BAADHI YA SABABU ZA KUVUNJIKA NDOA NA MIGOGORO ISIYOISHA
UTANGULIZI
Neno la Mungu ndilo Kweli ( Yohana 17:17) na choichote kilicho kinyume au tofauti na Kweli ni uongo na udanganyifu wa shetani ambaye ni mwongo na pia ni baba wa uongo. (Yohana 8:44) Ndoa takatifu; msingi wake, ujenzi wake, uimara wake, kudumu kwake, kufanikiwa kwake, kuimarika kwake, usalama wake, kutimiza kwake makusudi, mapenzi ya, na mpango wa Mungu NI PALE WANANDOA WANAPOENENDA KATIKA KWELI YOTE! YAANI, WANAPOITII KWELI KWA KULITENDA NENO LA MUNGU KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU ALIYEMO NDANI YA MUME NA NDANI YA MKE! Kinyume na hapoi ndoa hii itakuwa chombo cha kuyafanya mapenzi ya shetani ulimwenguni! Itakuwa kama ndoa ya Adamu na Hawa baada ya kuasi na kufukuzwa kutoka katika uwepo wa Mungu bustanini Edeni! Matatizo yote ya ndoa ni matokeo ya kuliasi neno la Mungu na kutoliheshimu, kutolijali, kutolizingatia, kutoliishi, kutolifanya kuwa ndiyo mamlaka ya juu zaidi kuliko zote nay a mwisho; yaani, kutojitia chini ya uongozi na mamlaka ya Neno la Mungu ndani yake Kristo Yesu. Tutaangalia baadhi ya maandiko ambayo yametoa magizo na maelekezo kwaz wanandoa ili kuwafanya waishi na kuenenda sawasawa na neno la Mungu huku wakiyafanya mapenzi yake ulimwenguni! Ndoa imara hufanya familia imara! Familia imara hufanya kanisa imara na taifa imara ndani yake Kristo Bwana na Mwokozi wetu. Kama kuna suluhisho moja na utatuzi pekee wa matatizo yote ya ndoa basi ni UTII WA KWELI!!
1:0 KUTOISHI KWA IMANI
Biblia inasema, “Mwenye haki wangu ataishi kwa imani” (Habakuki 2:4 & Warumi 1:17). Katika Agano jipya ili uwe mwenye haki ni lazima UMWAMINI YESU NA KUTUBU DHAMBI ZAKO, NA KUMPOKEA MOYONI MWAKO KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO BINAFSI. Hii inasababisha akusafishe na kukuosha dhambi zako zote na kukupa uzima wa milele au maisha ya milele yasiyoharibika! Maisha hayo ni UTAKATIFU NA UPENDO WA MUNGU NDANI YAKO! Maisha ya namna hii yanatokana na utii wa kweli yote kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu ambaye ni Roho wa Kweli (Yohana 16:13 & Warumi 8:14) Biblia inasema, “Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, BALI IMANI ITENDAYO KAZI KWA UPENDO.” (Wagalatia 5:6)
Unaweza kutafsiri Utakatifu kama “IMANI YA YESU KRISTO ITENDAYO KAZI KWA UPENDO WA AGAPE” Nguvu ya imani hii ni AGAPE LOVE!! Na imani hii siyo imani iliyolala (dormant faith), bali ni IMANI ITENDAYO KAZI!! Ni maisha ya kulitenda na kuliishi neno kwa nguvu za Roho Mtakatifu!! Yesu alisema, “…….Mtu hataishi kwa mkate tu, ILA KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU.”(Mathayo 4:4) UTAKATIFU NI KUISHI KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU!!! (YAANI, KWELI YOTE!!) Watenda dhambi na wasioamini huchagua nini cha kutii na kukataa ‘yale mengine’ wasiyoyapenda na wasiyoyataka! Huu siyo utakatifu bali ni uovu ambao unamkaribisha shetani kwenye ndoa! Imeandikwa, “Wala msimpe Ibilisi nafasi.” (Waefeso 4:27) KUTOITII KWELI YOYOTE KWA WANANDOA NI KUMPA IBILISI NAFASI KWENYE MAISHA YENU!!! Ibilisi anakuja KUUA, KUIBA, NA KUHARIBU (Yohana 10:10) KILA CHEMA NA KIZURI KILICHO CHA MUNGU maishani mwenu. Msipotubu ataingia zaidi na kuharibu mahusiano yenu, kazi za mikono yenu, afya zenu, tabia za watoto wenu, vipato vyenu, kufikiri kwenu, maamuzi yenu, mipango yenu, kesho yenu, tabia zenu, NA HATIMA YENU YA MILELE!! Unaishi kwa imani wewe mume na wewe mke?
