HUWEZI KUMBADILISHA MWANADAMU, BALI MUNGU PEKEE NDIYE ANAYEWEZA!!
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 1:27
NA TENA,
Mwanzo 5:2
[2]mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
Male and female created he them; and blessed them, and called their name Adam, in the day when they were created.
Biblia inasema, Mungu ni Roho (Yohana 4:24)
>> Hivyo Mungu anapoumba mwanadamu kwa sura na mfano wake maana yake anaumba "roho"!! Yaani, Mungu Aliye Roho anaumba roho ya mwanadamu!! Anaumba roho ya mwanamume na roho ya mwanamke kwa neno lake kama tulivyoona kwenye andiko hapo juu!! Biblia inasema,
7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Mwanzo 2:7
Mtu ama mwanadamu aliumbwa hivi:
1) MWILI ULITENGENEZWA KWA MAVUMBI YA ARDHI (man's body)
2) KISHA MUNGU AKAMPULIZIA PUANI PUMZI YA UHAI, AMBAYO NDIYO roho ya huyo mtu (man's spirit)
3) NDIPO MWANADAMU AKAWA NAFSI HAI ( LIVING SOUL)-(man's soul)
>> Ndiposa twasema mwanadamu =[ roho + nafsi] + mwili, yaani mwanadamu ni roho mwenye nafsi naye anaishi kwenye mwili!!
>> Nafsi ilitajwa mara tu roho ilipoingia ndani ya mwili na hivyo kumaanisha kwamba nafsi iko na roho na huwezi kuitenganisha!.Yaani, roho ina nafsi! Mungu ni Roho na ana nafsi pia!!
>> Kuumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ni kule kuwa na roho na nafsi kama Mungu!! Tofauti ni kuwa Mungu hana mwili na kwamba roho na nafsi zetu zimetokana na yeye!!
>> Uhai au maisha yako kwenye roho!! Na hii ndiyo maana mtu alikuwa nafsi hai baada ya pumzi ya Mungu (roho) kuingia ndani ya mwili wake.
>> Nafsi ya mwanadamu ina maeneo matatu makuu,
1) Eneo la Mawazo/Fikra linalozaa akili kupitia tafakari au kufikiri. (MIND)
2) Eneo la Nia/Makusudi/Mapenzi (WILL)
3) Eneo la Hisia.(EMOTIONS)
HIVYO:
NAFSI(SOUL) = MAWAZO/AKILI/ FIKRA (MIND) + NIA/MAPENZI/MAKUSUDI (WILL) + HISIA (EMOTIONS)
>> roho ndiyo chanzo cha mawazo yote, yaani, mawazo ya roho yako ndiyo yanayokuwepo nafsini mwako. Lakini pia nafsi huwa inapokea na kuchakata mawazo ya roho zingine kutoka nje! Hivyo mawazo huwa yanaletwa kutoka rohoni (moyoni) au nje kutoka kwa wanadamu au roho za shetani!!! (mapepo)
>> Kwa kuwa mawazo ya nafsini ni mengi, nayo yatoka ndani na nje, hapa ndipo ushawishi mkubwa kuhusu mwelekeo wa maisha na maamuzi yote hukubaliwa na kupitishwa na kisha kutendewa kazi, ama kukataliwa na kutupwa!! Kiufupi Biblia inasema,
Mithali 23:7
[7]Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Akuambia, Haya, kula, kunywa;
Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
For as he thinketh in his heart, so is he: Eat and drink, saith he to thee; but his heart is not with thee.
>> MTU VILE ANAVYOFIKIRI AMA AONAVYO NAFSINI MWAKE NDIVYO ALIVYO, MAANA NDIVYO roho yake ILIVYOCHAGUA KUWA IWE, AU MAMBO YAWE! MTU VILE ALIVYO NI JUMLA YA roho YAKE NA MAWAZO YA NAFSI YAKE YALIVYO!!
>> MAWAZO YA MTU YALIYOKWISHA KUCHAKATWA NA KUKUBALIWA NDIYO HUPELEKEA MAAMUZI AU MAKUSUDIO AU MAPENZI YA MTU HUYO! YAANI, MTU HUYU SASA ANANIA AU KUKUSUDIA NAFSINI MWAKE KUTENDA AU KUENENDA SAWASAWA NA AKILI ZAKE ZILIVYO/ MAWAZO YAKE YALIVYO
>> KISHA MTU HUYU ATAFURAHIA KWA HISIA ZAKE KUFANYA AFANYAVYO AU KUTENDA ATENDAVYO KWA KUWA MOYO WAKE UMERIDHIA KUTENDA HIVYO!
>> TUNAPOSEMA MOYO MARA ZOTE TUNAMAANISHA roho YA HUYU MTU!! rohoni mwake ni moyoni na nafsini mwake!!
