JE! UNAMUONA NANI? YESU AU MWANADAMU?
Biblia inaeleza kwamba Kanisa ni mwili wa Kristo ulimwenguni (Waefeso 1:22-23). Lakini pia Kanisa ni Hekalu la Roho Mtakatifu ulimwenguni (1 Kor 3:16) Na hapa anasema,
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe. (1 Kor 6:19)
Maandiko yanasema sisi tuliookoka ni maskani ya Mungu katika Roho (Waefeso 2:19-20). Yaani, Mungu ameunganika na roho zetu zilizozaliwa mara ya pili na tumekuwa mmoja!! Biblia inasema sisi tumo ndani yake na Yeye ndani yetu, na hivyo tumekuwa mmoja! Paulo ameeleza vema kwenye Wagalatia 2:20; “Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilionao sasakatika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, amabaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” SI MIMI NINAYEISHI BALI KRISTO NDIYE ANAYEISHI NDANI YANGU!!!
Kama unaamini Biblia, Kama unaamini maandiko matakatifu, Kama unamwamini Yesu, BASI UNAPOMWONA MTOTO WA MUNGU ALIYEOKOKA UJUE UNAMWONA YESU!! KAMA HUMWONI YESU BADO UMO MWILINI AU HAUAMINI AU NI MTOTO MCHANGA KATIKA KRISTO AU NI MTENDA DHAMBI USIYEAMINI!! KWA NINI NIMESEMA HIVI??!
FILIPO ANATAKA KUMUONA BABA YAKE YESU
Biblia inasema,
Yohana 14:7
“Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua tena mmemuona.
Yohana 14:8
“Filipo akamwambia, Bwana utuonyeshe Baba, yatutosha.”
Yohana 14:9
“Yesu akamwambia, MIMI NIMEKUWAPO PAMOJA NANYI SIKUZOTE HIZI, WEWE USINIJUE, FILIPO? ALIYENIONA MIMI AMEMUONA BABA; basi wewe wasemaje , Utuonyeshe Baba?”
Yohana 14:10
“Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu;………….”
Yohana 10:30
“I and the Father are one (Mimi na Baba tu mmoja)”
1. UKIMJUA YESU (NENO) NDIPO UTAMJUA NA BABA YAKE YESU.HUWEZI KUMJUA MUNGU BABA YETU PASIPO KULIJUA NENO LILILO HAI LIDUMULO HATA MILELE AMBALO NDILO YESU!!! MAANA BABA NI ROHO WA NENO!-MST 7
2. FILIPO BADO ANANG’ANG’ANIA KUONYESHWA BABA-MST 8
3. MIMI NDIYE BABA YAKO FILIPO! MIMI NIMEKUWA PAMOJA NAWE SIKU ZOTE HIZI (MIAKA KARIBU MITATU) USINIJUE FILIPO??!! ALIYENIONA MIMI AMEMUONA MUNGU BABA!!! SASA UNAWEZAJE KUSEMA UNATAKA KUMWONA BABA AMBAYE UMEKUWA NAYE SIKUZOTE HIZI??!!- MST 9
4. AU FILIPO HAUAMINI KWAMBA MIMI NIMO NDANI YA BABA NA BABA YUMO NDANI YANGU??!! YAANI, MIMI NA BABA NI MMOJA??!!!-MST 10
5. YESU ALISHATANGULIA KUWAAMBIA WANAFUNZI WAKE KWAMBA YEYE NA BABA NI MMOJA!! HII INATOSHA KUHITIMISHA KWAMBA “MWANA WA MUNGU YESUNI MUNGU KWENYE MWILI!!!” (GOD IN THE FLESH)
Sasa Biblia inasema Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo Yesu amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama yote yamekuwa mapya!!! (2 Kor 5:17). Hii inamaanisha unapomwamini Yesu na kuokoka unakuwa unakuwa mtu mpya ndani yake kwa kuwa unakuwa umeumbwa upya roho yako kwa kuzaliwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu (Tito 3:4-5) Na pale anapokushirikisha Roho wake ukiwa umeshamwamini na unalikiri jina lake maana yake Yeye yumo ndani yako! Nilisemalo ni hili huwezi kuwa ndani yake Yesu pasipo Yeye kuwa ndani yako!!! Kwa kuwa lengo lake la kukuokoa ni WEWE NA YESU KUWA MMOJA!AMBAYO INAMAANISHA WEWE NA NENO MMEKUWA MMOJA! HII MAANA YAKE WEWE NA BABA NI MMOJA!! NA YOTE HII INAWEZEKANA KWA ROHO MTAKATIFU KAMA ILIVYOANDIKWA SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI NI KWA ROHO YANGU (ZECHARIA 4:6) Yohana aliandika; “Naye azishikaye amri zake hukaa NDANI YAKE YEYE(YESU) NAYE(YESU) NDANI YAKEYEYE (ALIYEOKOKA). Na katika hili tunajua kuwa anakaa ndani yetu kwa huyo Roho aliyetupa.”