1:1 KUTOSIMAMA KWENYE ZAMU NA NAFASI ALIZO WAWEKA MUNGU
Biblia inasema, “Bwana Mungu akasema, Si vema mtu huyo awe peke yake, NITAMFANYIA MSAIDIZI WA KUFANANA NAYE.” (Mwanzo 2:18)
Mume ni kiongozi wa familia na Biblia inamita kuwa ni kichwa! “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.” (1Kor 11:3) Yaani,
MUNGU NI KICHWA CHA
KRISTO. AMBAYE NI KICHWA CHA
MWANAMUME, AMBAYE NI KICHWA CHA
MWANAMKE
Huu ni utaratibu wa kiuumbaji!! Huu ndio mpangilio wa mamlaka Kuanzia kwa Mungu, Mwanawe pekee Kristo, Mwanamume, na kisha Mwanamke (Ndoa Takatifu). Yaani, MUNGU>> KRISTO >> MWANAMUME >> MWANAMKE! Hii ni mamlaka aliyopewa mwanamume ulimwenguni kwa Utaratibu wa Uumbaji wa Mungu Mwenyewe (God’s Own Order of Creation)
Matatizo mengi kwenye ndoa yanazaliwa pale mtu awaye yote anapojaribu kugeuza utaratibu wa kiuumbaji aliouweka Mungu mwenyewe kwa kupindua mamlaka ya mwanamume na kumpa mwanamke, au mwanamke mwenyewe kujitwalia mamlaka hii kama alivyofanya Hawa bustanini edeni kwa kukubali kushawishika na nyoka, na kisha kutwaa matunda aliyokatazwa kuyala akayala, na kisha kumletea mumewe naye ale! (Mwanzo 3:1-6) Alifanya maamuzi makubwa ya ndoa yeye mwenyewe peke yake pasipo kibali cha mumewe! Hii inamaanisha alitwaa mamlaka ya ndoa akafanya maamuzi kwa niaba ya mumewe pasipo hata kumshirikisha wala kupata ridhaa yake! DHAMBI IKAINGIA ULIMWENGUNI MPAKA LEO! Bado “nyoka” anafanya yale yale leo kwenye ndoa, kanisani, na kwenye jamii zote! Mungu hayumo kwenye maamuzi hayo yanayofanyika kinyume na kweli na hivyo shetani hupata nafasi ya kuingia na kuiba, kuua, na kuharibu kila chema cha Mungu na kuleta mitafaruku mingi ambayo hupelekea hata kuvunjika kwa ndoa nyingi! Mwanamume asiyejua nafasi yake au asiyewajibika kwenye nafasi yake kama Adamu alivyofanya naye ndiye ANAYERUHUSU UOVU UINGIE KWA KUUFUNGULIA MLANGO pale anaporidhia uasi wa mwanamke kwenye ndoa, kanisani, na kwenye jamii. Wewe mwanamume siyo Yesu na wala huwezi kuchukua nafasi ya Yesu kwenye ndoa au kanisani! Wewe mwanamke siyo mwanamume na kamwe huwezi kuchukua nafasi ya mwanamume kwenye ndoa, kanisani au kwenye jamii. Kujaribu kufanya hayo ni uasi, ni uovu , na ni kuzalisha matatizo ambayo shetani anafurahia kuyaleta maana amefunguliwa mlango na kupewa nafasi. Ndoa ya mwanamume asiyesimama kwenye zamu yak e na kutotimiza wajibu wake wa kimaandiko hazidumu na/au zimejaa matatizo mengi kwa kuwa Mungu hayupo katikati yake! Kukataa neno ni kumkataa Mungu, maana Neno ni Mungu (Yohana 1:1) Maisha ya mtakatifu ni maisha ya neno ambayo ndiyo maisha ya Yesu!!