>> MTU HALISI NI MOYO (ROHO) NA NAFSI, NA MANENO YA MTU HUYU NI MAWAZO NA FIKRA ZAKE AU AKILI ZAKE AMBAZO AMEZIPA SAUTI!! YAANI, AMENENA AU KUONGEA!! Imeandikwa:
"......kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake" (Mathayo 12:34)
>> HAYA YA MOYONI NDIYO YANAYOTOKA ROHONI MWAKE!!
>> HIVYO MTU UNAMTAMBUAJE KIROHO? UTAMTAMBUA KWA MATUNDA YAKE!! (MATHAYO 7:16,20)
>> MATUNDA NI MAWAZO YA ROHO YAKE AMBAYO UTAYASIKIA KUPITIA MANENO YAKE!!
>> MATUNDA NI MATENDO YAKE AYATENDAYO KWA MSUKUMO NA UONGOZI WA roho ILIYOMO NDANI YAKE!!
>> MATUNDA HUKUA KWENYE MATAWI YA MTI, NA MAWAZO HUTOKA KWENYE NAFSI YA ROHO YAKE!!
◇◇JE! UNATAKA ABADILIKE??!! AU UNATAKA KUMBADILISHA??!!
1) AONAVYO NAFSINI MWAKE NDIVYO ALIVYO (MITH 23:7)
>> ILI ABADILIKE VILE ALIVYO LAZIMA,
A) MAWAZO YAKE YABADILIKE, FIKRA ZAKE ZIBADILIKE, NA AKILI ZAKE ZIBADILIKE,
B) LAZIMA ABADILI NIA YAKE, ABADILI MAKUSUDIO YAKE, ABADILI MAPENZI YAKE, ABADILI MITAZAMO YAKE, ABADILI MISIMAMO YAKE, NA HII HAIWEZEKANI MPAKA ABADILI KUFIKIRI KWAKE!!!
>> ELIMU YOYOTE YA SHULE AU CHUO CHOCHOTE INAWEZA KUMUONGEZEA MTU MAWAZO MAPYA NA AKILI MPYA AMBAZO ZITATUMIWA MAISHANI MWAKE NA ILE roho ILIYOMO NDANI YAKE!! HII NDIYO MAANA HAMNA SHULE AU CHUO KINACHOOKOA!! MZINZI HABADILISHWI NA KUACHA UZINZI KWA SABABU ANA DIGRII SABA!! MTENDA DHAMBI HAACHI KUTENDA DHAMBI KWA SABABU AMESOMA SANA, BALI ATATUMIA USOMI WAKE KUTENDA DHAMBI KWA USTADI ZAIDI ILI ALETE MADHARA MAKUBWA ZAIDI, AU ANUFAIKE ZAIDI!!!
C) LAZIMA ABADILI HISIA ZAKE KWA KUANZA KUFURAHIA MAMBO MAPYA AMBAYO PENGINE PALE AWALI ALIKUWA HAYAFURAHII!!
1) JE! UNAWEZA KUBADILISHA ROHO YA MWANADAMU??!!
2) JE! UNAWEZA KUBADILISHA NAFSI YAKE MWANADAMU?
>> NI DHAHIRI HUWEZI KUBADILI CHOCHOTE KATIKA HAYA!! HIVYO HUWEZI KUMBADILISHA MWANADAMU KAMWE!! LAKINI WEWE MBONA UNAFIKIRI UTAWEZA KUMBADILI MWANADAMU KWA KUMPIGIA MAKELELE YASIYOISHA??!! KWA MAGOMVI KILA MARA??!! KWA MANENO YA HOVYO YASIYOFAA KILA SIKU??!! KWA KUMBANA NA KUMKANDAMIZA??!! KWA MATUSI NA VITISHO??!! KWA LAANA NA KULAZIMISHA??!! N.K.
>> KWA KUJARIBU HAYO ILI KUMBADILISHA MWANADAMU UTAVUNA JEURI, UBISHI, UKAIDI, UPINZANI, KUPUUZWA, KUTOSIKILIZWA, KIBURI, DHARAU, MIFARAKANO, MIGONGANO, MIVUTANO, MAGOMVI, UASI, UADUI, UCHUNGU MOYONI, N.K. VISIVYOISHA!!! UNAJARIBU KUFANYA YALE ANAYOWEZA KUYAFANYA MUNGU TU PEKE YAKE!!! KUMBUKA IMEANDIKWA,
Luka 18:27
[27]Akasema, Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu.
And he said, The things which are impossible with men are possible with God.
>> YALIYOKUSHINDA WEWE HAYAWEZI KUMSHINDA MUNGU!! LAZIMA UJE KWA MUNGU AKUSAIDIE!!!