>> IMANI KWA YESU NA UTII WA KWELI KWA KULITENDA NENO UNATHIBITISHA KWAMBA UMO NDANI YAKE NA KUNAKUHAKIKISHIA PIA KUBAKI NDANI YAKE!!!
>> UWEPO WA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO NA NGUVU ZAKE KUNAMAANISHA YESU YUMO NDANI YAKO!!!
Kama hivi ndivyo ilivyo inamaanisha WEWE UMO NDANI YAKE NA YEYE YUMO NDANI YAKO, NA HIVYO WEWE NA YEYE NI MMOJA!! SIRI NA LENGO KUU LA WOKOVU NI KWA ALIYEOKOKA KUFIKIA KUWA MMOJA NA YESU KAMA TULIVYOELEZA NA HAPO NDIPO UNAWEZA KUMZALIA MUNGU MATUNDA NA KUENENDA KATIKA BARAKA ZOTE ZA ROHONI ULIZOBARIKIWA NAZO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NDANI YAKE KRISTO YESU MWOKOZI (WAEFESO 1:3) UTAKASO WOTE UNAIMARISHA HUKU KUZIDI KUWA MMOJA NA YESU KUNAKOELEZEWA KAMA KUZIDI KUUMBIKA KWA YESU NDANI YAKO (WAGALATIA 4:19). NAKO NDIKO KUNAKOZIDI KUKUFANANISHA NA YESU ILI UFIKIE CHEO CHA KIMO CHA UTIMILIFU WAKE KRISTO.
YESU YUKO KAZINI HATA SASA NDANI YA ALIYEOKOKA!!
Katika Yohana sura ya tano Wayahudi walimjia juu Yesu kwa kuwa amemponya mtu siku ya sabato! Lakini yeye akawaambia kwamba MUNGU HUWA YUPO KAZINI WAKATI WOTE NA KAMWE HAPUMZIKI!
Yohana 5:17
“Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.”
>> MUNGU BABA ALIYE ROHO YUKO KAZINI HATA SASA, NA KWA KUWA YEYE NA YESU NI MMOJA, YESU NAYE YUKO KAZINI. MUUNGU HAJAACHA KUTENDA KAZI ILI KUKAMILISHA KUSUDI LAKE LA MILELE KATIKA KRISTO YESU. Paulo aliandika, “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.” (Wafilipi 1:6)
>> BWANA YESU YUKO KAZINI NDANI YA MKRISTO ALIYEOKOKA!!! Tangu alipookoka Bwana Yesu alianza kazi ya kumtakasa, kumuimarisha, kumfundisha, kumtengeneza, kumtia nguvu, kumuongoza, kumuelekeza, kumwezesha, n.k. huyu Mkristo aliyeokoka! Hivyo wakati wowote umwonapo aliyeokoka ujue kwamba Yesu yuko kazini ndani yake licha ya vyovyote umwonavyo alivyo, vyovyote anenavyo, au vyovyote atendavyo! JE! WEWE UNAWEZA KUMNYOOSHEA KIDOLE MUNGU AWAPO KAZINI? UNAWEZA KUIKOSOA KAZI AITENDAYO MUNGU? UNAWEZA KUIBEZA KAZI INAYOENDELEA NDANI YA MTOTO WA MUNGU KWA ROHO MTAKATIFU? Unaponena maneno yasiyo ya imani kumhusu mtoto wa Mungu maana yake unamkosoa Mungu aliyemo kazini ndani yake!! Mungu amesema ataimaliza kazi hiyo, lakini wewe unasema huyu mbishi! Huyu mwongo! Huyu anajiona bora! Huyu anajiona wa kiroho zaidi kuliko wote! Huyu anajiona anajua kila kitu! Huyu mbahili! Huyu amepotoka! Huyu ana imani potofu! Huyu hawezi kuingia mbinguni! Na maneno mengi kama hayo yenye kumkosea heshima na adabu Mungu aliyemuosha kwa damu yake