1:2 KUTARAJIA KUPOKEA ZAIDI KULIKO KUTOA
Imeandikwa, “…….ni heri kutoa kuliko kupokea” (Matendo ya Mitume 20:35b) Biblia kwenye kitabu cha Waefeso imetoa wajibu kwa mume wa kumpenda mkewe kama Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake (Waefeso 5:25); Na wajibu wa mke naye ni kumtii mumewe katika mambo yote kama vile kanisa linavyomtii Kristo (Waefeso 5:22); Jambo muhimu hapa la kuelewa ni kwamba upendo wa Mume unaoongelewa hapa ni ule upendo wa Mungu uliomiminwa mioyoni mwetu na Roho Mtakatifu tulipomwamini Yesu. (Warumi 5:5 & Matendo ya Mitume 2:38); na kwamba huyu ni Roho wa Upendo mwenye kutupa roho ya upendo yenye nguvu za pendo lake ili tuishi na kuenenda katika pendo hilo; na kwamba utiihuu wa mke ni ule utii wa kukubali na kujinyenyekeza chini ya mamlaka ya mume kumtii kama kumtii Bwana Yesu; hii ni roho ya utii kutoka kwa Bwana Yesu mwenyewe aliyemtii Baba yake kwa kila jambo! Hivyo mume anawezeshwa na Roho Mtakatifu na mke naye halikadhalika huwezeshwa na Roho Mtakatifu. Kanuni inayotumika ni ile ya kimaandiko: WEWE TIMIZA WAJIBU WAKO KWANZA PASIPO KUNGOJEA MWENZAKO NAYE AFANYE KWANZA!!! Biblia inasema, “Basi yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo, maana hiyo torati na manabii.” (Mathayo 7:12)
1. Mume unatakiwa kuanza kumpenda mkeo katika kuitii kweli; mpende hata kama yeye bado hakutii! Mpende hata kama bado yeye hakuheshimu! Upendo wa Kristo haungojei mkeo awe mwenye tabia ya rohoni, mcha Mungu, mtiifu sana n.k. Unatakiwa umpende hivyo hivyo alivyo sasa kama Kristo alivyokupenda wewe ukiwa muasi, mtenda dhambi, usiyemtaka Mungu kabisa! Mkeo ameokoka, anaendelea kutakaswa, na Mungu ameaanza kazi njema moyoni mwake (Wafilipi 1:6) ambayo ataikamilisha kwa wakati wake hata ajapo Kristo! Utii wako wa Kweli una nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko kwa mwenzi wako anayeonekana leo kuwa dhaifu kiroho, asiyetii, mwenye mapungufu mengi, ikiwemo tabia ile ya kunung’unika, kulalamika, na kujibu hovyomaneno ya kuumiza!! Kwa kila eneo analoonekana kuwa dhaifu wewe mume umefanya kazi ya imani kiasi gani ukishirikiana na Roho wa Yesu kumuombea, kuamini maandiko kwa ajili yake, kumvumilia, kuchukuliana naye, kuachilia, na kumsamehe maana hajui alitendalo??!! Lazima ufanye vita katika ulimwengu wa roho ambavyo vinaitwa vita vizuri vya imani kwa ajili ya mkeo! Mume wa rohoni hufanya haya na ndoa yake husimama licha ya mashambulizi yote ya adui na tufani za maisha kwa kuwa MUME NI MWENYE HEKIMA NA AKILI AMEJENGA NDOA YAKE JUU YA MWAMBA. (Mathayo 7:24-25) Vinginevyo migogoro