANA-KONDOO

MAOMBI YA WATAKATIFU

James 5:16 (NLT)  Confess your sins to each other and pray for each other so that you may be healed. The earnest prayer of a righteous person has great power and produces wonderful results.
>> Sehemu ya pili ya andiko hili inasema; "..........KUOMBA KWA DHATI YA MOYO NA KWA BIDII KWA MWENYE HAKI (AAMINIYE) KUNASABABISHA IACHILIWE NGUVU KUBWA NA HIVYO KULETA MATOKEO YA KUSHANGAZA." (Yakobo 5:16 b)
>> Hii inapatana na maandiko; "20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;"
Waefeso 3:20
>> NGUVU KUBWA MNO YA AJABU ITENDAYO MAAJABU, ISHARA, NA MIUJIZA HUZALISHWA KUTOKANA NA MAOMBI YA DHATI NA YA BIDII YA MTAKATIFU!! HII NI NGUVU YA MUNGU KWA ROHO MTAKATIFU AKAAYE NDANI YA MTAKATIFU! NI NGUVU YENYE KUYATENDA MAPENZI YOTE YA MUNGU YALIYOMO KWENYE NENO LAKE UNALOLIAMINI!! NA KUOMBA HUKU KWA IMANI KATIKA NENO KWA ROHO MTAKATIFU KUNAPELEKEA KUPOKEA HAJA ZOTE UZIOMBAZO MUDA ULE ULE UKIWA KWENYE KUSALI NA KUOMBA!! Biblia inasema,
"1 Yohana 5:14-15
[14]Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
And this is the confidence that we have in him, that, if we ask any thing according to his will, he heareth us:
[15]Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.
And if we know that he hear us, whatsoever we ask, we know that we have the petitions that we desired of him."
1. MTAKATIFU ANA UJASIRI ANAPOMWENDEA BABA YAKE KWA DAMU YA YESU
2. NAYE ANAPOMWOMBA BABA YAKE KWA JINA LA YESU HUFANYA HIVYO SAWASAWA NA NENO LAKE AMBALO LIMEBEBA MAPENZI YAKE! NENO LA MUNGU NDILO MAPENZI YAKE. HIVYO MTAKATIFU HUOMBA SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU KWENYE NENO LAKE!!
3. NA KWA KUWA SALA NA MAOMBI YAKE YANAMPENDEZA MUNGU BASI MUNGU NAYE SIKUZOTE HUWA ANAMSIKIA NA KUMSIKILIZA MTAKATIFU WAKE
4. MUNGU HASIKILIZI UPUUZI BALI HUSIKILIZA NENO LAKE LIKINENWA KWAKE YEYE NA MTAKATIFU KWENYE SALA NA MAOMBI! NA KWA KUWA NI MAPENZI YAKE HAYO YANAYOOMBWA BASI PALE PALE NA WAKATI ULE ULE MTAKATIFU ANAPOSALI NA KUOMBA MBELE ZAKE, MUNGU HUMPATIA HAJA ZAKE ZOTE HIZO
5. HIVYO MTAKATIFU AKIWA AMEMALIZA NA ANAPOTOKA KWENYE KUSALI NA KUOMBA KWAKE, HUTOKA AKIWA TAYARI ANAZO HAJA ZILE ZOTE ALIZOMWOMBA BWANA MUNGU MWENYEZI
>> JE! MUNGU ATAMJIBU BAADAE! HAPANA! MUNGU AMEKWISHAKUMJIBU TAYARI!!
>> SI HIVYO TU BALI MUNGU AMEKWISHA KUMPATIA HAJA ZOTE ZA MOYO WAKE ALIZOMWOMBA KWA JINA LAKE YESU!!
>> MTAKATIFU HUENDA KWENYE SALA NA MAOMBI KUPOKEA HAJA ZOTE ZA MOYO WAKE MAANA ANAKWENDA KWA BABA YAKE NA ANAKWENDA KUMFURAHISHA BABA YAKE KWA KUMKUMBUSHA NENO LAKE MWENYEWE NA KUMSIHI AYAFANYE YALE YOTE ALIYOYASEMA NA KUYAAHIDI KWENYE NENO LAKE MWENYEWE!! NDIPO MUNGU BABA YETU TULIOOKOKA, MWENYE KUSHIKA MAAGANO NA REHEMA, HUMPATIA PALE PALE HAJA NA MAHITAJI YAKE YOTE!!
>> HII INAONDOA KABISA KUHITAJI KOTE, KUPUNGUKIWA KOTE, KUISHIWA KOTE, KUKOSA KOTE, KUSHINDWA KOTE, MILIMA YOTE, UGUMU WOTE, KUSHINDIKANA KOTE, FADHAA ZOTE, HOFU ZOTE, WASIWASI WOTE, MASUMBUFU YOTE, WOGA WOTE, MATESO YOTE, MAUMIVU YOTE, MAGONJWA YOTE, UDHAIFU WOTE, MARADHI YOTE, DHAMBI ZOTE, UASI WOTE, TABU ZOTE, KUCHANGANYIKIWA KOTE, UHABA WOTE, MATATIZO YOTE, SHIDA ZOTE, UPOTOVU NA UKENGEUFU WOTE, KURUDI NYUMA KOTE, N.K.
>> HAYA YOTE ANAYALETA SHETANI KWA SABABU YA DHAMBI ZA MWANADAMU, MENGINE NI KUKOSA MAARIFA KWA MWANADAMU, NA PIA MAKOSA YA MWANADAMU MWENYEWE!!
>> HATA UNAPOKUWA UMEOMBA SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU NA KUPOKEA HAJA ZOTE ULIZOZIOMBA, BADO SHETANI HAAMINI WEWE UNAAMINI KWAMBA UNAZO HAJA ZOTE ULIZOMWOMBA MUNGU. HIVYO ATAINUA KILA AINA YA UPINZANI KATIKA roho NA KATIKA MWILI ILI UKITAZAMA KWA MACHO AU UKIANGALIA HALI ZINAZOKUKABILI UUAMINI UONGO HUO UNAOONEKANA NA UNAOPITA ILI UPOTEZE BARAKA ZAKO AU HAKI ZAKO KWA KUTOAMINI KWAKO!! MANENO YA KINYWA CHAKO NDIYO MARA NYINGI YANAONYESHA KWAMBA HAUJAAMINI!!! Utasikia; mambo magumu, hii haiwezekani, mtoto ameshindikana huyu, naumwa/anaumwa, kanisa linakwenda kuwa dini, kanisa limepotoka, hauwezi kufanikiwa, mke/ mume amenishinda, muovu, hafai, mkorofi, hanipendi, hajali, n.k Unaongea haya huku imeandikwa kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake (Mathayo 12:34) na tena kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa mtu hukiri hata kupata wokovu (Warumi 10:10)!! Hayo hapo juu yanatoka moyoni mwako na hivyo inamaanisha umeyaamini na ndiyo maana unayanena!! Sasa umeamini maaandiko yapi hata ukanena hayo uyanenayo??!! Ni dhahiri sauti ya shetani imo moyoni mwako na unaongea yale uyaonayo kwa macho na yale uyasikiayo kwa masikio yako!! Hii maana yake hauamini na wala hauishi kwa imani!! Hata kama uko kanisani miaka mingi wewe hauamini na unatenda dhambi! Hata kama unajiita mtumishi hauamini na unatenda dhambi!! HAUISHI KWA IMANI!!! Imeandikwa;
2 Wakorintho 5:7
"[7](Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)
(For we walk by faith, not by sight:)"
>> HUWEZI KAMWE KUUSHINDA ULIMWENGU HUU PASIPO KUAMINI!!