>> USIYOYAWEZA WEWE MWANADAMU MUNGU ANAYAWEZA!! HIVYO LAZIMA UJE KWAKE!!
>> HUTAWEZA KAMWE KUMBADILISHA MKEO, MUMEO, WANAO, NDUGUZO, BOSI WAKO, WAFANYAKAZI WAKO, WAZAZI WAKO, JIRANI ZAKO, RAFIKI ZAKO, WASHIRIKA WENZAKO, WATAKATIFU WENZAKO, VIONGOZI WAKO, N.K. LAKINI MUNGU ANAWEZA NA NI LAZIMA UJE KWAKE UOMBE MSAADA WAKE!!!
LAKINI KWANZA........!
>> Lazima ujue kwamba,
Yohana 9:31
[31]Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
Now we know that God heareth not sinners: but if any man be a worshipper of God, and doeth his will, him he heareth.
>> MUNGU HAWEZI KAMWE KUSIKIA SALA ZAKO AU MAOMBI YAKO UKIWA BADO NI MTENDA DHAMBI
Isaya 59:1-2
[1]Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
Behold, the LORD'S hand is not shortened, that it cannot save; neither his ear heavy, that it cannot hear:
[2]lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
But your iniquities have separated between you and your God, and your sins have hid his face from you, that he will not hear.
>> MTENDA DHAMBI USIJIDANGANYE KWA SALA NA MAOMBI MENGI, MUNGU HATAKI KUKUSIKIA KABISA!! AMEFICHA USO WAKE NA KUZIBA MASIKIO YAKE ILI ASIKUSIKIE MTENDA DHAMBI! DHAMBI ZAKO ZIMEUFICHA USO WAKE HATA HATAKI KUSIKIA!! LAZIMA KWANZA UAMUE KUACHANA NA DHAMBI MOJA KWA MOJA KWA KUMUAMINI YESU, KUZITUBIA DHAMBI ZAKO, NA KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO!!! HAPO NDIPO MUNGU ATAANZA KUSIKILIZA MAOMBI YAKO!!!
>> NA KWA WEWE ULIYEOKOKA HALAFU UKAJIKWAA NA KUANGUKA, AU UMERUDI NYUMA, AU UMEPATA SHIDA KWENYE NDOA, N.K. TUBU HALAFU UREJEE KWA YESU, NA UENDELEE KUISHI MAISHA YA UTAKASO!!! MUNGU HUWA ANAKUSIKIA NA KUKUTENDEA KWA KADIRI YA USAFI WA MOYO WAKO AU USAFI WA MIKONO YAKO!!
2 Samweli 22:21,25,27
[21]BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu;
Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.
The LORD rewarded me according to my righteousness: according to the cleanness of my hands hath he recompensed me.
[25]Basi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu;
Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
Therefore the LORD hath recompensed me according to my righteousness; according to my cleanness in his eye sight.
[27]Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu;
Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.
With the pure thou wilt shew thyself pure; and with the froward thou wilt shew thyself unsavoury.
>> U MWENYE HAKI KIASI GANI MBELE ZAKE??!! UNAISHI KWA IMANI??!! MAANA MWENYE HAKI WAKE HUISHI KWA IMANI!!! JE! U MTAKATIFU KIASI GANI MBELE ZAKE?! U MNYENYEKEVU KIASI GANI MBELE ZAKE??!!
>> MAJIBU YA MUNGU KWAKO YANATEGEMEA USAFI WA MOYO WAKO KAMA ILIVYOANDIKWA HERI WENYE MOYO SAFI MAANA HAO WATAMWONA MUNGU!! (MATHAYO 5:8)
>> NINASISITIZA USAFI WA MOYO KWA SABABU NI LAZIMA UMKABIDHI MUNGU WATU WALE WOTE UNAOTAMANI WABADILIKE ILI YEYE NDIYE AWABADILISHE!!
>> NA UKIANZA KUJA KWAKE UTAKUTA KANUNI HII HAPA:
Mathayo 7:3-5
[3]Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?
And why beholdest thou the mote that is in thy brother's eye, but considerest not the beam that is in thine own eye?
[4]Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
Or how wilt thou say to thy brother, Let me pull out the mote out of thine eye; and, behold, a beam is in thine own eye?
[5]Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Thou hypocrite, first cast out the beam out of thine own eye; and then shalt thou see clearly to cast out the mote out of thy brother's eye.