haitaisha na mwishowe talaka kumwacha Yesu (Neno) kwa kutoa talaka. UPENDO WA KRISTO WA MUME NI SULUHISHO LA KILA SHIDA NA UTATUZI WA KILA MGOGORO KWENYE NDOA! ASIPOKUWA NAO SHETANI HUTAWALA!! Kumpenda kwako mkeo huwa kunapelekea UTII WAKE KWAKO! Upendo wa Mungu ndani ya mume hupelekea utii wa mke kuongezeka kadiri unavyokaza kumpenda! UPENDO HUZAA UTI! UPENDO HAUANGALII ANAYOYAFANYA, AU ALIYOYAFANYA BALI UNAANGALIA NENO LA KRISTO LINAOONGOZA MAISHA YENU KWENYE NDOA! ANZA MUME KUMPENDA MKEO, ENDELEA KUMPENDA PASIPO KUACHA MPAKA UMUATHIRI YEYE KWA KUSABABISHA ANYENYEKEE CHINI YA MAMLAKA YAKO NA KUKUTII KWA KILA JAMBO MAANA AMEONA NA KUTHIBITISHA KWAMBA UPENDO WAKE KWAKE NI WA KWELI NA WA DHATI!! PANDA UPENDO UVUNE UTII WAA MKEO!
2. Mke unatakiwa kumtii mumeo sikuzote katika mambo yote pasipo kuacha licha ya mapungufu yote unayoyaona kwake au matarajio yako kwake asiyoyafikia au kuyatimiza! Utii wa kibiblia ni KUJINYENYEKEZA CHINI YA MAMLAKA YAKE NA KUMTII PASIPO KUTAZAMA TABIA NA MWENENDO WAKE AU MAPUNGUFU YAKE YOTE! Maana kama una Yesu moyoni mwako maana yake unaishi kwa imani! Na kama unaishi kwa imani wewe hauyaangalii yanayoonekana bali yasiyoonekana ( 2 Kor 4:18) kwa maana unajua kwamba hayo yote unayoyaona ni ya muda tu, bali yale yasiyoonekana uliyoyaamini kwa ajili ya mumeo kutoka kwenye neno (kwa Yesu) ndiyo ya milele! Mumeo ni mume wa kimaandiko! Huyu wa mwilini wa sasa anapita lakini yule uliyemwamini Yesu kwa ajili yake sawasawa na maandiko matakatifu ndiye anafunuliwa kwa ko hatua kwa hatua kadiri unavyovumilia, unavyotarajia, usivyokata tama, unavyokiri, unavyotabiri, unavyoomba katika sala zako, unavyotumia mamlaka uliyonayo kuvunja, kukemea, kuharibu, kubomoa, kung’oa, kubatilisha, kutengua, kuamuru, kujenga, kupanda, kutamka (declare), n.k. HUKU UKIENDELEA KUMTII NA KUEPUKA JEURI, MAJIBU YA KUUMIZA, KUMLAUMU, KUMDHARAU, KUMSEMA KWA MARAFIKI NA NDUGU ZAKO, KUMSEMA KWA WATOTO, KUMPINGA, KUMLAZIMISHA, KUJIBIZANA NAYE, KUGOMBANA NAYE, KUFANYA MAAMUZI PASIPO KUMSHIRIKISHA, N.K. Haya yote wanafanya wanawake waovu, wasiofaa kitu, wanaomtumikia shetani, wasioamini, akina Yezebeli na Delila, waasi, wakaidi, wasiotii, wenye kiburi, na wenye uchungu, ugomvi, na visasi mioyoni mwao! Haya ndiyo yanavunja ndoa na kamwe siyo tabia za mumeo! HIZO ZOTE ZINAVUMILIKA KAMA UNA UPENDO WA KRISTO MOYONI MWAKO! 