ambayo wewe unaikanyaga kwa kumrudisha Yesu msalabani ndani yake huyo unayemnenea mabaya kana kwamba unaujua mwisho waqke au kana kwamba una uhakika hatatubu wala hatabadilika!!! Uhakika huo umeupata wapi wakati yeye aliyemfia msalabani amesema ATAIMALIZA KAZI YAKE YAKE YA REHEMA, MSAMAHA, NA UTAKASO ALIYOIANZA NDANI YAKE HUYO ALIYEOKOKA???!!! UNAMDHARAU MUNGU? UNAIDHARAU KAZI YAKE AIFANYAYO NDANI YAKE ALIYEOKOKA UNAYEMNENEA UPUUZI KWA KINYWA CHAKO? Mtenda dhambi huwezi kamwe kuijua kazi yake Mungu aitendayo kama ilivyoandikwa; “ Kama vile wewe usivyoijua njia ya upepo ni ipi, wala mifupa ikuavyo tumboni mwake mjamzito;KADHALIKA HUIJUI KAZI YAKE MUNGU AFANYAYE MAMBO YOTE.” (Mhubiri 11:5)
>> Mungu haangalii kama mwanadamu bali yeye HUUTAZAMA NA KUUTANGAZA MWISHO TANGU MWANZO (ISA 46:10)
>> KAMA UNGALIKUWA UNAAMINI NA WEWE UNGALIUTANGAZA MWISHO TANGU MWANZO!! USINGETANGAZA HAYO UYAONAYO AU UYASIKIAYO LEO!! (ISAYA 11:3)
“……wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake.” (Isaya 11:3)
>> KAMA UNATOA HUKUMU KWA KUYAFUATA YALE UYAONAYO KWA MACHO YAKO AU YALE UYASIKIAYO KWA MASIKIO YAKO HII INATHIBITISHA BADO UKO DHAMBINI, UKO MWILINI, AU NI MTOTO MCHANGA KIROHO!! HAUJAJUA BADO KUISHI KWA IMANI NI NINI NA UNAENENDA KIMWILI UKITUMIKISHWA NA KAWAIDA ZA KWANZA ZA ULIMWENGU HUU! YAANI, KAMA WEWE KUJUA KWAKO, KUELEWA KWAKO, NA KUFAHAMU KWAKO NI MPAKA UONE AU KUAMBIWA NA WANADAMU, UJUE BADO UKO CHINI YA IMAYA YA SHETANI MAANA IMEANDIKWA; “….TUNAENENDA KWA IMANI NA SI KWA KUONA.” (2 Kor 5:7) NA TENA; “MWENYE HAKI WANGU ATAISHI KWA IMANI (WARUMI 1:17)
Imani lazima ikupe uhakika wa mambo yatarajiwayo nay ale yasiyoonekana yawe bayana kwako! (Waebrania 11:1). Unapokuwa umeamini;
1. LAZIMA UWE NA UHAKIKA WA KESHO YAKO, NA YAKE, NA YAO! LAZIMA UWE NA UHAKIKA WA KESHO YA KILA JAMBO, KILA NENO, NA KILA KITU!!! Hii ni kwa kuwa umemwamini Alpha na Omega, Mwanzo na Mwisho, Wa Kwanza na wa Mwisho!!!! Imani inakuhakikishia kuufikia au kutimia kwa mwisho ulionenwa na andiko au uliotabiriwa au kutimizwa kwa ahadi iliyoahidiwa!! Neno la Mungu lina majibu yote ya maswali yote, utatuzi wote wa matatizo yote, na suluhisho la kila tatizo! HII INAONDOA KABISA MASHAKA YOTE, WASIWASI WOTE, HUZUNI YOTE, KUFADHAIKA KOTE, KUCHANGANYIKIWA KOTE, KUKATA TAMAA KOTE, WOGA WOTE, HOFU YOTE, KUSITA SITA KOTE, KUBABAIKA KOTE, MASUMBUFU YOTE, HASIRA NA GHADHABU ZOTE, UCHUNGU WOTE, KUVUNJIKA MOYO KOTE, KUTOJUA KOTE, KULALAMIKA KOTE, KUNUNG’UNIKA KOTE, KULAUMU KOTE, NA KUKOSOA KOTE N.K.