>> BADILIKA WEWE KWANZA, MPENDEZE MUNGU WEWE KWANZA, UWE MTAKATIFU WEWE KWANZA, JITAKASE WEWE KWANZA, NYENYEKEA WEWE MWENYEWE KWANZA, TUBU WEWE MWENYEWE KWANZA, MTII MUNGU WEWE MWENYEWE KWANZA, ONDOA BORITI YAKO WEWE MWENYEWE KWANZA, TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO WEWE MWENYEWE KWANZA, NDIPO MUNGU ATAONA HAJA YA KUSHUGHULIKA NA VIBANZI VYAO!!
>> KWA NINI UNATAKA VIBANZI VYAO VITOKE WAKATI WEWE HUTAKI KUTOA BORITI YAKO KWANZA??!! HIYO YESU AMEIITA roho ya unafiki!! TUBU KWANZA NA KUACHA UNAFIKI NDIPO UTAONA MABADILIKO KWA WAPENDWA WAKO MBALIMBALI!!
>> WEWE KWANZA, KISHA WAO BAADAE!! WEWE KWANZA KISHA MKEO/ MUMEO BAADAE!! WEWE KWANZA KISHA HUYO MWINGINE BAADAE!! TOA BORITI, TUBIA ĶWA DHATI DHAMBI ZAKO!!
Mithali 28:13
[13]Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;
Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
He that covereth his sins shall not prosper: but whoso confesseth and forsaketh them shall have mercy.
>> KANUNI NI KUZIUNGAMA DHAMBI ZAKO KWA YESU NA KUZIACHA KABISA, ILI UWE MTAKATIFU, NDIPO UTAPATA REHEMA (ONDOLEO LA DHAMBI)
>> YESU ANASEMEHE DHAMBI, NA KUZIONDOA, NA KUKUPA UZIMA WA AMA MAISHA YA MILELE KWENYE UFALME WAKE WA MILELE!! KUTUBU NA KUZIRUDIA DHAMBI ZILE ZILE NI UONGO WA SHETANI ALIOWADANGANYA WALE WASIOTAKA KUACHA DHAMBI!!
>> KWA NINI UKIRI DHAMBI ZAKO HALAFU BADO DHAMBI HIZO ZIENDELEE KUBAKI NDANI YAKO??!! INA MAANA MUNGU AMESHINDWA KUiZIONDOA??!! DAMU YA YESU YA AGANO ILIMWAGIKA KWA AJILI GANI KAMA DHAMBI HAZIONDOKI???!!!
Mathayo 26:28
[28]kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
For this is my blood of the new testament, which is shed for many for the remission of sins.
1 Yohana 3:4-6,8-10
[4]Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
Whosoever committeth sin transgresseth also the law: for sin is the transgression of the law.
[5]Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
And ye know that he was manifested to take away our sins; and in him is no sin.
[6]Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
Whosoever abideth in him sinneth not: whosoever sinneth hath not seen him, neither known him.
[8]atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
He that committeth sin is of the devil; for the devil sinneth from the beginning. For this purpose the Son of God was manifested, that he might destroy the works of the devil.
[9]Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
Whosoever is born of God doth not commit sin; for his seed remaineth in him: and he cannot sin, because he is born of God.
[10]Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
In this the children of God are manifest, and the children of the devil: whosoever doeth not righteousness is not of God, neither he that loveth not his brother.
>> WATOTO WA MUNGU HAWATENDI DHAMBI, NA WATOTO WA SHETANI WANATENDA DHAMBI
>> HAIJALISHI UNA DINI AU DHEHEBU GANI KAMA UNATENDA DHAMBI ZISIZOONDOKA MOJA KWA MOJA BADO HAUJAOSHWA KWA DAMU YA AGANO YA YESU!! Ungelikuwa kiumbe kipya sasa!! (2 Kor 5:17)
>> SASA MTENDA DHAMBI BADO UTATAKA WATENDA DHAMBI WENGINE MUNGU AWABADILISHE WAKATI WEWE MWENYEWE HUTAKI KUBADILIKA??!! BADILIKA WEWE KWA KUINGIA NDANI YA YESU ILI UWEZE KUWASOGEZA HAO MBELE ZA MUNGU KWENYE MAOMBI, DUA, SALA, NA MAOMBEZI!!!
1 Timotheo 2:1-4
[1]Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
I exhort therefore, that, first of all, supplications, prayers, intercessions, and giving of thanks, be made for all men;
[2]kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
For kings, and for all that are in authority; that we may lead a quiet and peaceable life in all godliness and honesty.
[3]Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;
For this is good and acceptable in the sight of God our Saviour;
[4]ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.
Who will have all men to be saved, and to come unto the knowledge of the truth.
>> NI MUNGU BABA PEKEE (ROHO) NA MWANA WAKE PEKEE YESU (NENO LAKE ) NDIYE ANAYEWEZA KUMBADILISHA MWANADAMU AWE KIUMBE KIPYA (2 KOR 5:17)
>> Mwamini Yesu na umtumaini, naye atafanya!!