1 wakorintho 13:7 inasema, “Upendo huvumiliayote, huamini yote, hustahimili yote, hutumaini yote.” HAPA ANASEMA “YOTE” NA SIYO BAADHI!! Kwa nini unadai talaka? Kwa nini unataka kumuacha? Kwa nini ulimkimbia? KUKOSA KWAKO UPENDO WA MUNGU NA KUTOTII KUMESABABISHA HAYO! Kosa ni lako na siyo lake! Wewe kama ungalishirikiana na Roho Mtakatifu usingefikia kuikacha ndoa au kutaka talaka! Tubu na ukatengeneze mambo ya nyumba yako vinginevyo utaangamia!! Kumbuka imeandikwa, “Kama ukikubali na kuti utakula mema ya nchi;bali kama ukikataa na kuasi utaangamia kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.”(Isaya 1:19-20) WALIOVUNJA NDOA WOTE WAKO HATUA MOJA KABLA YA KUTUMBUKIA JEHANAMU!! USALAMA WAO NI KUTUBU NA KUREJEA KUTENGENEZA MAMBO YA NYUMBA ZAO KABLA HAWAJAFA (Isaya 38:1) TUBU NA UTOKE HARAKA KWENYE NDOA YA UZINZI ULIYOINGIA BAADA YA KUACHANA NA MUMEO/MKEO!!
>> Utii wa mke kwa mumewe una nguvu kubwa ya kusababisha mumewe ampende zaidi! Kama ilivyo kwa mume, mke kumtii mumeo hupelekea kupendwa zaidi! PANDA UTII VUNA UPENDO WA MUME! Usianze kusema hanipendi! Je! wewe unamtii na kujinyenyekeza kwake kwa kiwango kipi??!! Mungu ameweka kanuni yake ya ANZA KUTENDEA VILE UNAVYOTAKA KUTENDEWA NA UENDELEE KUFANYA HIVYO PASIPO KUACHA, KUKATA TAMAA, WALA KURUDI NYUMA!! IMANI ITENDAYO KAZI KWA UPENDO (GAL 5:6) HUVUMILIA!!
1:3 UBINAFSI, UCHOYO, NA UBAHILI KWENYE FEDHA NA MALI
Mungu alipomuumba mwanadamu kwenye kitabu cha Mwanzo Biblia inasema,
28 “Mungu AKAWABARIKIA, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; MKATAWALE samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila mkiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
29 “Mungu akasema, Tazama, NIMEWAPA kila mche utoao mbegu, ulio juu ya nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo CHAKULA CHENU;” (Mwanzo 1:28-29)
Baraka za Mungu kwa mwanadamu zilikwenda kwa MWANAMUME NA MWANAMKE KWA PAMOJA! Mungu hakumbariki Adamu peke yake na baraka zake, wala mwanamke peke yake na Baraka zake! Mungu ALIWABARIKI…!!! Baraka hizi zilikusudiwa kuwa zimilikiwe kwa pamoja (corporate blessings). Baraka zote za ndoa ni za mume na mke kwa pamoja na wala si za mume peke yake wala mke peke yake. Kuhusu pesa, utajiri, na baraka za mali na vitu (money, wealth, and material blessings) kwenye ndoa, lugha sahihi ni VYETU na wala siyo CHANGU au CHAKO, YANGU au YAKO, LANGU au LAKO n.k. Ndoa inatawaliwa na kuongozwa na roho ya ushirika! UMILIKI FEDHA NA MALI NI WA KIUSHIRIKA! Anguko liliingiza roho za shetani za ubinafsi, uchoyo, ubahili, na ubinafsi mioyoni mwa wanadamu na kuwabadilisha wafanane na shetani NA KUPOTEZA ILE SURA NA MFANO YA MUNGU!! Hapa ndipo penye kupotosha kusudi zima na mpango wa Mungu kwenye ndoa! Mwanadamu akadanganyika na kuwa na mawazo maovu kuhusu mwanadamu mwingine!