2. Lazima yote yasiyoonekana unayoyatarajia ukiwa na uhakika nayo yawe bayana kwako! Yaani, yawe katika miliki yako! Lazima uwe unayamiliki yale yote uyatarajiayo kwa kuwa umemwamini Yesu! Kwa kuwa umeliamini neno! HII INAONDOA UHITAJI WOTE, UPUNGUFU WOTE AU KUISHIWA KOTE!!
3. LAZIMA MATATIZO YAWE YAMEONDOKA YOTE KABLA HAYAJAONDOKA, SHIDA ZIMEKWISHA KABLA HAZIJAISHA, WATU WAMEBADILIKA KABLA HAWAJABADILIKA, WATU WAMETAKASIKA KABLA HAWAJATAKASIKA, IMEKUWA KABLA HAIJAWA, IMETOKEA KABLA HAIJATOKEA, IMEWEZEKANA KABLA HAIJAWEZEKANA, UMEPONA KABLA DALILI HAZIJATOWEKA, MILIMA IMENG’OKA WAKATI BADO IPO, NURU IMENG’AA WAKATI BADO GIZA LIPO, N.K. YAANI, KILE UKIONACHO KWA MACHO, AU UKISIKIACHO KWA MASIKIO, AU VILE UJISIKIAVYO KWENYE MWILI VIWE NI UONGO BALI NENO NA AHADI PEKE YAKE LIWE NI KWELI!!!
4. NENO LA MUNGU NA AHADI ZAKE NI KWELI PASIPO KUJALI WEWE UMESIKIA NINI, UMEONA NINI, AU UNAJISIKIAJE KWENYE MWILI WAKO!! UMEITWA KUISHI KWA IMANI! HAYO MAISHA YA KUONGEA KINYUME NA NENO KUHUSU KANISA, KUHUSU MWILI WA KRISTO, KUHUSU WATOTO WA MUNGU, NA KUHUSU WATAKATIFU NDIYO MAISHA ANAYOYAPENDA SHETANI MAANA UNAYAFANYA MAPENZI YAKE!!! UNAISHI DHAMBINI!! HII NDIYO MAANA IMEANDIKWA KWA MANENO YAKO UTAHUKUMIWA NA KWA MANENO YAKO UTAHESABIWA HAKI (MATHAYO 12:37)
>> Wewe huwa unamuona nani unapokusanyika na watakatifu? Unamuona Yesu au unawaona wanadamu? Je! Kwako kanisa ni jengo? Unamsema vibaya Yesu kwa kuusema vibaya mwili wake? Una tofauti gani na Sauli wa Tarso aitwaye Paulo alichokuwa akikifanya mpaka akatokewa na Bwana Yesu njiani alipokuwa akielekea Dameski kuwatesa na kuwafunga wanafunzi wa Yesu?
“…..ghafla ikamwangukia kotekote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini,akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?Akasema, U nani wewe Bwana?Naye akasema, MIMI NDIMI YESU UNAYENIUDHI WEWE.” (Mdo 9:3-5)
>>MIMI NDIMI YESU UNAYENIITA WEWE NAJIONA WA KIROHO, NINAJIVUNA, SINA UPENDO, NAJIONA NAJUA KILA KITU, NINA ROHO NYINGINE, NI MBAHILI, NIMEPOTOKA, NINA IMANI POTOFU, MWONGO, NAONGEA TU MAWAZO YANGU, SIINGII MBINGUNI,MBISHI, NINA HASIRA, NINA UCHUNGU, NINANENA KWA LUGHA ZA MASHETANI, N.K. HAYA YOTE NA MENGI MENGINE KAMA HAYO UMEYAPATA KWA NANI??!! KWA YESU!! LA HASHA! HAYO UMEYAPATA KWA BABA YAKO SHETANI AMBAYE HAMNA KWELI NDANI YAKE NA WALA HAKUSIMAMA KWENYE HIYO KWELI TANGU MWANZO; NA SIKU ZOTE HUSEMA UONGO KWA FAIDA YAKE MWENYEWE. NAYE NI BABA WA HUO UONGO!!! (YOHANA 8:44)