1 Yohana 5:4
[4]Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
For whatsoever is born of God overcometh the world: and this is the victory that overcometh the world, even our faith.
>> Huwezi kushinda kwa kulaumu, kunung’unika, kulalamika, kukosoa, kuhukumu kwa hukumu ya macho, kulalamika na kunyoosha vidole!! HUKO NI KUONGOZWA NA MACHO!! Moyo wako umejaa unayoyaona na unayoyasikia badala ya kujaa neno!!! (Wakolosai 3 :16) Daudi alisema, "11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi."
Zaburi 119:11
>> Wewe umejaza watu moyoni, habari mbaya, tik tok videos, pornograph, mizaha, na mambo ya dunia hii yasiyo na maana!! UTAOMBAJE UKASIKIWA HUKU MOYO WAKO SI SAFI NA UMEJAA DUNIA NA MAMBO YALIYOMO? HII NDIYO MAANA WATU WANAFUNGA NA KUOMBA LAKINI BADO WANATENDA DHAMBI, BADO DHAMBI ZINASHAMIRI, UOVU UNAZIDI N.K. SALA NA MAOMBI YAO MUNGU HAKUWASIKIA!!!

>> YE HAVE NOT BECAUSE YE ASK NOT!!
>> HAMNA KITU KWA KUWA HAMWOMBI!!
>> MKIOMBA HAMPATI KITU KWA KUWA MNAOMBA VIBAYA MVITUMIE KWA ANASA ZENU!! (YOU ASK SELFISHLY AND FOR SELFISH PURPOSES)
>> WATAKATIFU HUOMBA SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU YALIYOMO KWENYE NENO LAKE!!!
>> HUWEZI KUVIPIGA VITA VIZURI VYA IMANI KAMA HAUKUPOKEA HAJA ULIZOOMBA PALE ULIPOSALI NA KUOMBA KWANZA!

Marko 11:24
[24]Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Therefore I say unto you, What things soever ye desire, when ye pray, believe that ye receive them, and ye shall have them.
>> LAZIMA UPOKEE NA KISHA UKASHINDANE MIELEKA NA FALME, MAMLAKA, WAKUU WA GIZA HILI, NA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO!! (Waefeso 6:11-12)
Waefeso 6:12
[12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
For we wrestle not against flesh and blood, but against principalities, against powers, against the rulers of the darkness of this world, against spiritual wickedness in high places.

>> UKISHINDA VITA VYA IMANI AMBAVYO NI VITA VYA KIROHO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDIPO ZILE HAJA ULIZOZIPOKEA ULIPOSALI NA KUOMBA, UKAZING'ANG'ANIA SHETANI ALIPOJARIBU KUKUNYANG'ANYA KUPITIA SHIDA, DHIKI, ADHA, MATESO, KUPUNGUKIWA, KUISHIWA, KUHITAJI, DALILI ZA MAGONJWA, MAUMIVU, N.K. ALIYOKULETEA, NA UKAMSHINDA KWA NENO (IMEANDIKWA...!); NDIPO ZITADHIHIRIKA ZOTE KWENYE ULIMWENGU WA MWILI!! UBARIKIWE NA BWANA
>> SOMO LITAKALOFUATA: JINSI YA KUVIPIGA VITA VYA IMANI/ VYA KIROHO!!





Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post