MUME WA ANGUKO:
1. Anadhani kuwa kichwa maana yake kila kitu ni chake kwenye ndoa na familia.
2. Anafikiri kuwa fedha alizojaliwa kuzipata ni zake yeye peke yake na kwamba anaweza kuzitumia vyovyote vile atakavyo yeye pasipo kujali mkewe na watoto!
3. Anadhani mkewe ni ombaomba ambaye lazima apige magoti kwanza kumwomba yeye mwanamume ili ampe fedha, au mali zozote.
4. Anadhani kumpa fedha au mali yoyote mkewe ni hisani tu na siyo lazima au siyo wajibu wake kufanya hivyo.
5. Haoni umuhimu wala ulazima wa kuweka wazi mapato yake yote kwa mkewe na njia alizotumia kuyapata mapato hayo.
6. Anaona kuwa anaweza kuzitumia baraka za mali, fedha, na utajiri nje ya ndoa na familia kuhonga, kufanya anasa, kufanya dhambi pasipo kujali mke na familia.
7. Huwa ana tabia ya ubahili ambao unamfanya kuumia sana anapolazimika kutumia fedha kwa ajili ya mkewe na familia! Yeye hutaka alimbikize tu fedha na isilete faida hata kwa mkewe na familia.
8. Hamshirikishi mkewe na wala hafanyi majadiliano na mkewe kuhusu mipango ya maendeleo ya ndoa na familia; haoni umuhimu wa kufanya hivyo kwa kuwa anadhani kuwa kichwa maana yake yeye ndiye kila kitu na anajiona kama mungu mtu naye hupenda kumburuza na kumlazimisha mkewe na familia wafuate vile tu atakavyo yeye.
9. Hasikilizi mawazo mazuri ya mkewe au watoto kuhusu maendeleo ya ndoa na familia kifedha, mali, na utajiri. Yaani, yeye ni Mr Hashauriki na Hambiliki!! n.k.
MKE WA ANGUKO:
1. Badala ya kukaa kwenye zamu yake ya kimaandiko ya kumwombea mumewe na kuvipiga vita vya imani kwa ajili ya mumewe, yeye huwa ni mwenye kulalamika, kunung’unika, kulaumu, kukosoa, na kuhukumu tu sikuzote. Mara nyingi kama siyo zote utakuta hakuna alichoamini kuhusu mumewe kazini, kwenye biashara zake au kazi za mikono yake; yani, hana neno lolote la Mungu kuhusu kazi ya mikono ya mumewe, wala fedha zinazopita mkononi mwa mumewe, wala akili na ufahamu wa mumewe kuhusu kupangilia mipango ya kifedha na maendeleo ya familia, wala maamuzi ya mumewe ndani ya nda na familia na huko anakofanyia hiyo au hizo kazi za mikono yake; mumewe hana “cover” (ulinzi) ya maombi ya mkewe na hivyo kuwa “vulnerable” (kushambuliwa kirahisi) katika ulimwengu wa rohona nguvu za giza. Hajui na wala hazingatii kwamba imeandikwa; “……..Kwa maana Bwana ameumba neno jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.” (Yeremia 31:22) Mwanamke wa namna hii hamwamini Mungu, hamtumainii Mungu, na wala hana ushirika na Mungu na ndiyo maana hawezi kwenda mbele za Mungu kusemezana naye kuhusu mumewe, wanawe, kazi ya mikono ya mumewe, na huduma aliyopokea mumewe kutoka kwa Bwana Yesu. Yakobo alisema “………wala hamna kitu kwa kuwa hamuombi. (Yakobo 4:2d) Mungu hafanyi kitu na pia hafanyi vile mke huyu anavyotamani kwa kuwa haombi!! Mamboyakienda kombo anamlaumu mumewe!! Huyu ni mtoa vibanzi badala ya kutoa boriti lake kwanza, tabia ambayo Yesu aliita kuwa ni unafiki (Mathayo 7:1-5)
2. Pale anapokuwa amejaliwa kipato au mapato naye hudhani kuwa sasa amepata uhuru wa kifedha mbali na mumewe, na kwamba sasa anaweza kufanya mambo yake mwenyewe pasipo kuhitaji kumuombaomba tena wala kumshirikisha mumewe. Pale bustanini nyoka alimdanganya Hawa akafanya hilo hilo! ALIFANYA MAAMUZI YANAHUSU NDOA PASIPO KUMSHIRIKISHA MUMEWE KWANZA! Aliamua kutwaa yale matunda yaliyokatazwa kuyala AKAYALA KWANZA! Kisha akamletea mumewe ale, naye AKAYALA!!! 1) Mwanamke alidanganywa na nyoka akaasi! 2) Adamu aliridhia uasi wa mkewe naya akala WAKAANGUKA DHAMBINI! Ndoa ya anguko ni ndoa ya watenda dhambi ambayo inaundwa na HAWA ALIYEDANGANYWA NA KUASI pamoja na ADAMU ALIYERIDHIA UASI WA MKEWE AKAASI! Hawa utawakuta kanisani kama mchungaji na mchungaji, askofu na mama askofu, mume mshirika wa kawaida na mkewe, kiongozi wa taifa na mkewe kama Ahabu na Yezebeli (1 Wafalme 18 &19), n.k. Ni kweli Biblia inasema mke mwema hakosi kupata mapato; “Huangalia shamba akalinunua;KWA MAPATO YA MIKONO YAKE hupanda mizabibu.” (Mithali 31:16) Biblia hapa imesema kwa MAPATO YA MIKONO YAKE, na wala haikusema KWA MAPATO YAKE AU KWA FEDHA YAKE MWENYEWE! Kule kusema mapato ya mikono yake kunamaanisha mke mwema huwa ana kipato na mapato! Lakini haimaanishi kwamba HII NI FEDHA YAKE YEYE MWENYEWE PEKE YAKE! Yeye kama msaidizi lazima awe na mapato ambayo atayatumia kumsaidia mumewe kifedha! Mke mwema ni MSAIDIZI KIFEDHA PIA kama alivyo msaidizi kiroho, kiakili, kihisia, kimwili, kimali na vitu (materially) na kijamii! Mke asiye na Mungu humficha mumewe kipato chake, hukataa kuchangia chochote nyumbani au huchangia kidogo sana kwa madai kwamba yeye mume ndiye kichwa na hivyo lazima abebe mzigo wote! Mke mtenda dhambi wa anguko huwa na uchungu sana moyoni, yaani, anaumia sana moyoni kutoa fedha kwa ajili ya majukumu ya hapa na pale ya ndoa na familia!! Yeye hudhani sasa ndio wakati wa kufanya mambo yake ambayo wakati mwingine huyafanya kwa siri pasipo hata kumwambia mumewe! Shetani ameweka akili mbovu na mawazo maovu ndani ya mke wa anguko kuwa FEDHA ZAKE NI ZAKE PEKE YAKE NA ZA MUMEWE NI ZAKE PIA! Yaani, mke huyu muovu huwa anazigawanya fedha kwenye mafungu mawili: FEDHA ZAKE na FEDHA ZA MUMEWE, naye hujiona ana haki kwenye fedha za mumewe lakini mumewe hana haki kwenye fedha zake! Migogoro mingi na misuguano huzaliwa hapa ambayo hupelekea hata kuvunjika ndoa kwa sababu ya wanandoa kuiacha kweli na hivyo kumkataa Yesu ambaye ni Kweli (Yohana 14:6), Roho naye ni Kweli (1 Yohana 5:7); Mungu ni Kweli (Yohana 3:33); Unapoiacha kweli halafu ukapata matatizo kwenye ndoa yako usisingizie kwamba unaye Mungu, au Roho, au Yesu; maana hawa wote ni MMOJA! Ukiikataa Kweli wewe huna Baba wala Mwana!!
1:4 NAFASI YA NDUGU, JAMAA, NA MARAFIKI KWENYE KUCHOCHEA MIGOGORO YA NDOA NI IPI?
1:5 NI JINSI GANI KUTOJAZWA ROHO MTAKATIFU, NA KUTOENENDA KWA ROHO, KWA ALIYEJAZWA, KUNACHANGIA MIGOGORO NA HATA KUVUNJIKA KWA NDOA?
1:6 NI KWA NAMNA GANI KUTOKOMAA KIROHO NA KUINGIA KWENYE NDOA KWA WACHANGA KIROHO KUNACHANGIA MIGOGORO NA HATA KUVUNJIKA KWA NDOA?
1:7 NI KWA NAMNA GANI IMANI POTOFU KWA WANANDOA WOTE AU MMOJAWAO KUNACHANGIA MIGOGORO NA HATA KUVUNJIKA KWA NDOA?
>> Maswali haya ni homework yako ya kuongeza ufahamu! Hapa chini naweka maandko kadhaa ambayo kutozingatiwa kwake hupelekea migogoro na hata kuvunjika kwa ndoa; Mungu akuwezeshe kuhusisha maandiko haya na ndoa yako, na ndoa zinazokuzunguka kwa wewe mtumishi!
JARIBU KUONA NINI KINAWEZA KUVURUGA HATA KUVUNJA NDOA KWA KUTOYAISHI MAANDIKO HAYA??!!👇👇👇
1) 4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Waebrania 13:4
2)18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
Wakolosai 3:18
19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
Wakolosai 3:19
3) 22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
Waefeso 5:22
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
Waefeso 5:23
24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
Waefeso 5:24
25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
Waefeso 5:25
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
Waefeso 5:26
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Waefeso 5:27
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
Waefeso 5:28
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
Waefeso 5:29
4) 2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
1 Wakorintho 7:2
3 Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
1 Wakorintho 7:3
4 Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.
1 Wakorintho 7:4
5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
1 Wakorintho 7:5
6) 2 Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume.
Warumi 7:2
3 Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.
Warumi 7:3
7) 10 *Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;*
1 Wakorintho 7:10
11 *lakini ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.*
1 Wakorintho 7:11
8) 29 Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;
1 Wakorintho 7:29
9)33 bali *yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.*
1 Wakorintho 7:33
34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. *Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.*
1 Wakorintho 7:34
👆👆👆you must be busy looking for innovative ways to bring happiness, joy and smiles to your spouse!!
10) Malachi 2:14-16 (NLT) *You cry out, “Why doesn’t the LORD accept my worship?” I’ll tell you why! Because the LORD witnessed the vows you and your wife made when you were young. But you have been unfaithful to her, though she remained your faithful partner, the wife of your marriage vows.*
*Didn’t the LORD make you one with your wife? In body and spirit you are his. And what does he want? Godly children from your union. So guard your heart; remain loyal to the wife of your youth.*
“ *For I hate divorce!” says the LORD, the God of Israel. “To divorce your wife is to overwhelm her with cruelty, ” says the LORD of Heaven’s Armies.* “ *So guard your heart; do not be unfaithful to your wife.”*
>> KUKOSA UAMINIFU KWENYE NDOA, KUVUNJA AGANO LA NDOA, KUVUNJA NA KUKIUKA VIAPO VYA NDOA; YOTE HAYA YANAZUIA IBADA YAKO KWA MUNGU! HUWEZI KUMUABUDU MUNGU HUKU UNAMUABUDU SHETANI! MUNGU ANACHUKIA TALAKA!!